Kinga wanayokwenda kuwekewa Polisi 'undercover' kwenye Sheria inaweza ikahalalisha Polisi kufanya uhalifu dhidi ya binadamu kama Mtwara?

Wahalifu pekee ndio wenye hofu na hicho kipengele kama raia mwema hofu ya nini,sheria isiwe kikwazo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kushindwa kufanya kazi zao ipasavyo na kuendeleza usalama uliopo,katika marekebisho yaliyofanyika wahusika wawezeshe hizo agence kuweza kufanikisha shunguli zao hasa vitendea kazi na rasilimali fedha vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu.
Yule dogo kule mtwara alikua muhalifu? Lakini unapaswa kufahamu undercover Hawa wakiwa wanafanya uchunguzi huchukua hadi raia wema ili kuwasaidia uchunguzi.
Mfano yakitokea mauaji mtaani kwako, wanaweza kukubeba wewe pia ili wakuhoji. Na hapo kwenye kuhoji wanaweza kukutendea uhalifu
 
Wahalifu pekee ndio wenye hofu na hicho kipengele kama raia mwema hofu ya nini,sheria isiwe kikwazo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kushindwa kufanya kazi zao ipasavyo na kuendeleza usalama uliopo,katika marekebisho yaliyofanyika wahusika wawezeshe hizo agence kuweza kufanikisha shunguli zao hasa vitendea kazi na rasilimali fedha vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu.
Hapana kwakweli. Hii ikipita ni hatari sana. Tunajijua sisi ngozi nyeusi once kunapokuwa na loophole. Sheria ni vema ikaendana na hulka na tabia ya jamii husika. Fikiria tu kwasasa hivyo sheria haipo lakini kuna rafu nyingi sana.
 
Moja ya mapendekezo yanayopelekwa bungeni ni polisi kutoadhibiwa Kwa jinai pale wanapotekeleza majukumu Yao wakiwa undercover na kusababisha jinai . Kwa mfano polisi yupo undercover akapiga mtu RISASI akidhani ni mwalifu awezi kushtakiwa.

Ikitokea polisi Kuna maandamano au Kuna Jambo lolote la kutafuta haki linaendelea polisi wakataka kulizima na katika kulizima ikatokea jinai basi huyo askari atochunguzwa wala kufikishwa mahakamani Kwa tuhuma zozote.

Aina hizi za Sheria zinaletwa Tanzania Wakati Nchi nyingine ikiwemo Kenya walishafuta kesi hizi na Kinga za aina hii na kuziondolea mbali ambapo Kenya hata Rais akitenda jinai anashtakiwa. Tumeona Afrika Kusini na mataifa mengi yanayojali haki ya kuishi na haki ya Kila mtu yupo chino ya Sheria wakiongoa hizi Sheria. Kwa Tanzania Rais, Makamu, Waziri Mkuu, spika, judge, na Sasa police nao Wana Kinga. Kwa maana nyingine Wananchi pekee ndio wasio na Kinga ila watumishi wa umma wengi na wanasiasa wamewekewa Kinga.

Kwanini tunawaza kuhalalisha uhalifu Kwa watu wanaolipwa mishahara? Hivi hii Kinga ingekuwepo Leo Waziri Mkuu angeenda kuunda Tume ya issue ya Mtwara? Kwanini tusitegemee Kuanzia kesho kutwa Sheria ikipita basi Kila mauaji ya dola tunaambiwa yanafanyika undercover? Kwanini Sheria kama hizi zinapelekwa kwa hati ya dharura? Kuna uharaka Gani?

56A08B3B-9953-4CC4-951A-B368AD71ADBA.jpeg
 
Back
Top Bottom