Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,505
- 51,110
WAKILI MWABUKUSI ANATAKA MKUU WA MAJESHI AZUIE UVUNJIFU WA KATIBA.
"Nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba. Kazi ya kukamata wa halifu ni ya Jeshi la Polisi. Jeshi la wananchi halina mamlaka kisheria na kikatiba kuingia kufanya msako mitaani kwa kisingizio cha kutafuta sare zao. Jukumu lao ni kulinda mipaka ya nchi. Cha ajabu hawajatuambia walizipeleka lini huko mitaani au zilichukuliwa na nani au waliibiwa lini? This is more than a comic [Huu ni usanii]!
Mwanajeshi hana mamlaka ya kupekua mtu katika makazi yake au maungo ya raia. Hii ni kazi ya Polisi wetu. Isipokuwa pale kunapokuwa na hali ya hatari au tishio dhahiri la mapinduzi.
Sheria inaruhusu kukataa ukamataji haramu na iwapo jeshi litaingia kwa namna hii ni haki ya wananchi kukataa ukamataji au upekuzi haramu usiofuata sheria ikiwemo kumshtaki Mwanasheria mkuu na Mkuu wa Majeshi ili kulinda sheria na Katiba ya Nchi na kudai fidia ya usumbufu.
Kama jeshi limeibiwa sare zake likaripoti Polisi. Polisi wafanye uchunguzi na wakibaini kosa Polisi ndiyo wenye utaalamu wa kupeleleza uhalifu wa wizi. Jeshi au wanajeshi hawako juu ya sheria [hivyo] wapunguze mihemko.
Kumekuwa na ujasiri wa uvunjaji katiba na sheria na kuwatisha wananchi katika taifa letu katika uongozi huu wa sasa na kwa hili hatutakubali na tutalitolea tamko rasmi kupinga vurugu hizi katika utumishi wa umma.
Mkuu wa Majeshi awajibike haraka kuzuia ukora huu wanaotaka au kupanga kuufanya!
Najisikia aibu sana kuishi na kushuhudia viroja hivi. Mungu bariki Watanganyika! Mungu ibariki Tanzania! Mungu waadhibu na kuwakemea madhalimu wote.
Boniface Kajunjumele Mwabukusi!