Maudhui ya jumla na athari za sheria mpya ya TISS

MWANDAMBO

Member
Feb 2, 2011
19
17
IMG_20230105_170439.jpg
IMG_20230105_170439.jpg

Sheria ya Usalama wa Taifa (TISS) iliyopitishwa na Bunge la Tanzania.


1. Sheria hii imewapa Kinga (Immunity) maafisa wa Usalama wa Taifa dhidi ya makosa ya Jinai kutokana na majukumu yao. Masharti haya mapya ni tofauti na masharti ya sheria hii kabla ya mabadiliko haya, ambapo maafisa wa Usalama wa Taifa hawakuwa na kinga dhidi ya makosa ya Jinai na walikuwa na kinga kwenye eneo la makosa ya Madai pekee. Maana yake ni kwamba, hata kama afisa wa Usalama wa Taifa akiua katika majukumu yake kimakosa, hatowajibika kwa mujibu wa sheria hii na hali hii itaongeza hamasa ya wao kukiuka sheria na kuhatarisha maisha ya watu kwenye jamii.

2. Sheria hii inakiuka msingi wa kikatiba wa Katiba yetu ya Tanzania (1977) ambao unatutaka Raia wote nchi hii kuwa sawa chini ya sheria au watu wote kuwa sawa mbele ya sheria. Lakini sheria hii inatengeneza matabaka ya watu wenye kinga ya haki na sio na kinga ya haki pia, imewabagua baadhi ya watendaji wa serikali kwenye masuala ya haki. Kundi hili la maafisa wa Usalama wa Taifa ambao sasa wana Kinga dhidi ya Jinai, lina ongeza idadi ya watu ambao wana Kinga dhidi ya Jinai kisheria nchini, AKIWEMO Waziri Mkuu, Spika wa Bunge kama tunavyofahamu kutokana na maboresho ya sheria zilizopo.

3. Sheria hii imewapa Maafisa wa Usalama wa Taifa haki, mamlaka ya Kipolisi ya ukamataji. Hapo kabla kwa mujibu wa sheria hii kabla ya mabadiliko haya, Afisa wa Usalama wa Taifa hakuwa na haki ya kisheria ya kukamata mtu. Mamlaka hayo yaliachwa kwa Polisi pekee au pengine kwa maelekezo ya vyombo vingine vya kisheria kama Mahakama lkn bado utekelezaji wake ulipaswa kufanywa na Polisi pekee. Hatari ya jambo hilo ni kwamba, maafisa wa Usalama wa Taifa na ambao kwa mujibu wa sheria hii mpya ambapo wameongezewa kinga juu ya usiri wao (kutokujulikana) wakikukamata hakuna pahala Pa kwenda kukutafutia na kwasababu hawajulikani na Haijulikani watakupeleka wapi. Tunaweza kushuhudia kupotea kwa watu au mauwaji holelaholela kutokana na mamlaka haya mapya ya Kipolisi.

4. Sheria hii mpya imempa mamlaka na Haki Rais wa nchi kujua Mipango, mienendo ya wagombea wa Urais wa vyama vingine pamoja na kudhibiti usalama wao au ni kusema kwamba, usalama wa wagombea wa Upinzani uko rehani na mikononi mwa Mgombea mwingine wa Urais. Jambo hili ni hatari kutokana na historia ya siasa ya nchi yetu, Utamaduni wa vyombo vyetu vya dola vinqvyotumika kuhatarisha maisha ya wapinzani na wakosoaji ikiwemo matishio na kesi za kubambikiwa na kubwa zaidi, Rais anaweza kuwa Mgombea wa uchaguzi husika au akawa anatoka kwenye chama Tawala na hivyo kuhatarisha usalama wa wagombea wengine wa upinzani.

5. Sheria hii mpya ya TISS inamfanya Rais wa nchi kuwa kiongozi wa kijeshi. Anaweza kufanya au kuendesha nchi kijeshi (Millitary Orders) na kusababisha hatari kubwa ya kuminywa kwa demokrasia na Utawala wa sheria na zingatia kwamba yeye pia ana kinga dhidi ya jinai.

KWANINI TUNAPASWA KUHOFIA NA KUPINGA MABADILIKO HAYA.

1. Rais wa nchi ambae alitangaza mchakato wa maridhiano wa Kitaifa na kuchukua hatua kadhaa zenye sura ya mwelekeo wa kurejesha utengamano na kuaminina Kitaifa, anakwenda kinyume na mahubiri yake. Anacho hubiri sicho anachokitenda. Ushahidi ni utungaji wa Sheria hii na kuepelekea Bungeni kwa Hati ya dharula, sheria ambayo linakwenda kinyume na dhamira ya utengamano na Kuimarisha misingi ya demokrasia na kinyume chake ameendelea kupoteza muda kwenye mchakato wa Kupatikana Katiba Mpya.

2. Rais ameendelea kuteua (Watu) wakuu kwenye maeneo nyeti ya Serikali na yanayogusa maslahi mapana ya umma au maeneo ambayo yalitumika kusababisha madhila kwa makundi mengi kwenye jamii na yaliofanyika kwenye awamu iliyopita na hata ktk awamu hii yake ya sasa, watu hao ambao walikuwa sehemu ya madhila makubwa dhidi ya makundi mengine (Wahanga) kwenye jamii. Kitendo hicho kinatoa tafsiri kwamba, Rais Hana nia ya kujenga mshikamano wa kitaifa au kuleta mageuzi makubwa ya kisiasa bila ubaguzi. Kuwateau wahalifu ni kupuuza na kutukana madai ya waathirika.

3. Rais wa nchi, amesema kwamba ameunda Tume ya Haki jinai, tume ya mabadiliko ya Sheria kandamizi, pamoja na kwamba Miongoni mwa walioteuliwa kwenye Tume hiyo ni sehemu ya wahalifu, watuhumiwa wa ughandamizaji, lakini kubwa ni kwamba, Rais ameendelea kutunga sheria kandamizi hata kabla ya kazi ya msingi ya maridhiano kufanyika ikiwemo utungaji wa Sheria hii mpya ya Usalama wa Taifa.

4. Rais na chama chake wameridhia mchakato wa Kupatikana kwa Katiba Mpya, lakini matendo yake ni kinyume na dhamira hii, kwasababu utengenezaji wa sheria ya Usalama wa Taifa kama nilivyoielezea hapo Juu, haukupaswa kuwa wa kwanza tena kwa hati ya dharula kabla ya Katiba Mpya, Kwasababu katiba Mpya inaweza kutoa mfumo mpya wa sheria ya Usalama wa Taifa ambao unaweza kuwa tofauti kabisa na sheria hii pendekezwa na Bunge ya sasa. Kitendo hicho ni wazi kwamba Rais Hana nia ya kupatikana kwa Katiba Mpya na dhamira kamili ni kujipatia mamlaka ya udhibiti wa siasa za nchi hii, upinzani na ukosoaji hususani nyakati za uchaguzi Mkuu na kipekee sana kudhibiti ukosoaji dhidi ya Ufisadi na uhalifu wa serikali na maafisa wake dhidi ya umma.

5. Rushwa na Ufisadi.
Ni wazi kwamba, Rais ametunga sheria hii kuweka msingi wa ulinzi wa Rushwa na Ufisadi mkubwa ambao tayari umeanza kuhushuhudia, kwenye biashara ya mkataba wa uuzwajibwa Bandari za Tanganyika, uuzwajibwa wa Hifadhi za Ngorongoro. Rais anahitaji sauti za umma dhidi ya Mikataba mbovu, dili za Rushwa na Ufisadi kunyamazishwa bila upinzani wowote ule na sheria ya Usalama wa Taifa ndio silaha sahihi ktk hilo. Rais analinda Ufisadi.

Anderson Ndambo
andambo@yahoo.com
 
Kwa hiyo tuna majeshi,magereza,jkt,JWTZ,polisi na jeshi la watu wasiojulikana( JWW)
 
Back
Top Bottom