Muswada wa Sheria ya Usalama wa Taifa hauzingatii hatari ya kuwapa watu wengi wasioweza kusimamiwa kinga dhidi ya makosa jinai

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Kilicho fanyika kinyamela hivi karibuni kinahusu bunge la Tanzania kupitisha muswaada utakao wafanya watumishi wa idara ya usalama wa taifa wasi shitakiwe kwa kosa lolote la jinai. Muswaada huu ulipitishwa kwa malengo ya kuwalinda watumishi hawa katika shughuli zao za kila siku ambazo wanaweza kuhusika na makosa ya jinai.

Lakini je, makosa ya jinai yana jumuisha nini na nini haswa huonekana kama kosa kwenye jamii yetu?. Sheria siku zote huandaliwa kulinda maadili ya jamii fulani na mara nyingi huendana na kinacho onekana kuwa sawa hata kwa Mwenyezi Mungu. Huwezi kusema kwamba una mlinda mtu ambaye amekusudia kumuua au kumuibia binadamu mwenzake bila sababu ya msingi.

Tuseme kwamba neno "Jinai" linahusisha mambo mengi sana. Sheria hii ingetakiwa ichambuliwe na kina zaidi na maandishi yote ya sheria hii yawe sehemu ya mabadiliko haya. Uchambuzi huu utawezesha vyombo vya kulinda usalama wa raia kufahamu mipaka ya idara ya ya usalama wa taifa.

Kwasababu ya haya kufanyika, mwongozo huu unaweza kutumika vibaya kwa malengo ya kuwa nufaisha watu fulani. Ili sheria hii iwe na mantiki, inabidi ielezee kwa undani zaidi kuhusu makosa ya jinai ambayo idara ya usalama wa taifa imepewa kinga na shughuli zenye tija zinazoweza kuwafanya wafanye makosa haya ya jinai.

Vyombo vya kulinda usalama na mali za watu kama idara ya polisi vingetakiwa kuhusishwa na kutoa tafsiri ya sheria hii kabla ya kupitishwa bungeni.

Tutambue kwamba, tuna utaratibu wa jinsi ya kuwaadhibu wanao vunja sheria za jinai. utaratibu huu upo kwenye mkusanyiko wa sheria unaoitwa "Penal code". Sheria hii, imekiuka mwongozo uliopo kwenye penal code na kwasababu hiyo inaweza ikawa "Unconstitutional". Sheria kama hizi, zingetakiwa kupitiwa na jopo la mahakimu kabla ya kujadiliwa bungeni kwasababu wabunge wetu hawana utaalam wowote wa kuchambua sheria nyeti kama hizi.

Ningependa kuona idara ya usalama wa taifa inafanya kazi kwa weledi bila kuhitaji sheria gandamizi kwa watanzania kama hizi. Natumai Rais Samia ataliangalia hili kwa jicho lingine kabla ya kutia sahihi muswaada huu na kuufanya uwe sheria. Nguvu ya mahakama siku zote ndio mkombozi katika suala zima la kuhakikisha kwamba idara zote zinafanya kazi kwa uadilifu na kwa madhumuni ya kutenda mema bila usimamizi.


 
Alafu badae wakitoka madarakani Sheria ikianza kuwaumiza wao ama watotowao sijui watasemaje.
 
Alafu inampa mwajiriwa kukufanya lolote hata kama kukukata panga bila kustakiwa yeye akijibu tuu 'nilikuwa kazini 'hana kesi hapo sheria imemlinda kufanya lolote
 
Back
Top Bottom