View attachment 1761867

UkiZoom kwenye hiyo Picha utaona madhara ya Tufani kwenye maeneo ya Pwani Tufani hiyo ilikuwa inaitwa Haiyaan ilipiga Philipines na kuuwa watu Maelfu

View attachment 1761868
Kimbunga kiko wapi mkuu,maana ulishabikia sana mpaka ukatuletea picha za some hurricane battered places.Una roho mbaya sana aisee,dah!Yaani ninyi watu hamuitakii mema nchi yetu kabisa,ila Mungu tunayemuamini ataendelea kututetea tu.Sijui nchi yetu ikiharibika wewe utaishi wapi.
 
Ilikuwa ni kutahadharishana au pia ni kosa
Mkuu
hatu-tahadharishi hivyo.Hivi unajua subliminal message iliyokuwa sent kwa watu as a result of your message:this is how you will be battered by cyclone Jobo!Sasa nikuambie nikuambie nini, this is how the devil works:kuleta hofu na kukatisha watu tamaa and without hope people perish.Hivi vitu viwili vinaleta pia magonjwa sana,and that is what the devil wants.Sasa wewe ni mtumishi wa Shetani?Kama.ndio tuambiane!
 
Kikawaida cyclones huwa hazikimbilii towards the equator. Zikifanya hivyo huwa zinakosa nguvu na kutawanyika. Kwa maana hiyo hatari kubwa kwa hii Cyclone ya Jobo ni Lindi na Mtwara (9 degrees S) na sio Dar (6 degrees S).

Ndiyo maana cyclones nyingi zinazoanzia bahari ya Hindi huwa zina gain southwards na kuishia Madagascar au Mozambique. Hii ya ku gain northwards towards the equator kwa kweli ni ajabu

Kikawaida ni vigumu kutokea cyclone/hurricane/typhoon 5 - 7 degrees South or North of the Equator sababu kuna Coriolis Effect ndogo. Dar ni 6 degrees South of Equator kwa hiyo ideally cyclone itadhoofishwa na kutawanyika inapokaribia Dar. Ndiyo maana Lindi na Mtwara (9 degrees S) makes more sense.

Huku kwetu kwenye Southern hemisphere cyclones zote huwa zinaenda clockwise, hata vimbunga n.k......kwenye Northern hemisphere huwa ni anti-clockwise. Sasa tunapo approach Equator huwa hii phenomenon inapungua na tunapoenda mbali na equator inaongezeka....na kwenye equator yenyewe hakuna hii effect......cyclones huwa hazikimbilii equator. Kwa mfano unaweza kufanya practical kidogo.....tukijaza sink maji tukiyafungulia yatazunguka clockwise sababu tupo Southern hemisphere ila kwa wenzetu waliopo northern hemisphere (mfano Uingereza) itakua anti-clockwise....na waliopo equator mfano Kenya au Uganda yataanguka tu straight down! Ndiyo maana inavyosemwa kitaenda northwards hapo ni ajabu sana.

Kinadharia....the worst that can happen kwa Dar ni mvua tu tena kwa kiasi chake. Kitakutana na mengi ya kukiresolve njiani mpaka kifike Dar. Imesahaulika tu kukumbushia oceanic currents,......maana kikiwa njiani kwa upande uliosemwa kutokea kitakutana na Mozambican current hivyo kitapunguzwa nguvu sana.

Vurugu inaweza kuwa kusini hasa Mafia, Rufiji na kwenda Lindi na Mtwara. Dar si rahisi....kikija northwards kuanzia (Dar) na kuendelea maeneo mengine northwards kweli kitakua kimefanya Job kama wanavyokiita Jobo 😅
 

Attachments

  • VID-20210425-WA0031.mp4
    11.5 MB
Back
Top Bottom