Lindi na Mtwara zatahadharishwa kimbunga cha Jobo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imetahadharisha mikoa ya mwambao wa Bahari ya Hindi hasa mikoa ya Lindi na Mtwara kuhusu kimbunga cha Jobo ambacho kipo kaskazini mwa Madagascar

Kimbunga kitasababisha ongezeko la upepo na mawimbi katika bahari ya Hindi. TMA wanaendelea kufuatilia kuangalia uelekeo wa kimbunga hicho

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari ya upepo na mawimbi iliyotolewa na TMA.

1619027526290.png
 
TMA hawa hawa waliwapomza jamaa wa jangwani la taarifa zao
 
Kwa mtwara lazima wachukue tahadhari kwa mvua km hizi za Dar Mtwara ni mafuriko tayari.
 
Kimbunga Jobo kinaelekea Tanzania, ni cha aina yake tokea 1952​

Apr 22, 2021 11:22 UTC
  • Kimbunga Jobo kinaelekea Tanzania, ni cha aina yake tokea 1952
Kimbunga kikali zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Tanzania miongo ya karibuni kinatazamiwa kutua katika ukanda wa pwani ukiwemo mji wa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa, kimbunga hicho ambacho kinajulikana kama Jobo kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutua Tanzania tangu mwaka 1952.

Kwa mujibu wa taarifa, jana kimbunga hicho kilionekana kaskazini mwa Madagascar kikiwa na kasi ya kilomita 83 kwa saa.
Utabiri unaonyesha kuwa kimbunga hicho kitapita eneo la Ushelisheli leo Aprili 22 kikiwa na kasi ya kilomita 130 kwa saa na kinatazamiwa kutua Tanzania Aprili 24 au 25.

4bsgd8175e8fb51epmq_800C450.jpg
Upepo mkali wakati wa kimbunga Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadahrisha kuwa kimbunge hicho cha Bahari ya Hindi kinaweza kusababisha upepo mkali na mawimbi makubwa baharini katika maeneo ya Lindi na Mtwara. Aidha kuna uwezekano wa kutokea mafuriko katika maeneo athirika.

TMA imesema itaendelea kufuatilia kimbunga Jobo na kuwapasha wananchi habari kuhusu tahadhari zinazopasa kuchukuliwa.
 
wenzetu wanakuwaga na vimbunga vina majina romantic kabisa mfano catrina ila sisi eti JOBO jamaan JOBO kweli this is unfair
 
Back
Top Bottom