TMA yatoa Tahadhari ya kutokea Upepo Mkali kuanzia Agosti 2, 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
1690871782922.png

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa utabiri unaoonesha kuna uwezekano wa kutokea Upepo mkali na Mawimbi makubwa kwa siku tatu mfululizo.

TMA imesema Uppeo huo utavuma kwa kasi ya Kilomita 40 na zaidi kwa saa na Mawimbi yanayofikia ukubwa wa Mita 2 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani na maeno ya Zanzibar.

Mikoa mingine ni maeneo ya Ziwa Viktoria ikiwemo Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Mara na maeneo ya ukanda wa ziwa Tanganyika ikiwemo mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa.

=============

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa kwa siku tatu ambapo utabiri umeonyesha kuna uwezekano wa kutokea upepo mkali na mawimbi makubwa.

Taarifa iliyotolewa na TMA inaonyesha kuwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumatano hadi Ijumaa kutakuwa na upepo mkali unaofikia kilomita 40 na zaidi kwa saa na mawimbi yanayofikia ukubwa wa mita 2.

Hali hii inatarajiwa kutokea katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi ikihusisha mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mikoa mingine ambayo inaweza kukumbwa na hali hii ya hewa ni maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria ikihusisha mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Mara na maeneo ya ukanda wa ziwa Tanganyika katika mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa.

Kufuatia hilo TMA imetaka tahadhari kuchukuliwa hasa kwa wanaofanya shughuli zao baharini na ziwani wakiwemo wanaotumia njia hizo kusafiri.

MWANANCHI
 
View attachment 2704557

Haya sasa wale wa msimbazi,mabondeni na milimani kazi kwenu sasa msije kusema kuwa hatujawaambia
 
Back
Top Bottom