Kikwete adai tatizo ni ujamaa!

Kikwete adai tatizo ni ujamaa!

........U only have one choice to choose from - JK, Mbowe, Lipumba, Mrema ambao wote ni maarufu ndani ya chama na sii ktk utendaji kazi wao..Kifupi wananchi hawana choice a viongozi bali wanapitisha moja kati ya majina waliyoletewa..
Mkuu kuna mfano mmoja MMD Zambia....Chiluba alimwangusha Kaunda wa UNIP.....Angalia baadae naye alifanya nini.

Mimi naamini na naomba mnisamehe TZ tunahitaji mtu kama Kagame ambaye ni dikteta na aupige fimbo na kutunyoosha kwa muda wa miaka mitano

Kweli sasa hivi sioni mtu ambaye ni patriotic kama Nyerere wa kutunyosha na kutuweka sawa......maana uwozo umeshamiri mizizi mpaka chini ngazi ya chini.
 
Kufilisi na ufisadi Mkuu ni vitu viwili tofauti. Narudia tena wakati wa Mwalimu hatukuwahi kabisa kusikia madudu kama haya ya kifisadi. Kwa hiyo kutaka kuyahusisha haya madudu mbali mbali ya ufisadi na Mwalimu Nyerere ni kumtomtenda haki Mwalimu kabisa. Alikuwa na mapungufu yake na ndio kuna watu waliovurunda katika mashirika mbali mbali ya umma lakini kuvurunda huko huwezi kulinganisha na wizi uliopo sasa kama ule uliofanywa na Mkapa wa kuiba Kiwira, kama ule ulifanywa wa kulazimisha kununua rada (Watanzania hata majani tutakula lakini lazima rada inunuliwe) kumbe walikuwa tayari wameshachora mchoro wao wa mabilioni, kutudangaya kwamba kampuni ya Houston, Texas inakuja kufua umeme kumbe ni wizi mtupu na sasa wanatakiwa kulipwa $94 million, kuingia kwa RITES mikono mitupu na sasa wanastahili kulipwa $87 million eti kwa kuvunja mkataba!

Sijui Nyerere alikukosea nini Mkuu hata kutaka kumuhusisha na mabaya yote nchi mwetu hata baada ya kung'atuka madarakani miaka 26 iliyopita.
Sinauhakika kama tunaelewana mkuu, na sina uhakika kama unaelewa maana ya neno UFISADI.

Ufisadi ni ufisadi tu (kama unaelewa maana yake), kinacho tofautisha ni zama na jinsi ya kufisadisha nchi tu, basi.

Tushukuru tu sasa atleast tunaweza kunyanyua vichwa na kufungua midomo yetu very wide, tukazungumza na mengine kuyasoma kwenye vyombo mbali mbali vya habari.
 
Sinauhakika kama tunaelewana mkuu, na sina uhakika kama unaelewa maana ya neno UFISADI.

Ufisadi ni ufisadi tu (kama unaelewa maana yake), kinacho tofautisha ni zama na jinsi ya kufisadisha nchi tu, basi.

Tushukuru tu sasa atleast tunaweza kunyanyua vichwa na kufungua midomo yetu very wide, tukazungumza na mengine kuyasoma kwenye vyombo mbali mbali vya habari.

Haya Mkuu mimi nilidhani utatoa mifano miwili mitatu ya ufisadi wa wale ambao waliokuwa madarakani wakati wa awamu ya Mwalimu waliotajirika na hatimaye kuwa matajiri wa hali ya juu (mabilionea). Usiku Mwema Mkuu.

 
Haya Mkuu mimi nilidhani utatoa mifano miwili mitatu ya ufisadi wa wale ambao waliokuwa madarakani wakati wa awamu ya Mwalimu waliotajirika na hatimaye kuwa matajiri wa hali ya juu (mabilionea). Usiku Mwema Mkuu.

Sawa mkuu, usiku mwema pia, ila natamani nchi ya Tanzania, viongozi wote, ninaposema wote namaanisha wooooooote, wawe toka chama tawala au vyama vya upinzani, yaani wote tuwapige chini, tuanze upya. Au nchi ichukuliwe na jeshi, tujuwe moja.
 
Sawa mkuu, usiku mwema pia, ila natamani nchi ya Tanzania, viongozi wote, ninaposema wote namaanisha wooooooote, wawe toka chama tawala au vyama vya upinzani, yaani wote tuwapige chini, tuanze upya. Au nchi ichukuliwe na jeshi, tujuwe moja.

Hii ya kuikabidhi nchi kwa jeshi mimi siiafiki Mkuu maana hao nao wakilewa madaraka hung'ang'ania kwa kipindi kirefu. Naamini kabisa tunaweza kupata viongozi wazuri katika vyama vilivyopo hasa CDM (mie si mwanachama kule labda siku za usoni) ambao wanaweza kabisa kuingia madarakani kupambana na mafisadi na kuhakikisha ufisadi unaangamizwa nchini mwetu na pia kuweza kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania na hatimaye kuleta maendeleo ya kweli ambayo yatawanufaisha Watanzania walio wengi.
 
Hii ya kuikabidhi nchi kwa jeshi mimi siiafiki Mkuu maana hao nao wakilewa madaraka hung'ang'ania kwa kipindi kirefu. Naamini kabisa tunaweza kupata viongozi wazuri katika vyama vilivyopo hasa CDM (mie si mwanachama kule labda siku za usoni) ambao wanaweza kabisa kuingia madarakani kupambana na mafisadi na kuhakikisha ufisadi unaangamizwa nchini mwetu na pia kuweza kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania na hatimaye kuleta maendeleo ya kweli ambayo yatawanufaisha Watanzania walio wengi.
Mtazamo wangu kaka ni kuwa vyama vyote hivyo, vina chembe chembe ile ile ye kutoka chama tawala, kila kiongozi ukimgusa, aliwahi kuwepo uko uko, aidha alitemwa au aliona hana maslahi, akaamua kugura chama. Labda tuchaguwe vijana waliozaliwa miaka ya 90's. Na kama mmoja wa wazazi wake walikuwa madarakani, naye atupishe.
 
Nakubaliana na point ya fikra za Ujamaa zinaimaliza TZ. Ubaguzi wa Kidini also ni major factor inayoimaliza TZ. Wawekazaji kutoka nchi za Kiarabu (Waislamu) wanaonekana kama ndiyo wezi zaidi kuliko Wazungu. Fikra za Nyerere za Ujamaa bado zinatawala miongoni mwa waTZ.
 
Hata hivyo vyama mbadala vmeshindwa kabisa kuja na sera mbadala za kulikomboa taifa kutoka kwenye umaskini.

Hii ni evidence kwamba viongozi dhaifu ni zao la wananchi, taifa dhaifu, lenye siasa lakini halina ideology.

Maneno mengi utekelezaji sifuri.



wananchi dhaifu ndio wanakuwa na nidhamu ya woga.

HIvi udhaifu wa watanzania ulianzia lini? au umesababishwa na nini?
Kwa sehemu kubwa serikali ni ya kulaumiwa kwa kukosa mipango endelevu ya kuwawezesha wananchi wajitambue na waanze kuwajibika..
 
Kiranga,
Mimi nilimsikia ITV. Napata ITV kupitia Tv4africa.com. Ni kweli aliyasema hayo. Lakini hilo tisa. Nijuavyo mimi, hayo ndiyo maoni sahihi ya Kikwete ambayo huyasema privately au miongoni mwa marafiki zake. Hana hata moja la kumsifia Nyerere. They are trying so hard to kill his legacy lakini naamini historia itawaumbua.

Sawa, tatizo ni ujamaa. Sasa wewe kama rais na mwenyekiti wa chama tawala, unafanya nini kuondoa tatizo?
 
Sawa, tatizo ni ujamaa. Sasa wewe kama rais na mwenyekiti wa chama tawala, unafanya nini kuondoa tatizo?
That is the question. The time to blame is usually very short. Then it is time to show leadership. You cannot claim, after 6 years in power, that the problem is policies that were killed more than 20 years now.
 
Kama watanzania sio wadhaifu watachaguaje viongozi dhaifu? unataka kuniambia viongozi dhaifu wanatoka mbinguni?

Viongozi ni miongoni mwananchi. Kama wananchi ni dhaifu lazima viongozi watakaopatikana ni dhaifu.
Viongozi ni miongoni mwa wananchi nani kasema?Utawala una tabaka.Kuna tabaka la watawala ambalo linaishi dunia yao wenyewe usijidai hujui.Viongozi dhaifu wanatoka kwenye hilo tabaka na si huko mbinguni unakouliza kama wanatoka.
 
Kwa mara ya kwanza ukweli umesemwa. Ujamaa ni adui wa maendeleo.

Mimi nawashangaa sanasana watanzania kukumbatia siasa isyo na kichwa wala miguu. Nyerere aliulizwa kuhusu siasa zake akasema hivi, ujamaa wa Tanzania ni aina ya "African Socialism". Mimi nataka kuwauliza, tangu lini mlisikia kuna siasa inaitwa African Socialism. Huu wazimu aina gani jamani?

Mnatudhalilisha na siasa zisizo miguu wala kichwa. Ajabu ya Nyerere utashangaa. Na sisi wazanzibari tuliwakataa na siasa hizi. Na ndio maana hatujaukubali muungano mpaka leo mambo yamekuwa moto moto. Siasa za ujamaa wa Nyerere ndio umeirudisha nyuma Tanzania kiasi yakuwa inatajika duniani kwa umasikini. Balaa tupu.

UJAMAA WA NYERERE NI ADUI WA MAENDELEO YA TAIFA.
 
..kwa kweli inachanganya mwenyekiti wa chama kinachofuata itikadi ya UJAMAA na KuJITEGEMEA anapotoa kauli kama hizi.

..hivi inawezekana tukawa na chama tawala cha kijamaa lakini serikali yake ikawa ya kibepari?

Du! Hilo lichama kila siku kujichanganya si juzi tu katibu mpya wa ccm amesema wanajivunia itikadi ya chama chao "UJAMAA NA KUJITEGEMEA" ambayo chadema haina?

Source bonyeza hapa
 
Ujamaa upi anaouongelea? Huo ujamaa ambao mimi mwenye miaka 20+ nausikia kwamba ulikuwepo hapa Tz? Nani anataka kuniambia babu yake na mapacha watatu wana ujamaa? Nani kasema mimi mvaa kandambili ya kulubasi (tairi ya gari) iliyotoboka na waziri anaetembelea gari ya mil200 ni wajamaa? Kama tungekuwa wajamaa nani angeingia mkataba na Richmond?

ACHENI KUMTAFUTIA LAWAMA Mwl J.K
 
Sina uhakika kama kasema hayo kwa kuwa source hakuleta conclusive events kuhalalisha mada yake,anyway kasema hakusema, SI SAHIHI kwa Mwanachama au kiongozi yoyote wa CCM kusema tatizo ni UJAMAA. Please kama haya maneno yametoka mdomo mwa mwanaccm No ni HATARI tena kupita HATARI.

ITIKADI YA CHAMA CHA MAPINDUZI ni "UJAMAA NA KUJITEGEMEA"mimi binafsi kama Dotcom Generation sina tatizo na ITIKADI hii au mlengo ambao mwasisi wa Taifa na BABA WA TAIFA aliuanzisha kwa kuzingatia HISTORIA YA YETU WAAFRICA na UTAMADUNI WETU wa kuishi pamoja kama JAMII.

Yeye Mwalimu kama kinara wa ITIKADI hiyo alitumia elimu yake kuunda mfumo wa kuishi wa aina yake [Unique] na aliona waafrika hapo kale waliishi kama jamii moja na mpaka sasa tuna maisha ya kijamaa kuanzia hadhi ya familia [Extended Family] mpaka hadhi kitaifa [Makabila].Leo hii Mhaya anaoa Mkurya, Mpare anao Mhangaza, Mchaga anaoa Mgogo, Mngoni anaolewa na Mmasai,kutoka hapo tunataifa la WATANZANIA ambao lugha ya mama ni KISWAHILI.

DOT COM GENERATION
: Ni kizazi cha Mchanganyiko wa makabila], ndio ujamaa wenyewe, ndio mazao ya mfumo huo ambao mwalimu aliusimamia kwa kuzingatia historia. Kwa kuona hilo pia Mwalimu akaongeza KUJITEGEMEA. Kujitegemea huku Mwalimu alitizama Mtanzania ataishi ndani ya jamii yake kama mwanajamaa lakini ataendesha maisha yake kwa kujitegemea huku akipata ushirikiano wa wana jamii yake.

Sikuzaliwa wakati Mwalimu anaanzisha mwelekeo wa Taifa hili, lakini nilimwelewa kupitia elimu ya Historia na sauti ya kulekodiwa [Recorded Speech] ambazo zimejaa ukweli wa maisha kwa kuzingatia ukweli sahihi wa UTU NA HESHIMA YA MWANADAMU.

Nina imani Mwalimu JK Nyerere si kuwa akuwa mdadisi wa mfumo wa KIBEPARI [CAPITALIST] kwa maana ya kuutumikia lakini katika namna inayozingatia mazingira ya kiafrika na sio kwa kukopi kama ulivyo toka ulaya na kuutumikisha kwenye mazingira ya Kiafrika yenye utamaduni na Jadi tofauti na Ulaya. Nafikiri mpaka kifo alichokua anatafuta ni jinsi gani awaelimishe watanzania waweze kuishi katika mfumo wa kujitegemea [Find your own bread una tofauti gani na Ubepari hapa katika njia ya Kiafrika].

Mwalimu JK Nyerere alizingati historia na utamaduni wa Kiafrika, Leo hii viongozi wengi wa Chama na Serikali wanaishi na Mama ama Baba zao majumbani mwao wakiwalea yote hiyo ni kwa sababu ndio jamii ya Kitanzania inavyotakiwa kuishi [Extended Family].[Kwa kukopi Ubepari wanaoukumbatia si wangewapeleka wazazi wao nyumba za kulea wakongwe kama mfumo wa Kibepari unavyojiendesha?]

Hatuitaji kukopi na kutumikisha mfumo wa kibepari [Copy and Paste] tunaitaji kubuni aina ya mfumo huo lakini unaozingatia HAKI na USAWA na mazingira yetu halisi kama Watanzania na Waafika,kama ni mechi ya mpira tunasema Fair Play Game. Kwa kuwa CCM ndio UJAMAA ndio ITIKADI YAKE basi inaangalia HAKI NA UTU WA MWANADAMU vivyo hivyo Serikali inayoundwa na chama hicho,na kuakikisha mlengo huo haupotezi maana bali unazingaia NYAKATI NA ZAMA.Hata leo hii ndoa ya mtoto wa Kifalme Prince Williams ni ya kifalme sawa kihadhi kabisa na ya Baba yake ama Babu yake lakini katika taswira na vionjo vya kisasa kwa kuangalia nyakati na zama za kizazi chake. [Theme ya kizazi chake]. Kama leo hii Morning BBC wanaendelea na Ku-document Royal wedding waingereza na jeuri yao ya kujali chao wamechanganya vionjo vya muziki kwa kudocument vionjo vya wimbo " I WANNA BE A MILLIONARE SO F................BAD NEXT QUEENE and OPRAL", NA Kionjo cha "ITS NOT ABOUT THE MONEY.

CCM KIMEKOSEKANA NINI KWA CHAMA CHA MAPINDUZI NA SERIKALI YAKE? Kuendeleza ITIKADI YAKE YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA KWA KUZINGATIA NYAKATI NA ZAMA MPYA.


Napata shida kuona wafuasi wa Mwalimu alioafundisha awafuati maelekezo yake na wameitupa ITIKADI ya CHAMA CHA MAPINDUZI. Leo hii Dot Com Generation, wanavyomwelewa na kukubali maelekezo yake, wazee hawa [TYPEWRITER GENERATION] wanajisikiaje kuona watoto na wajukuu zao wakiimba ''Kama sio juhudi zako Nyerere na nanii....................angesoma wapi? Kumbe Dotcom Generation wanajua ni bidii binafsi za mawazo ya Mwalimu kujenga Taifa lenye jukumu la kujenga UJAMAA kwa kutambua JAMII inajukumu la Kulea,Kusomesha, Kujali na kutambua jamii yatakiwa kuishi kwa kujaliana na kuheshimu binadamu mwingine hata kama kuna tofauti ya vipato.

Leo hii omba omba mitaani,serikali ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA kumilki ombaomba mpaka wa umri wa miaka minne [4] ni HATARI ZAIDI YA HATARI. Kwani kwa ITIKADI YA UJAMAA ,omba omba ni jukumu la Serikali [Basi tungekopi kwa mabepari tungesema state property] vyote hivyo hatupo.

Mwalimu ansasema unapokua unataka Uraisi ni kutaka Matatizo sio Neema,"Ikulu kuna nini?Ikulu ni Mzigo wa Matatizo,Unapita Mabarabarani huko Wananchi wako wanashida, shida za wananchi hao ni mzigo wako wewe".

Kwa mantiki hiyo kama KWELI Viongozi wa CCM ndani ya mioyo yao dhamila yao si kuendeleza TAIFA LA UJAMAA lenye mfumo wenye kuzingatia mazingira halisi ya Mtanzania wa leo na nyakati alizopita na zinazokuja, basi KWELI NITAANZA KUAMINI JAPO, NILIKUA SIAMINI KIFO CHA CCM [RISE AND FALL PRINCIPLE ILISHAANZA KUFANYA KAZI ZAMANI NA INAKARIBIA MWISHO NAFIKIRI]
 
unataka kusema TRA hawalipwi vizuri? EWURA? ATC?

Uongozi dhaifu unatokana na kuwa na taifa lenye watu dhaifu. Kama wananchi dhaifu unadhani viongozi madhubuti wanatoka sayari Jupiter au Gambia? Lazima watoke kwenye jamii hiyo hiyo.


aha ha haa! FA zamani nilihubiri sana swala la udhaifu wa raia kuwa ndio unasababisha udhaifu wa viongozi, ni dhana au falsafa ngumu kueleweka. Ndio maana nimekuwa nikililia sana dhana hii ieleweke. Huwezi ukamfuga mkurugenzi fisadi, kesho anapata ubunge na kuwa waziri ghafla anakuwa mtakatifu..atauendelea ufisadi tena kwa hali ya juu kwa sababu ndio tabia yake!

Tuna TAIFA DHAIFU KWA SABABU TUNA INSTITUTION DHAIFU( say makanisa na misikitini) Tuna INSTITUTION DHAIFU KWA SABABU TUNA FAMILIA DHAIFU, TUNA FAMILIA DHAIFU KWA SABABU TUNA AKINA BABA DHAIFU!! period
 
Hapa Kikwete kwa mara ya kwanza kaongea point yenye akili sana. wachangiaji wa mwanzo hili lililosemwa na kikwete lina ukweli midingi maofisini humo wakiritimba hata kwa wawekezaji wa ndani yaani private sector na wao ni kama paka na panya. Sijuwi kitaisha lini hiki kizaji cha Mwalimu Nyerere?.

Na kwa taarifa yenu kwa kila Mtanzania aliyefanikiwa kiuchumi kupitia private sector atakubaliana na haya isipokuwa wale mnaonufakaika na system zisizo wazi na ukiritimba, maana wao akili yao inaishia kuomba mgao eti kwa vile mtu amekuja kuchukua cheque yake.

Sasa hii inahusiana vipi na ujamaa? Nani amesema ukiritimba, uzembe, roho mbaya na maringo ndiyo ujamaa? Au hamjui maana ya ujamaa??
 
Kiongozi anayeongoza kwa visingizio siyo kiongozi hata siku moja. Inwezekana kweli ni matokeo ya ujamaa, ukoloni au uafrika wetu wenyewe (sisi ni wazembe). Yeye kama Kiongozi anatakiwa kuwa frontline kuwajenga watu wajiamaini kwa kuwapa matumaini. Iwapo yeye ataongoza kwa kulaumu historia ya watu anaowaongoza basi tujue tumeliwa sana (thanks Tume ya Uchaguzi) na hatutafika popote.

Nyerere kama kiongozi alikuwa na kila sababu ya kusema kuwa matatizo yetu yalisababishwa na ukoloni kwani huo ndio aliorithi na kila mtu alikuwa anafahamu madhala ya ukloloni; lakini kiongozi yule thabiti alisema kabisa na kuacha kwenye maandishi kuwa matatizo yetu ni umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma. Na akaamua kupambana na matatizo hayo kwa njia alizoona yeye, ikiwemo Ujamaa. Nimesikitishwa kujua kuwa Kikwete naye hajui kuwa Tanzania iliingiaje katika mfumo wa Ujamaa mwaka 1967 ambao ulilazimsihwa na mabavu ya Ujerumani Magharibi baada ya Muungano wa mwaka 1964.

Ningetegemea kikwete atuambie matatizo yetu ni yapi na anapambana nayo vipi; lakini alishanukuliwa akisema kuwa hajui kwa nini sisi ni maskini. Na leo tena anakurupuka na kusema kuwa anadhani ni kwa sababu ya ujamaa uliokufa miaka 25 iliyopita baada ya azimio la zanzibar.
 
Back
Top Bottom