Mkandara
Naona hujapata jiswi na chengu siku nyingi.
Wewe unakubali kabisa mfumo wa kikoministi/ujamaa ndo umewanufaisha viongozi harafu ukifika kwa Tz unapaa vihunzi.Kifupi mfumo ndo huo huo ndo maana utaona viongozi wa kikoministi/ujamaa ndio hao hao wanaomiliki na watoto wao na kudhibiti wengine.
Ukijichanganya mitaani na ukafanya kazi ndo utagundua ukoministi/ujamaa ni tatizo kuu kwa vizee vya Tanzania, mie nimefanya kazi bongo kama fundi mchundo lakini lilikuwa tatizo kubwa sana kwa vizee vya VETA.
Ulaya magharibi hakuna ukoministi/ujamaa wala sidhani kama kuna chama chochote kinachofuata ukoministi/ujamaa kule kuna u-coservative , u-liberali nk.
Mkuu haiendi hivyo hata kidogo,ifike mahala unisome nachoandika badala ya kurudia kitu kile kile..Matajiri wote nchi za Kimomunist sii viongozi wao bali Matajiri hata nchi za Kibepari ni koo zile zile za Kiutawala toka kwa Malkia,Mubarak hadi kwa Kenyatta na kina Kamuzu Banda...Lakini maajabu ni kwamba tunawakuta maskini viongozi ktk Ukomunist koo za kina Nyerere, Nasser, Haile Mariam, Samora na wengineo hivyo usitake kujumuisha kila kitu ili kuleta maana ya ujumla.
Nimesema ni kweli utawala wa Kikomunist ulikuwa na mabaya yake ingawa ,malengo yalikuwa mazuri na wataalam wote wa kiuchumi wanakubaliana kwamba Ujamaa ktk mazingira na tabia za binadamu hauwezi kufanya kazi kama kama vile ZBiblia na Kuran zinavyopinga Utajiri kwa kutumikisha wengine. na ifahamike kwamba Ubepari sii mfumo unaokubali utumwa au kuwatumia watu kama ngazi.
Ujamaa unaozungumziwa hapa sio ule unaopinga watu binafsi kumiliki njia kuu za uchumi au kuhodhi mali bali ni Fikra zinazopinga Ukoloni mamboleo kuwa ni sehemu ya Ubepari na ndio utaratibu unavyotakiwa.
Msome vizuri JK na upate kuelewa kwamba watumishi wa Umma wanakuwa na chuki au wivu wanapokuja WAWEKEZAJI wakifikiria kwamba ni wezi, hivyo tuhuma nzima za JK hazihusiani na Ujamaa unaotaka maisha bora kwa kila mwananchi kupitia itikadi na sera zinazoiwezesha serikali kufikia malengo hayo. Na JK hakueleza wazi kama fikra za kibepari anazozipongeza ni zipi dhidi ya Ubepari ambao unatumika leo hii kwa sababu kumtuhumu mtu mwizi ina maana WIZI upo na kuna watu wa naina fulani ndio wanatuhumiwa kwa wezi..
je JK kafanya utafiti kufahamu kwa uhakika kwamba hao wawekezaji sio wezi isipokuwa ni wananchi ndio wenye mawazo na fikra za Kijamaa? je ni Ujamaa unaposhuku rasilimali za nchi kuibiwa na wageni wawekezaji ikiwa hakuna policies zozote zinazolinda mali za wananchi hao..Je ni fikra zipi za Kibepari zinazokubali wawekezaji pasipo safety measures kuwa moja ya taratibu za kudhibiti uhalifu?..
Leo hii mkuu wangu ndani ya Ubepari huwezi kuondoka na Dollar elfu kumi (10,000) Marekani, UK au Canada pasipo kupata kibali lakini unaweza kuondoka/au kuingiza mamillioni Tanzania na tusione tatizo la moneylaundry lkwa sababu utajiri ni wako wewe mwananchi has nothing attached to rule and regulations hata kama hazikulipiwa kodi au zimepatikana kinyume cha sheria...
Mkuu wangu ni wivu na Ujamaa kuulizia kwa nini Barricks wanatupa ruzuku ya asilimia 3 wakati Sinclair akichukua 1.9 ya ruzuku hiyo zetu kwa matangazo na kuinadi migodi yetu..Ni Ujamaa kupinga Ufisadi wa kina Lowassa, JK, Chenge, Mkapa na wengineo kwa sababu wote tuna fikra finyu za chuki watu wengine wanapoendelea.
Na ajabu ya Mungu ni kwamba hawa viongozi ndio wanawatuhumu wananchi na watumishi wa serikali kuwa Waajamaa hali wao viongozi ndio wamekuwa ndani ya Ujamaa na kuutumikia miaka yao yote ya ajira iweje wao wasiwe Wajamaa ila kizazi hiki ambacho kimezaliwa wakati wa Mwinyi maanake ndio wengi utawakuta ktk sekta za uwekezaji, kodi na kuhamasisha wawekezaji..
Sisi hatutaki ku face reality, tunatafuta mchawi kila siku hali UZEMBE mkubwa umetokana na mfumo mzima wa kuiga ku nya kwa Tembo na sasa msamba unapasuka tunajiuliza kama ni uzembe wetu, fikra za Kijamaa na kadhalika hali Ubepari unakwenda na uwezo wenu, yaani tunajipima suti kulingana na mwili wetu ingawaje mshono ni ule ule..Sisi maskini hatuwezi ku apply policies za nchi za nje wala hatuwezi kuendelea kuomba na kupewa masharti hali dunia ya leo ni ya Utandawazi na soko huria.
Tunatakiwa kuwa part of the mzunguko wa kibiashara na sii watumwa ndani ya mfumo huu na ndio maana tume fail na kilichobakia ni kulana sisi wenhyewe..Tanzania imegeuka kuwa uwanja wa mwenye nguvu ndiye atakula nyama, na hii haitokani na Ujamaa bali tumekosa mambo muhimu sana ktk maendeleo ya nchi -
UONGOZI BORA...