X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,809
Mkuu platform ya siasa za Tanzania ni ile ile, viongozi ndio wale wale waliokuwa pamoja na Nyerere.Mhhhh! Nyerere kang'atuka 1985 miaka 26 iliyopita na waliomfuatia baadaye walijaribu kwa kasi sana kuachana na siasa za ujamaa na kutoiheshimu miiko ya Viongozi na maadili mbali mbali ya awamu ya Mwalimu na hata kulivunja Azimio la Arusha. Sasa baada ya miaka 26 ya kung'atuka kwa Mwalimu bado tunataka kuendelea kulaumu sera za Mwalimu za ujamaa na kujitegemea kwa madudu mbali mbali yaliyofanywa na Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete!? Mtamsingizia Mwalimu kila kitu kibaya hata vile ambavyo hastahili kabisa kulaumiwa.
Kinacho fanyika ni huyu kuingia chama iki huyu kuhama chama kile.
Hapa tunajifariji tu kushabikia vyama tofauti tofauti.
Nahisi labda watoto watakao zaliwa baada ya Urais wa kikwete ndio watakao ikomboa Tanzania.