Kikwete adai tatizo ni ujamaa!

Kikwete adai tatizo ni ujamaa!

Wanaulaumu Ujamaa kwa kushindwa kwa Ubepari; wanataka tuamini kabisa kuwa Ujamaa ndio tatizo la Tanzania. Lakini tukiwauliza nchi kama Uganda, Kenya, Zaire zilifuata mfumo gani - ubepari - tunashangaa mbona hawana sana tofauti na sisi? Wao walifikiri Ubepari ni "soko huru" au "Soko huria" na kwa muda mrefu hiyo ndiyo imekuwa nadharia yao.

Ukimuuliza JK ataanza "uchumi wa soko" a.k.a Ubepari na kutuelezea mambo ya "uwekezaji" na all the bs! Ubepari ni nadharia ya maisha siyo nadharia ya kiuchumi tu kama tulivyofndishwa katika classical economy au political economy na kama tunavyohubiriwa na mapebari wa CCM.

Tunaambiwa kuwa Ubepari ndio utatatua matatizo yetu yote kuwa tukiukumbatia bila kuuhojia au kuusahihisha (wakati wao walioutunga wameshaubadilisha kiasi kwamba unaonekana ni ndugu moja na Ujamaa na hawaachani) basi Tanzania itakuwa pepo.

Inasikitisha kuwa hakuna wananadharia ndani ya CCM - theorists - ambao wangeweza kutumia chembe zilizoko kwenye ubongo wao kuuchambua na kuuweka sawa mfumo ambao wanataka tuufuate. Kwa sababu tukianza kuuliza maswali yanayohusu Ubepari wa Tanzania mtashangaa kuwa watawala wetu walioshindwa wana fikra za Ubepari wa miaka ya 1970 wakati huo ukipambanishwa na Ukomonisti wa Kisovieti.

Leo hii Ubepari wa Kimagharibi unapambanishwa na Ukomonisti wa Kichina na mara moja tunatambua kuwa huitaji Demokrasia ya vyama vingi kuweza kuwa na mabadilishano ya kisiasa, huitaji uchumi usiomilikiwa na serikali au wananchi moja kwa moja ili kuweza kuleta maendeleo na kuwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja yanaweza pia kupatikana katika kuleta maendeleo ya jumuiya nzima.

Utaona kuwa fikra za Nyerere za Ujamaa zinakaribiana zaidi na za China ya leo kuliko fikra za Kikwete za Ubepari zisivyokaribiana na Marekani ya leo.
 
tutamuongelea Nyerere RIP na miaka 40 iliyopita, wakati tatizo liko mbele ya macho yetu, ni kweli tunatakiwa tuangalie nyuma ili tusirudie baadhi ya makosa, rejea hotuba ya Nyerere alisema tatizo lenu mnaacha mazuri na kucukua mabaya, huyu wa sasa hivi na hizi porojo zake ni kwamba ameshindwa kazi ya uongozi, sasa anatafuta mti wa kushikilia hauoni, matokeo yake atakuja kusema udini/ukabila nk ndio unadumaza kukua kwa uchumi wetu hata ujamaa wakati hiyo ndio sera kuu ya chama kimaandishi na ndio iliyo mpatia uraisi, amekuwa kama mtu aliye nunua gari wakati kuendesha hajui, ndio anaanza gari za siku hizi sijui caburator ipo wapi, or start za siku hizi sio za kuzungusha kama za zamani, oh haya matairi ya siku hizi tube less ni mabaya oh sterling power sio nzuri nk nk hadithi haziishi. kuna vitu vingine ambavyo ni vya msingi havi hitaji kuwa na ujamaa au ubepari kutekeleza lakini inachukua miaka 5 ndani ya ofisi yake au ndani ya akili yake kuongelewa au kutolewa uamuzi, halafu anataka kuwa singizia watendaji wazee/vijana/ujamaa, hao washuri wa ofisi yake wana fanya nini wa mambo ya uchumi, umeme nk , hapa juzi juzi aliunda kamati ya bomani kupoza mikataba ya madini, nini yeye mwenyewe amefanya kutekeleza hayo mapendekezo? suala la umeme toka yupo waziri na iptla yake mpaka sasa tatizo lipo, bado utasingizia ujamaa/wazee/vijana na yeye kama kiongozi yupo.

Ahsante sana Mkuu August, ningekuwa na uwezo wa kukugongea likes 100 basi ningefanya hivyo. Kikwete anatafuta mchawi wa kumtupia lawama lakini yeye mwenyewe hayuko tayari kukubali kwamba hana sifa yoyote ya kuwa kiongozi katika ngazi yoyote ile na hili ndilo linalosababisha matatizo makubwa mbali mbali ndani ya nchi yetu ukilinganisha na wakati wowote ule tangu tupate uhuru.
 
Makoye 2009,

Actions speaks louder than words, what the speech said and what China do are at opposite sides of the spectrum. The core of capitalism is free market with less state intervenation. In Germany, France and the rest of Scandinavian there is more government participation in the economy than the Chinese, so why should you call them capitalists and the chinese socialists considering the Chinese have less intervention than those western nations.

China can call itself whatever it wants but its attitude suggests otherwise. They should not refer to themselves as socialists anymore but rather fascists due to the government attitude and the governance style. They are more to the right, undemocratic, the government uses so much propaganda to portray the west as untrustworthy and what they do is best for the people (the propaganda is being played on both sides), too much powers lie with the central government and the nation is run by an elite few; all those are the crucial element of a fascists regime.

Therefore old chinese speaches do not coincide with its current approach economically nor support democratic ways of running the state or even having policies that aim at reducing inequality in their society, as china still has a large amount of poverty within its borders.
 
Hapa bana, wananchi wataimba mashairi ya kulaani uongozi uliokuwepo madalakani, watapiga na kelele, mpaka makoo yawakauke.

Kinachotakiwa ni kufanya maamuzi tu...! Na maamuzi yanayo takiwa ni kupiga chini vyama vyote vya siasa pamoja na hao wana siasa walikuwepo madarakani na wasiokuwepo madarakani. Nchi ishikwe na damu changa sasa, na ile dhana ya kusema kuwa vijana ni taifa la kesho, ikome mara moja...!

Ila tunaweza kuwa hakikishia kuwa viongozi wote wale waliokuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20+... Tutawaheshimu na kulinda hadhi zao, kama wastaafu wa kisiasa, sina uhakika kama wastaafu wa kisiasa nao wanalipwa PPF. Kama wanalipwa ni sawa, ila kwanza tutakata pesa na kuwalipa wale wastaafu wa EAC. Pesa iliyobaki ndio tutawafikiria wao.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
....Rais Kikwete alisema ujamaa ndio umesababisha watumishi wengi wa serikali kuona ubepari kama uadui hivyo hata mtu anayetaka kuja kuwekeza anasumbuliwa hadi anaamua kuondoka.

"
Kweli ujamaa ndio umetufanya tuone ubepari ni dhambi hivyo mwekezaji akija anaangaliwa kama vile mwizi, na hilo linafanya wawekezaji wengine kuamua kwenda kutafuta sehemu zingine za kuwekeza, sisi serikalini tumeligundua hilo na ndo maana tumeanza mkakati wa kuajiri vijana wengi zaidi wenye fikra mpya katika nafasi mbalimbali," alisema Rais Kikwete.

Jana nimelala nikifikiria kuhusu hayo maneno ya mkulu......mimi nafikiri kuna kitu hapa hatujaliangalia kwa makini.

Anapodai ati hawa watumishi wanawaangalia hawa wawekezaji ni kama wezi. Hilo ni kweli mwekezaji yoyote yule anapowekeza si bure anategemea faida kubwa na jinsi yoyote ile ya kukwepa kodi kwa sababu ameleta ajira.....kwa kifupi investor yoyote ni mwizi.

Pili naamini hawa watumishi ambaye mkulu anawekejeli ni wazalendo wanopenda nchi yao wanawakataa hawa matapeli ambao wengi wao wamepitia kwake mkulu and co kama vile Sinclair,Ticts,Vodacom nk wanavyoibia hii nchi.

Je mkulu kama kweli watumishi hawo walifanya hivyo anaweza kutaja ni wawekezaji gani ambao walikmbia?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapa bana, wananchi wataimba mashairi ya kulaani uongozi uliokuwepo madalakani, watapiga na kelele, mpaka makoo yawakauke.

Kinachotakiwa ni kufanya maamuzi tu...! Na maamuzi yanayo takiwa ni kupiga chini vyama vyote vya siasa pamoja na hao wana siasa walikuwepo madarakani na wasiokuwepo madarakani. Nchi ishikwe na damu changa sasa, na ile dhana ya kusema kuwa vijana ni taifa la kesho, ikome mara moja...!

Ila tunaweza kuwa hakikishia kuwa viongozi wote wale waliokuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20+... Tutawaheshimu na kulinda hadhi zao, kama wastaafu wa kisiasa, sina uhakika kama wastaafu wa kisiasa nao wanalipwa PPF. Kama wanalipwa ni sawa, ila kwanza tutakata pesa na kuwalipa wale wastaafu wa EAC. Pesa iliyobaki ndio tutawafikiria wao.

Mkuu X P

Hebu fafanua juu ya uamuzi wako mzito!! Unalenga nini ?
 
Hapa Kikwete kwa mara ya kwanza kaongea point yenye akili sana. wachangiaji wa mwanzo hili lililosemwa na kikwete lina ukweli midingi maofisini humo wakiritimba hata kwa wawekezaji wa ndani yaani private sector na wao ni kama paka na panya. Sijuwi kitaisha lini hiki kizaji cha Mwalimu Nyerere?.

Na kwa taarifa yenu kwa kila Mtanzania aliyefanikiwa kiuchumi kupitia private sector atakubaliana na haya isipokuwa wale mnaonufakaika na system zisizo wazi na ukiritimba, maana wao akili yao inaishia kuomba mgao eti kwa vile mtu amekuja kuchukua cheque yake.

Sawa kabisa, ukweli ndiyo huo lazima tubadilike.
 
Mkuu X P

Hebu fafanua juu ya uamuzi wako mzito!! Unalenga nini ?
Mkuu, unajuwa inafikia wakati mtu unachoka kusikiliza haya makelele yasio kuwa na mwisho, kila kukicha ni siasa tu...! Kila mtu anasifia chama chake ndio bora, wakati vyama vyote hivyo ukiviangalia viongozi wake waandamizi wametokea uko uko kwenye chama tawala.

Tunapokikataa chama tawala na viongozi wake, yatupasa pia kuwakataa na viongozi wa vyama vingine walio wahi kuwa kwenye chama tawala, kabla ya kuamia vyama vipya.

Ndio nikasema, bora tuanze upya. Lakini kama ya kuanza upya vijana ambao ndio wanaambiwa kuwa ni taifa la kesho, washakuwa watu wazima sasa, waachiwe waongoze nchi hii kuelekea kwenye maendeleo... Na wale wazee wetu walio ongoza au kuwepo madarakani tangia uhuru, umefika sasa muda wa wao kuaa pembeni.

kama walizoea kuwaita vijana kuwa ni taifa la kesho, basi sasa ni wakati wao wazee kuwa ni taifa lililopitwa na wakati, wawapishe vijana. Na hatutaki vijana ambao wazee wao walikuwa madarakani tunataka damu mpya.
 
...Hilo ni kweli mwekezaji yoyote yule anapowekeza si bure anategemea faida kubwa na jinsi yoyote ile ya kukwepa kodi kwa sababu ameleta ajira.....kwa kifupi investor yoyote ni mwizi.

Pili naamini hawa watumishi ambaye mkulu anawekejeli ni wazalendo wanopenda nchi yao wanawakataa hawa matapeli ambao wengi wao wamepitia kwake mkulu and co kama vile Sinclair,Ticts,Vodacom nk wanavyoibia hii nchi.

Je mkulu kama kweli watumishi hawo walifanya hivyo anaweza kutaja ni wawekezaji gani ambao walikmbia?

Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa, ila kuna investors wengine wanakataa kutoa rushwa huku wakitaka wasilipe kodi ndo maana watendaji wanawakatalia ama kuwazungusha mpaka wanalala mbele!
 
Hapa bana, wananchi wataimba mashairi ya kulaani uongozi uliokuwepo madalakani, watapiga na kelele, mpaka makoo yawakauke.

Kinachotakiwa ni kufanya maamuzi tu...! Na maamuzi yanayo takiwa ni kupiga chini vyama vyote vya siasa pamoja na hao wana siasa walikuwepo madarakani na wasiokuwepo madarakani. Nchi ishikwe na damu changa sasa, na ile dhana ya kusema kuwa vijana ni taifa la kesho, ikome mara moja...!

Ila tunaweza kuwa hakikishia kuwa viongozi wote wale waliokuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20+... Tutawaheshimu na kulinda hadhi zao, kama wastaafu wa kisiasa, sina uhakika kama wastaafu wa kisiasa nao wanalipwa PPF. Kama wanalipwa ni sawa, ila kwanza tutakata pesa na kuwalipa wale wastaafu wa EAC. Pesa iliyobaki ndio tutawafikiria wao.

Mkuu,
Umeongea neno zuri sana, wanasiasa wa sasa wa ccm na wa upinzani ni kuwapiga chini maana wana kitu common nacho ni ujamaa.

Ujamaa ni kitu hatari sana, anayebisha asafiri akajiridhishe huko ulaya mashariki jinsi ujamaa/ukoministi ulivyo hatari.

Hizo nchi baada ya kuutupa ujamaa tena miaka 10 tu iliyopita wameendelea wamepiga hatua kubwa mnooo, kama ujamaa ungeendelea hayo maendeleo waliyopiga sahivi nje ya ujamaa ndani ya miaka 10, ingewabidi wayafanye ndani ya miaka kama 400 ndani ya ujamaa/ukoministi.
 
Wanaulaumu Ujamaa kwa kushindwa kwa Ubepari; wanataka tuamini kabisa kuwa Ujamaa ndio tatizo la Tanzania. Lakini tukiwauliza nchi kama Uganda, Kenya, Zaire zilifuata mfumo gani - ubepari - tunashangaa mbona hawana sana tofauti na sisi? Wao walifikiri Ubepari ni "soko huru" au "Soko huria" na kwa muda mrefu hiyo ndiyo imekuwa nadharia yao.

Ukimuuliza JK ataanza "uchumi wa soko" a.k.a Ubepari na kutuelezea mambo ya "uwekezaji" na all the bs! Ubepari ni nadharia ya maisha siyo nadharia ya kiuchumi tu kama tulivyofndishwa katika classical economy au political economy na kama tunavyohubiriwa na mapebari wa CCM.

Tunaambiwa kuwa Ubepari ndio utatatua matatizo yetu yote kuwa tukiukumbatia bila kuuhojia au kuusahihisha (wakati wao walioutunga wameshaubadilisha kiasi kwamba unaonekana ni ndugu moja na Ujamaa na hawaachani) basi Tanzania itakuwa pepo.

Inasikitisha kuwa hakuna wananadharia ndani ya CCM - theorists - ambao wangeweza kutumia chembe zilizoko kwenye ubongo wao kuuchambua na kuuweka sawa mfumo ambao wanataka tuufuate. Kwa sababu tukianza kuuliza maswali yanayohusu Ubepari wa Tanzania mtashangaa kuwa watawala wetu walioshindwa wana fikra za Ubepari wa miaka ya 1970 wakati huo ukipambanishwa na Ukomonisti wa Kisovieti.

Leo hii Ubepari wa Kimagharibi unapambanishwa na Ukomonisti wa Kichina na mara moja tunatambua kuwa huitaji Demokrasia ya vyama vingi kuweza kuwa na mabadilishano ya kisiasa, huitaji uchumi usiomilikiwa na serikali au wananchi moja kwa moja ili kuweza kuleta maendeleo na kuwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja yanaweza pia kupatikana katika kuleta maendeleo ya jumuiya nzima.

Utaona kuwa fikra za Nyerere za Ujamaa zinakaribiana zaidi na za China ya leo kuliko fikra za Kikwete za Ubepari zisivyokaribiana na Marekani ya leo.
The funny thing kuhusu viongozi wetu ukifuatilia utagundua they play double standards,yani wanalaumu both ubepari na ujamaa all at the same time,depending on where they speak and the nature of the audience.Wao wanachukulia siasa kama mchezo,yani ile kauli ya "Siasa mchezo mchafu" wao wanaichukulia kiukweli kuwa siasa ni mchezo...Na kwahiyo wanakuja na kauli za kimchezo mchezo.Siasa zikitumika vyema ndiyo nguzo ya maendeleo ya Taifa.Na si michezo michafu ya kuturudisha nyuma.
Kulaumu both ujamaa na ubepari bila kutuambia solution na kuzifanyia kazi basi to me hiyo ni leadership failure.Je viongozi wakuu wanjua matatizo ya wananchi na Taifa kwa ujumla?Ushahidi unaonyesha hawafahamu,kwani hawajui sababu za umasikini wetu,at the same time wanablame ujamaa and sometimes ubepari.Ok hata tuki assume kuwa wanayafahamu matatizo yetu,then what are the solutions?Implementations?Yani no vision for our nation,na hivyo hata hatua za mwanzo tu za kufahamu matatizo yetu hatujazifikia.Kufahamu tatizo na kulielewa ni nusu ya kulitatua.
 
Wanaulaumu Ujamaa kwa kushindwa kwa Ubepari; wanataka tuamini kabisa kuwa Ujamaa ndio tatizo la Tanzania. Lakini tukiwauliza nchi kama Uganda, Kenya, Zaire zilifuata mfumo gani - ubepari - tunashangaa mbona hawana sana tofauti na sisi? Wao walifikiri Ubepari ni "soko huru" au "Soko huria" na kwa muda mrefu hiyo ndiyo imekuwa nadharia yao.

Ukimuuliza JK ataanza "uchumi wa soko" a.k.a Ubepari na kutuelezea mambo ya "uwekezaji" na all the bs! Ubepari ni nadharia ya maisha siyo nadharia ya kiuchumi tu kama tulivyofndishwa katika classical economy au political economy na kama tunavyohubiriwa na mapebari wa CCM.

Tunaambiwa kuwa Ubepari ndio utatatua matatizo yetu yote kuwa tukiukumbatia bila kuuhojia au kuusahihisha (wakati wao walioutunga wameshaubadilisha kiasi kwamba unaonekana ni ndugu moja na Ujamaa na hawaachani) basi Tanzania itakuwa pepo.

Inasikitisha kuwa hakuna wananadharia ndani ya CCM - theorists - ambao wangeweza kutumia chembe zilizoko kwenye ubongo wao kuuchambua na kuuweka sawa mfumo ambao wanataka tuufuate. Kwa sababu tukianza kuuliza maswali yanayohusu Ubepari wa Tanzania mtashangaa kuwa watawala wetu walioshindwa wana fikra za Ubepari wa miaka ya 1970 wakati huo ukipambanishwa na Ukomonisti wa Kisovieti.

Leo hii Ubepari wa Kimagharibi unapambanishwa na Ukomonisti wa Kichina na mara moja tunatambua kuwa huitaji Demokrasia ya vyama vingi kuweza kuwa na mabadilishano ya kisiasa, huitaji uchumi usiomilikiwa na serikali au wananchi moja kwa moja ili kuweza kuleta maendeleo na kuwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja yanaweza pia kupatikana katika kuleta maendeleo ya jumuiya nzima.

Utaona kuwa fikra za Nyerere za Ujamaa zinakaribiana zaidi na za China ya leo kuliko fikra za Kikwete za Ubepari zisivyokaribiana na Marekani ya leo.

Mzee mzima I salute you!

Haina haja ya kupoteza nguvu zetu kubishana na watu wasiolewa wanachokifanya bali kusubiri usiku uingie asubuhi ije wahesabu siku huku wakiendelea kuimba nyimbo ambazo hazipo tena kwenye soko la dunia. Chakufanya ni vijana wote kwa pamoja kuondoa hawa watu kwakuwa out compete technically sehemu zote kwenye siasa hasa ili hatimaye tuanza kujenga system inayoeleweka. Vinginevyo ni kama mgonjwa wa upungufu wa damu kusubiri donation ya damu kutoka kwa mbu!
 
Ujamaa noma sana hawa waliukataa kwa nguvu zote ujamaa ndani ya miaka 5 tu, angalia kilichotokea.

The złoty literally meaning "golden", is the currency of Poland. .
As a result of inflation in the early 1990s, the currency underwent redenomination. Thus, on 1 January 1995, 10,000 old złotych (PLZ) became one new złoty (PLN).
 
Waangalieni na hawa walivyokuwa masikini wakati hawajaamua kuutupa ujamaa na kuungana na ujerumani magharibi. Kabla ya vita ujerumani ilikuwa moja lakini walivyo jitenga tu nakuweka ujamaa wakawa wanasonga nyuma badala ya mbele. Ilikuwa inakula kwao mpaka wakaamua kuutupa ujamaa.

niambieni miaka 30 tu ku exercise ujamaa walikuwa tayari wameshaachwa na wenzao, haya na hawa tatizo lilikua nini?

The German Democratic Republic , informally called East Germany (German: Ost-Deutschland) by West Germany and other countries, was the socialist state established in 1949 in the Soviet zone of occupied Germany and in the East Berlin portion of the Allied-occupied capital city.

In 1989 a non-violent revolution overthrew the Communists. The Soviets refused to intervene, and the country soon reunited with West Germany and is now part of Germany.
 
The Czech Republic has one of the most developed industrialized economies. It is one of the most stable and prosperous of the post-Communist states of Central and Eastern Europe. GDP per capita at purchasing power parity was $26,800 in 2008, which is 82% of the EU average.
1990-1995
The "Velvet Revolution" in 1989, offered a chance for profound and sustained political and economic reform. Signs of economic resurgence began to appear in the wake of the shock therapy that the International Monetary Fund (IMF) labelled the "big bang" of January 1991.

Ukoministi/ujamaa ni nomaa nendeni mkaulize jinsi polisi walivyokuwa wana behave exactly kama polisi wetu.
 
Hapa Kikwete kwa mara ya kwanza kaongea point yenye akili sana. wachangiaji wa mwanzo hili lililosemwa na kikwete lina ukweli midingi maofisini humo wakiritimba hata kwa wawekezaji wa ndani yaani private sector na wao ni kama paka na panya. Sijuwi kitaisha lini hiki kizaji cha Mwalimu Nyerere?.

Na kwa taarifa yenu kwa kila Mtanzania aliyefanikiwa kiuchumi kupitia private sector atakubaliana na haya isipokuwa wale mnaonufakaika na system zisizo wazi na ukiritimba, maana wao akili yao inaishia kuomba mgao eti kwa vile mtu amekuja kuchukua cheque yake.
Ndugu upo sahihi kabisa. Kikwete huwa anasema ukweli na kwa wengi ni vigumu saana kuumeza. Nchi zote zilizoendelea sekta binafsi ndio injini kuu ya uchumi. Lakini ukifika Tanzania watu wanawaona wawekezaji kama wezi vile. Wale wanaofanyakazi serikalini wao wanaamini ndio wenye stahili kuu. Ipo mifano wazi ya athari za kijamaa. Angalia Cuba inavyodondoka taratibu.

Juzi fulani nilifika Cuba nikawa ninataka kufanya kaji transaction kadogo saana lakini watu kama wanane walihusika na ilichukua siku 3 kumaliza hiyo. Na huu ndio utendaji wa Kitanzania ambao umejaa mfumo wa kijamaa. Ukienda mahotelini au sehem zote za biashara angalia Watanzania wenzetu wanavyofanya kazi! Mfumo ni mbovu saana na ndio maana kila linalotokea hata yaliyo ndani ya uwezo wetu tunalaumu serikali.
 
Socialism and communism are ideological doctrines that have many similarities as well as many differences. It is difficult to discern the true differences between socialism and communism, as various societies have tried different types of both systems in myriad forms, and many ideologues with different agendas have defined both systems in biased terms. Some general points distinguishing the two concepts, however, can still be identified.

One point that is frequently raised to distinguish socialism from communism is that socialism generally refers to an economic system, while communism generally refers to both an economic and a political system. As an economic system, socialism seeks to manage the economy through deliberate and collective social control. Communism, however, seeks to manage both the economy and the society by ensuring that property is owned collectively, and that control over the distribution of property is centralized in order to achieve both classlessness and statelessness. Both socialism and communism are similar in that they seek to prevent the ill effects that are sometimes produced by

Sasa ujamaa wa Tanzania ulikuwa umejikita tu ktk economically? je CCM ilikuwa na mlengo gani? na je ccm ilikuwa haijihusishi na siasa? aah u-komunisti noma mie nawaambieni.
 
Waangalieni na hawa walivyokuwa masikini wakati hawajaamua kuutupa ujamaa na kuungana na ujerumani magharibi. Kabla ya vita ujerumani ilikuwa moja lakini walivyo jitenga tu nakuweka ujamaa wakawa wanasonga nyuma badala ya mbele. Ilikuwa inakula kwao mpaka wakaamua kuutupa ujamaa.

niambieni miaka 30 tu ku exercise ujamaa walikuwa tayari wameshaachwa na wenzao, haya na hawa tatizo lilikua nini?

The German Democratic Republic , informally called East Germany (German: Ost-Deutschland) by West Germany and other countries, was the socialist state established in 1949 in the Soviet zone of occupied Germany and in the East Berlin portion of the Allied-occupied capital city.

In 1989 a non-violent revolution overthrew the Communists. The Soviets refused to intervene, and the country soon reunited with West Germany and is now part of Germany.

je ujamaa wa scandinavia nao utasemaje.....siasa zote ni noma muhimu ni watendaji wanatafsiri vipi kiuntendaji
 
..kwa kweli inachanganya mwenyekiti wa chama kinachofuata itikadi ya ujamaa na kujitegemea anapotoa kauli kama hizi.

..hivi inawezekana tukawa na chama tawala cha kijamaa lakini serikali yake ikawa ya kibepari?
Alichosema mkuu ni kweli jamani ujamaa na zidumu fikra za mkulu ndio zimetufikisha hapa. Ujamaa na kujitegemea (ingawa hatukuweza kujitegemea) ni failure dunia nzima ussr ambayo ndio baba lao walishindwa. Wanapojaribu sasa wanajikuta bado wako nyuma na miaka 100 ya ukoministi imewaacha hoi na nyuma ukilinganisha na nchi ndogo tu kama south korea.

Ujamaa wa nyerere uliacha nchii hii katika ukwasi wa elimu ..watu hawana wanachoabudu zaidi ya fikra za mwalimu hata kama hazifai na hasi hakuna anamsema, na ndio mfumo mzima wa kikomunisti unavofanya kazi.

Ni mfumo wa dhulma usiojali haki za watu, usiojali raia kupata haki zao za msingi, lakini mfumo unaodumaza mawazo ya watu kwa kuona kila kitu ni cha serikali na chao hivo wana haki ya kupata kila kitu bureeee hata bila ya kufanya kazi ...umewafanya watu kuwa na mawazo ya kibaguzi.

Leo matokeo yake tanzania tunaogopa mfano soko la afrika ya mashariki la ajira..kisa tunajua hatuwezi kufanya kazi kwa ufanisi ...tumezoea bure na elimu yetu ni mbovu...na mentality ya wabongo ni kuwa serikali iwape kila kitu bure.....ati kwa sababu ujamaa uliwapa bure.....hawajui ni kwamba ujamaa na kujitegemea ulikua na honeymoon period yake .......baada ya kupata nguvu kutokana na kutaifisha na kunyanganya serikali ilikua hoi....hakuna kodi, hakuna kiwanda kinachofanya kazi kwa faida, hakuna uzalishaji wowote ilichobaki ni kuwaridhisha watu kwa propaganda...mara uhujumu uchumi,mara nduli , mara kufunga mikanda , mara noti zibadilishwe bila ya sababu za msingi, mara kesi za uhaini, mara siasa na kilimo.

Ukweli inatakiwa ujasiri sasa kwa kiongozi kusema ukweli kwamba tanzania tumeachwa nyuma na wenzetu kutokana na siasa ya nyerere ya ujamaa na kujitegemea...kutokubali makosa yetu na kutokubali kumkosoa mwalimu kwamba miaka yake 27 ya ujamaa imeidumaza nchii hii basi tutakua nyuma tu.

Tuseme wazi ujamaa haukutenda haki...na sasa kizazi kipya kianze kusomeshwa upya mfumo wa elimu unaomfundisha mtu kupenda kazi na bila ya kazi hakuna cha bure.

Dunia nzima, kila nchi inavutia wawekezeji..na bila kujidanganya kwa sasa bila ya wawekezaji wa nje hakuna ajira ..sisi wenyewe kutokana na ujamaa na kujitegemea watanzania wote ni walala hoi...hatuna uwezo...tuliambiwa pesa sio msingi wa maendeleo...na kuhusu mikataba mibovu ni matokeo ya elimu ya kivukoni.....
 
Back
Top Bottom