Kikwete adai tatizo ni ujamaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete adai tatizo ni ujamaa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Apr 22, 2011.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,021
  Trophy Points: 280
  ..kwa kweli inachanganya mwenyekiti wa chama kinachofuata itikadi ya UJAMAA na KuJITEGEMEA anapotoa kauli kama hizi.

  ..hivi inawezekana tukawa na chama tawala cha kijamaa lakini serikali yake ikawa ya kibepari?

   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Ndiyo matatizo ya kukurupuka na kutoa kauli bila kutafakari kwa kina. Dunia ya sasa anayoizungumzia ndiyo ipi? ya kuwakaribisha wawekezaji wasiolipa kodi? Wanaoruhusiwa kuchimba rasilimali na kutuachia 3% tu!? Au wawekezaji wa kutoka Houston, Texas Richmond/Dowans ambao ni matapeli tu na kumbe ni wa Kariakoo tu? Au wale wahindi wa RITES ambao walipewa 51% ya hisa za TRC bila kutoa hate senti moja na sasa wanatakiwa kulipwa $87 millioni, au hawa Wahindi walionunua Zain na Serikali kukosa kodi ya shilingi bilioni 500 kwa uzembe wao wa kufikiri?

  Ni aibu kuwa na mtu kama huyu katika nafasi yoyote ile ya uongozi.
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  1. Mkuu nitafurahia kama ungegusia source! Aliyasemea wapi haya maeneno!!

  2. Kama maneno yanavyojionyesha hapo .... kwakweli yanajieleza yenyewe ... kuwa Rais amechoka ... hana chochote alichoshikilia na kuamni kama nguzo ya kuongoza Taifa. Ame give up na ku give in... ! Amejitoa na kujiachia kwa watu wengine kabisa kuja kujenga nchi yake...!!

  3. Hicho alichokisema hakina maana sana ..lakini Kimemuonyesha moyo na maono yake ! anahitaji msaada mkubwa wa chadema kusukuma gurudumu la Taifa!!
   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Madai haya sio ya kweli.Hakuna mjamaa Tanzania ya leo.Huyu ni kiongozi aliyeshindwa anayetafuta mahali pa kufia.He is driven by an evil force either knowingly or unknowingly.
   
 5. A

  AridityIndex Senior Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa Kikwete kwa mara ya kwanza kaongea point yenye akili sana. wachangiaji wa mwanzo hili lililosemwa na kikwete lina ukweli midingi maofisini humo wakiritimba hata kwa wawekezaji wa ndani yaani private sector na wao ni kama paka na panya. Sijuwi kitaisha lini hiki kizaji cha Mwalimu Nyerere?.

  Na kwa taarifa yenu kwa kila Mtanzania aliyefanikiwa kiuchumi kupitia private sector atakubaliana na haya isipokuwa wale mnaonufakaika na system zisizo wazi na ukiritimba, maana wao akili yao inaishia kuomba mgao eti kwa vile mtu amekuja kuchukua cheque yake.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,021
  Trophy Points: 280
  Azimio Jipya,

  ..JK alikuwa anazungumza kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki.

  ..source ya taarifa hii ni magazeti ya ipp.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Maandishi hayaonyeshi kwamba hii ni direct quote (hakuna quotation marks)

  Na zaidi ya hapo hakuna source.

  Vitu viwili hivi vingeongeza credibility ya habari.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Apr 22, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Kikwete has a point! Lakini amesema kama vile siyo Rais! amesema kama vile anapiga porojo

  Rais mzuri ni yule anayejua tatizo na kulitatua tatizo, Mkapa alijua watanzania wavivu na akaleta uchapa kazi kwa kupunguza fedha kwenye mzunguko.

  Watanzania hawataki kuhuburiwa matatizo yao! wanataka solution , you are the best if not only candidate to solve our problems.

  Issues za ujamaa na matatizo yake zimejadiliwa sana humu, ni debatable, ni controversy, kuna nchi nyingi zimeendelea kwa ujamaa, na ziko nchi zenye ubepari leo hii wanatamani ujamaa!

  Kikwete pole, haukujua ikulu kuna nini na unatakiwa ufanye nini umebaki kuwa comedian like any other comedian, umebaki kulalamika kama wanaharakati!

  Heshima yako ni kujiuzulu tu, wenye akili watakusifia , kwenda na zigo la magogoni mpaka 2015 you may die on the way or you may end up crazy!
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kama hayo maneno ni kweli, basi hata mimi naunga mkono kauli hiyo. Siasa ya Ujamaa ni Zimwi linalo wasumbua viongozi wengi walioko madarakati.

  Kiasi viongozi wengi wamekuwa waoga kiasi cha kukimbia vivuli vyao.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Apr 22, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Moja ya tatizo ni hili: leo sikukuu, kesho hakuna kazi, Jumapili hakuna kazi, Jumatatu ni siku ya mapumziko, Jumanne nayo ni siku ya mapumziko. Sasa niambieni, kwa hali tuliyonayo sisi tunaweza kweli kumudu kutokufanya kazi siku zote hizi?

  Kwa hiyo hapo utaona kwamba moja ya matatizo yetu ni kuendekeza starehe na uvivu.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,021
  Trophy Points: 280
  AridityIndex,

  ..kuomba kitu kidogo then ni suala la RUSHWA na siyo Ujamaa kama anavyodai Raisi.

  ..pia kama wafanyakazi hawana nidhamu, na wanaomba rushwa, inawezekana kwamba tatizo liko kwenye mishahara na mafao.

  ..Raisi anapodai kwamba uzembe na urasimu serikalini unasababishwa na fikra za kijamaa nadhani ni upotoshaji.
   
 12. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  nakubaliana na wewe 101%
   
 13. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Kwa sheria hizi za uwekezaji tulizonazo......lazima mwekezaji tumuone kama mwizi tu.... hana faida hata chembe kwa wananchi......lazima turekebishe sheria ndiyo mwekezaji tutamwona ni mwenzetu.....
   
 14. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huyu kweli mropokaji sasa hizo fikra za ujamaa zinakuwa vipi kikwazo, as far as people are concerned they can die and be buried with the communist manifesto in their graves and it wont affect non'n.

  Someone needs to tell this bozzo the trouble is not what people think but rather unfriendly business policy (something which Mkullo and Ndullu havent a clue how to deal with) that is higher taxes and higher bank interest rates, capped with too much red tape.
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Apr 22, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,021
  Trophy Points: 280
  Waberoya,

  ..wakati wa awamu ya pili ya Mzee Mwinyi kulianza kujingeka utamaduni na mazingira ambayo hayakuwa conducive kwa wafanyabiashara waaminifu kufanya shughuli zao.

  ..tatizo alilolikuta Mkapa ni tabia ya kupenda ujanja-ujanja, biashara za kitapeli, na ukwepaji kodi.

  ..alichofanya Mkapa ni kuanza kusimamia ukusanyaji kodi, na kuchukua hatua za kudhibiti mfumuko wa bei na mzunguko wa fedha.

  ..morale na maadili ya watumishi wa umma iko chini, sasa JK anaanza kulaumu Ujamaa. mimi nimeishi wakati wa Ujamaa na watumishi walikuwa wanafanya kazi kwa kujituma kwelikweli. mambo yalianza kuharibika baada ya hali ya uchumi kuwa ngumu na wafanyakazi kuanza kushindwa kumudu maisha.
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kiranga,
  Mimi nilimsikia ITV. Napata ITV kupitia Tv4africa.com. Ni kweli aliyasema hayo. Lakini hilo tisa. Nijuavyo mimi, hayo ndiyo maoni sahihi ya Kikwete ambayo huyasema privately au miongoni mwa marafiki zake. Hana hata moja la kumsifia Nyerere. They are trying so hard to kill his legacy lakini naamini historia itawaumbua.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jokakuu,
  Mkuu kwa maneno ya JK sidhnai kama anastahili hata kuwa mwenyekiti na kiongozi wa CCM kwa sababu amepinga hadharani mrengo wa chama chake. Na labda kashindwa kuelewa vizuri kwamba hao wawekezaji wanapoingia nchi wameshafanya utafiti wao kuchambua baina ya siasa za Ujamaa na policies za uwekezaji..Kwa nini mnaendelea kuvuta Ujamaa ule hali viongozi wote wa Tanzania na watumishi wake ni Mabepari kupindukia, tena mirija isiyotakiwa ndani ya Ubepari wenyewe.

  Mtumishi wa Umma atamwona mwekezaji kama mwizi tu pale alipoona mkataba wa huyo mwekezaji hauna manufaa kwa nchi na hili halina fikra za Kijamaa au Kibepari. Pengine JK anahitaji kujifunza yeye nini maana ya Ubepari na tofauti zilizopo leo ktk mfumo huo tofauti na ule wa wakati wa vita baridi. Hakuna Mtanzania ambaye hapendi wawekezaji lakini sii kwa mtindo huu wa Ukoloni mamboleo kuuza na kuinadi nchi ichukuliwe pasipo manufaa kwao. Hata Mabepari waliobobea hao Marekani, Uingiereza, Japan na Canada wanapiga vita uwekezaji wowote ambao hauzingatii national interest bali kufuata na kupangiwa masharti na mwekezaji..

  Tanzania tunakabiriwa na Ufisadi uliopita mipaka yote ya uwekezaji kiasi kwamba kila mwekezaji kutoka nje huona watu wamelala..Lazima awe mwizi au fisadi vile vile kwa sababu wao ndio wenye kauli. hatuwezi kujifananisha na nchi zilizoendelea ambazo Ubepari kwao wanapanga masharti kwa wawekezaji hali sisi na umaskini wetu tunapangiwa masharti.

  UBepari nchi za Ulaya unategemea wawekezaji wa ndani yaani wananchi raia wa nchi hizo hali sisi tunategemea bepari ni mwekezaji kutoka nje kwa sababu wananchi wenyewe hawana uwezo huo...Haya tu yanatosha kuona tofauti za kitaalam ktk kuendesha Ubepari nchi zetu na hizo za Ulaya badala yake tunajaribu kuiga Ubepari wa Ulaya kwa sababu ndivyo tulivyofundishwa darasani..

  JK ameshindwa kabisa kufahamu tatizo la Tanzania ktk uwekezaji ila ametafuta visingizio pasipo kufanya utafiti wa kina kufahamu nini matatizo yetu haswa..UFISADI... Ufisadi ambao ndio mbegu ya kuimarika kwa Urasimu na ukiritimba ni sababu kubwa ya wawekezaji wenye nia nzuri kutowekeza Tanzania, kwani hakuna hata kitu kimoja ambacho kipo huru, rahisi na taratibu zake zinamwezesha mwekezaji kuweka makadirio ya investment, matumizi, muda na hata uwezekano wa kufanikiwa kufungua biashara aliyokusudia.

  KIla hatua ya uwekezaji nchini ina Ukiritimba unaojenga nafasi kubwa ya urasimu kwa sabahu ya mfumo duni wa kiutawala....Maadam kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake hakuna sheria tena inayoweza kudhibiti wanachokula mbuzi hawa.. Ni lazima uhonge kupata hata TIN namba, vibali, eneo na kama anategemea zana za uzalishaji kutoka nje atakwama bandarini kwa muida usiojulikana. JK katembelea wizara na kutazama tu utendaji kazi wake ktk nafasi ambazo tayari zimesimama badala ya kutazama sababu ya sehemu ambazo zimeshindikana..

  Kama angechukua muda kuwauliza wawekezaji hata kupitia balozi zao tu angepata upeo mzuri zaidi wa jinsi Ufisadi ulivyokithiri nchini kiasi kwamba wawekezaji wanashindwa kupata picha halisi ya uwekezaji in term of success. Hata mwananchi akitaka kuwekeza ktk jambo dogo sana inampa shida kufuatilia taratibu za upatikanaji wa vibali.. paper work ni nyingi zisizokuwa na msingi na kibaya zaidi ni ofisifi nyingi zinahusika na kibali kimoja tu hii ikiwa na maana mfumo za taratibu za kiuchumi nchini zimejenga zaidi nafasi za urasimu na ulaji kwa wafanyakazi wake.

  Lleo hii Tanzania hata mlinzi (gatekeeper) anataka apewe chochote ili upate kuingia ofisini na akikataa huna pa kwenda kulalamika. Na kila hatua unayokwenda lazima utoe hongo tena kwa kiwango wanachokijua wao kinyume kabisa na taratibu. Na usipofanya hivyo, kazi yako imelala na huna pa kwenda kulalamika..No one give a damn!..

  Nilipokuwa Bongo mshikaji wangu mmoja aliibiwa laptop yake toka ktk gari lake mitaa ya O'Bay.. tulipokwenda kutoa report polisi waliandika kesi ya jamaa kwenye jarida la kitabu using a pencil..Na tulipouliza walisema hawna karatasi hivyo tukaenda kununua karatasi na kalamu..Just imagine kituo cha O'bay polisi hakina karatasi achilia mbali kuwa na computer wala data base na leo tunazungumzia miaka 50 ya Uhuru. Je kutokuwa na vitu hivyo ni mawazo ya kijamaa au Wajamaa ni wao viongozi ambao wameshindwa kutoka ktk mfumo duni wa kizamani.Barabara zinajengwa kabla ya mifereji ya majitaka, umeme na njia za simu na maji.

  Miji mipya unajengwa na wananchi pasipo kupimwa lakini utakuta tayari Tanesco wameisha sambaza miti ya umeme wakati hakuna ramani za barabara..Again Tanesco wanatumia miti badala ya Aluminium poles zenye thamani ndogo zaidi na zinazodumu kuliko hiyo miti. Leo hii hatuna maji, Umeme na mvua kidogo tu iliyonyesha Dar mji mzima unanuka, kinyesi kinaelea barabara kuu utafikiri ni part of mapambo ya barabara.

  Jamani mwekezaji gani kweli atapenda kuwekeza Tanzania na sii Rwanda, Kenya au Uganda ambako kidogo wameweza kudhibiti urasimu ktk nafasi nyeti za uwekezaji. Makusanyo ya kodi bado ni ya kukadiliwa ina maana hakuna sheria wala utaratibu unaotoza mtu kulinganana kipato isipokuwa makisio..

  Hili tu linamfukuza mwekezaji yeyote kabla hajafahamu kuna njia za mkato..Katika business plan yeyote ile kiwango cha tax kinachotakiwa kulipwa kinatakiwa kiwe wazi kulingana na mapato ya mwekezaji lakini inapofikia mwekezaji kuanza kubishana na afisa wa TRA kuhusiana na kodi hapo tena huwezi kulalamikia Ujamaa bali sisi wenyewe kukurupukia Ubepari pasipo kujua kwamba Ujamaa wa leo ni part ya Ubepari vile vile, hivyo hauwezi kustafrika kama ni fikra finyu za watumishi wa umma wanapowatazama wawekezaji kama ni wezi wa mali zao.
   
 18. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  What made you say that?....got any uthibitisho?
   
 19. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sasa kama sisi kazini kwetu tuna umeme masaa mawili tu! Mgao unatufanya tukae tu! Sasa kama tutakuja kazini siku hizi zote, hli si ile ile? Mie naona sikukuu zinapunguza kuumwa na dhamira yaani ninapokea mshahara bil kufanya kazi!
   
 20. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #20
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu una uhakika na ilo la Siku ya Jumanne kuwa ni siku ya mapumziko?

  Maana kuna ofisi nimewasiliana nao wamenitaarifu, niwapigie siku ya Jumanne, sasa kama ni sikukuu, itakuwaje?
   
Loading...