KIGOMA: Rais wa Burundi, Evariste Ndaishimiye apokelewa na Rais Magufuli uwanja wa Lake Tanganyika, asema ana uhakika Dkt. Magufuli atashinda uchaguzi

wambagusta

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
2,507
2,000
Huu mwaka huu uchaguzi ccm wanatumia pesa nyingi Sana wasanii zaidi ya Mia moja. Wapanda malori zaidi ya alfu moja kila kata kila jimbo wanatembea na magufuli kila mkoa. Haya nchi marafiki Uganda ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ Burundi ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ฎ marais wao nao wana kuja kumuombea kura matukio yote hapo pesa inatumika sio bure . Nilichogundua binafsi kifo cha mkapa ni pengo kubwa Sana kwa ccm. Nakingine magufuli alikosea nini miaka minne iliyopita mbona lissu ananguvu kubwa Sana hii nguvu hanaipata wapi
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,377
2,000
Pinga pinga wanaumia roho najua

Na kama kawaida yao watakua wanafuatilia TBC1 japo ndo vinara wakuitukana

Tuumie kwa rais wa Burundi, ingekuwa rais wa US si mngeweka picha zenu za utupu hapa jukwaani? Ni makosa kwa sheria za kimataifa nchi moja kuingilia uchaguzi wa nchi nyingine. Hii sio kingine zaidi ya kuendekeza udictator uchwara.
 

Statistics

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
1,798
2,000
Amekuwa mnyenyekevu sana kwa kumuita jpm baba,

Amemsifia sana na kumwombea kura.


Je, wataalamu wa saikolojia, ujasusi na diplomasia huyu Generali evariste ndaishimiye anawinda nini Tanzania kwa siku za usoni?
 

secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
5,712
2,000
"Uzi ko sogokuru yavuye aho. Noneho uri umuvandimwe wanjye wamaraso reka tubane." ... .. sisi ni ndugu wa damu. Amesika bwana yule katika mapokezi.
Unkubweno ukwago ubutusi abenyo....
muwe mnaandika kiswahilli!
 

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,679
2,000
Hivi ni kwa nn jamaa anapenda kuwaalika madikteta tu tena kipindi hiki cha uchaguzi?๐Ÿค”๐Ÿค”
Zaidi ya hilo nasikia museven asili yake ni mhutu..... ๐Ÿ˜’๐Ÿ˜’

Tuendelee kujiuliza pamoja๐Ÿ‘๐Ÿ‘
 

Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,936
2,000
Leo Rais wa Burundi, Evarist Nditiye amewasili nchini kwa ziara ya kiserikali na anapokelewa punde na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

3:30 Asubuhi: Rais Magufuli ameshaingia uwanjani, kwa sasa wasanii kadhaa wanatoa burudani akisubiriwa Rais wa Burundi, Evarist Ndaishimiye

3:47 Asubuhi: Rais wa Burundi, Evarist Ndaishimiye amewasili uwanja wa Lake Tanganyika na kupokelewa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli. Baada ya mapokezi inapigwa mizinga 21.

Rais Magufuli: Tumempata ndugu yetu na rafiki yetu, Rais wa jamhuri ya Burundi ambae kwa mara ya kwanza tangu aapishwe kuwa Rais wa Burundi, ameamua nchi ya kwanza ya kuitembelea iwe Tanzania.

Amekuja kwa shughuli ya mazungumzo ya kiserikali na ndio maana baada ya kukaribishwa rasmi tulitakiwa tuondoke twende kwenye mazungumzo na kabla hatujazungumza tulitakiwa pia twende kwenye sherehe nyingine ya kufungua mahakama, iliyojengwa kubwa ya kanda hii ya Kigoma.

Yale ambayo tutaenda kuyazungumza na kukubaliana tutayatoa baadae lakini nataka kutoa ya utangulizi. Biashara kati ya hizi nchi mbili zimeanza kuongezeka.

Katika suala la madini, leo tutazungumzia kuhusu suala la kuruhusu nchi ya Burundi baadhi ya amdini yake kama dhahabu yawe yanakuja yanauziwa hapa Kigoma kwa sababu bahati nzuri, sisi Tanzania tumeshafungua maduka ya madini badala ya wenzetu Burundi kuhangaikia kupeka mahali pengine tuwaombe walitumie soko la madini hapa Kigoma katika kufanya biashara.

Pia leo tutazungumzia uwezekano wa kujenga mtambo wa kuchenjua madini ya nickel, Tanzania tuna nickel Kabanga lakini pia Burundi wana nickel sehemu yao na mazungumzo yashaanza.

Leo pia tutahusisha kwenye mazungumzo kuhusu ujenzi wa reli ya kutoka Uvinza Msongati hadi Kitega. Tunataka watu wa Kigoma wakitaka kusafiri pia, watumie majini, watumie reli, watumie ndege.

Tunataka kuitengeneza hub ya biashara hapa Kigoma, tunataka tujenge uwanja mkubwa, huu tuupanue uliopo ili ndege inapotoka Dar es Salaam, inatua Kigoma, inaenda Bujumbura.

RAIS NDAISHIMIYE: Zamani Watanzania wakiona Mrundi anakuja hapa walikuwa wanadhani kuna mambo mabaya Burundi lakini sasa hivi mimi nimekuja na salam za warundi wote, wanawasalimia sana kwa niaba yao nataka kwanza mheshimiwa Rais nikupongeze, umeijenga Tanzania, umeibadilisha.

Mimi nilikuwa nakuja hapa Kigoma na familia yangu, umeibadilisha nchi ya Tanzania na Kigoma, mimi nmeshangaa kwa muda mchache tu, nimeona Kigoma imebadilika. Nakupongeza sana.

Nakupa pole, najua mchoko wa kampeni. Nina uhakika kwamba wewe kuwa na wananchi wa Tanzania ni kama baba na watoto, nina uhakika sana kwamba utashinda uchaguzi tena sana.

Na Warundi wote wanasema, nikiwepo ningechagua Dkt. Pombe Magufuli. Burundi tanasema kwamba, Watanzania ni wazazi. Tanzania ni wazazi kwa sababu tangu zamani katika kupambania uhuru, mheshimiwa baba wa Taifa alikuwa anaenda bega bega na Rwagasore wa Burundi, yeye alimsaidia, akamfikisha UN wakaenda pamoja.

Wakati wa machafuko ya Burundi, Tanzania ilikubali kubeba msalaba wa Burundi, walipokea Warundi wengi wakimbizi tangu zamani na Tanzania walituonea huruma wakakubali kwamba wale warundi walikimbilia Tanzania zamani wakapata uenyeji, tunashukuru sana.
Birds of the same feather fly together! It was Mseveni and then Ndaishimiye.
 

1954

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
9,721
2,000
Kumbukumbu, 2015 Nkurunzinza alipinduliwa akakimbilia Tanzania...kwa sasa ni marehemu.
Wewe mwongo...kulifanyika jaribio la mapinduzi akiwa Ikulu Dar es Salaam kwenye mkutano wa viongozi wa Afrika Mashariki...akiwa kwenye mkutano na baada ya habari hizo akaondoka na kurejea Burundi na akazima jaribio Hilo...walioanzisha jaribio Hilo walifyekelewa mbali na wengine kukimbilia Rwanda waliowatuma...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom