Rais dkt. Mwinyi afungua maonesho ya biashara na uwanja wa maonesho

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ina mpango mzuri wa kujenga majengo ya kisasa ya Maonesho ya Biashara na kuwa kivutio kikubwa kwa wadau wa biashara, taasisi na mashirika ya kitaifa na kimataifa.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipofungua Maonesho ya 10 ya Biashara Zanzibar na kuufungua rasmi uwanja huo mpya wa Maonesho Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 10 Januari, 2024 katika shamrashamraza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Maonesho hayo yameshirikisha washiriki 5,00 kutoka Taasisi za Serikali, sekta binafsi, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wajasiriamali.

Vilevile Rais Dkt. Mwinyi ameitaka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya viwanda kulitangaza eneo jipya hilo la maonesho na kulifanya kuwa kimataifa.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amekubali ombi la kuanzishwa kitengo maalum kuendesha na kusimamia viwanja hivyo vipya.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza Wizara ya Biashara na Maendeleo ya viwanda kwa kuendelea kufanya miradi mikubwa ya maendeleo na kuacha alama , pia amewataka kushughulikia maendeleo ya viwanda nchini.
IMG-20240111-WA0007.jpg
IMG-20240111-WA0008.jpg
IMG-20240111-WA0014.jpg
IMG-20240111-WA0009.jpg
IMG-20240111-WA0011.jpg
IMG-20240111-WA0010.jpg
IMG-20240111-WA0012.jpg
IMG-20240111-WA0013.jpg
IMG-20240111-WA0005.jpg
IMG-20240111-WA0006.jpg
255629999998_status_7f46c171b53e49dc8d0be1c1365f7589.jpg
255629999998_status_5bf3c1e2bf62494491999382d646db60.jpg
255629999998_status_bac2625997c34fc48e60f368eb216140.jpg
255629999998_status_d5ea20da26ad49b892b9494bb6c51f08.jpg
255629999998_status_ee95610691c04df08bafada8d50244a2.jpg
255629999998_status_bb5a76c869f9461f98d0f963992eca18.jpg
255629999998_status_15d82b4c689648c5943d62e7d586ef78.jpg
255629999998_status_0fb9383bf9234107885a4a90530669c3.jpg
255629999998_status_a47e1e173afd42219c0fd399bc191c3f.jpg
255629999998_status_e10306cfa4ba4ccda287b492dbf05c0b.jpg
255629999998_status_322bef618a784f74a751791915732705.jpg
 

Attachments

  • IMG-20240111-WA0005.jpg
    IMG-20240111-WA0005.jpg
    104.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom