Rais Evariste Ndayishimiye: Uongozi wa Nchi ya Rwanda Unafadhili Vikundi Vya Uasi Dhidi ya Burundi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,044
49,728
Kwa mara nyingine Rais wa Burundi Evariste Ndamishiye ameishutumu Rwanda ya Paulo Kagame kuwafadhili Waasi wa kundi la Red Tabara Ili waendelee kufanya mauaji ya Warundi na kutaka kuipindua Serikali ya Gitega/Bujumbura.

Bwana Ndimishiye amesema licha ya kutumia diplomasia Kwa mda mrefu kujadiliana na Rwanda Ili kuwarejesha Burundi Waasi hao aliodai wanaofadhiliwa Kwa Hali na Mali na Serikali ya Kigali ila imeshindikana.

=======

Rais ameyasema hayo hivi leo akiwa kwenye mkutano na wananchi na waandishi wa habari, uliorushwa moja kwa moja na televisheni na redio ya taifa akiwa mkoani Cankunzo kwenye mpaka wa Burundi na Tanzania.

Rais huyo wa Burundi ameinyooshea kidole Rwanda kwa kile alichosema ni kuwasaidia kwa hali na maliwaasi hao wa Red Tabara, huku akielezea masikitiko yake kwamba juhudi zote za majadiliano na Rwanda juu ya suala hilo hazikufua dafu.

Alisema kwa takriban miaka miwili wamekuwa katika mazungumzo ili waasi hao warudishwe nchini Burundi, lakini hakuna muafaka uliofikiwa hadi sasa.

"Kama mnavyojuwa ndio waliohusika na janga la 2015. Kinachosikitisha ni kuwa tumeshindwa, kwani tungekuwa hatukushindwa wangetukubalia kuwarudisha nchini." Alisema

Aliongeza kuwa makundi hayo yanapewa hifadhi, mahitaji ya kiutu ikiwemo chakula, pesa za kutumia na nchi ya Rwanda na pahala salama kufanyia kazi zao.

Soma pia:Ndayishimiye ziarani Kinshasa kujadili amani, ushirikiano

Waasi hao walitajwa kuhusika na mauwaji na raia 20 na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa usiku wa tarehe 22 kuamkia 23 mwezi huu maeneo ya Gatumba karibu na mpaka mwa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Ama kuhusu taarifa kwamba baadhi ya wanajeshi wa Burundi waliopelekwa kusimamia usalama mashariki mwa Kongo wamekamatwa mateka, rais Ndayishimiye amekumbusha kuwa wanajeshi hao walipelekwa huko kufuatia mikataba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kwamba kutekwa kwao hakutosababisha makubaliano hayo kusimama, kwani Burundi ilikubali kusaidia kukabiliana na ugaidi duniani.
Ndayishimiye azungumzia pia siasa ndani ya Burundi

Swala jingine lilochomoza katika mkutano huo uliowajumuisha wananchi wa kawaida na waandishi wa habari, ambao ulitoa fursa kwa kila mtu aliyetaka kumuuliza swali rais huyo wa Burundi moja kwa moja, ni mfarakano ndani ya chama kikuu cha upinzani cha CNL.

Rais Ndayishimiye amemshauri mkuu wa chama hicho, Agathon Rwasa, kuhakikisha jawabu linapatikana ndani ya chama hicho, na kuonya kuwa tofauti na hapo huenda kukawa na matokeo mabaya, ikiwemo kusambaratika kwa chama.

=========

My Take: Burundi & DRC Waungan kuivamia Rwanda ili kumtoa Kagame kama Tanzania tulivyomtoa Idd Amin vinginevyo watapata tabu sana.

Mwisho Mbona Kagame haleti Chokochoko Kwa Tanzania?
 
View: https://www.instagram.com/p/C1c4ml4CClV/?igsh=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Hivi Burundi &DRC Waungana na kuivamia Rwanda ili kumtoa Kagame kama Tanzania tulimtoa Idd Amin vinginevyo watapata tabu sana.

Mwisho Mbona Kagame haleti Chokochoko Kwa Tanzania?

Si wanaswali kanisa 1 hao?
 
na yeye anashindwa nini kufadhili vikundi vya uasi vya rwanda, au aungane na mwenzie wa congo wamsambaratishe kagame?
 
Back
Top Bottom