Kifo cha RPC Mwanza: Maswali ya Bei Mbaya...

Kwa kweli Mwanza inatisha. Nashauri IGP afanye uhamisho wa askari wengi sana waliopo Mwanza. Coz wengi hawaaminiki na wamekuwa kwenye siasa zaidi. Kama watataka ushirikiana wapangue askari waliopo wawapeleke Lindi na Mtwara na wa Mtwara na Lindi waende Mwanza..just my suggestion to IGP.
 
wanamtandao,

nimesoma thread ya mauaji ya rpc wa mwanza, nikaamua kucopy maswali yote ya members kama yalivyo na kuyaleta hapa kama thread.

Naamini maswali haya ya wanajamvi yatasaidia kupata hadidu za rejea za watakaochunguza tukio hilo.

Ieleweke kuwa memberz wa hapa ndani pia ni polisi jamii.

(naomba mod usiunganishe na thread kuu)

1. Kwanini rpc asimwagize dereva kumpeleka dadake?
2. Kwanini asiende na walinzi wake?
3. Kama alikuwa na walinzi, je walijeruhiwa au kufa? Walinzi walizidiwa?
4. Ukomo wa kazi wa walinzi wake ni saa ngapi?
5. Je kwenye gari walikuwa wawili tu?
6. Dada mtu ameumizwa?
7. Jina la huyo dadake ni nani?
8. Intelijensia haikunusa mauaji kabla?
9. Kwanini auwawe?
10. Kwanini isidhaniwe ni vinyongo ndani ya jeshi la polisi?
11. Polisi wamejuaje wauaji ni majambazi? Nani ana uhakika kauwawa na majambazi?
12. Walikuwa wanagombea demu?
13. Sijui ni wale waliompiga hyness kiwia!?
14. Kikao cha harusi hadi saa 8 usiku?
15. Majambazi gani wanaothubutu kumvamia rpc, na je walitaka kumwibia?
16. Wamempora nini baada ya mauaji?
17. Alikuwa na gari binafsi au ya serikali?
18. Alivaa uniform au kiraia?
19. Hakuna visasi nyuma?
20. Nani ana uhakika kauwawa na majambazi?
21. Kikao kilikuwa bar au nyumbani kwa mtu?
22. Kama aliwamulika majambazi, je ni yeye tu aliyepita hiyo njia?
23. Dada mtu alichukua hatua gani baada ya tukio?
24. Aliwaona wahusika?
25. Risasi alipigwa eneo gani la mwili?

ufo=unidentfying flying object.
 
Mwongozo huu ni mzuri,ngoja tuone wanafanye na hadidu za rejea za zinaweza kua hizi labda.
 
Je hiyo risasi iliyotumika ganda lake halijaonekana????the killer has left no traces????there must be clues left there
Na wataalamu wanasema hakuna crime inayoweza kufanyika bila kuacha traces, na pia hakuna binadamu anayeweza kufuta alama zote za uhalifu.
Hata computer inaaminika haiwezi kufuta information permenently.
 
PJ hii hali ya ku-downplay mauaji ndiyo imetufikisha hatua hii, kama tungeendelea kuwa wakali kama zamani inapotokea mtu kauawa, sidhani kama kuna mtu angejaribu kufikiria kumuua kamanda wa polisi wa mkoa, tumeruhusu kutegemea riport za kisiasa, matamko ya kisiasa, n.k vyote hivyo hupingana na ukweli kwa dhahiri shari. Mwacheni naye awe victim wa system wanayoiasisi.

Haya maswali yangekuwa na maana kama ndugu zetu wanaouawa migodini, mikutanoni, machungani, mashambani, mabwepande mahospitalini etc wangepata haki yao, si mazishi pekee (mnyonge mnyongeni . . . . . .)
TUTAKUKUMBUKA LIBE.
 
kama alikuwa na gari ya serikali;

  1. Je, alikuwa na kibali cha kutumia gari ya serikali hadi usiku?
  2. Je, alikuwa na kibali cha Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani kuendesha gari ya Serikali wakati kuna dereva aliyoajiriwa kwa kazi hiyo?
  3. Je, matumiz ya gari ya Serikali kwa vikao vya Harusi, ni sahihi kwa gari ya Serikali?
  4. Mafuta ya gari hiyo yaliwekwa na nani?
  5. Je, kuna ruhusa ya kuongeza mafuta kwenye gari ya serikali ili litumike kwa shughuli binafsi?
Aisee!
Hakika mi nilijua maswali yameisha, kumbe kuna mambo ya msingi ambayo yanaweza kutoa majibu kadhaa!
Mkuu maswali yako ni magumu, na yanahusu zaidi sheria za utumishi wa umma na code of conduct makazini.
 
maswali mazuri sn ktk muongozo wa kesi. huyo anayesemekana kuwa ni dada mtu kama siyo daaaada mtu ndiye suspect no 1 kwenye haya mauaji, hope by now atakuwa underrested.
 
wacha wayaue.......wenyewe wanaua raia bila makosa...sasa wacha wao nao wauliwe.........ili waone uchungu wa kuua wengine.....hii ni msg tosha kwa Kova na genge lake la kina Kamhanda et al....
 
Swali lingine PakaJimmy kwa hali ya kawaida watu wakifanya mauwaji makubwa kama hayo, hawawezi kukuacha wewe ambae unawaona wakuache hai eti waishie kuku-search na kuondoka na baadhi ya vitu vyako, sasa kwanini huyu Dada nae hakudhuriwa? Je anaweza kuwakumbuka hawa watu kwa sura? Je baada ya tukio walikimbilia upande gani kwa usafiri gani au kwa miguu? Huyu Dada etu nae alichukua hatua gani baada ya tukio? Na hatua hio aliyochukua ilikua baada ya muda gani baada ya tukio? Je wakati wa tukio la kufyatua risasi yeye alijibana upande upi asipatwe hata na risasi moja??????? au kama walipiga risasi kwene vioo, je hakuna hata kioo kimoja kilichomkata huyu Dada???? Narudi tena

Sio risasi tu inayoua, je kuna watu au mtu yeyote alisikia hiyo milio ya risasi? Safari hii Mhesh.Nchimbi ataunda tuma au kamati ya uchunguzi?
 
Nashkuru kuwa nanyi wana JF wenzangu, kimsingi tumepoteza another JEMBE alafu wanajamii tusipende kuhusisha kila jambo na siasa. Tujaribu kukosoa wapi serikali yetu inakosea na kuipa ushauri wa bure najua tupo maintelgensia wengi humu ndani ya mjengo wa JF!!
 
kwani mungu hamjui shetani! Usijivike uso wa mbuzi!!!
Elewa kuna kazi za shetani na kazi za Mungu usituchanganye. Kama kafia katika ugoni Mungu anahusika vipi hapo na yeye ameshasema USIZINI amri ya sita.
 
huyo dada mtu walionapicha yake tuwekeni hapa maana tangu niliposikia hii taarifa usiku sikuwa naimani ya majambazi bali nilihisi ni maswala ya mapenzi aka kimada. maana wakubwa wanajiona wako juu ya ndoa za wenzao
 
Back
Top Bottom