Kifo cha RPC Mwanza: Maswali ya Bei Mbaya...

Kifo cha RPC Mwanza: Maswali ya Bei Mbaya...

Tehe teheee teheeeee! Nacheka kwa huzuni nikiwa chooni. Atakuwa amepigwa na kitu chenye ncha kali, na hawa lazima ni Chadema
 
Je, wamejuaje kuwa ameuawa kwa risasi na si kitu chenye ncha kali?
 
Je, huyu jamaa chini ya uongozi wake hakuna wanyonge waliouawa au kufungwa bila hatia?
 
Kweli watu wamechoka! Eti wauwaji sio ndio waliomteka Hyness kiwia?
 
Maswali muhimu ya kujiuliza.... hao wanaodaiwa ni majambazi waliomuua walijuaje kwamba RPC atatoka kwenye kikao muda huo na hataongozana na walinzi wake!? je, ni kweli hakuwa na walinzi?; je, alishindwa kumwachia dereva wake amrudishe huyo "dada yake?"; au usiku wote huo hakuwa na derava wake?; huyo anayedaiwa kuwa ni "dada yake" ni dada yake kweli?; vipi kuhusu mke wake, amehojiwa kuhusiana mauaji ya mume wake?; uitikio wa mke wake, muonekano wake kisaikolojia baada ya mauaji upoje?... haya ni maswali ya muhimu ambayo intelligensia inatakiwa kuwa na majibu yake.

Si rahisi kwa raia wa kawaida kuvamia gari ya rpc na kurusha risasi, hata kama ilikuwa si ya ofisini lakini ni lazima kuna kuvuja kwa taarifa nyingi tu kuhusiana na mwenendo wake kwa siku nzima ya tukio. JE, WALIOKUWA KWENYE KIKAO HICHO "CHA HARUSI" WAMEHOJIWA WOTE!??.

NAOMBA KUWASILISHA WADAU!!
 
Hujaandika la kwangu Mpwa; Sheria inasema Bar zinafungwa saa tano usiku, kwa working days, Jana ni Ijumaa ni siku ya kazi, Bar ilifungwa saa ngapi? Kama sio saa Tano, yeye kama Kamanda alichukua hatua gani? au na yeye aliivunja sheria ile ile anayotakiwa kuilinda? Na kama Bar ilifungwa saa tano, yeye alikua wapi na huyo Dada yake had saa saba? Kizungumkuti
Elli una uhakika kama bar zote zinafata sheria kwa kufunga katika muda muafaka?
:confused2:
 
Last edited by a moderator:
Mpwa hio sio concern yangu, concern yangu kubwa ni kwamba, huyu akiwa kama kiongozi ambao kila siku ndio wanasema Bar zifungwe muda huo, kwanini yeye asiwahimizie wafunge? Nilipata kusikiliza kipindi kimoja cha Chanel Ten cha Polisi Jamii na yule Mama alisisitiza kuwa( Ni askari) lazima Bar zote during workdays zifungwe saa tano, na kwamba wale wanaondelea zaidi ya hapo wakamatwe. Hapo ndipo nilipojengea point yangu
Elli una uhakika kama bar zote zinafata sheria kwa kufunga katika muda muafaka?
:confused2:
 
Mpwa hio sio concern yangu, concern yangu kubwa ni kwamba, huyu akiwa kama kiongozi ambao kila siku ndio wanasema Bar zifungwe muda huo, kwanini yeye asiwahimizie wafunge? Nilipata kusikiliza kipindi kimoja cha Chanel Ten cha Polisi Jamii na yule Mama alisisitiza kuwa( Ni askari) lazima Bar zote during workdays zifungwe saa tano, na kwamba wale wanaondelea zaidi ya hapo wakamatwe. Hapo ndipo nilipojengea point yangu
Ok nimekuelewa Elli
 
je mkewake alikuwa anataarifa kuhusu kikao? na je naye mke wake alikuwepo kwenye kikao? na wanapo rud alianza kumshsha mke wake ndipo akampeleka dada yake?.kazi ipo.
 
Hata wanyakyusa tumesikia na tumeshangaa sana wababe wa wanyakyusa kumbe wanaroho na miili ya nyama?Mm nilidhani ni sisi kina Mwa mwa mwa!!!Hongera kwa yaliyowapata Polisisiemu,Nape anasemaje!!!?Tuendelee kuishi tuone wanyonge mungu anawapiganiaje
 
hata ukipata majibu haisaidii, yote ni mipango ya Mungu.

Mungu asihusishwe na madhaifu ya kibinadamu. Yasingemkuta yaliyomkuta basi angemdanganya mkewe:mara oh tulikuwa kwenye operesheni ya kulinda makanisa yote ya Mwanza, honey si unajua leo jioni Waislamu walivyochoma makanisa huko Mbagala? au, leo wife nimechoka sana, hii kazi ya upolisi mimi nitaiacha kabisa, kazi gani isiyo na mapumziko, n.k.

Kweli wake zetu ni wavumilivu.
 
Hapa bado kuna utata!!! taarifa nyingi zinazotolewa zinakinzana, maswali muhimu ni haya:
1. huyu mwanamke aliyekuwa na marehemu anaitwa dorcas moses au doroth moses?
2. marehemu alipotoka kwenye kikao alitoka na doroth/dorcas kwa pamoja au alikutana naye njiani ndio akampa lift?
3. kuna habari zinasema alikutana naye njiani ndio akampa lift... je, hapo njiani ni marehemu ndio alianza kusimamisha gari au dorcas/doroth ndio alimsimamisha!?
4. mtoto wa dorcas/doroth anaeleza mama yao aliwaaga anaenda kwenye kikao cha harusi, je kama kikao alichoenda sicho alichokuwa marehemu..kimeshajulikana kilifanyikia wapi? na huko kwenye hicho kikao dorcas alikuwa na nani?
5. Je, kama marehemu na dorcas/doroth walitoka pamoja kwenye kikao florida hotel, watu wanaosadikiwa ni majambazi waliomuua rpc walijuaje safari ya wawili hao kuwa itaishia getini kwa dorcas/doroth!???
6. hata kama marehemu alikutana na dorcas njiani, swali ni lile lile.. walijuaje hawa watu mpaka wakawasubiri pale getini?
7. Je, simu za dorcas/doroth zimeshachunguzwa kuangalia mawasiliano aliyofanya ndani ya masaa 48 hadi 60 at least?
8. mtoto mmoja wa dorcas anaeleza hawamjui kabisa rpc na hawajawahi kumuona, je ilikuwa mara ya kwanza kwa marehemu kufika nyumbani kwa dorcas!???

NAOMBA KUWASILISHA WADAU!!
 
Upelelezi ni taaluma kama ilivyo udaktari, uhandisi n.k.
Mara tukio linapotokea kama la marehemu RPC, sharti eneo zima(ikiwemo gari la marehemu) lizingirwe/lizuiliwe watu wasiliharibu na kupoteza chembechembe na mabaki ya wahalifu walioyayaacha wakati wanatenda na wakati wa
kuondoka kwenye eneo hilo.
Marufuku kujiwekea majibu kichwani kuhusu tukio, majibu hupatikana kutokana na upelelezi
Muda ule mara baada ya tukio huwa ni mzuri sana kupata ushahidi wazungu wanauita "golden hour"
Mpelelezi lazima ajue njia waliyoingilia wahalifu kabla ya tukio na ile waliyooitumia kutoroka baada ya tukio
Eneo lote lazima lipekuliwe kitaalamu kwa uangalifu sana kwa kuwashirikisha wataalamu mbalimbali
Ni kanuni ya Profesa Edmund kuwa kila mgusano/msuguano huacha alama kila upande unaoweza kusaidia
ufuatiliaji/upelelezi na ushahidi mahakamani. Hivyo upekuzi huo utapata alama, mabaki na vijinasaba vya wahalifu hao
katika eneo la tukio(ni pamoja na ndani na juu ya bodi la gari, njia waliyoingilia na waliyoitumia kutorokea)
Vitu vitakavyosaidia kuwakamata watuhumiwa ni pamoja na alama za vidole, DNA, pamoja na vitu vingine watakavyokuwa walividondosha au kuvichukua katika purukushani ya kutenda uhalifu au kutoroka.
Mambo hayo hapo juu ndiyo huunganishwa na majibu yaliyotolewa na mashahidi wa tukio, waathirika wa tukio na watuhumiwa wakati wa mahojiano ambayo yatafanyika kwa watu mbalimbali wakiwemo majirani wa eneo la tukio na raia wema watakaojitolea taarifa.
SPECULATION(Kama hizi za mleta uzi huu) ni mbaya sana katika utekelezaji wa haki jinai, huweza kupotosha ukweli
kisha kuadhibu asiyestahili kwa kutumia hisia badala ya ushahidi.
Nawashauri tuwe tunatazama kipindi cha Criminal Investigation kinachorushwa hewani kupitia kituo cha "Zone Reality" ya DSTV.
 
Huyu ndugu ameshatutoka hata rudi milele, tujue nasi tupo njiani twamfuata.tukeshe tukiomba
 
yule afisa uhamiaji aliyekoswakoswa kuuwawa baada ya gari lake kupigwa risasi tano na kusema jeshi la polisi lilitaka kumuua makusudi hawezi kuwa anahusika?barlow alisema jamaa aliingia kwenye mtego wa polisi kwa kuonekana eneo la mtego kwa muda uleule na gari lilelile
 
Back
Top Bottom