Kifo cha RPC Mwanza: Maswali ya Bei Mbaya...

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,725
Wanamtandao,

Nimesoma thread ya mauaji ya RPC wa Mwanza, nikaamua kucopy maswali yote ya members kama yalivyo na kuyaleta hapa kama thread.

Naamini maswali haya ya wanajamvi yatasaidia kupata hadidu za rejea za watakaochunguza tukio hilo.

Ieleweke kuwa Memberz wa hapa ndani pia ni Polisi jamii.

(Naomba Mod usiunganishe na thread kuu)

1. Kwanini RPC asimwagize dereva kumpeleka dadake?
2. Kwanini asiende na walinzi wake?
3. Kama alikuwa na walinzi, Je walijeruhiwa au kufa? Walinzi walizidiwa?
4. Ukomo wa kazi wa walinzi wake ni saa ngapi?
5. Je kwenye gari walikuwa wawili tu?
6. Dada mtu ameumizwa?
7. Jina la huyo dadake ni nani?
8. Intelijensia haikunusa mauaji kabla?
9. Kwanini auwawe?
10. Kwanini isidhaniwe ni vinyongo ndani ya Jeshi la Polisi?
11. Polisi wamejuaje wauaji ni majambazi? Nani ana uhakika kauwawa na majambazi?
12. Walikuwa wanagombea demu?
13. Sijui ni wale waliompiga Hyness Kiwia!?
14. Kikao cha harusi hadi saa 8 usiku?
15. Majambazi gani wanaothubutu kumvamia RPC, na je walitaka kumwibia?
16. Wamempora nini baada ya mauaji?
17. Alikuwa na gari binafsi au ya serikali?
18. Alivaa uniform au kiraia?
19. Hakuna visasi nyuma?
20. Nani ana uhakika kauwawa na majambazi?
21. Kikao kilikuwa bar au nyumbani kwa mtu?
22. Kama aliwamulika majambazi, je ni yeye tu aliyepita hiyo njia?
23. Dada mtu alichukua hatua gani baada ya tukio?
24. Aliwaona wahusika?
25. Risasi alipigwa eneo gani la mwili?
 
kweli kwa maswali hayo Jf ni home of great thinker,aje kova atujibu maana naamini sio kila mwenye bunduki na risasi ni jambaz.je vipi kama aliuwawa na polisi akidhaniwa jambazi?
 
Nadhani umeleta maswali mazuri sana lakini hujaitendea haki heading yake. Imekaa kiutani zaidi.
 
Ingawa sijui lolote, akili yangu imekataa kuamini hiyo ni kazi ya majambazi. Kinachonisikitisha ni kuwa sasa hivi ni ngumu sana kujua kipi ni kipi maana almost kila kitu kimekuwa ndivyo sivyo.
 
Mimi kama nilivyochangia kwenye thread kuu, kuna mengi SANA yaliyojificha kwenye mauaji ya kamanda Barlow. Tuwaachie wahusika wachunguzane ingawa sote twajua kuwa the guy has gone forever.
 
wana kaz kweli kujitetea na dunia hii ya utandaazi hata ukificha jambo huwezi ficha lote,hata ukifanikiwa kuficha it will be the matter of time ukweli utakuwa wazi.
 
Hujaandika la kwangu Mpwa; Sheria inasema Bar zinafungwa saa tano usiku, kwa working days, Jana ni Ijumaa ni siku ya kazi, Bar ilifungwa saa ngapi? Kama sio saa Tano, yeye kama Kamanda alichukua hatua gani? au na yeye aliivunja sheria ile ile anayotakiwa kuilinda? Na kama Bar ilifungwa saa tano, yeye alikua wapi na huyo Dada yake had saa saba? Kizungumkuti
 
Duh haya bana hakimu anahukumiwa na hakimu mwenzake. Eeeeh wataona uchungu sasa ila kwa hapa bado kuna kakesi ka kujibu iweje hawajatoa picha,askari aliokuwa nao.
Wanasema wake za watu sumu

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
PakaJimmy nashauri upunguze hayo maswali angalau yabakie matano; 27 ni mengi sana na mengine yamejirudia
 
Last edited by a moderator:
je anayedaiwa kuwa dadake je ni dada kweli?
Je mke wake hausiki na mauaji haya kwa majibu ya upelelezi wa polisi kwamba mauaji yamesababishwa na wivu wa kimapenzi?
Je hawezi kuwa amejiua?...
 
Back
Top Bottom