Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
Maswali mazito ambayo Polisi wanatakiwa kuyafanyia kazi haya hapa;-
1."Kwa nini Deus Mallya alianza urafiki na marehemu hivi karibuni ndani ya wiki tatu au
nne na urafiki huo ukawa karibu kwa haraka namna hiyo?

2."Kwa nini Deus Mallya ndiye alikuwa anashinikiza hiyo safari ya usiku wakati watoto wa Chacha na mke wake walikuwa wanamshauri asisafiri siku hiyo usiku?

3.Ilikuwaje Deus ana shida na safari hiyo kuliko watu wengine wakiwemo marehemu mwenyewe na watoto wake na mke wake?

4."Kwa nini hapo awali Deus hakutaka ajulikane kwamba yeye ndiye alikuwa anaendesha
gari hilo.

5."Kwa nini Deus hajaeleza kuhusu huyo mtu wa tatu aliyeonekana kuwa pamoja
na waliopata ajali?

6."Kama huyo mtu wa tatu alitoweka baadaye kuonekana na waliofika katika eneo
la ajali alikuwa anakimbia nini?

7.Kwa nini Laptop ya Deus ambayo alikuwa anafanyia kazi zake nyingi ilitoweka baada ya ajali wakati simu na fedha zilikutwa katika eneo la ajali?

8."Je ni kawaida wananchi wa kawaida kuona kwamba ni muhimu kuchukua Laptop kuliko kuchukua simu na fedha?

9.Kwa nini Deus alidai kwamba waliondoka Dodoma saa 9 mchana wakati familia yake inajua kwamba waliondoka baada ya saa 12 jioni?

10.Kwa nini Deus hakutaka ifahamike kwamba waliondoka usiku?

Ili polisi wajivue lawamani inabidi wafanye uchunguzi kwa kufuata maswali hayo.
 
Polisi hawawezi kuchunguzwa kama serikali haijakubali.

Na hakuna atakayeweza kuomba uchunguzi zaidi ya familia ya marehemu....Chama chake labda wangeweza kuwa na ushawishi.. lakini walishamsimamisha.

Tumeshasahau ya Ballali ndugu zangu?

Si mlisema serikali haimuhitaji?

Sasa kama serikali ikisema haina haja na wachunguzi wa nje kwasababu haijaulizwa na wanafamilia...Si ni sawa tu na pale familia ya Ballali ilipokataa kutowa ushirikiano kwa kuiomba serikali ikubaliane na uchunguzi wa kifo chake kama ni kweli KAFA?

Ama mazingira ya uhitajikaji wa watu hao wawili kisiasa... yani wangwe na Ballali ni wa tofauti?

Wote si watu wanaotumiwa kisiasa kwa maslahi ya vyama hivyo pinzani vya ccm na chadema?
 
inawezekana mheshimiwa kilimba hausiki na malya au anakwepa kwa sababu ya hali aliyonayo mallya kwa sasa...ila hapo pana jambo linalokwepwa na ndo linaleta waswas na kutojiamini kwa mheshimiwa huyu.
 
Polisi hawawezi kuchunguzwa kama serikali haijakubali.

Na hakuna atakayeweza kuomba uchunguzi zaidi ya familia ya marehemu....Chama chake labda wangeweza kuwa na ushawishi.. lakini walishamsimamisha.

Tumeshasahau ya Ballali ndugu zangu?

Si mlisema serikali haimuhitaji?

Sasa kama serikali ikisema haina haja na wachunguzi wa nje kwasababu haijaulizwa na wanafamilia...Si ni sawa tu na pale familia ya Ballali ilipokataa kutowa ushirikiano kwa kuiomba serikali ikubaliane na uchunguzi wa kifo chake kama ni kweli KAFA?

Ama mazingira ya uhitajikaji wa watu hao wawili kisiasa... yani wangwe na Ballali ni wa tofauti?

Wote si watu wanaotumiwa kisiasa kwa maslahi ya vyama hivyo pinzani vya ccm na chadema?

Alafu sisi waTZ hivi tunakaougonjwa kakusahau nini imekuja hii ishu ya Chacha vyombo vyote vya habari na jamii kwa ujumla vimeamia huko.Ikija mpya tena hivyo hivyo mafisadi wanaendelea kutanua na mashangingi yao.
 
Guys,
Binafsi sioni tatizo la haki kwamba ipo tu kwa baadhi ya watu wenye wadhifa fulani..Hata Yule Saadam Hussein aliponyongwa nilishikwa na hasira, huruma na mchanganyiko wa kuona kwamba haki haikutumika..Kwa hiyo sii kweli kwamba maadam Chadema walisema Chacha Wangwe alikuwa na Njama za kukiua chama ama kumwondoa Mbowe haina maana alistahili kifo na kwamba viongozi wa Chadema wafurahie kifo hiki badala ya kulia kinafiki.

Huyu kijana kusema kweli anaweka mashalka makubwa sana tena mimi baada ya kuona maelezo ya baba yake ndio kwanza nimezidi kumhofia zaidi..Huyu kijana alipomaliza shule ya msingi alihamia dar na akaweza kujisomesha jambo ambalo baba yake hafahamu aliweza vipi.. anachofahamu ni kwamba mwanae kajifunza mambo ya Komputa na msanii mzuri tu ktk uchoraji!..(hii ndio kamba kubwa ya majasusi wote kwa familia zao) Kama kweli huyu kijana alikuwa mchoraji iweje awe ktk msafara wa viongozi tena Ulaya Zurich ambako inasemekana aliacha pasi yake ndani ya ndege!..Yet, aliweza kubadilisha ndege kuendeklea na safari.. mhhhh!Aliweza vipi kuunganishwa na msafara huo kisha basi tunaambiwa tena alikwenda hadi Libya na baadhi wabunge hawakufahamu sababu ya huyo kijana kuwepo ktk msafara huo!..Hii ina maana aliweza kuingia Libya na kutoka bila pasi halafu akashuka Nairobi kukutana na sijui mtu gani kabla hajarudi Dar... Hee jamani kweli huyu mtu wa kawaida kama Mkandara hapa!

Kweli wazee hii imekaa sawa kwenu?

nadhani ktk hiyo safari pia alikuwa anamtafuta mtu hapo ili ambalalli ila nadhani alimkosa..... sikilizia sasa kesiyake itakavo kufa kwa danadana... kwani wale waommwagia tindikali kubenea si ndo dizain hizi hizi tuu
 
Alafu sisi waTZ hivi tunakaougonjwa kakusahau nini imekuja hii ishu ya Chacha vyombo vyote vya habari na jamii kwa ujumla vimeamia huko.Ikija mpya tena hivyo hivyo mafisadi wanaendelea kutanua na mashangingi yao.

Kwa kifupi hoja ya wachunguzi wa nje inatakiwa kupigiwa kelele na wanafamilia na siyo sisi hapa jf!
Mimi nilipingwa hapa niliposema uchunguzi wa kifo cha Ballali ufanywe na FBI...Wakabisha watu hapa especially ndugu wa Ballali wakiongozwa na jasusi....Na mimi kuendlea kuuliza kulisababisha chuki sana ambayo bado ipo kiaina...Sasa ndio maana nilishasema huwa sipendi double standard....MIMI NAPENDA FAIRNESS...FITNA KWANGU MWIKO!
 
Maswali mazito ambayo Polisi wanatakiwa kuyafanyia kazi haya hapa;-

1."Kwa nini Deus Mallya alianza urafiki na marehemu hivi karibuni ndani ya wiki tatu au
nne na urafiki huo ukawa karibu kwa haraka namna hiyo?

2."Kwa nini Deus Mallya ndiye alikuwa anashinikiza hiyo safari ya usiku wakati watoto wa Chacha na mke wake walikuwa wanamshauri asisafiri siku hiyo usiku?

3.Ilikuwaje Deus ana shida na safari hiyo kuliko watu wengine wakiwemo marehemu mwenyewe na watoto wake na mke wake?

4."Kwa nini hapo awali Deus hakutaka ajulikane kwamba yeye ndiye alikuwa anaendesha
gari hilo.

5."Kwa nini Deus hajaeleza kuhusu huyo mtu wa tatu aliyeonekana kuwa pamoja
na waliopata ajali?

6."Kama huyo mtu wa tatu alitoweka baadaye kuonekana na waliofika katika eneo
la ajali alikuwa anakimbia nini?

7.Kwa nini Laptop ya Deus ambayo alikuwa anafanyia kazi zake nyingi ilitoweka baada ya ajali wakati simu na fedha zilikutwa katika eneo la ajali?

8."Je ni kawaida wananchi wa kawaida kuona kwamba ni muhimu kuchukua Laptop kuliko kuchukua simu na fedha?

9.Kwa nini Deus alidai kwamba waliondoka Dodoma saa 9 mchana wakati familia yake inajua kwamba waliondoka baada ya saa 12 jioni?

10.Kwa nini Deus hakutaka ifahamike kwamba waliondoka usiku?

Ili polisi wajivue lawamani inabidi wafanye uchunguzi kwa kufuata maswali hayo.

Pia kuangalia possibilities nyingine nyingi tu. 'Actors' hapa ni wengi.
Hayo maswali unaweza kujiuliza pia baada ya kumwondoa Mallya miongoni mwa suspects.

.
 
Iweje yeye Mwenyekiti anatumia gari la kifahali ( Vogue ) na kuzunguka nchi nzima na hellicopter wakati Makamu wake wa Mwenyekiti anapanda Corolla limited E100 mbovu inapita ikichomoka matairi ovyo na kupelekea kifo cha Kiongozi mkubwa wa chama.

Tofauti ya maisha kati ya kibopa huyu na mh ni kubwa mno, napata wasiwasi na utawala ndani ya chama.

Hali hii ilijitokeza kati ya John Garang na Kiir Mayadit, ilisababisha Kiir kuhamia rikwamba na kumwacha Garang Juba. Wakati watoto wa Garang wanasoma ulaya, familia ya kiir ilikuwa Nairobi mtaa wa Langata kwenye nyumba ya kupanga.

Makamanda wa SPLA walikuwa kipenzi cha Kiir, wakaona isiwe tabu wakamshusha Garang. Hali hii ndo maana Wangwe aliamua kupambana na kibopa waziwazi.

Launt Kabila yalimkumba yaleyale, alivyotinga Kinshasa aliwaona kadogoo hawana maana akaanza madili ya ajabuajabu, mlinzi wake nambamoja Rashid Kasereka akaamua kumfutilia mbali.

Nani ajuaye labda Mallya (kadogoo, chokoraa, kuleana) alizurumika hela ya fulana? akaona isiwe tabu naanza na huyu huyu! (kama kweli kahusika.) kwanini wanachachawa nae wakati ni mtu wao, komu anamjua! mnyika hamjui! Kibopa kimya!

Kama kweli mh angekufa kisiasa basi muuaji asingepatikana kama muuaji wa ouko, tom mboya, olaf palme. au angejaribu kutoroka kama Rashid Kasereka na kuishia kupigwa risasi nayeye!

Ukweli tatizo liko kwenye administration ya chama, tusitafute sababu za kisiasa.
 
Makamba alikutana na Wangwe kikao cha faragha aseme walikubaliana nini ama walitofautiana nini?

Mkuu,

Hata Rostam Aziz ahojiwe maanke amekua akihusishwa sana na mgogoro huo.Nakubali,CHADEMA nao wahojiwe na polisi pia kuhusiana na hii ishu na vile vile CCM wahojiwe maanke hawa ndiyo wanaoonekana wako katika position nzuri na maelezo yenye kulisaidia jeshi la polisi.Hapa tunataka fair play
 
Iweje yeye Mwenyekiti anatumia gari la kifahali ( Vogue ) na kuzunguka nchi nzima na hellicopter wakati Makamu wake wa Mwenyekiti anapanda Corolla limited E100 mbovu inapita ikichomoka matairi ovyo na kupelekea kifo cha Kiongozi mkubwa wa chama.

Wee Eddy,
Hivi unajua DONGE la ubunge kwa mwezi likoje? Si hawa nasikia wanatamba na MASHANGINGI? Hata mie hili linanipa shida. Niliona hata Mwakyembe akiingia kwenye gari ndogo kama hiyo ya Wangwe. Sasa ukweli uko wapi? Wabunge siku hizi hawapati MASHANGINGI? Je kwa kipato chao cha ubunge na marupurupu, haitoshi kwao kupata gari zuri tu la kufanyia kazi? Au ndiyo kubana matumizi maana nasikia sijui ana watoto 12?
 
Iweje yeye Mwenyekiti anatumia gari la kifahali ( Vogue ) na kuzunguka nchi nzima na hellicopter wakati Makamu wake wa Mwenyekiti anapanda Corolla limited E100 mbovu inapita ikichomoka matairi ovyo na kupelekea kifo cha Kiongozi mkubwa wa chama.

Tofauti ya maisha kati ya kibopa huyu na mh ni kubwa mno, napata wasiwasi na utawala ndani ya chama.

Hali hii ilijitokeza kati ya John Garang na Kiir Mayadit, ilisababisha Kiir kuhamia rikwamba na kumwacha Garang Juba. Wakati watoto wa Garang wanasoma ulaya, familia ya kiir ilikuwa Nairobi mtaa wa Langata kwenye nyumba ya kupanga.

Makamanda wa SPLA walikuwa kipenzi cha Kiir, wakaona isiwe tabu wakamshusha Garang. Hali hii ndo maana Wangwe aliamua kupambana na kibopa waziwazi.

Launt Kabila yalimkumba yaleyale, alivyotinga Kinshasa aliwaona kadogoo hawana maana akaanza madili ya ajabuajabu, mlinzi wake nambamoja Rashid Kasereka akaamua kumfutilia mbali.

Nani ajuaye labda Mallya (kadogoo, chokoraa, kuleana) alizurumika hela ya fulana? akaona isiwe tabu naanza na huyu huyu! (kama kweli kahusika.) kwanini wanachachawa nae wakati ni mtu wao, komu anamjua! mnyika hamjui! Kibopa kimya!

Kama kweli mh angekufa kisiasa basi muuaji asingepatikana kama muuaji wa ouko, tom mboya, olaf palme. au angejaribu kutoroka kama Rashid Kasereka na kuishia kupigwa risasi nayeye!

Ukweli tatizo liko kwenye administration ya chama, tusitafute sababu za kisiasa.

mkuu wangu,umechambua na kuainisha hoja yako vizuri sana .Lakini naomba kutofautiana na wewe.Nikuulize swali moja,Je Range Rover analotumia Mbowe ni la kwake ama ni la Chama?

Je,Corrola ya wangwe n i yake ama ni Ya CHAMA?

Tofauti za kimaisha zilitokana na background ya kila mmoja kabla hawajaingia kwenye siasa.Na hilo sio Tatizo hata kidogo
 
Wee Eddy,
Hivi unajua DONGE la ubunge kwa mwezi likoje? Si hawa nasikia wanatamba na MASHANGINGI? Hata mie hili linanipa shida. Niliona hata Mwakyembe akiingia kwenye gari ndogo kama hiyo ya Wangwe. Sasa ukweli uko wapi? Wabunge siku hizi hawapati MASHANGINGI? Je kwa kipato chao cha ubunge na marupurupu, haitoshi kwao kupata gari zuri tu la kufanyia kazi? Au ndiyo kubana matumizi maana nasikia sijui ana watoto 12?

Na wake watatu.Hivi kweli hili nalo lilikua ni tatizo la kumsingizia mtu au Chama?
 
Wee Eddy,
Hivi unajua DONGE la ubunge kwa mwezi likoje? Si hawa nasikia wanatamba na MASHANGINGI? Hata mie hili linanipa shida. Niliona hata Mwakyembe akiingia kwenye gari ndogo kama hiyo ya Wangwe. Sasa ukweli uko wapi? Wabunge siku hizi hawapati MASHANGINGI? Je kwa kipato chao cha ubunge na marupurupu, haitoshi kwao kupata gari zuri tu la kufanyia kazi? Au ndiyo kubana matumizi maana nasikia sijui ana watoto 12?

Sikonge,

Mwakyembe ana shangingi labda kama uliloliona lilikuwa gari la pili. Sijui ni gari model ipi maana mimi sio mpenzi wa magari ila ni gari kubwa 4W.

Zitto aliwahi kuandika hapa, kama sikosei ni kama wanapewa 20M bure, pesa zingine wanakopeshwa na pia hakuna tax.

Walio wengi wanatumia hizo pesa kulipa madeni ya kuhonga kupata uheshimiwa na kuimarisha nyumba zao au kuoa mke mwingine.

Binafsi siungi mkono hizo pesa kutumika kununulia magari waheshimiwa. Laiti zingewekwa kusaidia vijana kupata ajira na kujiajiri, zingelikuwa na faida zaidi kwa nchi.

Wabunge wana mishahara yao, kwanini wasikope magari kwa kutumia hiyo mishahara yao kama wafanyakazi wengine?
 
Huu ndio ugonjwa nchini kwetu, professionals hawalipwi vizuri, matokeo yake wote wanakodolea macho ubunge badala ya kudeliver kwa maendeleo ya nchi. Maprofessor wanaacha kufundisha, madakari wanaacha kutibu, walimu wanaacha kufundisha, wanakimbilia kwenye the most highly paying job without sweating, just for sleeping you get a lot of money. Lobbyist and most business people they get into it to get close to ministers for winning insider deals like fake contracts we've seen recently. We've to change this vision for our political system.
 
Shadrack Sagati
Daily News; Wednesday,August 06, 2008 @00:01

Habari nyingine
Vyuo vikuu vifunze uzalendo-KKKT
Miradi Ziwa Tanganyika kuanza Novemba
Veta Mikumi wavumbua ufuaji umeme kwa betri
Watoa taarifa Polisi waombwa wasijisifu
DC aomba benki kuwapatia mabilioni ya JK
Ataka Serikali imsimamishe mkandarasi
Kivuko kipya Pangani kuletwa Mei
Wagombea kutolazimishwa kupima Ukimwi
Sabco laua Mbeya
Kortini kwa kughushi milioni 969/- za Citi Bank

Familia ya aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, imesema inahisi ajali ya gari iliyosababisha kifo cha ndugu yao ilikuwa ya kupangwa. Taarifa ya familia iliyotolewa na Profesa Samwel Wangwe kwenye Jukwaa la Wahariri jana Dar es Salaam, ilisema kuwa chanzo cha ajali iliyosababisha kichwa cha marehemu kupasuka zaidi ya mara moja bado kina utata mkubwa, kama ajali hiyo ilipangwa au ilikuwa ya kawaida.

“Pia kuna utata kama ajali iliyopasua kichwa cha ndugu yetu ilitokea pale katika eneo la ajali au kabla,” ilisema taarifa hiyo na kusisitiza kuwa familia ina mashaka na chanzo cha ajali kutokana na taarifa mbalimbali zinazopingana, hasa zinazotolewa na Deus Mallya na baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio.

“Hali hiyo inastahili uchunguzi wa kina.” Wangwe alifariki Julai 28 baada ya kupata ajali mkoani Dodoma wakati anaelekea Dar es Salaam. Mallya aliyekuwa pamoja na marehemu, alinusurika katika ajali hiyo. Profesa Wangwe alisema familia imejiuliza maswali kadhaa kati yake ni “Kwa nini Deus Mallya alianza urafiki na marehemu hivi karibuni ndani ya wiki tatu au nne na urafiki huo ukawa karibu kwa haraka namna hiyo?

“Kwa nini Deus Mallya ndiye alikuwa anashinikiza hiyo safari ya usiku wakati watoto wa Chacha na mke wake walikuwa wanamshauri asisafiri siku hiyo usiku? Ilikuwaje Deus ana shida na safari hiyo kuliko watu wengine wakiwemo marehemu mwenyewe, watoto wake na mke wake? Pia familia imeendelea kuhoji,

“Kwa nini hapo awali Deus hakutaka ajulikane kwamba yeye ndiye alikuwa anaendesha gari hilo...kwa nini Deus hajaeleza kuhusu huyo mtu wa tatu aliyeonekana kuwa pamoja na waliopata ajali? Wanafamilia hao pia wameendelea kuhoji, “Kama huyo mtu wa tatu alitoweka baadaye kuonekana na waliofika katika eneo la ajali alikuwa anakimbia nini?

Kwa nini Laptop ya Deus ambayo alikuwa anafanyia kazi zake nyingi ilitoweka baada ya ajali wakati simu na fedha zilikutwa katika eneo la ajali? “Je, ni kawaida wananchi wa kawaida kuona kwamba ni muhimu kuchukua Laptop kuliko kuchukua simu na fedha? Kwa nini Deus alidai kwamba waliondoka Dodoma saa 9 alasiri wakati familia yake inajua kwamba waliondoka baada ya saa 12 jioni?

Kwa nini Deus hakutaka ifahamike kwamba waliondoka usiku? Kutokana na maswali hayo, familia imesisitiza kuwa ajali hiyo inastahili ifanyiwe uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli. “Inawezekana kabisa si ‘reckless driving (uendeshaji wa kizembe)’ peke yake.” Wanafamilia pia wameahidi kufuatilia na kushirikiana na polisi katika upelelezi huo ili kubaini ukweli wa chanzo cha ajali hiyo.

Imewaomba raia wote wenye taarifa yoyote kuhusu uhusiano kati ya Mallya na marehemu Chacha na wengine watoe habari kwa polisi ili kusaidia katika upelelezi huo. Familia hiyo imesema uchunguzi uliofanywa na madaktari matokeo yake hayajatoka, kwani inachukua muda kufanya uchambuzi kamili wa kile ambacho mtaalamu alikiona katika uchunguzi wa mwili wa marehemu.

Profesa Wangwe alisema familia inaamini kwamba matokeo hayo yakitolewa yatakuwa kielelezo kimojawapo katika vielelezo vitakavyotumiwa na polisi katika upelelezi wa kifo cha ndugu yao. Wangwe alisema walilazimika kutoa taarifa kuwa mwili haukukutwa na risasi, kwani kabla hata uchunguzi huo kukamilika tayari yalikuwapo maneno yaliyozagaa mjini Tarime kuwa alikutwa na risasi mbili kichwani.

Alisema katika hali hiyo wawakilishi wa familia waliamua kwamba ilikuwa vema kutoa tamko la awali kutokana na kile walichoshuhudia pale hospitalini Tarime ambapo uchunguzi wa mwili wa marehemu ulifanyika. Wakati huo huo, viongozi wa vyama vya upinzani, Joseph Mbatia wa NCCR-Mageuzi, Augustine Mrema wa Tanzania Labour (TLP) na Profesa Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi (CUF), jana wamewasilisha kile wanachodai ushahidi kuhusu utata wa ajali hiyo na nyendo za Mallya.

“Tumewasilisha kwa Kamishna Chagonja (Paul) kwani ndiye anayekaimu ukuu wa polisi,” alisema Mbatia. Katika hatua nyingine, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Tarime kimesema wakati wa msiba wa Wangwe kulijitokeza kikundi cha wahuni waliotokea Musoma mjini kwa lengo la kufanya fujo.

My Take:

Watu wa Chadema Tarime wanajuana. Maneno ya Kiranja siku ile yaweza kuwa na ukweli kuwa kikundi hicho kilipangwa toka awali.
 
Jamani this is interesting, mi naomba PROF. LIPUMBA TAFADHALI ADHIBITISHA KAULI YAKE DHIDI YA MALYA...!

Ujasusi wa mallya watega kitendawili.

na Edward Kinabo, Tanzania DAIMA

SERIKALI ya Libya imesema haifundishi ujasusi na wala haijawahi kutoa mafunzo hayo kwa Deus Mallya, anayedaiwa kuendesha gari lililokuwa limembeba aliyekuwa Mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe (CHADEMA).

Hayo yalisemwa jana na Balozi wa Libya nchini Tanzania, Dk. Ahmad El Ash Hab, alipohojiwa na Tanzania Daima kwenye ofisi za ubalozi huo, zilizopo Upanga, Mtaa wa Kilombero, jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo inatokana na madai yaliyotolewa hivi karibuni na viongozi wakuu watatu wa vyama vya upinzani, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Augustine Mrema (TLP), kuwa Deus Mallya ni jasusi aliyefuzu mafunzo hayo nchini Libya, ambayo yanahatarisha usalama wa taifa.

Alisema Libya ina vituo mbalimbali vya elimu na vyuo vikuu, ambavyo vinafundisha fani mbalimbali zenye manufaa kwa jamii na haina kituo wala chuo kinachofundisha ujasusi.

“Sisi tuna vituo na vyuo vikuu kwa ajili ya kuandaa wataalamu wa fani mbalimbali zenye manufaa kwa jamii na wala hatuna vituo vya kufundishia ujasusi,” alisema.

Balozi huyo alisema Libya inaheshimu wanasiasa wote hapa nchini, mfumo wa siasa uliopo na viongozi wake, na hasa uongozi wa Rais Kikwete na inaheshimu pia uhuru wa vyombo vya habari na sheria inayolinda uhuru huo hapa nchini.

Kutokana na hali hiyo, alisema ni vyema kila mtu anapotumia uhuru huu, awe mkweli na makini, badala ya kusema na hata kufikia hatua ya kuchafua mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Libya na Tanzania.

Alisema kwa kipindi kirefu sasa, uhusiano wa Libya na Tanzania katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii, umezidi kuwa mzuri na wenye manufaa na kwamba Libya haitakubali kuona mtu yeyote anaingilia kati na kutoa kauli zinazochafua uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili.

Alisema kwa kuwa wanasiasa hao wameahidi kupeleka ushahidi wao katika vyombo vya usalama, na kwa kuwa suala lenyewe bado lipo chini ya uchunguzi wa vyombo hivyo, Libya itabaki ikisubiri kukamilika kwa uchunguzi huo kabla ya kuchukua hatua zinazostahili.

“Kwa kuwa jambo hili lipo kwenye uchunguzi, sisi hatuoni haja ya kutangulia kutoa hukumu, tunasubiri vyombo vya usalama vikamilishe kazi yake, ndipo tutachukua hatua zinazostahili,” alisema.

Akizungumzia uhusiano uliopo baina ya nchi yake na Tanzania, alisema Libya imekuwa na ushirikiano mzuri na Tanzania katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu, uchumi, na mazingira.

Alisema mathalani Libya na Tanzania zimekuwa zikibadilishana wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na kuna wanafunzi wengi kutoka Tanzania wanaosoma nchini humo, huku wa kwao wakiwapo hapa nchini wakijifunza Kiswahili.

Mrema, Lipumba na Mbatia, mwishoni mwa wiki walikuwa na mkutano na vyombo vya habari, ambapo walidai Mallya ni jasusi aliyepata mafunzo nchini Libya.

Viongozi hao waliahidi kutoa ushahidi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom