Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
inaweza kuthibitisha kwa kuwa wangwe ndiye aliyewapa(nionavyo).Mpaka kieleweke si alisema marehemu Wangwe alishawahi kukutana na RA pale Kempski?



Waraka uligeuzwa?ina maana wewe unao ule ambo haukugeuzwa?sheria ya TISS ya 96 inasemaje?on both sides as Zitto said it can also apply to CHADEMA..

Unajua Mjadala wa Suala la Wangwe tuliuanzisha sisi hapa JF,na itabidi tuamallize siye wenyewe.Mwanakijiji aliuanzisha na tena akauandikia katika makala ya Gazeti.

Mzee inabidi umalize tu kesi uliyoianzisha


Tangu jana ulipokiri kuwa wewe ni mtu wa CCM sitashangaa unapotetea hapa na kuandika kuwa ni sahihi kwa CCM kuwa na waraka huo na kuusambaza siku moja kabla ya kifo chake, tena unasambazwa kwa makatibu wa CCM nchi nzima.

Pili,hao CCM wanapaswa kujitoa humo walimo kwani kama leo wanamuona Wangwe kama hero wao ,basi kuna mambo mengi huwa wanafanya kuliko haya machache ambayo yanaanza kuonekana ,wanafiki mwisho wao ni kupata aibu na kuumbuka , ona sasa MACCM YANAVYOUMBUKA ,KUMBE NDIVYO YALIVYOOOOOOO....
 
Malya ni jasusi au ni muuaji?

Swali lako Icadon ningelipenda kujibu kama Mallya awe ni muuaji ama jasusi, wote ni wauaji tu. At the end hata jasusi huhakikisha ANAUA. Huyu Mallya tunamuita JASUSI kwa sababu zaidi ya kuua alikofanya lakini ni Jasusi kwa mbinu alizotumia ukizingatia ameacha kiwingu cha maswali namna alivyofanikisha mauaji hayo.
 
Kweli ni ajali ya kawaida, lakini pia lazima ijulikane huyo Mallya alikuwa na role gani? na mbona maelezo yake ni ya kujikanaanya!? na uhusiano wake na Wangwe ulikuwa wa nini? Hivyo ni vitu muhimu watu kujua..
 
Ina maana hawa mafisaid bado wan ngvu kubwa kiasi hiki mpaka leo?Umekubali wana uwezo wa kufanya watakavyo.Wameweza hadi kuugeuza?

basi unajua waraka wa Madini aliouacha Wangwe..wameugeuza in maana wewe una huo waraka wa Madini.na kwa maneno ya Zitto


sasa CHADEMA ni ndugu wa Wangwe kwa seria ipi?wewe umeutoa wapi?kama na zitto atakuwa nao huo ambao umegeuzwa basi na yeye atashitakiwa kwa sheria hii..tunauzunguka Mbuyu


NB:Mie ni mkabila ndiyo,ila nimejifunza tabia hii kutoka kwa wachaga![/QUOTE]


Mkuu

sasa ukome kuwatishia watu na masters yako ambayo haikusaidii kufikiria,zitto aliinukuu hiyo sheria ya Usalama wa Taifa 1996,kisha akasema Inakuwaje CCM ambayo haina uhusiano wa Kindugu au hata wa KIITIKADI wawe na waraka huo? Suala la CHADEMA kuwa nao lina uhusiano wa Kiitikadi kati ya Wangwe na CHADEMA.Sasa wewe umeshakurupuka na Kuropoka. Hata form 4 leaver anweza kuielewa kabisa bila wasiwasi.Umeniacha na mshangao na usomi wako.

Kuhusu ukabila,Mkuu kama wewe ni Master's holder unaongea shallow namna hii,tutegemee nini kutoka kwa walimu wa primary school ambao ndiyo tuliowapa jukumu zima la kulea wadogo zetu na kuwafundisha kuwa ukabila,udini na ubaguzi wa rangi ni mbaya? Kama huna cha kuandika hapa ni bora ukae kimya ili watanzania tuishi kwa amani kuliko wewe msomi kutumika kama kio cha jamii kinacholeta uchochezi wa kikabila.

However,bado ninaheshiu michango yako mingi inayojenga jamii yetu ya kitanzania
 
Na ndio maana nikasema inaweza kuhamia kwenye Uislam na ukristo...Na pia nilitowa msisitizo kuwa Deus Mallya sijui ni kivipi alikubaliwa na mke wa KATI.
Na ni nani alimuunganishia marehemu na mke huyo mwarabu?
Maana mh Rais na yeye si ana mke mwarabu?
Ndugu zangu USALAMA WA TAIFA HAUPO TENA...Na ninasema kuwa kama hakuna wazalendo wa kweli ambao hawataki kuliingilia hili swala kati...Basi kuna shida!
Ni wazi usalama umegawanyika kama nilivyosema awali na inawezekana group baya la wanausalama mafisadi limemtumia agent wao ili kufifisha juhudi za wale wanausalama safi.

Shida iko hapo....TUNAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA SANA KWENYE USALAMA WETU WA TAIFA!
Hii si njia sahihi kabisa....Mwiran,mchina na mrusi vs m west....Kazi iko!

Watakaolikomboa Taifa ni TRUE BANTU...WAKISHIRIKIANA NA WALE WENYE NIA NZURI BILA KUJALI RANGI ZAO WALA DINI ZAO!

Rastafarianism nayo naona itapata UMAARUFU SANA...Kwani wao hawataki kugawanya na mwarabu wala mzungu!

Kuna kazi ngumu sana na huyu JMushi, naona sasa post zake nitakuwa naziruka bila kuzisoma. Sijui kama wengine pia wanatatizika naye kiasi hiki.
 
wa kweli Makamba inabidi ilisaidie jeshi la polisi.Hata hao wenyeviti wa mikoa na wilaya waliopokea hizo nyaraka inabidi wasaidie polisi kwamba wao walizipataje kama makamba kadai hakuuuona huo waraka.

Lazima tujue interest ya CCM na wasambazaji wa waraka huo,na hili la makamba kudai ni wapenzi wa Wangwe ndiyo wanaohuika basi bado ana nafasi kubwa wa kulisaidia jeshi la polisi maanake inaonkana anawafahamu na kama anawafahamu lazima wana uhusiano na CCM,Makamba pamoja na wangwe.Hawa wana msaada mkubwa kwa jeshi la polisi
 
Makamba alikutana na Wangwe kikao cha faragha aseme walikubaliana nini ama walitofautiana nini?
 
what has this got to do na TRUE BANTU? ......unataka kutwambia mwenye tone la damu ya mchanganyiko hafai kuleta mabadiliko tanzania?

ningekuomba uache ku generalize watu.
 
. Kwa habari za kipaparazi ni kuwa Mallya alikwenda Libya kwenye mkutano wa siku tatu na alikwenda pamoja na mufti shaban simba na wabunge wa CCM. ulikuwa mkutano wa kujadili kuunganisha Afrika tu.

Nitafuatilia zaidi kujua nini kimewafanya viongozi watatu wa upinzani waliobaki wenyewe Tarime kuja na hadithi hiyo.
PM

shaban simba -kiongozi wa kidini

wabunge wa CCM-viongozi wa kisiasa


MAllya-----------

how come hii kombo imeenda kujadili kuunganisha Afrika tu.

kama unafatilia uwepo waviongozi tarime, sasa nataka ufatilie na utupe majibu yenye akili kuhusu hii Combo

haijakaa sawa


watu wameamka
 
nashindwa kuelewa hili suala unataka kulifikisha vipi kwenye dini jmushi!

kwa kuwa RA muajemi basi ni muislam na kama ni muislam basi "kamuua" wangwe kwa propaganda za kiislam?!!

sikudhani kama mtu hapa JF atakuwa na upeo mdogo wa kufikiri kama huu!
 
Wanabodi,
Natanguliza samahani mbele ya haya nitakayo yasema kwa sababu sina hakika kama yamekwisha zungumziwa.
Moja ni kuhusiana na Prof Wangwe ambaye inaonyesha kabadilisha msimamo wake kuhusiana na kesi hii, limewatatiza wengi lakini wameshindwa kufahamu kwamba hata Vyombo vya Usalama kama Polisi wanaweza kubadilisha msimamo kulingana na ushahidi unavyo zidi kupatikana. Mkisiwa wa kwanza akawa huru, na mtu mwingine kabisa nje akavutwa ndani kama mhusika maadam file halijafungwa. Na hata kama limefungwa linaweza kufunguliwa upya na madai mapya kabisa yakatokea!. Hii haina maana Polisi ni wajinga kufikia uamuzi wa kwanza.

Nikirudi ktk sakata hili la wangwe nimesoma mahala wanabodi wakihoji hoja ya wangwe ambayo ilikuwa iwakilishwe bungeni.. Ukweli ni kwamba ninavyofahamu mimi mbunge yoyote anayetaka kuwakilisha hoja huipeleka kwa Spika ili apatiwe ruksa na hupitiwa kuangalia nafasi yake, uzito wake na kadhalika. Kisha mbunge hujulishwa kwamba hoja yake itasimama. kama mnakumbuka vizuri Dr. Slaa alipeleka hoja ya BoT bungeni ikakataliwa au kwa namna fulani alishtuka yeye kwamba haiwezi kukubaliwa. Zito pia (kama sikosei ama mbunge fulani) kuna sehemu kama nakumbuka vizuri alihoji kuhusiana na swala moja ambalo halikuwa ktk hoja yake ya awali (inayotambuliwa na spika) kiasi kwamba ilitolewa nje hali uzito wake ulikuwa mkubwa... sasa basi kama Wangwe alikuwa na hoja ambayo alitaka kuiwakilisha bungeni kuna uwezekano mkubwa kuwa spika ameisha ipata, lakini hapo hapo kwa kutumia njama CCM wanaweza kabisa kuibadilisha na kuweka hoja tofauti kwa sababu sio lazima Chadema wafahamu hoja ya Wangwe ambayo ilikuwa inawakilisha jimbo lake kama mbunge wa Tarime..Nasema hivi kwa sababu wapo wabunge wa CCM ambao huingiza hoja kuuliza viongozi wa wizara fulani bila viongozi hao kuwa na taarifa za hoja hiyo nje ya bunge.
Hakuna kiongozi wa CCM aliyejua kwamba mama Kilango angeuliza swali kuhusiana na Mafisadi wa EPA kabla ya bunge kuanza ila kuna uwezekano watu wa karibu naye iwe ndani ya CCM, ama marafiki wanaweza kuwa nataarifa hiyo kutokana na ukaribu wao kwa mtoa hoja...
Hofu yangu kubwa isije kuwa CCM wakaunda FITNA na kusema kwamba hoja ya Wangwe inahusiana na Mbowe wakati swala na matatizo ya ndani ya chama cha Chadema huwasilishwa kwa wanachama wa chama hicho wazee, ama viongozi wa chama na sio bungeni..
Kwa hiyo tuwe macho tuelewe kwamba hapa CCM wanaweza kusuka FITNA na dalili zimeshaanza kujitokeza kiasi kwamba mimi hapa najiuliza ilikuwaje CCM wawe na nakala za malalamiko ya Wangwe kuhusiana na viongozi wa Chadema hali marehemu alisema anapeleka kesi hiyo kwa wanachama na hata ikibidi kufika Mahakamani atakwenda kupata haki yake.. hapo hapo tunaelewa wazio kwamba laptop yake ilipotea ama kuibiwa!...
I mean guys kweli hapo kijijini kibaka aibe laptop na kuacha simu za mkono..Of all the thing -laptop ndio ya kwanza kuondoka na huyu Mallya mbali na msukosuko wa ajali aliweza kufahamu kwamba laptop imechukuliwa na vibaka..
Muda gani alikuwa nao kutazama vitu vilivyoibiwa na ashindwe hata kuwafukuza wezi kwa sababu hakuwa na jeraha, alitoka mzima hana hata vumbi!..
Guys something is very wrong!...Ndivyo hata FBI huunda kesi zao jamani tusifikirie tu kwamba hii ni ajali na Mungu ndiye aliyepanga....Basi kama ni kweli Mungu ndiye aliyepanga (mawazo yalifungana na Utumwa wa akili) inakuwaje Mungu huyo huyo amhukumu moto wa Jahanam muuaji hali ni yeye aliyepanga kifo hicho sio muuaji?..
Guys Mungu katupa uwezo wa kuchagua kati ya mema na mabaya.. ni uchaguzi wetu sisi wenyewe ktk kila matendo yetu.. na yeye hujalia mema au mabaya kutokana na maombi yetu wenyewe kufanikisha azma zetu..Shetani ambaye ni nafsi za ubaya wa binadamu hutuangamiza sisi wenyewe hakuna mkono wa Mungu ktk mema ama mabaya na ndio maana tutahukumiwa kwa kila tuliyoyafanya(if you believe in judgement day..).Hii ni imani yangu mimi binafsi..

Mkuu, wangu Mkandara,

Maneno yako ni mazito sana .Kwa kweli hapamJF tuna vichwa.Keep up the same spirit bro.

BTW. Sidhani kama Makamba ataweza kujinasua kwenye hili sagga. Pia kuhusu jimbo la Tarime nahisi CCM wanataka kujiandaa kwa kuwayumbisha yumbisha opposition ili wao wanyakue hilo jimbo kwani hilo ndiyo lengo lao kuu maanke hata Marehemu alishawahi kulalamika kipindi fulani hivi.

suala la Kaka wa marehemu kutakiwa kama lulu na upinazani au CCM ni ajenda nyingine maanake yeyote atakayemsimamisha basi itategemea na jinsi wanatarime wanavyomfikiria huyu bwana
 
CHADEMA wana undugu na wangwe?


Gembe huyoooooooooooooo!!!!!!!

Mkuu
"Zitto aliinukuu hiyo sheria ya Usalama wa Taifa 1996, kisha akasema Inakuwaje CCM ambayo haina uhusiano wa Kindugu au hata wa KIITIKADI wawe na waraka huo? Suala la CHADEMA kuwa nao lina uhusiano wa Kiitikadi kati ya Wangwe na CHADEMA.
 
Originally Posted by Gembe
Kwa taarifa yako tu,

Mie siyo mtu wa Rostama ila ni mtu wa CCM.
 
nimezungumza na anton komu, mkurugenzi wa chadema, ambaye amehojiwa na polisi jana kuhusu kijana mallya, anchoeleza ni kuwa mallya ni mbangaizaji, misheni town. yeye alikuwa anshinda pale chadema kama mbangazizaji, na akabahatika kwenda kwenye hiyo tripu ya libaya. namna alivyoweza kuwa karibu na wangwe ni kama viongozi wengine wanavyojipatia wapambe. kwa kadiri mnavyomkuza huyu kijana ni kadiri muda ambao ni dhahabu unapotea bure.

huyu pia ni mkazi wa huko manushi kibosho, ni mbangaizaji kwenye ile dizaini ya kutumwa kabandike matangazo ya mkutano, maara kakodishe kipaza sauti n.k
anton komu 0713 615603
 
Nendeni pg.179 huyu Gembe ndio alisema kuwa yeye sio wa ROSTAM ilka ni wa CCM na alisema wakati akilumbana na KIRANJA.

Gembe ,kama ulivyosema jana kuwa wewe una MASTERS DEGREE, kumbuka kuwa maandishi yanadumu milele, hayafutiki.

Sasa naona leo unageuza kibao kuwa hata CHADEMA ziko mbili kama CCM,hilo halihitaji kusemewa na mtu wa CCM kama wewe ,linapaswa kusemwa na mtu wa CHADEMA , kama wewe ulivyo wa CCM na kusema kuwa wewe sio wa ROSTAM ILA NI WA CCM.
 
Hadi sasa naamini kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufuatilia nyendo zote za Marehemu Chacha Wangwe kwa muda wa wiki mbili ama hata mwezi kabla ya "ajali" ilipomkuta. Ni muhimu kujua kila aleye ongea naye na kama kuna link na hizi siasa zinazoendelea ni muhimu kuwabana kujua waliyokuwa wakiongelea, nini mantiki ya makutano yao na nini kilijiri baadaye

Vilevile ni muhimu kuangalia account za Mallya na hata za Marehemu. Kwa Mallya ni kudetect fedha zisizoeleweka lakini pia kujua mahusiano yao ya Marehemu yalianza lini na yalikuwa katika hali gani. Maana nasikia kuwa Marehemu alikuwa na tabia ya kuamini sana watu na kuingia nao ubia wa kibiashara. Kwake yeye zaidi ilikuwa kuwawezesha wahangaikaji wenzake.

Vilevile kama CCM walikuwa wameshamshawishi kuingia huko kitu ambacho sikiamini kwa kujua mazingira ya kisiasa ya TARIME na chuki yao dhidi ya CCM na Serikali...lakini pia CCM kuna utamaduni wa kuwapatia wanaoasi vyama vyao TAKRIMA ambayo mara nyingi huwa kuanzia millioni 20 kuenda mbele. Mzee Wassira, Msabaha aliyekuwa CUF, Kaborou ni ushahidi mzuri katika hili.

Kwa wanaohoji ni kuhusu RASTA za WAngwe hapo zamani ni kweli alikuwa nazo na alikuwa ana tabia ya kutembea na picha akiwa na RASTA na kule Tarime ni maarufu kama CHACHA Rasta. Marehemu alilazimika kuondoa Rasta kwa ushauri ama shinikizo la MWALIMU NYERERE alipokuwa anataka ushauri wake ili yeye ajiunge na harakati za siasa.....Hata hivyo marehemu alibaki kuwa muumini mkubwa wa falsafa za Kirasta wakati wote na hiyo ndiyo naweza kusema kuwa ilikuwa msingi mkubwa wa fikira na matendo yake daima.....

Kuhusu Prof Wangwe ni kweli yeye ni mwanachama wa CCM na pia aliwahi kugombea ubunge wa Afrika Mashariki kupitia CCM ambapo yeye pamoja na mama KABAKA walikuwa wanamlaumu Marehemu CHACHA kwa kitendo chake cha kuungana na wenzake wa CUF na kina Zitto kususia uchaguzi ule kama sababu ya yeye Prof Wangwe kushindwa. Hivi sasa ni mjumbe wa NEC ya CCM na pia kuna madai kuwa kuingia kwake kwenye siasa kulichangiwa na siasa za Marehemu Wangwe ambaye ni mdogo wake kwa UBINAMU.

Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa Prof Wangwe na Marehemu CHACHA RASTA Hawakuwa karibu kama watu wanavyodai hapa lakini Prof Wangwe naweza kusema ndio mtu pekee aliyeweza kutumia vizuri busara zake kupunguza jazba na propaganda zilizokuwa zinaitafuna familia kidogokidogo.

Kuna madai kuwa msimamo wa sasa ni kujitahidi kuendana na muono wa baadhi ya wanafamilia ambao walifikia kumshambulia kuwa amepewa hongo kusema kuwa kifo cha CHACHA RASTA kilikuwa cha ajali ya kawaida. Wapo wafanyao hivyo kwa maslahi ya kisiasa na ya binafsi na wapo wafanyayo hivyo kwa mashaka halisi kabisa yaliyojengeka katika fikira zao ambao mimi pia naungana nao mkono.

Tanzanianjema
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom