Kifo cha Mhe. Chacha Wangwe na uchunguzi wake

Status
Not open for further replies.
By the way leo nimesikia kwenye news kwamba serikali ya Libya kupitia balozi wao wanamjia juu LIPUMBA kwamba nchi yao haifundishi ugaidi wala Ujasusi, kwahiyo wanasubiri maelezo/uchunguzi wa polisi ili wale naye sahani moja!

Hili jambo naona linazidi zua mambo!

getting hot and interesting!
 
Habari za Wangwe sasa zapigwa `stop`

2008-08-07 09:56:26
Na Romana Mallya

Vyombo vya habari pamoja na taasisi nyingine, vimepigwa marufuku kufanya upelelezi kuhusu ajali liliyomuua aliyekuwa Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya CHADEMA, marehemu Chacha Wangwe.

Badala yake, vyombo hivyo vimetakiwa kuacha kazi hiyo ya upelelezi ifanywe na Jeshi la Polisi.

Onyo hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. Eliezer Mbuki.
Aidha, Bw. Mbuki amevitahadharisha vyombo vya habari na taasisi kuwa, kama vitaendelea kuandika habari hizo, vitawajibishwa.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Bw. Mbuki alisema habari zinazoendelea kuzungumzwa na kuripotiwa katika vyombo vya habari kuhusu tukio hilo, zinaweza kuleta madhara baada ya upelelezi wa polisi.

Marehemu Wangwe, alifariki dunia kwa ajali ya gari Julai 28, mwaka huu wakati akiwa safarini kutoka mjini Dodoma kuja jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Deus Mallya aliyekuwa pamoja na marehemu Wangwe, tayari amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Dodoma akikabiliwa na mashtaka ya kuendesha gari la marehemu akiwa hana leseni na kwa mwendo wa kasi na hivyo kusababisha gari hilo kupinduka na kumuua Mbunge huyo.

``Endapo vyombo vya habari vitaendelea kuandika habari hiyo na baadaye kuonekana kuwa vilipotosha ukweli, itasababisha vyombo hivyo kuwajibishwa,`` alisisitiza.

Alisema kutokana na madhara hayo, wahusika wanaweza kuwajibishwa kwa kuvuruga upelelezi na kuingilia uhuru wa Mahakama.

Hivi karibuni, baadhi ya vyombo vya habari na wanasiasa, wameripotiwa kumtuhumu Mallya kuwa ni jasusi aliyewahi kupata mafunzo hayo nchini Libya.

Mkurugenzi huyo wa Mashtaka, aliyasema hayo alipotakiwa na Nipashe kutoa msimamo wake kuhusu habari zinazoendelea kuandikwa na kuibua mambo mbalimbali wakati kesi hiyo ikiwa tayari imefikishwa mahakamani na polisi wanaendelea na uchunguzi wao.

``Mimi nadhani tuliachie Jeshi la Polisi lifanye kazi yake ya kupeleleza tukio zima la ajali na vyombo vingine navyo visubiri upelelezi huo, kwani kwa kuendelea kuibua mambo na baadaye kuonekana ni uongo yanaweza kuleta madhara na kuwajibishwa`` alionya.

Aidha, Bw. Mbuki alisema Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Bi. Sakina Dotoo alitoa maelezo mazuri kwa vyombo vya habari, hivyo hakuna haja ya kurudia kwani maelezo yake yanajitosheleza.

Alisema Bi. Sakina alisema kuwa, lengo la jukwaa hilo ni kuleta usawa wa habari na kwa kila mtu na jukwaa hilo halifungamani na upende wo wote wa chama cha siasa na aliahidi kuwa watasimama katika msimamo huo.

SOURCE: Nipashe
 
Hivi na jf nayo haiangukii kwenye vyombo vya habari?
Mods tafadhali fungeni threds hizo kabla jf haijapata madhara mengine..Unless jf iwe imesajiliwa nje ya Tanzania.
Ila kama thats the case..Then wasomaji wa jf wanaweza kuletewa balaa huko bongo.
 
Polisi wabeza ushahidi wa kifo cha Wangwe
Shadrack Sagati
Daily News; Thursday,August 07, 2008 @00:01

Polisi imebeza ushahidi uliowasilishwa kwao juzi na viongozi wakuu watatu wa vyama vya upinzani juu ya utata wa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe (Chadema), kwa maelezo kuwa ushahidi huo ni wa kuokota mitaani.

Kamishna wa Polisi Paul Chagonja ambaye alipokea ushahidi huo juzi, aliliambia gazeti hili kuwa kilichowasilishwa na viongozi hao sio ushahidi bali ombi la kutaka jeshi hilo lifanye uchunguzi wa kina wa kifo cha Wangwe, kwa maelezo kuna utata.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, juzi walikwenda ofisini kwa IGP kuwasilisha kile walichosema ni ushahidi juu ya ujasusi na umafia wa Deus Mallya aliyekuwa na Wangwe wakati ajali iliyosababisha kifo chake (Wangwe) ilipotokea eneo la Pandambili, Dodoma, siku 10 zilizopita.

Mallya, kwa sasa yuko rumande baada ya kufikishwa mahakamani Ijumaa iliyopita, akituhumiwa kwa makosa matatu ya kusababisha kifo cha Wangwe, kuendesha gari kwa kasi na bila leseni. Kabla ya kwenda Polisi, viongozi wa upinzani waliwaambia wanahabari kuwa wana ushahidi, kuwa Mallya yuko kwenye mtandao wa Mafia na ana mafunzo ya ujasusi, hivyo wanaamini atakuwa amehusika kwenye ajali ya Wangwe.

Waliahidi kumpatia ushahidi huo IGP ili aufanyie kazi. “Ni kweli wamekuja tukaonana, lakini hakuna cha ushahidi wowote juu ya yale waliyowaambia waandishi wa habari juu ya Deus Mallya na utata wa ajali. “Wameniomba suala hilo polisi tutumie busara kubwa kutokana na utata uliopo, lakini hakuna ushahidi mwingine…kitu walichonisisitizia ni kwamba ajali ile ina maslahi kwa taifa, kwa Chadema hasa kutokana na maneno yanayosemwa,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, viongozi hao walimwomba aamuru Polisi wafanye uchunguzi wa kina wa suala hilo na katika kipindi kifupi walimaliza mazungumzo. Kwa mujibu wa Chagonja, kwa vile viongozi hao hawakuwapo eneo la ajali Polisi wanaamini kuwa walichowaeleza ni mambo ya kusikia mitaani.

Kwa mujibu wa Kamishna huyo, Polisi wameridhika kwa kiasi kikubwa na uchunguzi uliofanywa na madaktari na taarifa ya madaktari wa familia. Aliongeza yeye binafsi alitarajia kupokea ushahidi mzito lakini badala yake viongozi hao hawakuuwasilisha na muda mwingi walizungumzia kuishukuru Polisi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Issa Machibya, kwa busara walizotumia wakati wa vurugu kwenye msiba wa Wangwe.

Chagonja alisema; “Waliniomba nifikishe shukrani zao kwa mamlaka za mkoa wa Mara.” Kamishna huyo aliongeza kuwa baada ya majadiliano hayo, baadaye Mrema alianza kutoa maombi yake ya kutaka Polisi imrudishie vifaa vyake ambavyo vilikamatwa miaka kadhaa iliyopita. “Mrema aliomba kama kesi dhidi yake imemalizika ni heri wamrudishie vifaa hivyo kwani ana kazi navyo,” alisema.

Kamishna Chagonja alisema baada ya kupata maelezo hayo yeye aliwataka wao kama viongozi wa vyama vya siasa kutofanyia kazi mambo yanayosemwa mitaani. Chagonja alisisitiza kuwa ajali iliyotokea ni ajali ya kawaida na kwa kuwa viongozi hao hawakuwapo eneo la tukio hawawezi kukusanya ushahidi wa mitaani juu ya tukio hilo.

Kamishna huyo alisema baada ya kuona ushahidi huo hauisaidii Polisi, aliwaeleza kuwa busara wanayotaka polisi waitumie ni kwa wao kama viongozi wa watu kutofanyia kazi maneno yanayoweza kuhatarisha amani. Kuhusu tamko la familia, Chagonja alisema kuwa tamko hilo halijafikishwa ofisini kwa IGP, hivyo hawezi kulizungumzia.

“Sisi tunasema kama kuna watu wana ushahidi wakiwemo wana familia wajitokeze waje tuzungumze, watusaidie namna ya kupata ushahidi wa kile wanachodai". Bosi huyo wa Polisi alivitaka vyombo vya habari pia kuwa makini katika kuripoti masuala hayo, kwani baadhi ya mambo yanayoandikwa yanaweza kuzidisha chuki miongoni mwa jamii.
 
Obfuscating Orwellian orangutans!

Halafu inashangaza "wanamapinduzi" wetu humu wanavyo cower with tail between legs.

Ana sheria gani huyu bully?
 
Hakuna Kufungana Mdomo Hapa! Hakuna Kutishana, Tutazungumza Na Kuandika Mpaka Jua Lisogee, Na Sayari Ya Jupita Iwe Jirani Na Dunia.
 
Kupeleleza nini kilitokea katika ajali ya Marehem Wangwe si kazi ya Polisi tu.

Upelelezi ni kazi ya mtu yeyote yule mwenye Interest na jambo husika.
Hana sheria wala uwezo wa kuzuia vyombo vya habari, watu binafsi na taasisi nyingine zote kuendesha upelelezi wao.
Mh Mbuki asilete undava usio na mpango kwenye hii kesi.
Tutaendelea kupeleleza na kutafuta ukweli wa nini kilitokea kabla na baada ya ajali, tukipata habari mpya na yenye kubeba uzito hatutasita kuiweka hewani.
Eti tuwaachie Polisi!
Polisi wenyewe wauaji na maharamia wakubwa.
Huyo DPP mwenyewe haramia, kazi yake kubwa ni kufukia maovu ya wanasiasa kwa kuipindisha sheria pale yeye aonapo panafaa.

Sasa hivi tuna operate kutoka Level au floor ya 7 tunazidi kuteremka;wasubiri tukifika Ground Level, patakuwa hapatoshi kabisa hapo GL Wote watahamia kwenye Nyumba walo zinunua huku ughaibuni.
 
IF ni kweli kuwa wamepeleka maneno ya mitaani ni aibu kwa kambi nzima ya upinzani kwni viongozi wakuu kama hawa wanatakiwa kuwa serious kwani jamii inawaangalia .

Sasa kama jamii itawaona kuwa kila wanachosema hakina maana sana itawapunguzia heshima na pia heshima ya upinzani itaporomoka sana .

Washauriwe vizuri na washauri wao.
 
Habari za Wangwe sasa zapigwa `stop`

2008-08-07 09:56:26
Na Romana Mallya

Vyombo vya habari pamoja na taasisi nyingine, vimepigwa marufuku kufanya upelelezi kuhusu ajali liliyomuua aliyekuwa Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya CHADEMA, marehemu Chacha Wangwe.

Badala yake, vyombo hivyo vimetakiwa kuacha kazi hiyo ya upelelezi ifanywe na Jeshi la Polisi.

Onyo hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. Eliezer Mbuki.
Aidha, Bw. Mbuki amevitahadharisha vyombo vya habari na taasisi kuwa, kama vitaendelea kuandika habari hizo, vitawajibishwa.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Bw. Mbuki alisema habari zinazoendelea kuzungumzwa na kuripotiwa katika vyombo vya habari kuhusu tukio hilo, zinaweza kuleta madhara baada ya upelelezi wa polisi.

Marehemu Wangwe, alifariki dunia kwa ajali ya gari Julai 28, mwaka huu wakati akiwa safarini kutoka mjini Dodoma kuja jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Deus Mallya aliyekuwa pamoja na marehemu Wangwe, tayari amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Dodoma akikabiliwa na mashtaka ya kuendesha gari la marehemu akiwa hana leseni na kwa mwendo wa kasi na hivyo kusababisha gari hilo kupinduka na kumuua Mbunge huyo.

``Endapo vyombo vya habari vitaendelea kuandika habari hiyo na baadaye kuonekana kuwa vilipotosha ukweli, itasababisha vyombo hivyo kuwajibishwa,`` alisisitiza.

Alisema kutokana na madhara hayo, wahusika wanaweza kuwajibishwa kwa kuvuruga upelelezi na kuingilia uhuru wa Mahakama.

Hivi karibuni, baadhi ya vyombo vya habari na wanasiasa, wameripotiwa kumtuhumu Mallya kuwa ni jasusi aliyewahi kupata mafunzo hayo nchini Libya.

Mkurugenzi huyo wa Mashtaka, aliyasema hayo alipotakiwa na Nipashe kutoa msimamo wake kuhusu habari zinazoendelea kuandikwa na kuibua mambo mbalimbali wakati kesi hiyo ikiwa tayari imefikishwa mahakamani na polisi wanaendelea na uchunguzi wao.

``Mimi nadhani tuliachie Jeshi la Polisi lifanye kazi yake ya kupeleleza tukio zima la ajali na vyombo vingine navyo visubiri upelelezi huo, kwani kwa kuendelea kuibua mambo na baadaye kuonekana ni uongo yanaweza kuleta madhara na kuwajibishwa`` alionya.

Aidha, Bw. Mbuki alisema Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Bi. Sakina Dotoo alitoa maelezo mazuri kwa vyombo vya habari, hivyo hakuna haja ya kurudia kwani maelezo yake yanajitosheleza.

Alisema Bi. Sakina alisema kuwa, lengo la jukwaa hilo ni kuleta usawa wa habari na kwa kila mtu na jukwaa hilo halifungamani na upende wo wote wa chama cha siasa na aliahidi kuwa watasimama katika msimamo huo.

SOURCE: Nipashe

The writer got it wrong, DPP alikuwa anavishauri tu vyombo vya habari siyo kutoa amri. Amri huwa hazitolewa kwa kuongea kwenye simu. Amri haitoi nafasi ya maneno ... mimi nadhani... NO amri inazingatia sheria. Hizi media zitatupeleka pabaya.
 
Hata kama the writer got it wrong na DPP "alishauri" tu, DPP was wrong as thi infringes freedom of the press, their right of expression and their right to earn a living.

Sasa wasiandike kwa kina habari hot magazeti yasipouzwa wakija nyumbani kwake kutafuta chakula atawalaumu?
 
Bado hatuwezi kuanza kuzidharau kazi za wazalendo kama Mrema.
Kwangu binafsi Mrema is one of the bravest....Na ni CHAGUO LA RAS!
Kama kweli media ilitumika kuwamaliza kina Sumaye na Maleccela..Itakuwa vipi kwa Kamanda wetu aliyehama chama?
Mrema FOR PRESIDENT...
Kama kuna mwenye namba ya Mrema naomba munisaidie kwani wengine tunataka kuwasliliana na MKOMBOZI WA WANYONGE!
 
Polisi walisha maliza uchunguzi wao sasa tunataka wafanye zaidi ya uwezo wao? (siwaungi mkoni lakini huo ndo uwezo wao kwa mujibu wa maelezo wanayopewa au ujuzi walionao au ???)
 
Sikusema Mrema aingile uchunguzi wa polisi...Nilisema Mrema ni MKOMBOZI WA WANYONGE NA NDIYE CHAGUO LA RAS.
 
Bado hatuwezi kuanza kuzidharau kazi za wazalendo kama Mrema.
Kwangu binafsi Mrema is one of the bravest....Na ni CHAGUO LA RAS!
Kama kweli media ilitumika kuwamaliza kina Sumaye na Maleccela..Itakuwa vipi kwa Kamanda wetu aliyehama chama?
Mrema FOR PRESIDENT...
Kama kuna mwenye namba ya Mrema naomba munisaidie kwani wengine tunataka kuwasliliana na MKOMBOZI WA WANYONGE!

you should be his campaign manager, u doin a good job!
 
do u think this is true!?....

Yaani washtue taifa halafu waongee maneno hayo tu na mapolisi!....... Lakini viongozi wetu wa kiafrika hawashindwi!..... Lakini mmmmhhhh!
 
Hawa polisi utasikia wanataka kushirikiana na wananchi ,japo waliowasilisha huo ushahidi ni viongozi wajuu lakini watakuwa wamewasilisha kama wananchi ambao wangehitaji kusikia ,kwani yazungumzwayo mitaani ni mambo yanayokwenda mdomo kwa mdomo kutokea sehemu iliyotokea ajali.kusema ni maneno ya mitaani kiongozi huyo wa polisi atakuwa amekosea pakubwa sana na itabidi wananchi wawe macho juu ya kauli alizotumia kuponda mawasilisho yaliofanywa na hao viongozi.
Kuna kiongozi kama yeye ambae alionekana na mapanga na visu eti vilikamatwa kutoka kwa CUF,huyu kiongozi wa Polisi nina wasi wasi nae kwa jinsi alivyotoa ripoti ya wakuu hao kuwa ni ushahidi wa mitaani,ushahidi wa mitaani utakuwa na faida ikiwa unaambiwa ndani ya gari hakukuwa na kitu ambacho kingesababisha fuvu kufunguka na ubongo kumwagika ,hivi polisi hapo haioni ukweli,wa kutakiwa maelezo ya kina kwa wananchi kuwa hali hiyo inaweza kutokea ikiwa abiria aligongo gea au hand brake ,ni maelezo ya polisi ndio yatakayoweza kuelezea hoja zilizowakilishwa ,nionavyo Mkuu huyo wa polisi ameshindwa kufahamu kilichowakilishwa hapo au ni kutaka kuzima ukweli ili mambo yaishe kwa haraka,kwa hili mkuu amekwenda mbali sana na ndio tunaporudi kwa akina Zombe na Mahita na ushahidi wao wa kujilabu kwamba wao wanajua sana kiasi ya kutokeza kwenye TV na mapanga ili kutoa maelezo dhidi ya CUF.
Ikiwa viongozi wakuu wamejaribu kuwepo karibu na polisi kutoa maelezo ambayo wao Viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakiyapokea kutoka kwa wananchi kwa njia tofauti na pengine za karibu zaidi kuufikia ukweli kuliko polisi ,iwe ni ajali ya kawaida au ya kupangwa basi naamini viongozi hao wana njia nzuri zaidi za kuyafahamu yaliojiri kuliko polisi. Lakini polisi kwa kujiona wao wanajua zaidi wametumia nafasi hiyo kuvunja na kupuuza waliyoarifiwa ,halafu mnasema mnaomba ushirikiano na wananchi hivi mnataka tuwaelewe vipi ikiwa mambo yenyewe ni hayo ya kubeza na kupuuza ?
Mkuu huyu ametoa maelezo kupinga na kupuuza wakati yeye sio mhusika mkuu aliekusudiwa kupewa maelezo hayo ,kama ni ushahidi hakutakiwa kueleza chochote iwe kweli au si kweli ,huyu ni lazima tuwe nae macho huenda ikawa ni katika wanaotumiliwa,alichotakiwa ni kuyafikisha kwa Mkuu wake IGP Mwema alichokifanya ni kosa na anafaa kuwajibishwa.
 
you should be his campaign manager, u doin a good job!

Kieleweke...Mimi ni Ras na niliondoa dreadlocks..Baada ya kifo cha Wangwe nazirudisha nili ahidi.

Napster...Shukran...Naomba namba ya Mrema kwa wale waliyonayo..Ningeshukuru sana.
Mimi nawaambia..ccm wakisikia RUMOURS kwamba chaguo la wananchi ni Ras Mrema...Basi nakwambia watafanya mabadiliko kama mwalimu alivyotaka kwani mzee wa KIRARACHA NI SAFISHA SAFISHA NA MAFISADI WATAKAMATWA NDANI YA SIKU SABA!
Mrema ni WARRIOR...HUYO APEWE NCHI WAKATI HUU WA SAFISHA SAFISHA..Halafu baadaye tunaanza kupanda mbegu mpya..Ila kiongozi anaye FIT kwa siasa zetu za kina MRAMBA NA MKAPA...CHENGE NA YONA... ambao hata JK hawawezi..HAWA WAACHIWE MREMA..MKOMBOZI NA SAUTI YA MYONFE...HUYU NI CHAGUO LA RASTA!
A TRUE WARRIOR!
 
Polisi wabeza ushahidi wa kifo cha Wangwe
Shadrack Sagati
Daily News; Thursday,August 07, 2008 @00:01

Polisi imebeza ushahidi uliowasilishwa kwao juzi na viongozi wakuu watatu wa vyama vya upinzani juu ya utata wa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe (Chadema), kwa maelezo kuwa ushahidi huo ni wa kuokota mitaani.

Kamishna wa Polisi Paul Chagonja ambaye alipokea ushahidi huo juzi, aliliambia gazeti hili kuwa kilichowasilishwa na viongozi hao sio ushahidi bali ombi la kutaka jeshi hilo lifanye uchunguzi wa kina wa kifo cha Wangwe, kwa maelezo kuna utata.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, juzi walikwenda ofisini kwa IGP kuwasilisha kile walichosema ni ushahidi juu ya ujasusi na umafia wa Deus Mallya aliyekuwa na Wangwe wakati ajali iliyosababisha kifo chake (Wangwe) ilipotokea eneo la Pandambili, Dodoma, siku 10 zilizopita.

Mallya, kwa sasa yuko rumande baada ya kufikishwa mahakamani Ijumaa iliyopita, akituhumiwa kwa makosa matatu ya kusababisha kifo cha Wangwe, kuendesha gari kwa kasi na bila leseni. Kabla ya kwenda Polisi, viongozi wa upinzani waliwaambia wanahabari kuwa wana ushahidi, kuwa Mallya yuko kwenye mtandao wa Mafia na ana mafunzo ya ujasusi, hivyo wanaamini atakuwa amehusika kwenye ajali ya Wangwe.

Waliahidi kumpatia ushahidi huo IGP ili aufanyie kazi. “Ni kweli wamekuja tukaonana, lakini hakuna cha ushahidi wowote juu ya yale waliyowaambia waandishi wa habari juu ya Deus Mallya na utata wa ajali. “Wameniomba suala hilo polisi tutumie busara kubwa kutokana na utata uliopo, lakini hakuna ushahidi mwingine…kitu walichonisisitizia ni kwamba ajali ile ina maslahi kwa taifa, kwa Chadema hasa kutokana na maneno yanayosemwa,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, viongozi hao walimwomba aamuru Polisi wafanye uchunguzi wa kina wa suala hilo na katika kipindi kifupi walimaliza mazungumzo. Kwa mujibu wa Chagonja, kwa vile viongozi hao hawakuwapo eneo la ajali Polisi wanaamini kuwa walichowaeleza ni mambo ya kusikia mitaani.

Kwa mujibu wa Kamishna huyo, Polisi wameridhika kwa kiasi kikubwa na uchunguzi uliofanywa na madaktari na taarifa ya madaktari wa familia. Aliongeza yeye binafsi alitarajia kupokea ushahidi mzito lakini badala yake viongozi hao hawakuuwasilisha na muda mwingi walizungumzia kuishukuru Polisi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Issa Machibya, kwa busara walizotumia wakati wa vurugu kwenye msiba wa Wangwe.

Chagonja alisema; “Waliniomba nifikishe shukrani zao kwa mamlaka za mkoa wa Mara.” Kamishna huyo aliongeza kuwa baada ya majadiliano hayo, baadaye Mrema alianza kutoa maombi yake ya kutaka Polisi imrudishie vifaa vyake ambavyo vilikamatwa miaka kadhaa iliyopita. “Mrema aliomba kama kesi dhidi yake imemalizika ni heri wamrudishie vifaa hivyo kwani ana kazi navyo,” alisema.

Kamishna Chagonja alisema baada ya kupata maelezo hayo yeye aliwataka wao kama viongozi wa vyama vya siasa kutofanyia kazi mambo yanayosemwa mitaani. Chagonja alisisitiza kuwa ajali iliyotokea ni ajali ya kawaida na kwa kuwa viongozi hao hawakuwapo eneo la tukio hawawezi kukusanya ushahidi wa mitaani juu ya tukio hilo.

Kamishna huyo alisema baada ya kuona ushahidi huo hauisaidii Polisi, aliwaeleza kuwa busara wanayotaka polisi waitumie ni kwa wao kama viongozi wa watu kutofanyia kazi maneno yanayoweza kuhatarisha amani. Kuhusu tamko la familia, Chagonja alisema kuwa tamko hilo halijafikishwa ofisini kwa IGP, hivyo hawezi kulizungumzia.

“Sisi tunasema kama kuna watu wana ushahidi wakiwemo wana familia wajitokeze waje tuzungumze, watusaidie namna ya kupata ushahidi wa kile wanachodai". Bosi huyo wa Polisi alivitaka vyombo vya habari pia kuwa makini katika kuripoti masuala hayo, kwani baadhi ya mambo yanayoandikwa yanaweza kuzidisha chuki miongoni mwa jamii.

Nilijua tuu, Shame on them
Baada kushughulikia makosa ya msingi marehemu kumruhusu Deus kuendesha gari tunatafuta mchawi.
Je kuna viongozi wetu wangapi wanaendeshwa na madereva walionunua leseni amboyo ni sawa na kuwa huna
Mimi mwenyewe nilitoa kidogodogo kupata leseni yangu kihalali nilifele kwenye test
Lengo letu sasa hivi kurudisha uzalendo wetu wa zamani na sio kuhubiri siasa za chuki
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom