Kiatu cha kiume china 5000 bongo unauziwa 120,000/=

Kiatu cha kiume china 5000 bongo unauziwa 120,000/=

Unachotetea ni kitu gani kwa mfano hapo kama sio kulia kwenyewe huko? Wewe tulia iwapenye
Mtu anunue kiatu elfu tano uuziwe elfu tano una wazimu sio bure,

Panda ndege nenda China ukanunue vya elfu tano
 
Alibaba,taobao,1688,madeinChina,Global source huko kwenye hayo masoko bidhaa ni bei za kutupa kabisa! Wachina waaminifu unaagiza mzigo unakufikia vizuri kwa bei kitonga

Kule tiktok wachina wanaikataa alibaba wanasema tusitumie ina mawinga wengi. Bora hiyo mitandao mingine uliyoitaja ndo straight from the source.
 
Serikali yenyewe inawatumia wachina kwenye ujenzi sababu wako cheap sana na high quality sembuse raia. Acha kina shivo wale mema ya africa.
 
Wachina wake tu,hawa wabongo wenzetu wanatuzinguA sana.hisense tv inchi 50 china ni laki Moja tu huku wanatuuzia milioni Moja na nusu
Kweli mkuu au ni gharama za usafiri na utitili wa kodi? Maana Waswahili kisingizio chao kodi siyo rafiki kwa Mfanyabiashara na TRA wanawabambikia kodi
 
Google:

1. Production cost.
2. Brand.
3. Goodwill.
4. Targeted Market

Ukisoma hivyo vitu utaelimika sana sana sana!

Note:

1. China wana product za Africa.
2. Wana product za USA
3. Wana product za Europe.

Mimi mfanya Biashara nikinunua product USA ambazo ni za China, haziwezi kuwa na bei sawa na product za China kwa ajili ya Africa!
 
Wachina komaeni hapo hapo, Mbaka Hawa Wachawi Wakinga Waombe Poo Wajinga kabisa Hawa, kitu Cha kuhuza Shilingi elfu 5, Hawa Wachawi Wakinga wa Kariakoo Wanauza Shilingi elfu 70 kenge kabisa
Duuuh mbali sana yani kutoka elf 5 mpaka elfu 70 si bora uende Mlimani city ukakinunue kule hakuna msongamano unapulizwa na Ac na hakuna vibaka kama Kariakoo.
 
Alibaba unanunua sh 3000-5000 usafiri na kodi mpk bongo sh 2000...jumla 7000 tu hawa ndigili wanakuja kukuuzia mara kumi yake ...
Mkuu niliangalia be za Alibaba nikaogopa nikajua ni matapeli kwasababu nilipiga hesabu bidhaa zake bei anayouza ni ndogo mara mia ya hapa mbogo, yani sikuamini nilijua ni utapeli utakuta TV elf 70 lakini bongo Laki 9.
 
Mkuu niliangalia be za Alibaba nikaogopa nikajua ni matapeli kwasababu nilipiga hesabu bidhaa zake bei anayouza ni ndogo mara mia ya hapa mbogo, yani sikuamini nilijua ni utapeli utakuta TV elf 70 lakini bongo Laki 9.
Tv gani inauzwa hivyo? Usidanganyike. Wachina wenyewe ndio wanaouza tv kama Ailyons kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwa jumla ambao nao wanakuuzia wewe. Tena wachina wenyewe wapo kariakoo pale pale. Hakuna tv ya sh 70k uje uuziwe sh 900k. Huo ni uongo wako.
 
mkuu, sikuhizi wachina wanatengeneza hapahapa, mbagala kuna kiwanga cha mawigi, kisemvule kuna kiwanda cha yeboyebo, kibaha toyo ,inabubwa hapahapa, gypsam board tena zimeandikwa made in german, vingunguti kuna kiwanda cha Iphone, tatizo hamsalimii watu tungewaonyesha machimbo acha akina vunjabei wawapige
 
Back
Top Bottom