Kiatu cha kiume china 5000 bongo unauziwa 120,000/=

Kiatu cha kiume china 5000 bongo unauziwa 120,000/=

Dawa itawaingia taratibu tu mtaelewa. Hizo zote ulizotaja, kwani unakatwa bidhaa moja kwa shilingi ngapi? Unajua ninyi mmekuja kujikuta mna akili sana kuliko sisi wengine, ila muda wenu waja, mtabaki mkisimulia tu tulikuwaga tunafanya hivi
Dawa inawaingia ninyi mnaolia kuuziwa kiatu laki na ishirini, Mimi umeona nimelia nn hapo, njoo taratbu mkuu
 
Watu Wana asili ya kuibia wengine Ila wanajiita ni wafanyabiashara.
Mfuko wa sukari unanunua kwa 135k unauza 137k, ukiuza mifuko 50-100 kwa siku unayo laki 1-2 kwa siku ndio biashara cheki mzunguko wa biashara,wachina waje wengi na wanayo mitaji hata wapandishe Bei za fremu. Subiria na jengo la UBUNGO zamani likamilike. Maisha hayatakiwi kuwa magumu kabisa , Kuna blenda china inauzwa 15k bongo 120k.
Kwa ULIMWENGU huu wa wasomi na mtandao wataroga watu,
Yaani inabidi watu waumize kichwa zaidi.
Saivi wachina wanadai kuwa wazungu wananunua kwao vitu like Gucci bags wakifika kwao wanaandika made in Italy or France so wanauza mbaya.
Hata mie Kuna sahani nikinunua za Durex zimeandikwa made in France kumbe ni za kichina na nikavimba kuwa nanunua bidhaa ya france kumbe ni za kwa mtogole.
Kweli kabisa.
 
Kwani wachina hizo bidhaa wanazouza zinasafirishwa kwa njia tofauti na wanazotumia wabongo mpaka watofautiane bei?
Mifumo ya Tanzania Ina upuuzi mwingi

Utajuaje mchina akifika customs halipii au anatoa percent ndogo sana kwakuwa anaingiza kontena nyingi, wakati mbongo labda kajitahidi kontena moja au mbili Tena sio Kila wiki au mwezi baada ya miezi kadhaa ?

Tatizo tusiwe wa kulaumu huku mkiijua serikali yetu vizuri,

Kwann mchina auze rahisi na mbongo auze ghali,

Mean kama wote wanalipia customs tax sawa Ina maana mchina ana uhakika wa kushusha kontena kila wiki na kumlazimu kushusha bei tofaut na mbongo ambaye hata kontena jingine hajui ataagiz lini

Hatuwezi kufanana, hapo kikubwa ni kuwa mchina ana uhakika wa upatikanaji wa mzgo wakati wote Vs mbongo upatikanaji wake ni wa msimu msimu hapo lazima bei ziwe tofauti baharia,



Labda pitia hapa imebidi ni edit Ego is the Enemy
 
Tatizo linakuja hapa

Mtu katoa hela kwa supplier katengeneza mzgo ukawa wa kutosha,

Sema moja, Purchasing price

Kumbuka mzgo upo china sio mwenge, anatumia njia gani ya kusafirisha ? Kama ndege au maji,

Tuchukulie kontena moja tuu la ft 20

Atalipia Kodi, customs, hapa zipo nyingi nyingi inategemea na uagizaji wako sasa

Atalipia wharfage charges kama inahitajika

Atalipia shipping line charges,

Atalipia clearing fees wakati wa kutoa kontena,

Atalipia usafiri bandarini kwenda dukani au stores,

Atalipia washusha mzgo ndani ya kontena na kuipanga,

Kumbuka anamlipa mchina kwa USD hata kama ana CRDB USD kuzipata dollar alinunua kwanza CRDB TZS Kuna makato,

Kuna makato wakati analipia mzgo

Siwezi andika vitu vyote ni kazi Tena sio nyepesi
You can compute mathematically tuone kiatu cha 5k kwa china kinafikaje bongo kiuzwe 60k.
Mbona Sasa wachina wao wanauza Bei rahisi so don't they incur those costs sir?
Are they apply for black people not Chinese.
Hapa unajaribu ku defend Ila hauwezi ikafikia hapo ,yaani ngoja saivi itajulikana mfanyabiashara ni nani.
Mie hata kiatu kimefika bongo kina 15k gharama zote naweka 17-18k nauza jumla kuanzia hata pcs 24-36 nakamata hela natembea naagiza mzigo mwingine. Siangalii faida kubwa sana
 
Mtaji wa Wanyonyaji wa Waafrica ni Ujinga. Ujinga wenye majina mengi utaskia ndo “Utamaduni wetu” “Mila zetu” au ndo “desturi yao” shubaamit!!

Werevu hawasikilizwi, hawapewi platforms za kuwafikia watu wengi.. Mwerevu akizungukwa na wajinga anakua hatarini.
Ila ni kipindi cha mpito Mkuu, it gonna get ugly before it becomes beautiful
Bongo shida exposure,, ....unakuta kundi la watu linashikwa akili na watu fulani tu ambao mfukoni panasoma vizuri,...ila kwa sasa mambo yanaanza kufunguka watu kutoka nje kumewasaidia kinamna
 
You can compute mathematically tuone kiatu cha 5k kwa china kinafikaje bongo kiuzwe 60k.
Mbona Sasa wachina wao wanauza Bei rahisi so don't they incur those costs sir?
Are they apply for black people not Chinese.
Hapa unajaribu ku defend Ila hauwezi ikafikia hapo ,yaani ngoja saivi itajulikana mfanyabiashara ni nani.
Mie hata kiatu kimefika bongo kina 15k gharama zote naweka 17-18k nauza jumla kuanzia hata pcs 24-36 nakamata hela natembea naagiza mzigo mwingine. Siangalii faida kubwa sana
Nilijaribu kuwaonesha kitu sasa wengi wakanivamia

Tuseme wewe ndo supplier hapo kariakoo, maake so wote wenye maduka wanaweza kuagiza kontena china,

Mimi navyojua supplier kwa hesabu za haraka haraka atauza kulinganana gharama za uagizaji zilivyokuwa, ambapo bei yake Haina ttzo

Ttzo linakuja wakishanunua kwako kama supplier akikiweka dukani hapo hapo kariakoo, au kwenye meza ndo atapiga bei anayoona inafaa,

Maake supplier akiuza laki na 20 vipi yule anayenunua akaweke dukani au kwenye meza atauza shngp?

Ttzo sana sana sio supplier

Ila pia mchina na sisi ni tofaut kabisa
 
Lete usahihi sasa,usipinge,hoja hupingwa kwa hoja,niliwahi agiza subwoofer kwa mtu alieenda china alinunua 30000 tu spika Tano,akaniambia nimpe 50,000 na mpaka Leo ninayo,ukitaka picha ntakuwekea hapa.
Kuna memory kadi ya 128GB mchina aliniletea kwa 5k nikamwambia hapa bongo ni 87k akashangaa kinyama.
Ninazo mashine za kuchaji za kunyolea wanangu mchina aliniletea kwa 37k ulizia bongo Sasa , ninazo mwaka wa saba huu hapa wanangu hawapendi saluni.
 
Niende china kufanyaje na mchina katufuata huku huku bongoland 😀
Kusafiri ni ushamba wa kizamani Kila kitu unaagiza umekaa labda na wewe Kama hujawahi panda ndege ukaenda nje. Unaagiza Amazon, Alibaba umekaa ndani unakunywa chai ya maziwa ya ng'ombe wa KIENYEJI anayekula majani kutoka wilaya ya Serengeti,bunda na bariadi
 
Kuna siku supermarkets na supply chain yote ya nchi hii ITASHIKILIWA NA WACHINA.

Hiyo siku ikifika mtakuwa kama mbwa kwenye nchi yenu na mtalia na kusaga meno maana WACHINA ndo watapanga bei za viberiti na condoms.

Kwa kifupi mtatawaliwa tena kama ambavyo hali ilikuwa kabla ya 1961. Matajiri wakubwa watakuwa wachina na wata-influence hadi mnachokula maana chain yote watakuwa wao tu.

Wachina watakuwa wana-fund kampeni za wanasiasa, watakuwa na lobbying groups zenye nguvu na watapanga hadi Rais awe nani. Maelekezo ya kuhusu nani awe Rais yatakuwa hayatoki Dodoma, yatatoka BEIJING

Mwafrika ni kama kenge. Huwa haamini kitu mpaka kimkute.

Ukoloni sio lazima watu waje na vifaru. Just control the supply chain and you are good
Mbona haya yanafanyika mkuu kwani magharibi na USA si wanapanga Ila sio kuuza kiatu cha 5k kwa 60k unasingizia hizo charges unazoita kwa English ili kuwapoteza wengi.
Elewa maagizo hayatoki Dodoma Bali yanatoka nje huko , hujaona jpm akatolewa unamuona yaya you're anatafutwa kuuliwa.
Tuko kwenye ukoloni unaogopa. Kuna watu walitamani mzungu angeendelea kuwepo Mana tungekuwa mbali mno kaja mwafrika hakuna anachofanya ni kuwaumiza blacks wenzake. Hilo lisikupe hofu tunalitaka litokee Ila sio tiketi ya kuuza kitu karibu 12 ya Bei uliyochukulia
 
Mwanzoni nilikua nawaonea huruma sana wabongo wa kariakoo wakilalamika kwanini wachina wamejazana kariakooo, na walizunguka media mbali mbali kuonyesha ubaya wa wachina, kumbe siri wanaijua...

Wachina kule kwao bidhaa ni bei ndogo sana, wakawa wanashangaa kwanini wabongo wanajazana kuja kuchukua bidhaa? Wakaamua kuja kufanya utafiti wakakuta majamaa yanapata faida mara 4 na bei waliyochukulia, yaani ukiachana na Kodi n.k bado faida wanapata kubwa saana wakiuza jumla....

Mfano nimeona kiatu Cha dollar 2, hapa kariakoo naambiwa ni 60,000/= kwahiyo nikawa nashangaa, yaani unataka kusema Kodi pamoja na usafiri ni zaidi ya 40,000/=.

Cadet za kiume jeans wanauza 20,0000/= wakati china ni 3000/=... Ngoja waje wawanyoooshe.

Wafanyabiashara wa china wameanza kuonyesha bidhaa halisi na bei halisi mtandaoni jambo ambalo limeathiri Moja Kwa Moja mifumo ya kibiashara ya kimataifa, hususani kweli AliExpress, temu, shein n.k ....

Binafsi sina tatizo na hii ya uwapo wa Wachina iwapo tu mamlaka zetu zitahakikisha bidhaa wanazoleta huku zina quality ya juu, kama ambavyo wanapelekea Europe, Canada na US. Au at least ziwe na kiwango fulani. Tatizo hawa Wachina na hao wafanya biashara wa Kariakoo, wanaenda kuleta mavitu low quality wanatuuzia huku kwa bei kubwa.
 
Mbona haya yanafanyika mkuu kwani magharibi na USA si wanapanga Ila sio kuuza kiatu cha 5k kwa 60k unasingizia hizo charges unazoita kwa English ili kuwapoteza wengi.
Elewa maagizo hayatoki Dodoma Bali yanatoka nje huko , hujaona jpm akatolewa unamuona yaya you're anatafutwa kuuliwa.
Tuko kwenye ukoloni unaogopa. Kuna watu walitamani mzungu angeendelea kuwepo Mana tungekuwa mbali mno kaja mwafrika hakuna anachofanya ni kuwaumiza blacks wenzake. Hilo lisikupe hofu tunalitaka litokee Ila sio tiketi ya kuuza kitu karibu 12 ya Bei uliyochukulia


Unaposema nje unamaanisha nini? Mimi niko very specific kwamba Wachina wanaelekea huko. Na sasa hivi wanachuo chao huko Kibaha "wanatrain" CCM na viongozi wake.

Sasa niambie ni wafanyabiashara gani wa Kimarekani wana influence sasa hivi ya kuchagua nani awe Rais? Maana hoja yako ilijikita hapo.
 
Unazoongea hapa bado hazina uhalisia wa gharama uuze mpaka mara mbili yake...Kama utabisha basi itabidinikupe maelezo zaidi.
Tanzania vitu vingi vipo bei juu kwa sababu ya kodi hapo Zambia tiles za 28,000 kiwandani kwa Mchina hapa Tanzania zinauzwa 68,000 mpaka 75,000 kodi ipoh juu na gharama nyinginezo ukitaka kujua hili nenda tu hapo black Nakonde/Tunduma.
 
Back
Top Bottom