Kama hujawahi kabisa kuagiza mzigo kutoka China ni bora kuazia Kariakoo au Nairobi Kenya

United ya Ferguson

JF-Expert Member
Oct 29, 2021
2,770
5,427
Kwa uzoefu nilioupata nikiwa Kariakoo kutoka Kwa wafanyabiashara mbalimbali na kutumia uzoefu wangu mwenyewe wa kuagiza mizigo kutoka China kuja Tz kama wew Ndio unaanza Kwa mara ya kwanza kabisa kutaka ku export China to Tz na unaanza kabisa biashara Njia Bora zaidi ni kuaza kununua mzigo pale pale kariakoo au kwenda Nairobi Kenya kununua Kwa wauzaji wakubwa wanaouza jumla Kwa wafanyabiashara mbalimbali

Tuseme unataka kuaza kuagiza boxer za kiume na vesti zake au labda bags like ponaso,Marcelo.jaribu kutafta wazoefu na soko la kariakoo wakusaidie kupata wauzaji wa jumla ununue mzigo kidogo kidogo uaze taratibu kuuza ukitafuta jina na ukiaza process za wew kujua ABC za kusafirisha mzigo kutoa China kuja Bongo zinakuaje
Mfano kitu ambacho inabidi utambue mzigo kutoa China kuja Tanzania unachukua muda gani had kufika usije kufanya haraka kulipa Kodi frame halafu unategemea mzigo utoke China Ndio uaze kuuza itakula upande wako mfano kunakipindi.

Unaweza kukaa hadi mwezi minne ukisubiri mzigo hadi ufike na tayari umelipa frame huku ukingoja mzigo kutoka China Kwa mwezi minne na huna mzigo mwingine wa kuuza dukani itakula kwako pia inabidi utambue gharama za usafirishaji wa mizigo kutoka China kuja Tz zipoje je nikisafirisha simu gharama zake ni sawa na nikisafirisha viatu au mzigo unachajiwa kutokona na thamani yake au Nafasi unayochukua wakati wakusafirisha pia inabidi ujue ni Njia ipi Bora ya kusafirisha mzigo kutoka China .

Unaweza kuimudu mfan kusafirisha mzigo Kwa Njia ya Ndege ni rahisi na haraka lakini inagharama kubwa ukilinganisha Na Maji kwenye Ndege mzigo unachajiwa Kwa kilo Kila kilo moja ya mzigo ina gharama zake kwahyo usije kujikuta faida unaacha kwenye gharama za usafiri na gharama inategemea na kampuni Na Je ukitumia Njia ya Maji ni kampuni Gani zipo fasta kweny kusafirisha mizigo je mapembelo , silent ocean nazinginezo na gharama zao wanachaji vipi mfano kweny Cargo za kusafirisha mizigo Kwa Njia ya Maji wanachaji Mzigo kwa CBM ivo vitu ni vya msingi sana kuvielewa kabla yakuamka na kuaza ku export mzigo kutoka China kuja Tz

Pia kitu kingine Cha kujiuliza Nitaenda kiwandani kutengeneza mwenyewe au Nitaenda kununua mzigo ambao upo tayari dukani na gharama za kununua mzigo uliotayali kununuliwa Ni sawa Na wakiwandani kutengeneza kiwandani ni inachukua muda Gani hadi mzigo kuwa umekamilika siku, mwezi , wiki ,Na Je oder zao wanaaza na pice Ngapi 500,1000,2000,5000,10000

Jambo Lingine la kujiuliza Ni miji ipi naweza kupata masoko na viwanda vya bidhaa za bei nafuu ni Yiwu, Je Yiwu ni maarufu Kwa bidhaa Gani, Gaungzhu ni marufu Kwa bidhaa ipi Hong Kong ni maarufu Kwa bidhaa ipi mfano Hong Kong ni mji maarufu sana kwakua na Simu za bei Chee ayo ni maswali ya msingi ya kujiuliza kabla hujarudi na kuaza kutukana wachina

Pia kuwa makini na aina ya Bidhaa unayotaka kwenda kuagiza kutoka China mfano katika bidhaa zakunazo makina sana ni bidhaa za Nguo hasa Nguo za wanawake Nguo za kike ni zinaenda na mitindo sana unaweza kwenda china ukanogewa na unafuu wa bei ukabeba mzigo wa kutosha unakuja mjini unakuta hizo Nguo watu walishazishusha zimepitwa na wakati wameleta fashioni nyingine ikala upande wako Maana Biashara ya Nguo inahitaji mtu mwenye jicho sana la kutambua mitindo na aina za material za kutengeneza Nguo

Vitu vipo vingi sana apo nimeacha
kuzungumzia habari za kutapeliwa na wachina ,kutumiwa mzigo ambao hukuchagua pia series za kuagiza mzigo mfano nitakua naagiza mzigo Kwa awamu au niataagiza mzigo mkubwa mwingi Kwa mara mara moja Kwa ajili ya kuuza mda mrefu au isije ikatokea umeagiza mzigo kidogo ukafika town ukauza ukaishia ukaaza kujipanga kusubiri mzigo mwingine upya kumbe ungeweza kusafirisha mzigo ki awamu mfano wakati mzigo wako unapokea kuwe na mzigo mwingine upo njiani unakaribia kufika hii mbinu wanatumia wafanyabiashara wengi sana pale kariakoo wanaagiza mzigo Kwa series

Yote Tisa biashara za ku export mzigo kutoka china kuja Tanzania zinaweza kukutajirisha Kwa haraka sana pia ni Biashara ambazo zinaweza kukufirisi Ndani ya mda mfupi sana kama hautakua makini

Kariakoo Na Nairobi Kenya ni best option Kwa mgeni kabisa kweny game la biashara
 
inamana kilo mzigo huchukua miezi mi4 au ilitokea imechelewa ndo inafika miezi mi4
Hapana sio Kila mzigo huchukua miezi minne Kuna mingine inaweza kuchukua miezi miwili tu ukawa umefika ila inabidi ujiandaee kiakili kweny usafirishaji wa mizigo kuchelewa Kwa mizigo nikitu ambacho Huwa hakiepukiki
 
Mkuu kwa mtu ambaye ndio ameanza biashara ya duka la simu au nguo na anahitaji kwenda kuagiza mzigo China anatakiwa awe na jumla kiasi gani cha pesa minimum gharama zote za nauli,viza na manunuzi.
 
Back
Top Bottom