Katibu wa TEC: Maaskofu wanahitaji kuisoma mikataba iliyosainiwa, walipoitwa hawakuambiwa kulikuwa na nini

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,128
Katibu wa TEC Padre Dr. Kitima amesema Maaskofu wanahitaji kuusoma mkataba, walikuwepo watatu na walipoitwa hawakuambiwa kuna nini ila walichosikia ni kuwa Maoni ya Wananchi yamezingatiwa.

Maaskofu walikuwa wanawasemea Wananchi na "Walichosikia" maoni ya Wananchi yamezingatiwa, amesema.

Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema muda ukifika mkataba utapelekwa kwenye Kamati ya Bunge.

Kitima.jpg

Barua ya mwaliko
 
Mwanasheria anasema mkataba utapelekwa bungeni,wakati umeshasainiwa tayari?

Isije ikawa kama kipindi kile cha JPM aliposhika hatam,akaanza kulalamikia mikataba ya kipindi cha nyuma.vWataalam wauone huo mkataba,ukute tunachoelezwa na kilichomo ni tofauti.Anyway kikubwa maendeleo.
 
Namuunga mkono na miguu kabisa.

Mkataba uwekwe hadharani kwa kuwa mwenye nchi ni Mwananchi na anapaswa kujua yaliyomo yamo.

Tupokee taarifa ya kusainiana mkataba huu kwa tahadhari sana.

Kama nchi tunalipishwa mabilioni ya dollar kwa mikataba mibovu viongozi wetu waliotuingiza kama hawajui kusoma na kuona kesho kwenye vision yao.
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima aliyekuwepo Ikulu wakati mikataba hiyo ikisainiwa alisema maaskofu wanasubiri kuona maandishi ya kilichomo ndani.

“Maaskofu wanahitaji kuusoma, kusikia tu hakutoshi. Walikuwepo watatu kushuhudia tukio na walipoitwa hawakuambiwa kuna nini, lakini walichosikia wameona angalau kuna kusikilizwa kwa maoni ya wananchi na maaskofu walikuwa wanawasemea kwa sababu rasilimali za wananchi zilikuwa hatarini,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
samia Hilo suala la hili limkataba la bandari ilikuwa afe kipa afe beki ilikuwa harudi nyuma na ndio mana kafanya aliyoamua kuyafanya ili DP uanze kazi bandarini.

Kuna ajenda ya siri sana inafichwa juu ya suala hili waTanganyika tuombe sana

Imagine mwarabu wa DP kabla hata hajaanza kazi bandarini keshafika Njombe kuangalia ardhi ili awekeze huko sasa unajiuliza wamekuja kwa ajili ya bandari au na mambo mengine?
 
Back
Top Bottom