VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Halikuwa jambo la kiungwana. Wahusika mnisikie na kunielewa. Jana, pale Ikulu Chamwino kwenye utiaji saini mikataba mitatu ya uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kati ya Serikali/TPA na DP World vilirushwa vijembe kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Tuliofuatilia tunajua kuwa pale ukumbini alikuwepo Askofu Liberatus Sangu kama mwakilishi wa TEC. Wahusika mkaanza kumtumia Mrisho Mpoto kurusha vijembe. Badala ya kughani au kuimba kama ilivyotarajiwa, Mpoto alitoa hotuba na kutamba alivyotaka.
Akadai kuwa kwakuwa mikataba sasa iko vizuri 'hata waliokuwa wanapinga wamehudhuria pale na watakula nao chakula'. Kila mmoja anajua kuwa waliotoa Tamko ni TEC. Na jana walikuwepo pale. Kwanini uwepo wao uonekane ni kuunga mkono mikataba iliyosainiwa jana?
Kiukweli, vijembe vya Mpoto na wengineo vilimkosesha amani na utulivu Askofu Sangu. Akajiweka 'busy' na kuchukua 'notes' huku akishindwa hata kuwatazama wazungumzaji au majirani zake. Askofu Sangu alikuwa kwenye wakati mgumu. Hakukuwa na haja ya mambo yale.
Kama maoni ya watanzania yamezingatiwa, tuonesheni mikataba iliyosainiwa jana!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mpwapwa, Dodoma)