TPA yaeleza sababu mkataba uwekezaji Bandari Dar kuwa siri

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
IMG_20231024_092823.jpg


--
Wakati baadhi ya wadau wakitaka kuwekwa wazi kwa mikataba ya uwekezaji na uendelezaji Bandari ya Dar es Salaam, Serikali imesema ni vigumu kutekeleza hilo, kwa kuwa ni kinyume na matakwa ya kisheria.

Mikataba hiyo ya miaka 30 ni ilisainiwa juzi Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Dubai kupitia Kampuni yake ya DP World.

Baada ya kusainiwa, baadhi ya wadau waliozungumza na Mwananchi, kwa nyakati tofauti walipongeza hatua hiyo na kutaka mikataba iwekwe wazi ili kuwapa fursa zaidi ya kuisoma na kuichambua kwa kina.

Miongoni mwa waliozungumzia jambo hilo ni Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Chama cha ACT-Wazalendo.

Katibu Mkuu TEC, Padri Charles Kitima aliyekuwepo Ikulu wakati mikataba hiyo ikisainiwa alisema maaskofu wanasubiri kuona maandishi ya kilichomo ndani.

“Maaskofu wanahitaji kuusoma, kusikia tu hakutoshi. Walikuwepo watatu kushuhudia tukio na walipoitwa hawakuambiwa kuna nini, lakini walichosikia wameona angalau kuna kusikilizwa kwa maoni ya wananchi na maaskofu walikuwa wanawasemea kwa sababu rasilimali za wananchi zilikuwa hatarini,” alisema

Mkurugenzi wa Jukata, Bob Wangwe alisema ili kujiridhisha na kauli kwamba mikataba hiyo imezingatia maoni ya wananchi ni vema ikawekwa wazi.

Kwa wao ACT Wazalendo walisisitiza hoja ya uwazi wa mikataba hiyo kwa jamii kwa kuwa Serikali inawajibika kwa wananchi wanaotakiwa kujua kilichomo.

Mikataba iliyosainiwa ni mkataba wa nchi mwenyeji (HGA), mkataba wa upangishaji ardhi na mkataba wa uendeshaji wa bandari gati 4 – 7 na uendeshaji wa pamoja wa gati 0 – 3 kati ya TPA na DP World kwa shughuli za kibiashara na za kiserikali.

Kauli ya TPA

Akizungumza na Mwananchi, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa alisema sheria za kimkataba zinazuia kuwekwa wazi kilichomo ndani.

Mbossa akizungumza kwa simu akiwa nchini Zambia kwenye ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan alisema mikataba ya kibiashara kwa mujibu wa sheria haiwekwi hadharani.

“Mkataba wa kibiashara kati ya TPA na DP World haitolewi hadharani kwa sababu kila mtu ana washindani wake,” alisema

Alisema kipo kifungu cha sheria kinachosisitiza usiri kwa pande zote na kuheshimu makubaliano na kikikiukwa kinaweza kusababisha kuvunjwa kwa mkataba na au fidia.

“Ukikiuka unaweza kusababisha kuvunja mkataba au kulipa fedha tena zinaweza kuwa nyingi tu. Lakini ukiwaonyesha washindani wake wanaweza kusema mbona hawa mmewapa mambo mazuri na ukiwaonyesha washindani wetu wanaweza kutumia vibaya. Lakini kama kuna mtu anataka kuiona kuna njia za kufuata,” alisema

Hata hivyo Mbossa hakueleza njia zinazopaswa kufuatwa kwa mtu anayetaka kujua kilichomo ndani ya mikataba hiyo.

Kauli kama hiyo ilitolewa pia na mmoja wa walioshiriki majadiliano ya mkataba huo ambaye hakutaka kutajwa jina lake akisema kisheria mikataba ya kibiashara haiwekwi hadharani.

“Jamani ile si ni mikataba ya kibiashara na kisheria inakuwa siri, sasa wanatakaje iwekwe wazi, tuvunje sheria?” alisema.

Mwananchi, pia lilizungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Harold Sungusia ambaye alisema kuwekwa wazi kwa mkataba kunatokana na makubaliano.

Alisema mara nyingi mikataba ya kibiashara haiwekwi hadharani kutokana na vifungu vya usiri vinavyotaka watu wachache ndiyo waone kilichomo.

Hata hivyo, mwanasheria huyo alisema kuwekwa wazi kwa mkataba huo kutasaidia kuongeza uwajibikaji na kudhibiti rushwa pamoja na kutoa fursa kwa wananchi kueleza maoni yao juu ya jambo hilo kwa kuwa lina masilahi ya taifa.

"Kwa miaka mingi, hata wabunge wamekuwa wakilia kunyimwa mikataba mingi ambayo Serikali imeingia na kampuni binafsi na hata wakiipata inaweza kuchelewa kujadiliwa na kufanya uamuzi juu ya suala hilo," alisema.

Kutokana na hilo, Sungusia alipendekeza mabadiliko ya kifungu cha sheria kinacholazimisha usiri ili kandarasi ambazo Serikali inatia saini ziwekwe wazi na kuongeza uwajibikaji.

Katika shughuli ya utiaji saini, Rais Samia alisema Serikali ilisikiliza michango na maoni mbalimbali iliyotolewa na TLS, vyama vya siasa, wanaharakati huru, vyombo vya habari, viongozi wa dini na wastaafu.

Chanzo: Mwananchi
 
Tutaipata tu maana hata IGA walitaka iwe siri lakini sasa tunayo, kuanzia kwenye preamble mpaka page ya mwisho yenye sahihi iliyokosewa
 
kwa hiyo spinning doctors waka shauri na makonda apewe Uenezi ...

issue ya makonda ime trend kuliko Mkataba wenyewe
 
Sheria ya mwaka 2017 sovereignty Act inataka mambo yawekwe hadharani.

TUNDU LISSU ATAKA UTHIBITISHO WA MAONI YA WATANZANIA KWENYE MKATABA WA BANDARI

View: https://m.youtube.com/watch?v=ESF8k8agTDo
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA ambaye yupo nchi Marekani ameibua hoja hiyo nzito wakati akiongea na diaspora ya waTanzania waishio nchini Marekani

Sheria hii haijafutwa na ilishindikana kurekebishwa baada ya jaribio la serikali kutaka kufanya hivyo baada ya Azimio la Bunge la June 10 , 2023 kuhusu kuuza bandari zote kwa DP World.

Kufuatia kushindwa kwa jaribio hilo serikali, basi ni wajibu umma ukafahamishwa kwa kuona kuna nini ndani ya mikataba 3 ya DP World kuendesha Bandari ya Dar es Salaam ambayo ni shirika la umma na pia ni sehemu ya maliasili za Taifa kama sheria ya mwaka 2017 Sovereignty Act inavyotamka .

Maliasili inayotamkwa ndani ya Sovereignty act 2017 ni mali ya watu (umma) maji, mito, bahari, anga, madini .

This 2017 Sovereignty Act declares permanent sovereignty of the People of the United Republic of Tanzania over all natural wealth and resources and provides with respect to exploitation of resources for the benefit of the people of Tanzania...

TOKA MAKTABA 2017:

Kupitia sheria ya 2017 sovereignty act, Prof. John Kabudi afafanua junsi Utajiri wa Taifa utakavyolindwa

View: https://m.youtube.com/watch?v=31G4xOXY5Dw&pp=ygUYU2hlcmlhIHlhIDIwMTcgbWFsaWFzaWxp
Waziri wa katiba na sheria, mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ameuwasilisha kwa niaba ya serikali sheria hiyo inapendekeza kulipa bunge mamlaka ya kupitia mikataba ya madini, mafuta, pamoja na gesi. Kwamba sheria ya 2017 inazuia mtu au kikundi cha watu kujitwalia kwa kificho cha mkataba na kutoa maamuzi ya jinsi mali ya asili ya Tanzania itakavyotumika ....
 
kwa hiyo spinning doctors waka shauri na makonda apewe Uenezi ...

issue ya makonda ime trend kuliko Mkataba wenyewe
Labda Makonda anakuja kuisisitiza serikali kuzingatia sheria inayokataza VPN...
Natania jamani siyo kweli.😃
 
Back
Top Bottom