Kassim Majaliwa: Namuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala la uhaba wa mafuta nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 12, Kikao cha 8, leo Septemba 7, 2023.

Ratiba:
  1. Hati za kuwasilishwa Mezani​
  2. Maswali kwa Waziri Mkuu​
  3. Maswali ya kawaida​
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Namuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala la ukosefu wa mafuta nchini.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekiri uwepo wa changamoto ya uhaba wa mafuta nchini wakati akijibu swali la Rashid Shangazi, Mbunge wa mlalo (CCM) aliyetaka kufahamu mipango ya Serikali katika kukabiliana na changamoto kubwa ya uhaba wa mafuta nchini.

"Kwanza nikiri kwamba tunazo changamoto za upatikanaji wa mafuta nchini kwa sababu baadhi ya vituo kwenye maeneo mbalimbali vimekuwa vikikosa mafuta na watanzania wanaohitaji huduma hii maeneo kadhaa tumeona wakiwa wanalalamika kukosekana kwa mafuta" amesema.

Waziri Majaliwa amesema zipo jitihada kadhaa zinazofanywa na Serikali kuondoa tatizo la uhaba wa upatikanaji wa mafuta na amemuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala hili, muhimu zaidi nishati yenyewe ipatikane nchini.
 
Mzigo mzito unambebesha jogoo! Kweli duniani kuna viroja.
 
Hiyo ndio itifaki inavyotaka , Rais anamuagiza PM, PM anamuagiza DPM, DPM anamuagiza Waziri, Waziri anamuagiza Karibu Mkuu na Katibu mkuu anawaagiza watendaji wakuu wa idara na taasisi zilizopo chini ya wizara na hao pia wanawaagiza watumishi wengine. Hapo hakuna mzigo mzito kwa mtu wala nini
 
... naona wamemtupia NWM kamba (uwaziri wa mafuta) na kacheo ka kishkaji kasikotambuliwa na Katiba kupunguza makali ya kundi lile. Watoto wa mjini ni hatari sana!
 
Hiyo ndio itifaki inavyotaka , Rais anamuagiza PM, PM anamuagiza DPM, DPM anamuagiza Waziri, Waziri anamuagiza Karibu Mkuu na Katibu mkuu anawaagiza watendaji wakuu wa idara na taasisi zilizopo chini ya wizara na hao pia wanawaagiza watumishi wengine. Hapo hakuna mzigo mzito kwa mtu wala nini
... unfortunately, it is the same person. Ajiagize mwenyewe halafu ndio amwagize KM!
 
Hiyo ndio itifaki inavyotaka , Rais anamuagiza PM, PM anamuagiza DPM, DPM anamuagiza Waziri, Waziri anamuagiza Karibu Mkuu na Katibu mkuu anawaagiza watendaji wakuu wa idara na taasisi zilizopo chini ya wizara na hao pia wanawaagiza watumishi wengine. Hapo hakuna mzigo mzito kwa mtu wala nini
Kwaiyo DPM anajiagiza?
 
"Kwanza nikiri kwamba tunazo changamoto za upatikanaji wa mafuta nchini kwa sababu baadhi ya vituo kwenye maeneo mbalimbali vimekuwa vikikosa mafuta na watanzania wanaohitaji huduma hii maeneo kadhaa tumeona wakiwa wanalalamika kukosekana kwa mafuta" amesema.
... soon baada ya tangazo la EWURA kupandisha bei za mafuta pump zote nchini zili-burst kwa kuzidiwa na wingi wa mafuta. Tatizo sio uhaba perse; kuna kitu kingine - nchi imekuwa ya cartels hii.
 
Back
Top Bottom