Waziri Mkuu Majaliwa ataka waajiri sekta binafsi kuzingatia afya za wafanyakazi kazini

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Wakurugenzi wa makampuni binafsi nchini kuzingatia afya za wafanyakazi mahala pakazi akidai kufanya hivyo ni kulinda haki za binadamu.

"Kwa kuwa nyinyi waajiri nitoe wito kwenu zingatieni afya ya wafanyakazi na usalama mahala pakazi"

Pia ameongeza kuwa "Nasisitiza kuwa usalama na afya mahala pakazi sio tu moja ya matakwa ya kisheria bali ni haki za binadamu"

Akisoma hotuba ya Waziri Mkuu aliyealikwa kuwa mgeni rasimi kwenye maadhimisho ya '200 CEO's Business Forum' yaliyofanyika Posta Jijini Dar es salaam Agosti 11, 2023,Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema kuwa "Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kulinda nguvu kazi ya taifa na mitaji ya wawekezaji na imeelekeza watendaji wake kuanza mchakato kuridhia mkataba namba 155 na ule wa namba 187."

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alituma mwakilishi ambaye alisoma hotuba hiyo, ambapo pia katika hotuba hiyo ilieleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji huku akibainisha kuwa milango yao hiko wazi kama kuna jambo lolote ambalo linaitaji maboresho.

Ikumbukwe baadhi ya wafanyakazi kutoka baadhi ya makampuni wamewai kusikika wakilalamikia mazingira ya kazi yanavyohatarisha usalama wao. Madai hayo yamekuwa yakitolewa kwa nyakati tofauti.

Taasisi ambayo imekuwa ikishirikiana na wadau kuandaa jukwaa hilo (200 CEO's Business Forum) ilibainisha dhamira kuwa kuchochea mabadiliko chanya kwenye sekta binafsi nchini na kuleta mageuzi katika kufanikisha uwepo wa mazingira rafiki zaidi ya kufanya biashara nchini Tanzania. Ambapo baadhi ya wadau wa karibu ambao wamefanikisha tukio hilo ni Benki ya CRDB ambayo mdau muhimu katika sekta binafsi nchini katika huduma za kifedha na biashara.

Jukwaa hilo limewakutanisha Wakurugenzi na wadau mbalimbali kutoka kwenye sekta binafsi nchini ikiwemo makampuni ya kibiashara, taasisi za kifedha na wadau wa kisera kutoka serikalini na kwenye sekta binafsi pamoja na washiriki wengine huku mijadala mbalimbali ikiendeshwa kwa lengo la kuibua hoja na maoni yanayoweza kuleta mabadiliko baada ya kuratibiwa na kuwasilishwa kwenye mamlaka husika.
 
Back
Top Bottom