Katikakatika ya Umeme na Uhaba wa mafuta yamtia kikaangoni Majaliwa mbele ya Wajumbe wa NEC, ashusha rungu kwa Mawaziri husika

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,545
2,175
IMG-20231128-WA0009.jpg

===

Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM), imeelekeza kupatiwa ufumbuzi wa haraka wa kero ya kukatika kwa umeme, upungufu wa mafuta ambao huwa unajitokeza ingawa si mara kwa mara na changamoto ya bei ya mazao ya kilimo.

Pia, katika kikao cha NEC kilichofanyika Novemba 29, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, wajumbe walijadili kuhusiana na huduma za afya, hususani kwa wazee, wajawaziti na watoto, pamoja na mpango wa bima ya afya kwa wote.

Hayo yalielezwa Novemba 30, 2023 na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, alipozungumza na wananchi wa Jimbo la Rufiji, mkoani Pwani, katika mkutano ulioandaliwa na mbunge wa jimbo hilo, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, kueleza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

"Chini ya Mwenyekiti Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kile kikao (NEC) kilifanyika siku nzima, mambo yote tuliyojadili ni yale yaliyohusu wananchi, tulijadili kuhusu kukatikatika kwa umeme, tatizo la mara moja moja la upungufu wa mafuta, tatizo la bei ya mazao; korosho, pamba, tumbaku, kahawa, alizeti na mengine yote," alisema Kinana.

Alisema, Rais Dkt. Samia alimtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kutoa majibu ya hoja zilizotoka kwa wajumbe wa NEC ambapo alifanya hivyo, akisaidiwa na mawaziri wakiwemo Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigilu Nchemba, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Ndugu Kinana, alisema kwamba wajumbe wa kikao hicho walizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.

Alisema, Mwenyekiti wa CCM Dkt. Samia, alimtaka Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdulla kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa ilani.

Kinana alisema, Mwenyekiti alisisitiza changamoto zilizozungumzwa na wajumbe wa NEC kuhusiana na sekta mbalimbali zipatiwe ufumbuzi mapema iwezekanavyo kama alivyowahi kuagiza siku za nyuma.

"Mambo haya utekelezaji wake utafuatiliwa kwa karibu na Mwenyekiti mwenyewe," alisisisitiza Makamu Mwenyekiti Kinana.
 
Nadhani majibu mazuri atupe Mwenyekiti / Rais sababu kuhusu umeme yeye ndio alichagua hata wale waliopwaya na kuondoka hence kumpa mtu mwanya wa plausible deniability kwamba alikuta mambo ni mabaya zaidi....

By the way wakati yeye anasema mpaka miezi sita alikuwa anatoa taarifa wapi (haya mambo ni kama kumpiga nyoka kwa kupiga mkia badala ya kichwa ) Siasa Siasani
 
Rule No 01.

States that, " The boss is always right"
 
Nili
VIVA CCM VIVA, VIVA MCHENGERWA VIVA, VIVA KINANA VIVA

View attachment 2830314
View attachment 2830318
Niliwahi kukutana na mjomba angu mjini akiwa anatokwa jasho eti akitembea kwa miguu kuelekea kijijini,akaniomba nauli. Kabla sijampa akeeleza kuwa alikuja mjini kwa usafiri wa bus kwa ahadi ya kupewa baiskel na nauli ya kurudia na viongozi wa CCM,ghafla tu baada ya hayo maelezo nikabadili sura na kuendelea na shughuri zangu.
 
View attachment 2830312
View attachment 2830332
===
Na MWANDISHI WETU

"Mambo haya utekelezaji wake utafuatiliwa kwa karibu na Mwenyekiti mwenyewe," alisisisitiza Makamu Mwenyekiti Kinana.

=====
Kwenye bima ya afya, serikali iache kufanya afya za watu kuwa biashara.
NHIF sasa wako zaidi kibiashara kuliko huduma.
Huwezi kukataa kumpa mtoto mdogo kadi ya bima ya afya ati mpaka wakusantane mashuleni.. Swali la afya ya mwananchi ni la serikali na sio la mtu binafsi.
Lazima serikali ibebe wajibu wake.
 
Nili

Niliwahi kukutana na mjomba angu mjini akiwa anatokwa jasho eti akitembea kwa miguu kuelekea kijijini,akaniomba nauli. Kabla sijampa akeeleza kuwa alikuja mjini kwa usafiri wa bus kwa ahadi ya kupewa baiskel na nauli ya kurudia na viongozi wa CCM,ghafla tu baada ya hayo maelezo nikabadili sura na kuendelea na shughuri zangu.
Ulimkosea sana ndg yako
 
Kutatua tatizo la umeme tunahitaji wataalam kuliko wanasiasa.
Hata hivyo, changamoto kubwa ni kwamba taifa huweka matumaini ya moja kwa moja kwa wanasiasa ambao waweza kuwa wajinga, wapiga deal kupitia makampuni ya kigeni, na kwa sababu ya ujinga wao wanadanganywa zaidi na zaidi.
Siyo rahisi kusimamia na kuongoza kitu usichokijua.
 
===

Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM), imeelekeza kupatiwa ufumbuzi wa haraka wa kero ya kukatika kwa umeme, upungufu wa mafuta ambao huwa unajitokeza ingawa si mara kwa mara na changamoto ya bei ya mazao ya kilimo.

Pia, katika kikao cha NEC kilichofanyika Novemba 29, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, wajumbe walijadili kuhusiana na huduma za afya, hususani kwa wazee, wajawaziti na watoto, pamoja na mpango wa bima ya afya kwa wote.

Hayo yalielezwa Novemba 30, 2023 na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, alipozungumza na wananchi wa Jimbo la Rufiji, mkoani Pwani, katika mkutano ulioandaliwa na mbunge wa jimbo hilo, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, kueleza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

"Chini ya Mwenyekiti Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kile kikao (NEC) kilifanyika siku nzima, mambo yote tuliyojadili ni yale yaliyohusu wananchi, tulijadili kuhusu kukatikatika kwa umeme, tatizo la mara moja moja la upungufu wa mafuta, tatizo la bei ya mazao; korosho, pamba, tumbaku, kahawa, alizeti na mengine yote," alisema Kinana.

Alisema, Rais Dkt. Samia alimtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kutoa majibu ya hoja zilizotoka kwa wajumbe wa NEC ambapo alifanya hivyo, akisaidiwa na mawaziri wakiwemo Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigilu Nchemba, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Ndugu Kinana, alisema kwamba wajumbe wa kikao hicho walizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.

Alisema, Mwenyekiti wa CCM Dkt. Samia, alimtaka Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdulla kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa ilani.

Kinana alisema, Mwenyekiti alisisitiza changamoto zilizozungumzwa na wajumbe wa NEC kuhusiana na sekta mbalimbali zipatiwe ufumbuzi mapema iwezekanavyo kama alivyowahi kuagiza siku za nyuma.

"Mambo haya utekelezaji wake utafuatiliwa kwa karibu na Mwenyekiti mwenyewe," alisisisitiza Makamu Mwenyekiti Kinana.
Kazi iendelee mbele zaidi
 
Back
Top Bottom