Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.


JIBU LANGU KWA MASATU NA WENZAKE

Masatu kati ya watu wote wewe usijitahidi kuwa mtetezi wa Amina na kuja na madai ya kujifanya kuwa hili suala ni "so private" kwamba halistahili kuzungumzwa na ya kwamba watu hawatakiwi kuulizia habari au kutoa maoni yao. Wakati sisi wengine tumezungumza tangu dei wani kuhusu binti huyu na msimamo wote haujabadilika na kutaka haki yake iheshimiwe na uhuru wake kulindwa wewe Masatu ulikuwa wapi? Tuliposema kuwa kuna mambo ambayo ni private na hili la vijana hawa (sikumchagua Zitto peke yake kama mnavyofanya nyinyi) ni jambo la aibu na wajibu wao (kama walichodaiwa kufanya ni kweli) kwanza kabisa ni kwa familia zao na familia zao siyo wana JF! Nenda usome maandiko yangu tena ya utetezi wa Amina na Zitto nikawaambia mapema kabisa hili suala tuache kama Zitto anataka kuja kusema atakuja kusema, mkasema najaribu kuwanyamazisha watu kwamba kuna mtu ambaye ni mkubwa kuliko hii forum. Kwa ujasiri na pasipo kigugumizi mkajitokeza "kutetea heshima ya forum hii".

Ni wewe uliyekuja na kusema
"chonde chonde jamani, tusiwaseme marehemu nawaomba sana".
Ingawa lengo lako lilikuwa ni zuri hata hivyo ulijikuta kuwa umesahau kile mlichokisimamia. Kwamba hakuna kitu ambacho ni private. Tatizo ni kuwa leo mmegundua kuwa mtu akifa kumbe anastahili heshima fulani na kuna mambo fulani ambayo ni private. Tatizo ni kuwa ni nyinyi mliovunja kanuni ya mambo binafsi na kwa uthabiti wa maneno yenu wenyewe mkadai kwa ujasiri kama kejeli kwa kauli mbiu yangu kuwa "yote yanazungumzika na kama tumewazungumza so and so basi tutazungumza mambo haya ya Zitto". Hivi kweli mnafikiri kama ni Zitto ndiyo angekuwa amekufa mngedai heshima hiyo?

Wakati tarehe 8 mwezi Mei niliposema hali ya Amina ni mbaya, na tukaanzisha na zile tsheti na tukasema mwacheni aseme. Kama hataki kusema asilazimishwe na kama anataka kusema asinyamazishwe wewe ulikuwa wapi? Niliposema, wamemnyang'anya simu na mawasiliano yoyote yale, na nikasema uhuru wake wa kikatiba umeingiliwa wewe ulikuwa upande gani? Au umesahau. Mshirika wa upande wako ajiitaye "Mtanzania" akaja na kusema hivi bila hata ya kufikiri ili kuniumbua kuwa mimi nasema uongo Ni kweli unaweza kufikiri natafuta ujiko, ujiko wa nini, silipwi, sigombei Ubunge, Amina siyo ndugu yangu, vijana wa Ukraine siyo wanangu, yule mama ambaye alifiwa na kijana wa kitanzania kule Zambia nikamsaidia atafute familia yake Handeni simjui mimi… binti aliyebakwa Dar na mbakaji kuachiliwa hadi nilipoingilia kati (of course u didn't know that) ni ujiko gani ninaupata mimi? Katika haya yote wewe ulikuwa wapi?

Kada Mpinzani akajenga hoja kunionesha kuwa mada yangu "silencing of an MP" haikuwa na msingi wowote na kusema hivi kwa mbwembwe zote za ajuaye Nikamjibu Kada Mpinzani kwa hekima ya mvi zangu:

Angalia Ukurasa wa 57 wa "Kashfa"

Leo nadaiwa kutenda dhambi kwa kusaidia mwili wa kijana wa kitanzania kurudishwa nyumbani baada ya kuuawa Brazili, linashikiliwa hilo kwenye shingo yangu kama nira, ati naambiwa ni kosa la milele nililolifanya kwa vile huyo kijana wanadai alikuwa ni muuza madawa. Nakubali kuwajibika kwa hilo. Ninawapenda watanzania wenzangu na sitawahukumu kiurahisi hivyo. Nikuambie mapema, leo Nchimbi akipatikana na madhara yoyote tutapiga kelele ukweli ujulikane kwani hatuko hapa kwa kutafuta kisasi. Soma makala yangu J'tatu ambapo nimemtetea Nchimbi. Wakati wewe na wenzako mnaangalia kila jambo nisemalo kwa mwanga wa "Uchadema na UCCM" mimi hilo sina, kwani maslahi pekee ni ya Tanzania na kiapo pekee nilichowahi kula ni cha kulinda Katiba ya Tanzania! Leo mtanzania yeyote akipata matatizo mahali popote duniani NITATUMIA uwezo wangu wote kumsaidia, nikishindwa nitatafuta watu wengine wasaidie! Hata watu tunaobishana hapa, sina kinyongo na mtu hata mmoja na wakitaka msaada wangu nitawapa 100% licha ya kwamba wengine watasema kwanini umsaidie yule?

Masatu, mmevunja principle moja kubwa na hiyo principle imeanza kuwavunja. Nakumbuka nilivyowasihi sana kwamba jamani tukubaliane kuna mambo private na mengine tuyaache hivyo. Na nikawahakikishia kuwa mkikubali kwamba hakuna mambo private kitakuja kuwageuka hamkuelewa ninazungumzia nini… Leo mmegeuka kama makamanda wa Privacy.. kwamba kwa vile sasa ndugu yetu ni marehemu basi kisisemwe kitu chochote, kwamba wakati sisi wengine tunapigia kelele tukaonekana wehu na watuwa kutafuta misifa leo mmejipanga mistari "kumtetea" Amina! Mambo mengine yanastahili kuwa na haya ngaa kidogo. Msimamo wangu wa kumtetea Amina tangu akiwa hai haujabadilika, haya ya kutunza usiri wa mambo ninayoyajua bado ipo, na kwamba kama Zitto anataka kusema jambo anayo haki hiyo na asipotaka nitaitetea haki hiyo mpaka kifo. Isipokuwa alazimishwe na mahakama vinginevyo hakuna cha kumlazimisha mtu kusema. Chombo pekee ambacho raia wanauwezo na haki ya kukilazimisha kufanya ni serikali yao.

Watu wanadai ati natafuta ujiko. Ujiko wa nini kwenye kifo cha mtoto wa watu? Furaha gani mimi ninapata baada ya kupiga kelele zote hizi? Ungejua jinsi moyo wangu ulivyoumia, ungejua jinsi undumbula gwangu ulivyochubuka, ungejuwa motema wane ulivyobubujika machozi, ungejua umtima wanene ulivyojisikia majonzi ungeelewa. Machozi yangu hayana ujiko! Naelewa mmezoea viongozi wababaishaji wanaofanya jambo ili wanufaike kwa namna fulani, naelewa mmezoea kupigwa porojo na ni vigumu kumpata mtu ambaye "what is you see is what you get". Najua watanzania tumezoea mazingaombwe na viini macho.... friends, what you see with me is what you get... what I'm saying online, is what I say in real life! Of course, I have my shortcomings and udhaifu...and believe me I have plenty.. ila kutafuta haki, usawa, kuwajibika viongozi nitasimama hata kama nitasimama peke yangu na kuwa kituko!

Masatu na wenzako, Mmevunja principle ya mambo binafsi baada ya kuhakikisha mmeshusha ile alama ya heshima na mambo binafsi chini mno, na kufikia kufikia kuwaita watu wazinzi, wezi wa wake za watu, wakatajwa mama zao hapa kwa kashfa n.k na nakumbuka nilikuuliza Masatu unafikiri vipi kuhusu mama wa Zitto kuletwa hapa na kuvuliwa nguo hadharani na mmoja wa mashabiki wako ukajibu "no comment"! Leo hii una ujasiri wa kuja kunishambulia hadharani hivi ati umegeuka kuwa mtetezi wa Amina na privacy! Give me a break! Watetezi wa Amina wapo na wanajulikana na hawahitaji sifa za mtu. Na jumatatu, tutaanza moja na tutaendelea jumanne. Kama kwa maneno yenu na kutumia msiba kuwa mtatunyamazisha hapa, ati kwa vile leo mko wengi, na ya kwamba mmeleta balance of power mmekosea. Hatunyamazi.

Nimewakalia kimya kwa sababu najua watu ni wasahaulifu, lakini mashambulizi yako hapo juu sikuweza kuyanyamazia, na you picked on a wrong dude… siogopi, sihofii, siabudu sanamu ya mwanadamu yeyote, sipendelei, sipendi.. na simama kwa upande wa wale wanaohitaji sauti. Kama unafikiri mkinifanya mimi kuwa mada itanifanya kwa namna fulani nipatwe na kigugumizi, wrong! never been scared, not today.. not ever! What is the worst that can happen to me? ABSOLUTELY NOTHING.

I'M OUT.. MEET ME MONDAY FOR THE FIRST DOSE OF REALITY
 
Hahahaha...Mwanakijiji kwa mikwara na wewe hujachacha...eti utatoa namba na anuani...
Nakumbuka sijui ilikuwa tanzatl...uliwahi kutoa anuani na watu wakaifuatilia and it was a dead end
 
Mwanakijiji,
Kifupi ni kwamba wote wanaomlaumu Zittto wana maana kuwa wanaamini kuwa marehemu Amina Chifupa alitembea nje ya ndoa!... Hii ni kumtukana marehemu na hata siku moja wasitake kuonyesha huruma kwa Marehemu hali swala la ngono linahusu watu wawili.
Inasikitisha sana kuona hawa jamaa wakimsakama Zitto kisha wanamwonea huruma marehemu ktk crime hiyo hiyo kama vile Chifupa alikamatwa kwa nguvu.
Nafikiri hawafahamu uzito wa maneno yao na ndio maana wengi humu wameanza kudai kuwa marehemu alikuwa mgonjwa wa ngoma!... haya yote ni matusi na Inshaallah mwenyezi ndiye hakimu wa mahakimu na mjuzi kuliko wote...
Kesho kwao!

Halafu huyu Nigger J na Mkapa (ktk picha) wamehusiana vipi na hii mada?
 
Mkandara kinachoudhi leo wanajifanya wana decence ya maadili mema! Bila woga hata haya wanajitamba ati ni "ndugu wa marehemu" na wanamtetea hapa..! Akitajwa Amina kwa jina baya walikurupuka kupiga kelele huku wao wenyewe wakimuita Zitto "mzinzi" na "mwizi" wa mke wa mtu! Halafu bila ya hata ya kupepesa macho wanatutaka tukae kimya tungojee muda wao! Walisema JF is bigger than anybody.. now they want to change the rules!
 
haikuwa dead end.. they just couldnt find it...Niwapatie hapa tena...?

I sure don't need it...
And neither has anybody asked for it here..at least to my knowledge
You just volunteered to give it out...so if you want to...go ahead and knock yourself out
 
Nyani... of course sikumaanisha wewe... I got enough threats.. so, kama wanasoma hapa wajue siwaogopi!!!
 
aaaahh, sasa hapa inakuwaje jamani mbona pamechafuka ! naona tena mwanakjj anakuja na kuniita mie shabiki wa akina masatu na wenzake, yaani kisa nilipinga hoja yako, sasa wapi huko tunakoelekea ? mie nilisema nilivyoona ( ndio uzuri wa uhuru wa maoni ) lakini sasa naona mzee nawe unataka kunisailensisha ! mwake humo ?kupingana hoja ni jambo la kawaida kabisa kama kweli tunataka mabadiriko hivyo usishangae kupingwa ! mimi sipo na mkataba na mtu yeyote humu aidha katika kukubaliana mambo au kupingana. naombeni tuwe watu huru jamani, tupingane na tusipigane wala kurushiana matusi.
 
nakubali ulichokuwa unasema ni kweli na sasa tumeyaona and i was wrong, nakubali hiyo ! kwa maana wote tulikuwa na different senses at the time making me wrong, and making u right ! lakini kamwe sitoweza kumpinga mtu yeyote hapa JF eti kwa kuwa fulani yupo against na fulani na kadhalika. am independent ! anyway naombeni tuwe huru katika kutoa maoni na tukubali kukosoana !
 
Never under estimate umuhimu wa madhehebu kwa wenye imani za kidini na haswa waislam

Sasa unataka kutuambia kuwa MASHIA ni sawa na SUNNI? sasa hiii hoja haiwezi kwenda mbele bila kukubali nafasi ya madhehebu na hukumu zao katika hili

mimi nilichoquote ni aya za Quran zinazozungumzia talaka tatu coz wewe ulisema katika uislam hakuna talaka tatu, jee ulisahau kuhusu madhehebu? kwa nini ulisema Medi na Amina hawawezi kurudiana tena kwa sababu wameachana kwa talaka moja kwa hiyo mpaka aolewe na mume mwengine ndipo yeye (Medi) aweze kumuoa tena, sasa ulisahau kama dhehebu lao lilikuwa linawaruhusu?
 
Jembajemba,

Ninavyofahamu mimi ni kuwa madhehebu yote ya kiislamu yanayofuata Quran yana hizo talaka tatu kama ilivyoandikwa. Ila yanatofautiana katika namna ya utoaji wa talaka tatu hizo kwa vile Quarani haikutoa maelezo hayo. Kuna madhehebu mengine yanakubali zitolewe tatu zote kwa mpigo, kuna madahebu mengine yanayoruhusu mwanamme kuandika talaka moja tu lakini aonyeshe kuwa ina uzito wa na talaka tatu, na kuna madhehenu mengine yanayotaka talaka hizo zitolewe kwa siku tofauti. Lakini swala la talaka tatu ni swala la kwenye Quran; hakuna madhehebu ya kiislamu yanaweza kufundisha nje ya Quran.
 

Kichuguu,

Nimekusoma mkuu, hata mimi hivyo ndivyo ninavyoelewa kuhusiana na talaka.

Sijui mwezetu (Barabara) habari ya talaka moja kaipata wapi? pengine ana Qurani yake?
 

barabaraya18,

tunakuomba kwanza ujibu suala uliloulizwa na mzee Kichuguu si unaruka ruka tu.
 
Kada, niwie radhi na nimesahihisha pale. I was a little bit fired up kutokana na post ya Masatu...no hard feelings.
 
kuna tuhuma kuwa mh zitto hakuenda kuuaga mwili wa marehemu mh chifupa

hali mabayo inaibua masuali mengi, na kuuliza huo ukaribu ambao yeye amejisifia kuwa alikuwa nao.



pia inatoa maswali kuwa zitto si rafiki wa kweli maana kwenye shida yeye hazuki.

yule ambaye anatuhumiwa na hata yeye mwenyewe marehemu mh nchimbi ameshiriki kikamilifu.

nnaomba wanaojua hili suali watukwekee bayana au ndio protokoli imemzuia???????
 


Mtumwitu,

Sio kwamba namtetea Zitto, ila yaonesha swala hili lajieleza toka bungeni:-
Spika alitangaza majina ya wabunge walioteuliwa kuliwakilisha bunge, na jina la Nchimbi likiwemo, isitoshe yeye ndo alikuwa mwenyekiti wamarehemu AC.

Jina la Zitto halikuwemo, kwa upande wa wawakilishi wapinzani. Hivyo kwenda kuaga mwili,angekuwa ametoroka bungeni. KOSA!.
 
Mtumwitu,

Swali lako linaweza kuwa na majibu mengi sana ambayo yote yanaweza kuwa sahihi. Jibu jepesi ni kuwa Zitto hakuwa amechaguliwa na spika kuwa mmoja wa wawakilishi wa bunge kwenye msiba ule, wakati huyu Nchimbi alikuwa ameteuliwa.

Unaweza kuuliza tena kuwa kwa nini asingelazimisha awe mmoja wao au kwa nini hakuja kama mwombolezaji binafsi. Jibu la swali hilo linategemea na taratibu za bunge kama inawezekana mbunge kughaili maagizo ya spika, na vile vile huenda kiungwana pia isiwe vizuri kujionyesha kwa mme wa Marehemu Amina ambaye alikuwa ameshamtuhumu Zitto kutembea na mke wake ambaye ndiye aliyefariki na walikuwa hawjamaliza tofauti hizo; siyo vizuri kuongeza chumvi juu ya jeraha. Kumbuka kuomboleza siyo lazima mtu ajionyeshe msibani; kuna wanoajionyesha lakini siyo waombolezaji halisi.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…