Karibu tushauriane na kupeana uzoefu wa manunuzi ya chakula kwa ajili ya mwezi mzima

Mafuta yapo ya alizeti lita tano.

Wewe itakuwa hauishi kwako au huenda huwa unapikiwa ndio maana huelewi vitu vingi
Badala ya Alizeti lit 5 inanu ua zaituni Lita 1 Tsh 20,000/= na Alizeti lit 2 Tsh 10000/= halafu panga matumizi utamaliza miezi mi 2 bila kununua mafuta ya kula/ kupikia
 
Kijiko kinawekwaje, nimekua interested hapa. Zikiwa kwenye mfuka au bakuli.?

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app

Mfuko wa plastic
IMG_1674.jpg

Ukishaweka unatia kijiko unafunga mfuko wako
 
Ivo vyakula vyote ukiviendekeza mwisho wa siku presha na kisukari vinakuhusu.
Unakula balanced diet. Wali kidogo ,nyama au samaki na mbonga za majani nyingi. Hakikisha kwenye sahani yako kuna wanga kiduchu,mboga za majani nyingi,nyama au samaki kidogo. Na maziwa walau glass moja.
 
Maharage yanachemshwa kg Moja yanaliwa Mara 6
Hizo mara sita piga mara kilo 3..mwezi utafika? Hata Kama unachanganya na majani...by the way...mboga za majani zinatakiwa ziliwe mda wote na vitu vingine...sio ziliwe peke yake...mambo ya Kula ugali mwiingi na majani ni utapiamlo Tu...
 
Unakula balanced diet. Wali kidogo ,nyama au samaki na mbonga za majani nyingi. Hakikisha kwenye sahani yako kuna wanga kiduchu,mboga za majani nyingi,nyama au samaki kidogo. Na maziwa walau glass moja.
We mama unajua lishe...angalau...huwezi kuniulia watoto Kwa utapiamlo...
 
Hizo mara sita piga mara kilo 3..mwezi utafika? Hata Kama unachanganya na majani...by the way...mboga za majani zinatakiwa ziliwe mda wote na vitu vingine...sio ziliwe peke yake...mambo ya Kula ugali mwiingi na majani ni utapiamlo Tu...

Eiish maharage 1Kg ule Mara sit na yasikutoshe monthly?

Kuna siku za nyama,samaki ,kuku soseji Dagaa,choroko njegere mbaazi?!?
 
Unaweza kushare vyakula unavyonunua na jinsi unavyovitunza ? Nimependa maelezo yako.
Hivi vyakula unaweza weka kwenye freezer.
Njegere.
Viazi, mihogo, ndizi mbichi...menya pack kwenye mifuko ya plastic. Wakati wa kupika unatoa kwenye freezer moja kwa moja jikoni usiache viyeyuke. Njegere usichemshe..unga moja kwa moja.
Nyanya kama huna friji ziweke sehemu kavu pamoja na malimao. Malimao hufanya nyanya zisiharibike mapema.
 
Habari za jioni wakuu,

Binafsi nimekuwa nikipitia changamoto sana nifanyaje au ninunue vyakula gani ambayo vitaweza kunifikisha mwezi mzima.

Naombeni uzoefu wenu katika hili, ni nini unazingatia, utaratibu upi unautumia kwenye kufanya manunuzi ya chakula.

Ukiweza kusema ni vyakula gani huwa unapendelea kununua na kuweka ndani itakuwa vyema zaidi. Asanteni, Uzi tayari.
Mimi uwa nanunua mchele, sembe, unga wa ngano, viazi, mafuta lita 5 kwa mwezi, nyama nanunua kwa wiki inachemshwwa inawekwa kwenye friji huku samaki mara moja moja napenda wakiwa fresh. Nyanya, mboga za majani na matunda hayo ni kila sku mbili maana inabidi yawe fresh. kinachobaki ni kuwabadilishia menu katikati kwa kuwanunulia vyakula visivyokaa
 
Mm nina familia ya watu saba nakaa nao huwa nanunua hivi..
1. Mchele 30kg
2. Sembe 10kg
3. Maharage 5kg
4. Sukari 10kg
5. Cooking oil 5kg
6. Dagaa 1kg
Vitu vingine huwa nanunua kidogo kidogo kama nyama wastani wa 2kg per week na samaki hivyo hivyo, sometime maini 1.5kg au hata utumbo pia 2kg. Nyanya sado moja,viazi sado moja,carrot 2kg, vitunguu 2kg, hoho 1kg
 
mchele kilo 10, unga muogo kilo 3, sembe kilo 6, samaki sato kg 4, nyama kg 10, mayai trei 1, sukari kg2 , chumv paket 3 . Vitu vingine bora uwe unanunua kwa wiki ili visioze kama nyanya , vitunguu maj/saumu, limao, matunda, mbogamboga, tangawz list kubwa sana..
Nyanya anaweza kununua sado halafu akazisaga.Akimaliza anazipika hadi zinawiva akiwa ameiwekea mafuta.ikipoa anaweka frijini inaganda inakuwa kama nyanya ya kopo tu.
 
Back
Top Bottom