Utafiti wa TWAWEZA Waonesha Gharama za Maisha, Ukosefu wa Ajira/Kipato na Uhaba wa Chakula Kuwa Mambo Makubwa Yanayowaumiza Watanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Shirika lisilo la Kiserikali la TWAWEZA East Africa linafanya uzinduzi wa matokeo ya utafiti mpya wa Sauti za Wananchi.

TWAWEZA itashirikisha umma matokeo hayo yenye uwakilishi wa kitaifa kutoka Sauti za Wananchi - ambalo ni jukwaa la kupigia kura kwa njia ya simu ya mkononi.

Utafiti huo mpya unaangazia maoni ya Wananchi kuhusu uchumi kwa jumla na hasa tozo ya miamala ya pesa kwa njia ya simu.

Sauti za Wananchi ni utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa kwa njia ya simu za mkononi, na unatoa takwimu za maoni ya raia kuhusu maendeleo katika jamii yetu.

Je, wananchi wana maoni gani kuhusu hali ya uchumi na tozo Nchini?

Je, tozo zimeathiri vipi matumizi yao ya huduma za pesa kwa njia ya simu?



UPDATES | 25 AGOSTI, 2022

Fuatilia Mubashara kupitia Chaneli ya Youtube ya JamiiForums



Takwimu zimekusanywa kutoka kwa wahojiwa 3,000 kuanzia Oktoba na Novemba 2021 na Juni na Julai 2022 kupitia jopo maalum la Sauti za Wananchi

Miongoni mwa yaliyomo kwenye Ripoti hiyo ni pamoja na Nusu ya Wananchi waliohojiwa wataja masuala ya Kiuchumi kuwa changamoto kubwa inayokabili Kaya zao

- Gharama za Maisha, Ukosefu wa Ajira n.k
Karibu nusu ya wananchi wote waliohojiwa (48%) wanataja kupanda kwa gharama za maisha kuwa miongoni mwa matatizo matatu makubwa yanayozikabili kaya zao kuliko masuala mengine. Ikifuatiwa na ukosefu wa ajira na fursa nyingine za kujiingizia kipato (29%), vile vile tatizo la njaa na uhaba wa chakula (26%).

Matatizo haya matatu makubwa yanayozikabili kaya nyingi nchini Tanzania yote ni masuala ya kiuchumi.

- Athari za Uviko-19, Vita ya Ukraine na Urusi
Uchumi wa Tanzania umekumbwa na matatizo miaka michache iliyopita ikiwemo Janga la UVIKO-19, lililotikisa Uchumi wa Dunia Vita ya Ukraine na Urusi imesababisha kuongezeka kwa bei ya Mafuta na Vyakula Duniani, huku Tanzania ikiwa haijachukua hatua za kutosha kukabiliana na hilo

- Matatizo Kwenye Huduma za Kijamii
Mbali na matatizo ya Kiuchumi, Wananchi wametaja matatizo mengine kwenye Huduma za Kijamii ikiwemo Vituo vya Afya (23%), Upatikanaji wa Maji safi (20%), Huduma za Usafiri (17%) na mapungufu katika Sekta ya Elimu (15%)

- Je, Nchi Ipo Kwenye Muelekeo Sahihi?
Wananchi wanaosema Nchi iko kwenye mwelekeo sahihi ni 30%, haiko kwenye mwelekeo sahihi ni 25% na wenye hali ya sintofahamu ni 44% Matumaini yao kuhusu Uchumi yako chini sana. Wanaosema hali ya uchumi ni mbaya ni 41% na wanaosema ni mzuri ni 9%

Kuna tofauti ndogo ya mtazamo kati ya makundi ya watu kuhusu mwelekeo wa jumla wa nchi. Kutokuwa na uhakika kunabaki kuwa mtazamo mkubwa. Wakati wananchi wenye umri mkubwa wanasema nchi kwenye mwelekeo mzuri, wakazi wengi wa Dar es Salaam wanaona nchi haina mwelekeo mzuri.

- Vipaumbele vya Wananchi
Vipaumbele vikuu ambavyo Wananchi wangependa Rais ashughulikie ni gharama kubwa za Maisha (46%) na ubovu wa Vituo vya Afya (42%), Huduma duni za Usafiri (35%), Ubora wa Elimu (28%) Kukosa kazi/ Fursa za kuingiza kipato(27%), Upatikanajiduni wa maji safi (17%) nk

- Kuboreshwa Huduma za Kijamii
Aidha, Wananchi wanasema wameona kuboreshwa kwa Huduma za Kijamii katika kipindi cha Miezi 6 iliyopita, hasa Sekta ya Elimu (68%) Pia, Uhuru wa Kujieleza umeboreshwa (60%), Uhuru wa Kisiasa umeimarika (56%), Ulinzi na Usalama (59%)

- Wakazi wa Dar na Ukosefu wa Ajira na Fursa za Kipato
Wakazi wa Dar es Salaam wanalalamikia zaidi tatizo la ukosefu wa Ajira na fursa nyingine za kipato tofauti na wakazi wa maeneo mengine Pia, wanataja kukabiliwa na masuala ya uhalifu na usalama, ingawa matatizo haya ni madogo kwenye maeneo yote.

- Mitazamo Yakinzana Miongoni mwa Wananchi kuhusu Suala la Kodi
Katika kodi, wananchi wengi wana mitazamo inayokinzana kwa wakati mmoja Karibu wananchi wote (90%) wanakubaliana na wazo la msingi kwamba kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi. Lakini wengi (75%) wanasema kuwa kodi ni kubwa na watu wanahangaika kuilipa. Uchambuzi wa kina unaonesha kwamba kuna mkanganyiko wa wazi kabisa kuhusiana na maoni ya wananchi juu ya mfumo wa kodi. Karibu wote (88%) wanasema wangependa kulipa kodi bila shuruti, na wengine (67%) wanasema si vyema kuficha kipato ili kulipa kodi chini ya kipato.

- Wananchi Wapo Tayari Kukwepa Kodi
Hata hivyo, wananchi wanne kati ya kumi (42%) wanasema wangekwepa kulipa kodi kama wangeweza kufanya hivyo. Asilimia 63 ya wananchi wanasema ni wajibu wa wote kulipa kodi, hata kama huduma ni mbovu, lakini nusu (51%) wanasema kwamba huduma mbovu za jamii zinahalalisha ukwepaji wa kulipa kodi. Kwa hakika hizi ni kauli tata, inaonesha kwamba wananchi wana mvutano kati ya kufanya jambo sahihi na vishawishi vya kukwepa kulipa kodi.

Sababu kuu iliyotolewa ya watu kukwepa kodi ni kuwa watu wanahisi viwango vya kodi ni vikubwa mno Wananchi wanne kati ya kumi (39%) wanasema watu wanakwepa kulipa kodi kwa sababu wanahisi viwango vya kodi ni vikubwa, zaidi ya sababu nyingine yoyote. Sababu nyingine zilizotolewa ni pamoja na dhana ya kwamba hawalipwi mishahara mizuri (20%), kwamba kodi hazitumiki vizuri (15%), au kwamba watu hawajui namna ya kuwasilisha kodi zao (11%).

- Ugumu wa Wananchi Kuanzaisha Biashara
Wananchi wanahisi kuna ugumu katika uendeshaji wa biashara, lakini pia serikali inaboresha mazingira ya biashara. Idadi kubwa ya wananchi (88%) wanakubaliana na maoni kwamba gharama za kuendesha biashara zimeongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita. Idadi karibu sawa na hiyo (80%) pia inakubaliana na maoni kwamba kodi na ushuru vipo juu na ni vikwazo katika ukuaji wa biashara.

Hata hivyo, wananchi wengi pia wanakubali kwamba mazingira ya sasa ya kisiasa ya nchi (73%) na hali ya kiuchumi (63%) ni nzuri kwa biashara. Wengi pia wanakubali kwamba serikali inatengeneza fursa kwa biashara ndogo ndogo (72%) na kwamba sasa kuna fursa nyingi za biashara kuliko ilivyokuwa mwaka uliopita (67%).

- Huduma za fedha kwa njia ya simu zinatumiwa sana na wananchi
Idadi kubwa ya wananchi (75%) walieleza kuwa walitumia huduma za fedha kwa njia ya simu mwezi uliopita, ambapo nusu (47%) walifanya hivyo wiki iliyopita. Matumizi ya huduma hizo ni makubwa miongoni mwa makundi yote ya watu, lakini matumizi ni madogo kwa wale walio na viwango vya chini vya elimu na wale wanaoishi kwenya kaya zinazotegemea kilimo kama chanzo kikuu cha kipato chao

- Tozo za Miamala
Wananchi wengi wanafahamu kuwa kodi na tozo za huduma za fedha kwa njia ya simu ziliongezwa mwaka 2021 (80%) na zaidi ya nusu wanafahamu kuwa tozo hizo zilipunguzwa baadaye (55%)

Wananchi walio wengi hawakubaliani (23%) au hawakubaliani kabisa (34%) na tozo tangu ilipoanzishwa mara ya kwanza. Hata hivyo, walipoulizwa maoni yao kuhusu kupunguzwa kwa kiwango cha tozo, bado wananchi wengi zaidi hawakubaliani (32%) kuliko kukubaliana (18%) na mabadiliko hayo

- Wananchi Wapunguza Kutuma Fedha kwa Njia ya Simu
Wananchi wengi wanaripoti kupunguza kutuma fedha kwa njia ya simu tangu Julai 2021 (44%) kuliko wale wanaoripoti kuongeza kutuma fedha kwa njia hiyo (15%). Idadi ya wanaopokea fedha kwa njia ya simu imepungua tangu Julai 2021 (46%) kuliko wale wanaoripoti kupokea zaidi (14%). Wakazi wengi wa Dar es Salaam wana ripoti kupunguza kutuma/kutumia pesa kupitia huduma za fedha kwa njia ya simu (71%).

- Wananchi Wengi Hawajui Mapato ya Tozo Yanatumikaje
Wananchi hawana uhakika kuhusu matumizi ya mapato yatokanayo na tozo. Wananchi wengi wanasema hawajui (42%) mapato ya tozo yanatumikaje kuliko wanaosema wanajua (38%)

- Wananchi Wanakubali Kodi ni Muhimu Lakini Imekuwa Kubwa
Karibu Wananchi wote (90%) wanakubaliana na wazo la msingi kwamba kodi ni muhimu kwa maendeleo ya Nchi Lakini wengi (75%) wanasema kuwa kodi ni kubwa na Watu wanahangaika kuilipa.

- Wananchi Wangependa Kuona Mapato ya Tozo Yakienda Kwenye Miradi ya Maendeleo
Wananchi wangependa kuona mapato ya tozo za Miamala ya Simu yakielekezwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo lakini kipaumbele kikiwa Huduma za Afya (57%), Elimu (50%), ikifuatiwa na Ujenzi wa Barabara (38%) Huduma za Maji (33%), Umeme (20%), Kilimo (18%) na Mikopo (17%)

- Wananchi Wengi Hawana Uhakika na Mwelekeo wa Nchi
Kuna tofauti ndogo ya mtazamo kati ya Watu kuhusu mwelekeo wa jumla wa Nchi. Kutokuwa na uhakika kunabaki kuwa mtazamo mkubwa Wakati Wananchi wenye umri mkubwa wanasema Nchi ipo kwenye mwelekeo mzuri, wakazi wengi wa Dar wanaona Nchi haina mwelekeo mzuri
 
Ila jamaa alikuwa fala sana. Sasa ukiwa critisized ndiyo umnyang'anye mtu hati ya kusafiria? Hata aliokuwa anawatuma wafanye ujingaujinga na wao ni ng'ombe fulani hivi.
Na hakuna taifa linaloweza kusonga bila criticism. Mapambio na ngonjera kwa watawala hazitupeleki popote.

Nasubiri tu nisikie maoni ya watu juu ya tozo kwenye huo utafiti. Huenda yule kijana wa Lameck akajifunza jambo.
 
Hao Twaweza niwapiga debe tu yaleambayo wao wanayataka ndio majibu ya watanzania wanayaraka wanakuwa na madalali wao kile wanachokisema nitofauti nahali ilivyo mitaani nikama kule Kenya wakusanya maoni walisema odinga anashinda matokeo kapigwa kashindwa kutoa hata drooo.
 
Chanzo cha matatizo yote hayo ni UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019 NA UCHAGUZI MKUU 2020 uliojaa ukiritimba, matumizi mabaya ya nguvu
 
Na hakuna taifa linaloweza kusonga bila criticism. Mapambio na ngonjera kwa watawala hazitupeleki popote.

Nasubiri tu nisikie maoni ya watu juu ya tozo kwenye huo utafiti. Huenda yule kijana wa Lameck akajifunza jambo.
Naunga mkono hoja.
 
Who knows if those are cooked data? Ebu acheni ujinga, hao wanatafuta hela za wafadhili ili waonyeshe wanafanya utafiti na wafadhili watoe fedha. Simple question, huo utafiti hewa utaisaidia nini serikali? Tuwe wakweli, hawa ni wapiga dili kama wengine tu ili wapate fedha za sponsors wao, ila hakuna kitu hapo ktk utafiti hewa huo kitasaidia wananchi au serikali.
 
Watu 30,000 kwenye taifa lilo na idadi mkisio wa watu millioni 60 hu utafiti kwangu bado ni batiri hauna majibu sahihi kwa matatizo ya wananchi
 
Naona gharama za maisha kupanda zimekuwa changamoto kubwa sana hasa kwa wananchi wenye kipato cha chini na kisichoeleweka. Serikali ina cha kujifunza kupitia takwimu hizi. Uvumilivu una mwisho.
 
Back
Top Bottom