True Story: Nimefanya ngono zembe na binti mwenye VVU, Leo siku ya 28 toka tukio. Nina stress ya hali ya juu. Nahitaji kupata neno la tumaini

Mfalme_wa_Nyika

JF-Expert Member
May 24, 2023
389
863
Wakuu ni alfajiri hii siku ya leo, usishangae kwa nini nimeshika simu nakukaa kuandika uzi huu badala ya kujifunika gubigubi blanketi, hapo ujue ni kuwa usingizi umenipaa na dakika kadhaa zilizozopita nimetoka kumaliza kumeza kidoge kimoja kukamilisha dozi yangu ya siku ya 28 ya dawa za PEP ( dawa za dharula anazopewa mtu kuzuia kama alipata maambukizi ya VVU basi virusi hivyo visiweze kushika hatamu katika mwili wake na kumuathiri.

Nisiwachoshe, story iko hivi, sitasahau siku hiyo nilikutana na huyo binti (mwanachuo) takribani tarehe za mwanzoni hivi mwezi April 2023, nilikua narudi chuo kwani huwa nasoma masomo ya elimu ya uzamili katika chuo kikuu kimoja hapa nchini , na kwa kuwa siku za juma asubuhi mpaka jioni huwa nafanya shughuli zangu kwani mimi ni mtaalamu katika fani fulani basi katika harakati zangu zakujiongezea hii elimu ili kuweka sawa muda mimi huwa nasoma masomo hayo vipindi vya jioni hata usiku kulingana na ratiba za wakufunzi.

Basi siku hiyo nakumbuka nilikua naingia chuoni, nikiwa katika gari langu nikikatiza maeneo ya chuo ebana jicho langu katika kupepesa likatua kwa kikundi cha warembo watatu, walikua ni mafuta mno takribani wote na ni watoto wabichi ambapo kwa macho yangu nilijua wako katika their early 20's, basi moyo dhaifu nikawiwa kusimama maana roho iliuma kuacha kujaribu bahati labda nitapata mahali pakupoeeza upweke na ugwadu nilionao. Kwa maana mimi maisha ninayoishi ya jiji nililopo siyapendi yaani ni kazi tu na masomo ndio inaniweka hapa ila hili jiji silipendi kabisa hasa ukizingatia mimi ni mwanaume niliyekulia mikoani sehemu zenye utulivu wa hewa baridi flani nakutokuwa na msongamano na maisha stress. Hivyo nikiwa hapa mimi na kazi tu na masomo mara ukishangaa siku imeisha kesho tena inakuja mzunguko ule ule unarudi.

Basi pia katika umri nilionao nina mpenzi ila wa long distance kwani naye yuko huko ughaibuni kimasomo na ni takribani mwaka umepita hatujakutana kimwili hivyo bana siku hiyo kuona hao warembo pepo likaniingia nikasema nimechoka kukaa kinyonge no sweat nijitose.

Kifupi mimi sinaga makuu na najijua kuwa ni mtaalam sana wa mambo ya seduction ( kumuimbisha au kumuingia mwanamke mpaka akuelewe akupe unachotaka). Kwa kuwa nilikua kwenye gari ikabidi nifanye kuwapita kwanza nakuenda mbele yao kidogo kupaki gari nakushuka, ili kuepuka ushamba wa wanaume wengi (maana nimekuwa nikiona washkaji zangu wakifanya hivyo nakuambulia dharau kwani sio wanawake wote utawatisha kwa gari) kuwaita wasichana kwa miluzi ya psiii au ishara ya mikono wafatwe kwenye magari yao.

Basi nikarudi nyuma kuwaelekea mabinti hao wasomi na wao waliona kabisa jamaa kasimama kwa ajili yao na nilipenda hilo. Basi macho yangu yalikuwa kwa Janeth (code name) pisi kali kuliko zote katika ule utatu wao wakumeremeta. Sikufanya ajizi nikawasalimu wote nikamuomba Janeth asimame niongee nae kidogo wale wenzake kama kawaida wakatangulia mbele. Pisi alionesha ushirikiano maana sijisifii ila mimi ni aina fulani ya wale wakaka ambao almost kila mwanamke atavutiwa tu na mimi maana ndio imekuwa hivyo, sipatagi tabu kukubalika. Nikawa straight nikamweleza nia kuwa nimevutiwa nae akanipa namba zake basi nikawacha aendelee na rafiki zake mimi niwahi ratiba zangu za masomo yangu.

Sikumtafuta mpaka kesho yake, tukaanza ku click kwenye mawasiliano vibe kama lote kutoka kwa hako ka binti, kumbe nilikua naukimbilia moto bila kujua wala kuwaza.

Basi kwa kuwa unajua ratiba zangu ni kazini masomo ya jioni na nyumbani basi siku zinakuwa zinaisha kwa kasi na katika jiji hili busy lenye makorokocho mengi sikushangaa ilipita takribani wiki tatu sikuwa nimekutana kwa kumuona in person yule binti ila mawasiliano yalikuwa takribani kila siku and almost every moment, kwani ombi langu lilikuwa tayari limeshaafikiwa na akawa pisi yangu.

Basi siku moja nilipanga kukutana nae tukawa na day out kula na kutembea pamoja ili kupata kumfahamu nakumkagua zaidi kuona niliona vema au nilipigwa upofu.

Kiukweli nilichagua na nilijua nilichagua maana kila nilipokuwa nae macho yalikuwa juu yetu mpaka mademu wenzake tukiwa tunapita mahali niliona walikua wanamuangalia wengine jicho la wivu hivi au appreciation, usiseme wadume sasa macho kodo maana pisi ni pisi hakika.

Siku ile sikuwa na mbwembwe mimi huwa sipotezi muda ila niliona tu ile siku nisifanye lolote kwani nilimrudisha hostel yake mimi nikarudi maskani nilipopanga kwenye hili jiji ninalolichukia.

Nakumbuka ilikuwa takribani wiki ikapita katika tarehe za mwishoni mwa mwezi uliopita April, binti akanipigia kusema anaweza kuja kuspend time na mimi maskani home, nikasema kwisha mambo mazuri hayataki haraka hujileta yenyewe kama vile yaani, yaani usilolijua ni kama usiku wa giza ila siilaani siku ile maana sikujua kwa kweli ila ningejua nisingependa hata nimkaribishe.

Binafsi mimi huwa napenda mno afya yangu, na kifupi ndio maana niko makini sana kuchagua pisi na sipigi hovyo ndio maana almost mwaka ulikua umepita sijapiga ila sijui pepo gani aliniambia nijaribu kupunguza oil after all this time za ugwadu. Basi binti alipokuwa anakuja nikaanza kujiandaa kuwa na silaha incase lolote likitokea, nikawaza swala la what if huyu demu ana ukimwi!? Hilo wazo halikuingia akilini kabisa kwa jinsi nilivyomuona ila lilibaki akilini.

Nikapata wazo nimpigie mate wangu flani Daktari hospitali moja anipatie vipimo nimtume boda akawa hapatikani, basi bado kama kuna kasauti kakaniambia mtume boda hata kwenye pharmacy yakaribu akanunue.

Nikampigia simu akaenda juu kwa juu lakini akanirudia akaniambia amekosa , wakati huo mtoto tayari ndani ya nyumba keshafika kajilaza sofani anaangalia netflix na glass ya wine mimi niko jikoni napika something special maana kiukweli siku ile ilikuwa public holiday.

Kwa wale wanaume msioingia jikoni msiniseme sana kifupi nimekulia mazingira naona baba na mama wakiingia jikoni nakupika na wazee wako leo mwaka wa 45 kwenye ndoa. Na pia nimekuwa nikitengwa na kuwa mwanaume with specialty flani hivi nakupata point sana kwa mapisi yangu wakiona najua kupika hasa nikiwapikia mara moja moja.

Basi kila kitu kikawa sawa chakula na vinginevyo nikawa na pisi tumekaa, yeye alikua yuko kwenye boyfriend jeans flani na top alikua matata mno, nikamwambia ingia chumbani kuwa huru vaa something lightly huoni joto hili basi akaingia avaa moja ya vest yangu nakurudi pale seating room akiwa na chupi tu kwa chini.

Hakika nilipata tabu kuona hizo paja ile habari yakuwaza ukimwi ikawa imefutika kabisa. Nikawa tu nawaza kwa mchecheto kama papuchi hiyo iko hapo ni wewe tu. Niliogopa nikasitq nikasema mbona kirahisi hivyo?

sikuwaza sana na kwa uzoefu kwa kuwa sio mara ya kwanza kukutana na binti wa sampuli hiyo nilijua tu watoto wa kizazi kipya usasa mwingi mambo ambayo ninayapenda.

Kifupi kwa mkoa niliotoka wanawake wa huko ni wababe halafu wanajifanya kujua kukaza mno ilihali ni wachumba tu, demu unaweza muita maskani akaja kavaa minguo saba utadhani mwanajeshi, chupi juu yake tight juu yake ki hot pant juu yake msuruali juu yake mtandio ilimradi tu akupe tabu kwenye shughuli kutaka kumla tunda. Ila nilisema sipendi jiji hili ila kiukweli napenda wanawake walokulia jijini jinsi wako open minded kama ipo ipo hakuna kuvunga wala kusumbuana.

Na Janeth nilidhani ni mmoja wao hivyo alinikosha roho.

Mimi ni mmoja wa wale watu wasemao hatunywi pombe kabisa bali tunakunywa wine( as if wine sio pombe🤣), hivyo kwa habari ya afya na shughuli ilokuwa wazi na dhahiri mbele yangu nilijipatia a glass or two.

Nikawa tipsy kidogo baada yakula na kunywa nikajikuta tu katika lindi la mahaba, jemedari nilikua nauza mechi, mtoto alikua mzuri hakika na mimi sikuwa na kondomu wala nini nilijihakikishia tu mtoto yupo salama na kwa ile hali nilijikuta nishamsabahi kila pande za mwili wake.

Game ilianza kwenye mida ya jioni saa 10 hivi, nilimuandaa mtoto na alikuwa receptive kweli kwani sio kwa utelezi nilioupata, kwa ugwadu niliokuwa nao na ili nienjoy tu mtoto si utani nilikamia show kwani nilipiga mashine kwa takribani saa moja ndio nikamaliza kuwatoa wazungu.

Ila sijui ni mazoea au nini maana pamoja na utelezi wote nilikua najisikia tu kuongeza vilainishi kwa kuwa binti alikua hakatai ( maana kuna wanawake hawapendi uongeze mate au mafuta kwenye papuchi zako kudai sijui watapata nini nk sijui) basi mimi nawa namimina mifuta zaidi ili mradi niteleze triiiiiii mpaka mecca.

Nilienjoy show huku nikiepuka kuona kuchubuka . Na sijui kwa nini nilikua niko hivyo siku hiyo maana hofu yakuchubuka iliniingia nikawa natoa show kweli ila kwa tahadhari kuongeza vilainishi nk kwani hata mara baada yakumaliza niliwahi bafuni hatua tatu tu kutoka kitandani nakukojoa nakunawisha dushee actually kuoga na maji tiririka ili kwa imani kuwa sitapata maambukizi yeyote.

Ikumbukwe kuwa mpaka hapo sikuwa najua lolote kuhusu status ya afya ya yule binti nilikua nafanya yake kama desturi yangu tu. Basi baada ya gemu naye aliogopa ili mimi niliwahi kabla yake nikimwacha yeye hoi kitandani baadae kujikusanyana nakuoga.

Basi tukiwa naked, nilienda kuleta matunda kutoka kwa fridge, ndizi na tikitiki maji, nikawa nakula kula mimi ni mpenzi sana wa matunda hayo. Mtoto pembeni kaiva kumbe nilikua niko nacheza na grenade au bomu lakutega ardhini kwani mimi nilikua na habari sasa, mara tu baad ya dakika kumi kumi na tano nikajikuta narudia round, hii round kama ilivyo ya awali nilifanya kwa takribani dakika 30 mpaka 40 hivi kwa mujibu wa saa kwani mida ya saa moja moja na hivi usiku nilikua nahitimisha. Kama kawaida nikatumia mbinu zangu za desturi.

Basi katika ile tumelala tunapiga stori mbili tatu guilty conscious ikawa kama imeniingia si unajua majuto mjukuu, basi nikawa napiga stori mbili tatu kutaka kumchimba nakumjua binti huyo kwa undani, basi akaanza kuniambia kuhusu familia yao kuniambia mama yake amekuwa mgonjwa muda mrefu nk nikamuuliza mgonjwa wa nini akawa anasema kisukari nikamuuliza sio na magonjwa mengine akawa anasema hapana ila dalili zote zilikuwa kama sio kisukari na binti kama ananificha jambo, nikiangalia pia umri wa binti kichwa kikanicheza nikaingia wenge kuwaza mbali sana nikasema what if mamake ni ukimwi na what if huyu demu alizaliwa nao!?

Nilikosa tu amani, yaani sijui hata niliunganishaje doti ila niliwaza hivyo tu nakukosa amani, nikasema hakika hata kama nimekumbuka shuka asubuhi kumekucha ili niwe na amani nijue afya ya huyu binti. Basi nikafanya kumrudia mshikaji wangu dokta, huyu yupo next mtaa jirani, lahaula akapatikana akaniambia yuko kwake nimtume mtu ampe vipimo nikamvutia waya yule chalii wa boda akaenda, zana hizo hapo.

Mimi nilikua nishajipima siku moja iliyopita na my last kipimo kilichokuwa hapa maskani basi kwa kuwa hofu yangu ilikua yule binti nikamwambia tupime akafanya masiraha sawa akijua namtania ile kuona niko serious na zana mkononi akawa anaanza kulia kuleta excuse ooh mara naogopa sindano nk mara sitaki bana wakati mwingine, mimi nikawa nasema kimoyomoyo huyu fala (ashakuwa fala hapo sio pisi kali dakika chache zilizopita chezea hofu ya kifo wewe) Hanijui vema nikatumia busara kumshawishi akagoma sababu anayotoa sioni ina mashiko basi nikasema hapa huyu haondoki na gemu haliendelei mpaka nijue status yake, ili kuweka usalama na ushahidi vema nikapanga mpango wa haraka na kinyamera kichwani, nikasema hapa by hook or by crook atapima.

Niligeuka mbogo, nikaingia chumbani nikampigia jamaa angu flani hivi tunafanya nae kazi aje chap. Mpango nikiwa bao kichwani nikamwambia yule binti poa kwa kuwa hataki kupima basi nimrudishe hostel ila kuna jamaa angu anakuja basi tumsubiri tuende nae tumdrop yeye hostel mimi niendelee na mishe flani na jamaa angu usiku ule. Demu akiwa haelewi kichwa changu kinawaza nini, jamaa akaja, pale getini nikimpokea nikampa mchongo mzima kwa dakika chache tu huku tukiingia ndani, akamsalimia shem mimi nikazuga baada ya muda tusepe.

Nikawasha gari, hapo ni tupo watatu mimi na jamaa angu workmate na huyo manzi. Njiani ukimya ulitawala nikiwaza kutimiza mpango bila huruma ili nijue tu nikiweza nijiokoe nafsi. Basi maeneo ninayokaa kuelekea hostel kwake basi unapita chuo tunachosoma wote basi kuna miti mingi na msitu, nikaingiza gari pembeni ya barabara nakuingia ndani kwenye miti kisha nikapipa break nikazima taa.

Jamaa angu katulia si anajua mpango, basi nikamgeukia binti nikamwambia skia, nimekuheshimu ila naona hujiheshimu, umeshiriki ngono na mimi hivyo ujue tumeunganishwa na shida zako zinaweza nihusu and vice versa, hivyo nataka kujua hali ya afya yake. Ili kuepusha lolote tunaloweza kukufanyia hapa bila ushahidi wowote hapa utapima utake usitake.

Binti akaingia wenge maana mimi nilikua nimepaniki macho mekundu stress maana nilikua naona kuna kitu huyu binti ananificha, nikamuuliza uko salama, akasema ndio, nikasema leta mkono tupime, kifupi niko na utaalamu wakupima mtu utadhani ni daktari profesional lakini ujuzi huu ni katika kujifunza tu kutoka kwa machalii angu madaktari.

Pisi akawa anagoma ndio jamaa angu akaplay role akamwambia unataka kuiona kesho!? Pima. Demu akawa mpole akatoa mkono wake mimi nikaendelea nashughuli ila hata sijaweka kipimo chini ngoma ikasoma mstari wa HIV 1 na kufata wa pili wa kwenye C (control).

Kwa maana ya kwamba binti yule ni wa moto ana umeme ameukwaa. Wakati huo yule binti wala jamaa angu hawakuwa wanaangalia kipimo kwa sababu zao au kwa kuwa kipimo kile nilikifanya mali yangu binafsi kwani ilokuwa ni kwa mstakabali wa afya yangu hii ninayoipambania hadi sasa. Kwa hiyo nilikiweka karibu yangu kama kuku anavyokumbatia kifaranga wake.

Hakika niliona dunia imepasuka, nilipaniki, nikageuka kumwangalia yule binti ambaye alikuwa kama hajui lolote vile nikataka nimpasue vibaya mno mangumi ya ghafla na mateke ila kitu moyoni kama baridi iliingia ikiniambia acha tulia tuliza akili. Nikainama nikawa nawaza ndio nimeukwa kirahisi hivi!?

Aisee nikageuka chap nikamwambia jamaa angu washa gari aendeshe yeye, akiwa haelewi akishangaa nikasema nitakueleza mbele ya safari. Jamaa akawasha yule binti akawa anajifanya kung'aka vipi mbona hivyo nipe majibu yangu, ( nikamwangalia huku moyoni nawaza huyu maku ananionaje yaani ananichora ama ina maana hajui!?) Sikusema neno.

Akawa anazidi niambia nini!? Umeona majibu gani mbonw useme, niligeuka nikamwambia kwa sauti ya ukali kama simba mpaka rafiki yangu alistuka, niliropoka SHUUUUUT THE FAAAAAAKAP!!, akaniambia unanitukana kwa nini!? huku akianza kutumia silaha ya kike yakulia nione huruma ilihali ashatumia uchi wake kwa dhumuni lq kuniangamiza, kifupi niliamini alidharimia mpaka sasa naamini hivyo na hivyo nilikosa hata chembe ya huruma kwake, jamaa angu nikamwambia afike getini tu hostel kwake yule pisi na leo siingii ndani, jamaa akawa anashangaa ila alishanotice kitu nikamwambia tulia.

Nikamgeukia binti nikamwambia shuka akajifanya tena niambie majibu umeona nini, ile kuniambia vile mtanisamehe hasira ilipanda nikamzaba kofi moja ambalo sikujua alishuka kwa gari saa ngapi ila nikamuona tu akiingia getini hostel kwake akikimbia huku akilia. Nikamwambia jamaa yangu tung'oe isiwe tabu, kiufupi mimi katika maisha yangu sijawahi kuwa violent wala hata kumfinya mwanamke sembuse kupiga kofi!? Ila ile siku sijui unyamera ulitoka wapi!, Kifupi nilichanganyikiwa.

Nikawelekeza jamaa angu kituo cha kwanza kwa yule rafiki yangu dokta. Tukiwa njiani akaniuliza vipi mzee baba!? Nikatoa kipimo nikamuonyesha, mshkaji alipaniki nikamwambia ile mafuta ni moto na nimepiga round mbili kavu kavu masaa kadhaa yaliyopita, hapo ni takribani saa nne au tano zimepita toka kitendo cha maangamizi kifanyike ( kuuza mechi kwa mwathirika). Mshkaji aliwaza mno akinionea kama huruma vile nk kwani nilimsoma ila nilikuwa najikaza usoni kiume, kifupi hata mimi mpaka sasa kuna saa najihurumia na sijiamini.

Basi bila kuwaza paap kwa daktari mshikaji wangu yule alonipa vipimo, bila kuwaza nikampa kile kupimo jamaa akaniambia hii ni ngwese hakika HIV positive. Ila jamaa akaniambia ingieni ndani, hapo akaniuliza kama nilitumia kondomu na jinsi gani nilifanya basi nikampa Ubuyu wote kama nilivyoumwaga hapa, tukiwq watstu mshkaji dokta kwanza big up sana kwake kiukweli alinipa moyo akaniambia shinda hofu usiogope utapita hili. Akaingia chumbani kwake akatoka na kibobo sijui niitaje basi kipya ndani kina dawa 90 na akaniambia huyu ni mfanya maajabu anaitwa PEP.

Huyu atakufaa wakati wa dharula hii tena kwa kuwa umewahi zaidi ya sana atakufaa mno. Maana huyu hutumika ndani ya saa 72 (siku tatu baada yakuwa na hatari yakupata maambuzi) na mimi mda ule ilikua kama saa tano zimepita kwenda sita, akaniambia anza asubuhi kula kidonge kimoja tu kila siku mda huo huo ulioanza kwa siku 28 pekee.

Nikamuuliza mbona umenipa kopo complete 90 akasema kwa utani kuwa hizo zingine zitakusaidia kama utapata majanga wakati mwingine nikamwambia koma na shindwa katika Jina la Yesu....kifupi alinifariji nikawaza maneno yake nikapata matumaini nikasema huyu jamaa anaamini nitatoboza salama kweli au anasema kwa kuwa hili janga halipo mwilini mwake?

Basi tukaagana mimi na workmate wangu hao safari kurudi home, almost saa sita usiku jijini nikiwa hizo dawa PEP ila yule mshkaji wangu daktari akaniambia PEP ni dawa ngumu nitegemee mambo mageni na magumu muhimu nikomae kiume mpaka nimalize dozi, kwani wao wamekuwa wakiokoka na dharula mbalimbali kwa ajili ya PEP kama ikitumika sahihi, yaani ndani ya muda wake na kwa masharti uliyopewa.

Kifupi usiku ule nilikua na stress mno, nilitani tufike tu home, kifupi yule jamaa workmate angu kwa hali aliyoniona nayo akasema hata kwake haendi atachill maskani na mimi mpaka kesho kunipa kampani maana aliwaza naweza jiua or something. Maana sikuwa sawa. Nadhani mnajua kipenda roho hula nyama mbichi, unaweza pewa ushauri na mtu akakupa matumaini ila kuna muda unaona hayo natumaini mbona hayana nafasi, kifupi imani inapungua, na huo ndio ubinadamu.

Basi baada yakufika home, kiukweli usingizi hakuwepo mshikaji alikuwa nami seating room tukifarijiana mimi nikaingia chumbani nikimwacha akinetflika. Mimi mawazo yote kwa Janeth na tukio nililolifanya leo kwa kweli dunia usiku ule ilienda kwa kasi mno, sikupata jibu la usemi kwa nini watu wanapenda pepo lakini wanaogopa kifo au shida, jibu lilikuja nakujua maisha yana utamu wake hivyo hayana budi kuthaminiwa.

Kwa kweli nikawa macho ilipofika saa saba usiku nikasema hapana acha nianze kumeza zile dozi sisubiri asubuhi maana nilisoma the earlier the better. Nipita sebuleni mshikaji workmate kalala fofofo nikaingia jikoni nikatoa chakula kiporo nilichopika mda ule, maana sikuwa nimekula toka ile mara ya mwisho kabla ya tukio la janga and actually ni kama nilikula matunda tu maana si unajua ukiwa mtu unapika mara nyingi hamu yakula hicho chakula huwa ndogo so nilikua kama namsindikiza lile pisi janga.

Basi nikapiga hicho chakula usiku huo baada ya hapo nikatoa kidonge kimoja cha PEP nikapiga. Usingizi haukuja ila baada ya kama saa nikaanza sikia nguvu ya dawa yaani siwezi elezea maruweruwe yake nikaomba nitapate usingizi, Mungu si athumani nikalala ila sasa kulala kule sijawahi lala hivyo kwani nilikua sijui macho sijui nimelala yaani sielewi nilikua naona mauzauza mavitu yananiongelesha live kabisa kichwani yaani mpaka nastuka asubuhi jamaa angu ameamka naye akaniamsha kuniambia mda wa kwenda kazini nikamwambia anitolee udhuru huko kwani sitaweza kwenda na ilikua karibia weekend nikasema kazini mpaka jumatatu kwa hali yangu sijui kama ile siku ningeweza concentrate zaidi ningeonekana nina tatizo. Eeh bana siku hiyo ya kwanza actually wiki yote ya kwanza yakutumia dawa hizo za PEP ebana nilipatwa na ma side effect kibao za dawa, ila nilipambana, kichwa kuuma kama radi, yaani tumbo kuvuruga na kichefuchefu kujisikia kutapika utadhani mimi kidume nina mimba sijui ya pacha wangapi, kifupi nilikula malimao kushinda komba.....kutapika hutapiki ila cha moto nitakiona. Yule mshkaji wangu dokta alinipa moyo akaniambia kaza, maliza dozi yatapita.

Muda huu naandika uzi huu niko macho toka saa saba usiku nikiwa nimemaliza dozi yangu ya mwisho kidonge cha 28 baada ya siku 28 za jasho, stress, maisha shaghalabala kukosa muelekeo na hofu ya matokeo, yaani mpaka leo hii sijaenda kazini nimeomba udhuru ila ni kwa kuwa hofu imetanda maishani mwangu, what if nilipata HIV na PEP haijafanya kazi!?

Yaani nimesali sana huu mwezi mzima kila sala mpaka za ndege wa angani nadhani nikiomba nipate rehema na neema kikombe hiki kiniepuke. Nina imani ila kuna saa imani inaisha kabisa hasa nikiwa mwenyewe, nawaza hizi dawa ni siku 28 zimenifanya mbaya hivi!? What if ndio ije kuwa natumia maisha yangu yote kama vile waathirika wa ukimwi watumiavyo!? Kwa kweli sitaweza eeh Mungu anisadie.

Ilipofika siku ya 21 toka tukio la uwezekano kuambukizwa ukimwi, jamaa angu dokta alinipima ingawa bado ni katika muda wa window period nilitaka tu kujua, na majibu yalikua NEGATIVE ( bado virusi havionekani.) na leo siku ya 28 sasa takribani mwezi sasa nimejipima nikiwa nakuandika uzi huu maana dokta aliniachia vipimo nimekuta inasoma tena NEGATIVE.

NIMEMWAMBIA DOKTA MAJIBU HAYO KANIAMBIA INGAWA UNAWEZA KUSUBIRI MPAKA MIEZI MITATU IPITE NDIO UCONFIRM KAMA NI NEGATIVE, ILA KWA UZOEFU WAKE SIKU 30 TU ZINATOSHA, NA KATU NISITEGEMEE KIPIMO KITABADILIKA TENA KAMA NIMESOMA NEGATIVE HATA SASA.

Kiukweli jamaa kanipa moyo kama kawaida ila nawaza usikute ananipa moyo kwa kuwa mshikaji wake hataki kuniambia ukweli, maana kaniambia hiyo kwisha vita umeishinda niamini hilo.

Nimeona nilete hii experience kwenu wanazengo hasa ningependa kusikia kwa waliyoyapita kama mimi experience zao na wakatoboa ili kunipa moyo, niamini siku 60 majibu yatakuwa haya haya negative na hata siku ya 90.

Hasa pia madaktari wengine mliopo hapa mnipe ushauri ila kwa wale wa utani pia tanieni ila jua kuwa kufa nitakufa ila sipendi kufa nikiishi maisha ya adha ya kula ARVs maana mziki wa PEP umeninyoosha.

Asanteni nawasilisha🙏
 
Summary
Demu wake yuko nje ya nchi anasumbuliwa na genye hajatomba mwaka mmoja
jamaa kakutana na demu Janeth
Akaomba number ili ale mzigo
baada ya wiki tatu kala mzigo wa Janeth
jamaa akajisifu kapiga bao ndefu
kwa hofu ya ngoma akaomba wapime demu kagoma. Jamaa kafosi kumpima demu anagoma

jamaa kapaniki na anaonekana ni mtu wa kupanick hovyo
Umalaya wake umemponza kaanza kutumia PEP
mara maruweruwe mara hofu ya kuwa na ngoma hawezi Lala wala hana amani anausibiri miezi mitatu apime tena😀

story yote hii jamaa kapanick inakuwaje kama atapata ngoma😔😔
 
Nenda kapime wewe , uanze kutumia sembe , hii ishanikuta nouma Sana , nilikimbia ziwani kwenda kujiosha 😁, sku naenda kupimwa nulipitiliza kituo cha Afya badae nikarudi mdogo mdogo, Yule mpimaji akaniuliza endapo utakuta umeathirika utafanyeje , nikamjibu sjui nitakachofanya majibu yakitoka ndo nitakuwa na jibu sahihi... Sema Yule mpimaji naye alikuwa na tako la haja
 
Back
Top Bottom