Karibu tushauriane na kupeana uzoefu wa manunuzi ya chakula kwa ajili ya mwezi mzima

Lemaitre

Member
Aug 25, 2020
72
49
Habari za jioni wakuu,

Binafsi nimekuwa nikipitia changamoto sana nifanyaje au ninunue vyakula gani ambayo vitaweza kunifikisha mwezi mzima.

Naombeni uzoefu wenu katika hili, ni nini unazingatia, utaratibu upi unautumia kwenye kufanya manunuzi ya chakula.

Ukiweza kusema ni vyakula gani huwa unapendelea kununua na kuweka ndani itakuwa vyema zaidi. Asanteni, Uzi tayari.
 
Habari za jioni wakuu,
Binafsi nimekuwa nikipitia changamoto sana nifanyaje au ninunue vyakula gani ambayo vitaweza kunifikisha mwezi mzima. Naombeni uzoefu wenu katika hili, ni nini unazingatia, utaratibu upi unautumia kwenye kufanya manunuzi ya chakula. Ukiweza kusema ni vyakula gani huwa unapendelea kununua na kuweka ndani itakuwa vyema zaidi. Asanteni, Uzi tayari.
unaishi single au double au mpo triple tuanzie hapo
 
Mchele,maharage,nyama,sukari,unga wa ngano,mafuta ya kupikia,chumvi,maziwa,ketchup,mayonnaise,blueband,jam,Tambi .
Lakini hizi mboga nazo zinavitu vyake vyakupika pamoja kama nyanya, vitunguu, carrot, spices etc. Navyo huwa unanunua kiasi gani?
 
mchele kilo 10, unga muogo kilo 3, sembe kilo 6, samaki sato kg 4, nyama kg 10, mayai trei 1, sukari kg2 , chumv paket 3 . Vitu vingine bora uwe unanunua kwa wiki ili visioze kama nyanya , vitunguu maj/saumu, limao, matunda, mbogamboga, tangawz list kubwa sana..
 
Habari za jioni wakuu,

Binafsi nimekuwa nikipitia changamoto sana nifanyaje au ninunue vyakula gani ambayo vitaweza kunifikisha mwezi mzima.

Naombeni uzoefu wenu katika hili, ni nini unazingatia, utaratibu upi unautumia kwenye kufanya manunuzi ya chakula.

Ukiweza kusema ni vyakula gani huwa unapendelea kununua na kuweka ndani itakuwa vyema zaidi. Asanteni, Uzi tayari.
Binafsi kila kitu nanunua cha mwezi. Hadi mboga za majani!!!!!!

Mnaojifanya madr mpite mbali
 
mchele kilo 10, unga muogo kilo 3, sembe kilo 6, samaki sato kg 4, nyama kg 10, mayai trei 1, sukari kg2 , chumv paket 3 . Vitu vingine bora uwe unanunua kwa wiki ili visioze kama nyanya , vitunguu maj/saumu, limao, matunda, mbogamboga, tangawz list kubwa sana..
Kama unafridge si unaweza tunza ?
 
mchele kilo 10, unga muogo kilo 3, sembe kilo 6, samaki sato kg 4, nyama kg 10, mayai trei 1, sukari kg2 , chumv paket 3 . Vitu vingine bora uwe unanunua kwa wiki ili visioze kama nyanya , vitunguu maj/saumu, limao, matunda, mbogamboga, tangawz list kubwa sana..
Kama una freezer nunua nyanya nyingi. Zioshe..weka kwenye mifuko ya plastic weka kwenye freezer utakaa nazo miezi na miezi ila tu hazitafaa kwa kachumbari. Vitunguu swaumu haviozi na tangawizi pia kama hutaziosha zinatoboa mwezi. Weka sehemu kavu
 
Nikishanunua Dona 15kg Michele 10, mafuta Ya kupikia, na kujaza gesi basi. Nakuwa nabadili mboga tu. Kila Siku Asubuhi Kahawa, mchana Dona jioni wali/ pilau Hadi mwezi unaisha
😳 Mchele kilo kumi unafika mwezi? Na vitu vidogo vidogo kama vitunguu, nyanya unanunua kiasi gani?
 
Vitunguu sawa ila nyanya huwa nanunua kwa wiki. Carrot ,hoho hivyo sinunui vya mwezi maana vitaharibika. Mbonga mbonga kwangu nina bustani. Mchicha,matembele,kisamvu,mnavu.
Ooh! So hivi ni vema ukanunua kwa week, Hata kama una fridge ?
 
Kama una freezer nunua nyanya nyingi. Zioshe..weka kwenye mifuko ya plastic weka kwenye freezer utakaa nazo miezi na miezi ila tu hazitafaa kwa kachumbari. Vitunguu swaumu haviozi na tangawizi pia kama hutaziosha zinatoboa mwezi. Weka sehemu kavu
Unaweza kushare vyakula unavyonunua na jinsi unavyovitunza ? Nimependa maelezo yako.
 
Back
Top Bottom