Kanda ya ziwa ina mawe mazuri ambayo yanaweza kujenga barabara na mitaro mpaka vijijini lakini tumeshindwa

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
14,138
Reaction score
33,525
Ukianza kuingia singida na ukanda wa ziwa kuna mawe yanayo tumika kujenga misingi ya nyumba za huko.

Ingekuwa kwa wenzetu ndio wamepata haya mawe basi mpaka uchochoroni kungekuwa na rami.
IMG_1376.jpeg
 
Watawala hawataki haya mambo!
Wako biz kuhamisha hela kupeleka Dubai! Ufisadi, wizi, kuuza maliasili na rasilimali!
Maendeleo ya raia, raia watajijuwa!
Hata wakati wa kura, MTAWAPIGIA TU!
 
Ukianza kuingia singida na ukanda wa ziwa kuna mawe yanayo tumika kujenga misingi ya nyumba za huko.

Ingekuwa kwa wenzetu ndio wamepata haya mawe basi mpaka uchochoroni kungekuwa na rami.
View attachment 3336712
Mwanza kuna barabra za mawe, ila kwa uzoefu wangu naona kama ufundi wa kujengea mawe bado.

  • Barabara haziko plain kutokana na mpangilio wa mawe
  • Mvua ikinyesha ni kama kunateleza fulani.
 
Tz imejaa miti na mimea tiba lakini bado tunatimport dawa na chanjo hii ni ajabu.
Hadi Mungu tumeimport.
 
Haya mawe ni rasimali kubwa sana ila hayatumiki, wachina wanayamezea mate hawakosi cha kuyafanyia
 
Mbinu za kududumiza mwafrica ni kuhakikisha wanakuwa Duni maisha yao yote.

Mvua zikinyesha na baada ya madhara kutokea kama mafuriko na uchafu kujaa kila mahali na magonjwa kulipuka.
Basi huo ndio mpango mzima wa kuzidi kuwafanya muwe mnaruka madimbwi tu au kuvunja magari yenu au kufa kabisa.

Sio kuwa serikali za watu masikini hazijui au kushindwa kusafisha mji na kutengeneza miundombinu, hapana.

Wanataka mzubae huko milele.
Unadhani hakuna mabilioni nchini ya kufanya mambo haya?
Kweli Dar, Nairobi au miji mingine utafananisha na Kuala Lumpur? Au Bangkok?

Sio kuwa tunashindwa bali ni mbinu zao
 
Unahitaji resources kuyapasua, hii ni private sector initiative. Ikiwa serikali labda wanabania vibali vya kuyavunja na kutumia kwenye ujenzi hapo ndo shida
 
Tulipokosea pakubwa ni pale tulipoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma
Imagine!!

Babu Tale anapewa heshima kubwa kuliko Mtu mwenye Taaluma yeyote..

Matokeo yake Watu wanaacha Taaluma wanakimbilia siasani..
 
Mbinu za kududumiza mwafrica ni kuhakikisha wanakuwa Duni maisha yao yote.

Mvua zikinyesha na baada ya madhara kutokea kama mafuriko na uchafu kujaa kila mahali na magonjwa kulipuka.
Basi huo ndio mpango mzima wa kuzidi kuwafanya muwe mnaruka madimbwi tu au kuvunja magari yenu au kufa kabisa.

Sio kuwa serikali za watu masikini hazijui au kushindwa kusafisha mji na kutengeneza miundombinu, hapana.

Wanataka mzubae huko milele.
Unadhani hakuna mabilioni nchini ya kufanya mambo haya?
Kweli Dar, Nairobi au miji mingine utafananisha na Kuala Lumpur? Au Bangkok?

Sio kuwa tunashindwa bali ni mbinu zao
Shida ni kwamba toka uhuru tunajenga barabara tu na kusambaza umeme na zimekuwa ndio agenda, wakati wanajeshi wetu wanadai wamebuni mradi wa kokoto basi Ethiopia wanajeshi wake wamefungua kiwanda cha kutengeneza drones kwaajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na usafirishaji wa bidhaa. Masudi kipanja alipowaza na kudhubutu kutengeneza magari yakutumia umeme akachekwa, hivi ni nani katuloga.
Ukoloni wa kifikra bado upo. Tunawezaje kusubiti serikali itujengee barabara ilihali sisi ndio wanufaika wa hiyo barabara ndio pale mtu anasubiri ajengewe choo na serikali na huku anasoma kuwa serikali ndio ni watu na yeye ndiye miongoni wa hao watu. Kweli divide and rule imefanya kazi tumegapigwa ujasusi wakutosha pale tulipoletewa dini na chuki za kikabila na kishabiki. Tutawezaje kuungana na huku tunaitana kafiri, mara washirikina, mahasimu, chasaka, kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe, wakuja, n.k
Bado tuko jela ya fikra.
 
Mfumo wa siasa ulibuniwa na wakoloni purposely na nchi zote zilikabidhiwa nchi zikiwa tayari zimeandaliwa mifumo na hiyo mifumo ni ya wakoloni na hiyo tunaita siasa ni mifumo yao hali yakuwa mifumo yetu tumeitupilia mbali ili hali wao bado wanatumia mifumo yao ya asili mf. Uk bado wana Malkia sisi machief, watemi, mangi tuliaminishwa wanatunyonya je viongozi wakisiasa ni mara ngapi wamekutwa na kashfa za ufisadi. Hii haitatuacha Salama
 
Shida ni kwamba toka uhuru tunajenga barabara tu na kusambaza umeme na zimekuwa ndio agenda, wakati wanajeshi wetu wanadai wamebuni mradi wa kokoto basi Ethiopia wanajeshi wake wamefungua kiwanda cha kutengeneza drones kwaajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na usafirishaji wa bidhaa. Masudi kipanja alipowaza na kudhubutu kutengeneza magari yakutumia umeme akachekwa, hivi ni nani katuloga.
Ukoloni wa kifikra bado upo. Tunawezaje kusubiti serikali itujengee barabara ilihali sisi ndio wanufaika wa hiyo barabara ndio pale mtu anasubiri ajengewe choo na serikali na huku anasoma kuwa serikali ndio ni watu na yeye ndiye miongoni wa hao watu. Kweli divide and rule imefanya kazi tumegapigwa ujasusi wakutosha pale tulipoletewa dini na chuki za kikabila na kishabiki. Tutawezaje kuungana na huku tunaitana kafiri, mara washirikina, mahasimu, chasaka, kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe, wakuja, n.k
Bado tuko jela ya fikra.
Hakuna alieroga mtu, huu ni msemo tu.
Ila kiuhalisia hakuna viongozi wenye nia njema.

Wananchi mnalipa kodi kila siku na ni wajibu wa serikali kuhakikisha mahitaji yote wananchi wanayapata na huduma zote zinafanyika.

Haiwezekani mabilioni yanayoweza kufanya kazi yanaishia kwenye mifuko ya wachache, halafu kuna mzazi anamtafutia kazi mwanae au kumshawishi ajiunge na kazi ambayo itampa ulaji

Sio kuwa tumerogwa bali ukweli ni kwamba pesa zinazoingia serikalini ni nyingi kulingana na pesa zinazotumika kutengeneza vitu vya maana.

Hatuna maendeleo sio kwa sababu hatuna akili hapana
Ni kwa sababu tunadumazwa akili ili waendelee kula
Mbona Magu alihakikisha miradi inaisha haraka na kulazimisha yatokee
Tunashindwaje kuwalisha Ulaya na waarabu kwa mazao yetu?
 
Usemi wa nani katuroga haujamaanisha ushirikina hapana ila kuonesha ni kwakiasi gani mifumo yakikolono ilivyotuweka jela ya kifikra. Umesema vizuri kuhusu serikali hivi unajua serikali ni watu na sisi ndio tunawachagua hao viongozi, kama ukipewa 10k na kitenge unampigia kura ni lini tutahoji juu ya mambo yamsingi ili hali ukisikia wasiojulikana unafunga mdomo, hofu tatizo hofu.
 
Miaka mitano anakula posho tu
Screenshot_20250517_072112_Instagram~2.png
 
Back
Top Bottom