Bubu Msemaovyo
Platinum Member
- May 9, 2007
- 4,189
- 3,552
Moto uko katika vidole vya Muungwana. Sasa je atakaa kimya??? Kweli "....Kikulacho ki-nguoni mwako..." Jamaa wanamgeuka hivi hivi naye kimyaaaaa kama kameza pamba.
Nakushukuru sana kwa hii taarifa muhimu (it's an eye opener). Sikuwa na taarifa kabisa kuhusu hili (nadhani tuko wengi tu)! Pamoja na kwamba haoy magazeti hayauziki, ila ni muhimu sana kwa majukwaa ya ukombozi kama JF na magazeti yenye uzalendo kuweka hili suala wazi ili Watz wajue hili jambo. Hilo ndilo litakuwa hitimisho la njama zao! Kwani wataandika tu, hata TV itarusha matangazo hewani lakini mwisho wa siku wataambulia hukumu ya umma. Tuwasaidie Watanzania wenzetu wajue hii njama ya hatari sana. Sioni kitu gani EL anaweza kutufanyia akiwa raisi. Itakuwa ni sherehe (party) ya mbwa mwitu wenye njaa kuwararua mbuzi (WaTz) wasio na hatia (poor naive Tzn)! We should not (by hooks and crooks) let this happen.
hivi jamani mnataka kuniambia lowassa anaweza akawa raisi wangu???? Watz ndio bado tumelala hivi?????
sidhani kama kuna mtanzania wa kawaida atampigia kura lowassa. Ili kupiga kura kumchagua lowassa kuwa rais sharti kwanza uwe ni kichaa!!!!
Kampeni ya kummaliza kisiasa JK, Spika na wabunge kadhaa "wakorofi", imeanzishwa rasmi na Karamagi & Co. (Lowassa na Rostam) kupitia magazeti yao maalum ya AHSUBUHI NJEMA, TAZAMA, NYUNDO, TAIFA NA UMMA. Nia ni kuhakikisha JK anakuwa Rais kwa muhula moja tu na Spika Samuel Sitta na wabunge "wakorofi" hawarudi Bungeni mwaka 2010.
Magazeti hayo ambayo huchapishwa kila siku ya kazi kwa mpangilio, toka Jumatatu hadi Ijumaa, yanabeba ujumbe mahsusi wa ushawishi kwa umma kwamba: JK hana shukrani, kawatosa rafiki zake na kuwakumbatia "maadui"; Membe ni msaliti na anampotosha JK; Lowassa ni kiongozi safi na bora ambaye alionewa tu na Kamati ya Dk. Mwakyembe; bila Lowassa, Rostam, Karamagi, Makamba, Kingunge na wanamtandao wengine, JK hashindi uchaguzi wa 2010; Spika Sitta, Naibu Spika Anne Makinda na wabunge "wakorofi" wa CCM akina Anne Kilango, Mwakyembe, Selelii, Manyanya, Ole Sendeka, Kimaro, Zambi, Nkumba, Mpendazoe, Shellukindo (Bw. & Bi.), Mpesya, Ruth Msafiri na Nyalandu, ni wapinzani wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Magazeti haya yanahaririwa na waandishi walewale mamluki: Deodatus Balile, Manyerere Jackton, Charles Charles, Muhingo Rweyemamu, Prince Bagenda na Gama wa gazeti la HOJA. Baadhi ya makala huchangiwa na Salva Rweyemamu na Premy Kibanga wa Ikulu na Mbunge wa Kigoma Peter Serukamba ambaye alibubujikwa machozi na kuugua baada ya Lowassa kujiuzulu. Yalianzishwa kwa mtaji wa sh. milioni 300 alizotoa Karamagi kwa niaba ya Lowassa na Rostam, mara baada ya Lowassa kujiuzulu.
Taarifa ndani ya Chama Tawala zinasema magazeti haya yana baraka zote za Makamba. Ndiyo maana baadhi yake yanahaririwa kwenye ofisi za UVCCM na kwa kutumia kompyuta za jumuiya hiyo.
Kwa mujibu wa kikao cha KALOKIRO kilichokaa Morogoro hivi karibuni, magazeti hayo yatasaidiwa baadaye (karibu na uchaguzi mkuu) na magazeti ya RAI, MTANZANIA na THE AFRICAN. Mwakani, mtandao huo wa mafisadi unaanzisha kituo cha redio na televisheni. Lengo kuu ni kuwamaliza wote hao kisiasa na kumwinua Lowassa agombee Urais mwaka 2010.
Matoleo ya wiki mbili zilizopita za magazeti hayo yote yalikuwa na makala za kumsafisha Lowassa na kudai kuwa Sitta anamhujumu JK, Sitta ana lengo la kuhamia CHADEMA, Kimaro kapora shamba la chuo, Mwakyembe ni mkabila, Membe ni mfuasi wa Malecela, JK hana fadhila mfano wa dereva aliyesaidiwa kwa kusukumwa kutoka kwenye matope lakini akakataa kuwabeba waliomsaidia ili wasichafue gari lake n.k. NGOMA IMEANZA, MAKUBWA ZAIDI YAJA!
Moto uko katika vidole vya Muungwana. Sasa je atakaa kimya??? Kweli "....Kikulacho ki-nguoni mwako..." Jamaa wanamgeuka hivi hivi naye kimyaaaaa kama kameza pamba.
...muda si mrefu salva rweyemamu ataondolewa kwenye nafasi yake ya mkurugenzi wa mawasiliano ikulu...kwa sababu amewekwa pale kisiasa ...na madhara yanaaza kuonekana........
....kuhusu lowassa ..ukweli ni kuwa anao uwezo mkubwa kiutendaji kuliko ....kikwete...hilo sio siri,....
pm,
nakubaliana na wewe kwamba kama sio ujambazi, kwenye utendaji lowassa alikuwa na nafuu sana.
Pinda ni bomu kwenye utendaji, ila tu huenda sio jambazi kama lowassa.
Hapa mmetumia vigezo gani? Maana kuna mwingine anaweza akawa mtendaji mzuri kumbe kuna vitu anajaribu ku balance visionekane yaani Anakula huku anapuliza sasa sijajua huu uwezo wa Mheshimiwa EL umeupimaje hapa au ndio kwa zile shule za Uyoga (Shule za Kata) na Mvua ya Thailand?
Kampeni ya kummaliza kisiasa JK, Spika na wabunge kadhaa "wakorofi", imeanzishwa rasmi na Karamagi & Co. (Lowassa na Rostam) kupitia magazeti yao maalum ya AHSUBUHI NJEMA, TAZAMA, NYUNDO, TAIFA NA UMMA. Nia ni kuhakikisha JK anakuwa Rais kwa muhula moja tu na Spika Samuel Sitta na wabunge "wakorofi" hawarudi Bungeni mwaka 2010.
Magazeti hayo ambayo huchapishwa kila siku ya kazi kwa mpangilio, toka Jumatatu hadi Ijumaa, yanabeba ujumbe mahsusi wa ushawishi kwa umma kwamba: JK hana shukrani, kawatosa rafiki zake na kuwakumbatia "maadui"; Membe ni msaliti na anampotosha JK; Lowassa ni kiongozi safi na bora ambaye alionewa tu na Kamati ya Dk. Mwakyembe; bila Lowassa, Rostam, Karamagi, Makamba, Kingunge na wanamtandao wengine, JK hashindi uchaguzi wa 2010; Spika Sitta, Naibu Spika Anne Makinda na wabunge "wakorofi" wa CCM akina Anne Kilango, Mwakyembe, Selelii, Manyanya, Ole Sendeka, Kimaro, Zambi, Nkumba, Mpendazoe, Shellukindo (Bw. & Bi.), Mpesya, Ruth Msafiri na Nyalandu, ni wapinzani wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Magazeti haya yanahaririwa na waandishi walewale mamluki: Deodatus Balile, Manyerere Jackton, Charles Charles, Muhingo Rweyemamu, Prince Bagenda na Gama wa gazeti la HOJA. Baadhi ya makala huchangiwa na Salva Rweyemamu na Premy Kibanga wa Ikulu na Mbunge wa Kigoma Peter Serukamba ambaye alibubujikwa machozi na kuugua baada ya Lowassa kujiuzulu. Yalianzishwa kwa mtaji wa sh. milioni 300 alizotoa Karamagi kwa niaba ya Lowassa na Rostam, mara baada ya Lowassa kujiuzulu.
Taarifa ndani ya Chama Tawala zinasema magazeti haya yana baraka zote za Makamba. Ndiyo maana baadhi yake yanahaririwa kwenye ofisi za UVCCM na kwa kutumia kompyuta za jumuiya hiyo.
Kwa mujibu wa kikao cha KALOKIRO kilichokaa Morogoro hivi karibuni, magazeti hayo yatasaidiwa baadaye (karibu na uchaguzi mkuu) na magazeti ya RAI, MTANZANIA na THE AFRICAN. Mwakani, mtandao huo wa mafisadi unaanzisha kituo cha redio na televisheni. Lengo kuu ni kuwamaliza wote hao kisiasa na kumwinua Lowassa agombee Urais mwaka 2010.
Matoleo ya wiki mbili zilizopita za magazeti hayo yote yalikuwa na makala za kumsafisha Lowassa na kudai kuwa Sitta anamhujumu JK, Sitta ana lengo la kuhamia CHADEMA, Kimaro kapora shamba la chuo, Mwakyembe ni mkabila, Membe ni mfuasi wa Malecela, JK hana fadhila mfano wa dereva aliyesaidiwa kwa kusukumwa kutoka kwenye matope lakini akakataa kuwabeba waliomsaidia ili wasichafue gari lake n.k. NGOMA IMEANZA, MAKUBWA ZAIDI YAJA!
Kama yaliyoandikwa huko nyuma ni kweli basi ninakuwa na hamu ya kufanya utafiti kuhusu aina ya ubongo ulioko kichwani mwa Lowasa. Nadhani kuwa yeye ni mtu wa kawaida tu na yaliyozungumuzwa huko nyuma siyo sahihi.
Ila kama yote yasemwayo ni sahihi basi ni lazima Lowasa awe na tatizo fulani kiakili. Mtu huyu alikuwa amekwisha kabisa kisiasa mpaka baada ya Nyerere kufariki. Baadaye Kikwete akamrusha hadi kwenye spot ya tatu yenye nguvu sana nchini. Anasahau kuwa Kikwete alimweka katika nafasi hiyo huku kukiwa na kilio kuwa alikuwa hafai nafsi hiyo ila Kikwete akamezea. Akiwa na nguvu hizo alizopewe na Kikwete, akarudia tabia yake ile ile ya kuendekeza vitendo vya rushwa aliyokandiwa na Nyerere (hata kama yeye mwenyewe hakupokea taslimu kama alivyosikika akijitetea). Safari hii akahadhirika hadharani na kulazimika kuwa waziri mkuu wa kwanza katika historia ya nchi hii kujiuzuru katika mazingira yaliyogubikwa na rushwa. Je alitaka Kikwete amtetee vipi? Halafu bado ana ndoto ya kuwa rais wa nchi hii? Dah!! watu wengine bwana.
Huyu bwana bado anadhani watanzania ni wale wale wajinga aliowalia mali zao siku za nyuma hadi yeye mwenyewe akawa tajiri vile. Ngoja tumsubiri na hao vibaraka wake anaofanya nao upuuzi huko ndani ya CCM ndipo waje waipate.
Kama JK ni Rais basi Mtanzania YEYOTE yule anaweza kuwa rais wa Tanzania.
Unafikiri kuna mtanzania ambae hajui kupanda ndege tu na kukaa????