Kampeni ya magazeti mapya ya Karamagi & Co. Dhidi ya JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni ya magazeti mapya ya Karamagi & Co. Dhidi ya JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LazaroSMtindi, Nov 17, 2008.

 1. L

  LazaroSMtindi Senior Member

  #1
  Nov 17, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kampeni ya kummaliza kisiasa JK, Spika na wabunge kadhaa "wakorofi", imeanzishwa rasmi na Karamagi & Co. (Lowassa na Rostam) kupitia magazeti yao maalum ya AHSUBUHI NJEMA, TAZAMA, NYUNDO, TAIFA NA UMMA. Nia ni kuhakikisha JK anakuwa Rais kwa muhula moja tu na Spika Samuel Sitta na wabunge "wakorofi" hawarudi Bungeni mwaka 2010.

  Magazeti hayo ambayo huchapishwa kila siku ya kazi kwa mpangilio, toka Jumatatu hadi Ijumaa, yanabeba ujumbe mahsusi wa ushawishi kwa umma kwamba: JK hana shukrani, kawatosa rafiki zake na kuwakumbatia "maadui"; Membe ni msaliti na anampotosha JK; Lowassa ni kiongozi safi na bora ambaye alionewa tu na Kamati ya Dk. Mwakyembe; bila Lowassa, Rostam, Karamagi, Makamba, Kingunge na wanamtandao wengine, JK hashindi uchaguzi wa 2010; Spika Sitta, Naibu Spika Anne Makinda na wabunge "wakorofi" wa CCM akina Anne Kilango, Mwakyembe, Selelii, Manyanya, Ole Sendeka, Kimaro, Zambi, Nkumba, Mpendazoe, Shellukindo (Bw. & Bi.), Mpesya, Ruth Msafiri na Nyalandu, ni wapinzani wa Serikali ya Awamu ya Nne.

  Magazeti haya yanahaririwa na waandishi walewale mamluki: Deodatus Balile, Manyerere Jackton, Charles Charles, Muhingo Rweyemamu, Prince Bagenda na Gama wa gazeti la HOJA. Baadhi ya makala huchangiwa na Salva Rweyemamu na Premy Kibanga wa Ikulu na Mbunge wa Kigoma Peter Serukamba ambaye alibubujikwa machozi na kuugua baada ya Lowassa kujiuzulu. Yalianzishwa kwa mtaji wa sh. milioni 300 alizotoa Karamagi kwa niaba ya Lowassa na Rostam, mara baada ya Lowassa kujiuzulu.

  Taarifa ndani ya Chama Tawala zinasema magazeti haya yana baraka zote za Makamba. Ndiyo maana baadhi yake yanahaririwa kwenye ofisi za UVCCM na kwa kutumia kompyuta za jumuiya hiyo.

  Kwa mujibu wa kikao cha KALOKIRO kilichokaa Morogoro hivi karibuni, magazeti hayo yatasaidiwa baadaye (karibu na uchaguzi mkuu) na magazeti ya RAI, MTANZANIA na THE AFRICAN. Mwakani, mtandao huo wa mafisadi unaanzisha kituo cha redio na televisheni. Lengo kuu ni kuwamaliza wote hao kisiasa na kumwinua Lowassa agombee Urais mwaka 2010.

  Matoleo ya wiki mbili zilizopita za magazeti hayo yote yalikuwa na makala za kumsafisha Lowassa na kudai kuwa Sitta anamhujumu JK, Sitta ana lengo la kuhamia CHADEMA, Kimaro kapora shamba la chuo, Mwakyembe ni mkabila, Membe ni mfuasi wa Malecela, JK hana fadhila mfano wa dereva aliyesaidiwa kwa kusukumwa kutoka kwenye matope lakini akakataa kuwabeba waliomsaidia ili wasichafue gari lake n.k. NGOMA IMEANZA, MAKUBWA ZAIDI YAJA!
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  LazaroSMtindi,
  Hivi kuna ukweli ktk maneno uliyo andika mkuu wangu!.. Na kama kuna ukweli mkuu wangu basi haya ndio magazeti ya kufungiwa.. Kilichoandikwa hapa ni kizito kuliko hata Mwanahalisi na kinapotosha wananchi waliowachagua viongozi hawa...
  Kama kweli Chiligati ni mtetezi wa haki basi maelezo hayo hapo juu yanatosha kabisa kufungia magazeti haya ama kuwapeleka mahakamani wahusika wote...Nina hakika ushahidi wa madai yao ni mgumu kupatikana kuliko ule wa gazeti la Mwanahalisi..
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli. Politics is really a dirty game.
  Pia nakiri kuelekea uchaguzi ndio kipindi cha kuvuna kwa waandishi wa habari sio siri waandishi wanateseka sana kwa kusota juani kwa malipo duni huku wanataaluma wengine kama wanasheria wanapeta sana kwa malipo manono tena kivulini.
  2010 ni mwaka wa neema kwa wana habari.
   
 4. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwandishi wa JK (Premy) naye yuko? Mbona naona kama ni contradiction?
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mkandara,

  Penye moshi kuna moto unafukuta. Sasa ukisoma vizuri hiyo listi ya wanaotaka angamizwa, ndio hao ninaowaita CCM Mageuzi ambao wanang'angania kubakia CCM huku wajanja wachache hawawataki.

  Hii habari pamoja na kuwa imeletwa kama maoni, ni kitu ambacho nimekiona na kukizungumza upenuni tangu mwezi wa pili kuwa kutakuwa na kampeni kubwa sana ya kuwan'goa wale wote ambao si CCM Mafisadi ndani ya CCM.

  Je sasa waelewa kwa nini Mchungaji anakuwa mkali?
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Magazeti yenyewe hayana soko. Hayauziki. Wanajihangaisha kama ni kweli.
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Nov 17, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280

  ...hizi taarifa hapa tunazo kitambo.....na ukweli ni kuwa haya magazeti ,tv,na redio vyote vilikuwa tayari kwenda hewani miezi sita iliyopita...lakini vilikatishwa na moto wa ajabu uliounguza WASHIRIKA BUILDING.....mkurugenzi walikuwa wamempachika PRINCE BAGENDA...tunahisi kuwa moto uliounguza washirika building ulichomwa na personal intelligence wa kikwete ili kupunguza speed ya haya magazeti...........nadhani wamejipanga upya..

  kaka wild hawa watu wana pesa hawategemei mauzo ya issues ili waendelee .....siunaona RAI haliuzi lakini hawatetereki......
   
 8. L

  LazaroSMtindi Senior Member

  #8
  Nov 17, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WanaJF Mkandara, Pasco,Nurujamii, Rev. Kishoka na WildCat nimewasoma, nimewaelewa. Naomba mniamini, nilichoandika ni kweli kweli tupu. Kama mnakumbuka, nilishawadokeza kuwa nafanya kazi mojawapo ya kampuni kubwa ya RA. Nikigundulika ni mimi nachangia hapa JF, nitakuwa marehemu kesho ahsubuhi. Hawa watu wana mtandao wa nguvu sana, wana pesa na wana sauti kubwa kwenye vyombo vya usalama. Ni mtandao uleule uliompa ushindi JK. Wachache ni waadilifu, wamebaki na JK. Wengi wamefuata fedha za EPA, Richmond, Import Support - kikao kimoja tu cha KALOKIRO unalipwa 1m/= au 2m/=, utaacha kuunga mkono? Mwenyekiti wa operesheni nzima, kama nilivyosema awali, ni mzee wa Sumbawanga. Salva Rweyemamu hana record ya uzalendo, ni mamluki tu aliyeajiliwa na Richmond kwa msaada wa RA. Leo yuko Ikulu, atabadilika? Premy haelewi kuwa marafiki wa jana wa JK, ndo maadui wake leo. She is naive, anafuata mkumbo tu bila kuwa na bigger picture, bila kujua kuwa anamwumiza bwana mkubwa! Wahariri wa RAI wanajua hilo maana ndo wanaopokea "vigongo" kutoka kwa akina Salva. Niishie hapo maana naandika huku naangaza macho nisijeonekana Internet Cafe ahsubuhi nikichonga taarifa za JF.
   
  Last edited by a moderator: Nov 17, 2008
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nakushukuru sana kwa hii taarifa muhimu (it's an eye opener). Sikuwa na taarifa kabisa kuhusu hili (nadhani tuko wengi tu)! Pamoja na kwamba haoy magazeti hayauziki, ila ni muhimu sana kwa majukwaa ya ukombozi kama JF na magazeti yenye uzalendo kuweka hili suala wazi ili Watz wajue hili jambo. Hilo ndilo litakuwa hitimisho la njama zao! Kwani wataandika tu, hata TV itarusha matangazo hewani lakini mwisho wa siku wataambulia hukumu ya umma. Tuwasaidie Watanzania wenzetu wajue hii njama ya hatari sana. Sioni kitu gani EL anaweza kutufanyia akiwa raisi. Itakuwa ni sherehe (party) ya mbwa mwitu wenye njaa kuwararua mbuzi (WaTz) wasio na hatia (poor naive Tzn)! We should not (by hooks and crooks) let this happen.
   
 10. L

  LazaroSMtindi Senior Member

  #10
  Nov 17, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu umepiga ndipo! Umelonga kiuelewa. Umenikuna. Hawa watu hawahitaji fedha za mauzo za magazeti yao hayo ya udaku ambayo story zake nyingi ni za ubabaishaji tu. Wao wanauza message na soko lao kubwa ni Dar es Salaam. Fedha ya mauzo ni kwa ajili ya mamluki wao akina Prince Bagenda, Manyerere, Balile, na Muhingo. Magazeti haya yana kazi maalumu. Kwa mfano, gazeti la Nyundo lilipewa kazi moja tu kufanya: kumbomoa huyu kijana Nape kwa kumzulia kila jambo: si mtoto wa Nnauye, mpenda madaraka, mpuuzi, umri mkubwa utadhani Nchimbi ni teenager n.k. Kazi imefanyika, sasa gazeti hilo limesimama kidogo kusubiri assignment nyingine. TAIFA kazi kubwa ni kuwabamiza mastaa wa Mbeya na Kilimanjaro: Kimaro, Mwandosya, Kilango, Mwakyembe n.k. ndiyo maana magazeti mengi ya TAIFA yanauzwa Dar es Salaam, Mbeya na Kilimanjaro. Mkuchika aliingizwa mkenge na Salva na RA kuifungia MwanaHalisi. Walimpa shinikizo kubwa na kumpelekea ujumbe wa siri kuwa kabla ya kuwa Waziri alikuwa mfadhili wa MwanaHalisi. Of course huo ni uongo mkubwa, blackmail tupu. Lakini imefanyakazi.
   
 11. L

  Lorah JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2008
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  hahahahahaha! Uzuri JK nae anajua ukizoea kula vya wenzako nawe ukubali kuliwa.........................................., hapo ndipo
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  PM,
  Ninaposema hayauziki nina maana pia kwamba hayana wasomaji. Wakianzisha TV na Radio hapo hayo wanayotaka yawafikie watu wengi yatafika. Bahati nzuri ni kuwa wanajulikana kuwa ni watu hatari sio tu kwa ustawi na uchumi wa nchi yetu, bali hata kwa USALAMA na AMANI iliyopo. Walishindwa kumbakiza EL kwenye u-PM, hawataweza na majaribio mengine wanayo/watakayo fanya.
   
 13. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  What? Huyu wa Ikulu au mwingine? Mbona inanichanganya. Awe ndumila kuwili kiasi hicho? Naomba kuelemishwa.
   
 14. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Duh! Magazeti hayo hayapatikani nje ya Dar? Sisi tulio bara tutapataje maana sijawahi kuyaona isipokuwa TAZAMA ambalo kwa kweli limekuwepo kwa miaka hata kabla ya hiyo mitandao ya uchaguzo wa 2005!

  Sasa mbona baadhi ya waandishi ni waajiriwa na waandishi wa magazeti ambayo hayajatajwa hapo kama vile Balile (New Habari Coopration-RAI) na Muhingo ambaye ni Mhariri wa Rai? Au Mkuu unataka kutuambia kuwa hayo magazeti uliyoyataja hapo pia ni mali ya New Habari Corporation? Tujuze zaidi Mtindi.
   
 15. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2008
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hawa wanajaribu kumsumbua JK na kuifaya kazi yake iwe ngumu, lakini ukweli uko palepale kwamba kelele tunazopiga dhidi ya mafisadi wananchi wanaanza kuelewa, huwezi kuamini kuwa hadi vijijini wananchi wanafahamu ubaradhuli uliofanywa na mafisadi hawa. Hamtaamini nikiwaeleza kuwa baadhi yao mafisadi hawa hawana uhakika na ubunge 2010? ukifika majimboni, pamoja na pesa waliyo nayo, watu wengi wanapanga kuitafuna na kuwakataa vile vile.

  Bado najaribu kufikiria hiyo sherehe ya mbwa mwitu itakavyokuwa iwapo watshinda 2010?
   
 16. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mmhhhh Hii habari kama vile JK ameandaa watu kumuonea huruma vile?....

  Sio propaganda kweli hii jamani?
   
 17. M

  Masatu JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Habari ina mapungufu mengi ( half baked ) apart from mfano wa Nape hakuna maelezo na mifano halisi ya mateleo ya magazeti hayo kuonyesha hizo "kampeni" za kuwachafua watajwa.

  Kuna baadhi ya watajwa haiingii akilini kutokana na nyadhifa zao kushiriki katika jambo kama hilo, one can understand uhusika wa EL, Karamagi et al lakini Premy na Salva give me a break!
   
  Last edited: Nov 17, 2008
 18. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Masatu;

  Kumbe nawe umeona eeeeh?

  Kazi ipo humu JF!
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu we endelea kuwa TOMASO lakini itafika kipindi unaweza ukaja na kauli ya hii habari kuwa breaking news wakati ilisha julikana tayari hapo.
  Cha mhimu kama huamini uanze kujifanyia kautafiti kimya kimya.
  Lakini ukiangalia vimagazeti hivi vinavyo anzishwa kama uyoga ndo kazi yake hiyo.Kwa mfano kuna kigazeti kimoja hivi nafikiri kinaitwa Vioja kama sijakosea hiki kigazeti kina utamaduni wa kuwaponda ze Orijino Comedi sasa sielewi ni cha hawa jamaa EATV au lah maana kila tokeo chenyewe na akina Masanja,Joti n.k hata hayo aliyo taja mkuu hapo juu nayo hivyo hivyo yanawachamba watu kadhaa.
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wanaweza kuwa wanahusika bila wenyewe kujua, kama mabavyo Lizwan alihusika against baba yake bila kujua
   
Loading...