Kampeni ya magazeti mapya ya Karamagi & Co. Dhidi ya JK

Habari ina mapungufu mengi ( half baked ) apart from mfano wa Nape hakuna maelezo na mifano halisi ya mateleo ya magazeti hayo kuonyesha hizo mengine ya "kampeni" za kuwachafua watajwa.

Kuna baadhi ya watajwa haiingii akilini kutoka na nyadhifa zao kushiriki katika jambo kama hilo, one can understand uhusika wa EL, Karamagi et al lakini Premy na Salva give me a break!

Maswali makubwa ni je magazeti haya yapo?
Je hizo habari zenye malengo maalumu zimeisa chapishwa?
Kama yapo na habari zenye mlengo wa namna hiyo zimeisha chapishwa!...

kwa vyovyote vile ni mpango maalumu.. ambao watu wamewekeza kwake kwa ajili ya malengo maalumu. na wala sishangai watu hao kuwemo ama kwa kujua kabisa ( kama ilivo kuwa mtandao 2005) ama kutumika bila kujua!
 
Thats a very good job wanachokifanya maana yeye JK tumeshamchoka na sasa wao kama hizo akili zao zimeenda likizo wakitegemea tutampigia kura Lowassa then wameshindwa labda atapigiwa kura huko Monduli tuu!
 
Makubwa hayo. Siasa kweli ni mchezo mbaya. Sasa wakina Salva na Makamba vipi tena????????
 
Makubwa hayo. Siasa kweli ni mchezo mbaya. Sasa wakina Salva na Makamba vipi tena????????

Ushauri wa bure nawaomba wafanye haraka wamalizane kweli kweli bila kuoneana huruma maana the better for us spectators!
 
Wanaweza kuwa wanahusika bila wenyewe kujua, kama mabavyo Lizwan alihusika against baba yake bila kujua

Hao watajwa huwezi kuwafananisha na Ridhwan hata kidogo kuna watu kuchukuliwa msekule lakini sio hizo figure
 
halafu mkishamwondoa JK mnataka kumreplace na nani?

Dont tell me its Freeman Mbowe/Maalim Sefu/Lupumba/Mrema et al
 
Vita vya panzi....................!!!! Watatusaidia sana kama ni kweli. Maana Jamaa yetu kazi imemshinda na wala CCM hawana mpango wa kumtosa!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
halafu mkishamwondoa JK mnataka kumreplace na nani?

Dont tell me its Freeman Mbowe/Maalim Sefu/Lupumba/Mrema et al

Kama JK ni Rais basi Mtanzania YEYOTE yule anaweza kuwa rais wa Tanzania.
Unafikiri kuna mtanzania ambae hajui kupanda ndege tu na kukaa????
 
Kama JK ni Rais basi Mtanzania YEYOTE yule anaweza kuwa rais wa Tanzania.
Unafikiri kuna mtanzania ambae hajui kupanda ndege tu na kukaa????

Majita wewe mkubwa sasa, jambo linaloongelewa ni muhimu kwa mstakabali wa Nchi yetu na hii ukiangalia kwa mbaaaali unaiona (Kimbari)Mahakama ya kimataifa AICC-Arusha or the Hague!!!
 
Majita wewe mkubwa sasa, jambo linaloongelewa ni muhimu kwa mstakabali wa Nchi yetu na hii ukiangalia kwa mbaaaali unaiona (Kimbari)Mahakama ya kimataifa AICC-Arusha or the Hague!!!
Hapo siioni UNICTR Arusha wala ICTY.Angalia sababu za kutokea kwazo then linganisha na TZ.Kitakachotupeleka ni huko ni hiyo thread ingine hiyo inayoendelea ya vipaza sauti sijui mawaidha TBC 1
 
Je Mbowe ni Mtanzania??

Naona kuna watu wanaanza kuingia kwenye mtego wa kupoteza busara kwa kujadili watu badala ya mambo ya maana! Tujadili kwanza issue na si watu (especially hii ya presidential candidate)! Labda kama tunadhani kati ya watu karibia milioni 40 tuliopo Tz hakuna anayefaa kuwa raisi. Mimi naona tujadili kwanza majambo, na baadaye tunaweza kuleta hoja ya kuweka wazi sifa za mtu anayetakiwa kuwa raisi wetu wa 5. Kama hapa kwetu hapatikani basi tutaagiza toka nchi za nje (we will import). Vingevyo kuingiza majina kwenye hoja nyeti kama hii ni kututoa kwenye mstari wa mambo ya maana tunayojadili. Naona hili tatizo linazidi kukua hapa JF ambapo watu wengine wanakuwa na tabia ya kwenda off thread badala ya kuanzisha nyingine zenye mambo wanayoyataka. Ni vizuri tukajitahidi kukomalia issue iliyo kwenye mjadala!
 
Katika hali hii na upepo wa kisiasa hatuna budi kukaa macho vinginevyo mamluki wa kisiasa watashika kasi na kutupeleka pabaya. Na inawezekana wakabuni mbinu zingine kama hii imebumburuka. Wana JF tupashane!!!
 
Hao akina Balile washajulikana nia na madhumuni yao na kila Mtanzaia, so hata kama wataandika vipi kwenye hayo magazeti yao, (niyaite ya UDAKU) lazima hoja zao zitatiliwa mashaka tu. Labda wabadilishe majina.
Watamsafishaje EL wakati hata wao wenyewe wamechafuka tayari. Wakitaka kumsafisha EL waanze kujisafisha wao wenyewe kwanza.
 
Hivi JF hatuwezi kuja na gazeti letu jamani na likafika mpk Ndanda, Kigonsela na kwingineko ndani ndani ya nchi ili wananchi waweze kujua nini kinaendelea maana naona Vyama vya Upinzani vimechemsha kufikisha ujumbe au yawezekana wanaonekana wote njaa za madaraka.

Mimi naamini kila nchi wasomi huwa wanaaminiwa sana hasa kwa wale wenzetu walioko nje ya nchi na tathmini zao.

Please, JF Admn naomba kama kuna mpango wowote kuhusiana na hili, Binafsi nipo tayari kuchangia gharama.
 
Wanabodi,
Mimi siwezi kushangaa kabisa uwezo wa Mdanganyika kusaliti tajiri (Muajiri)wake... Salva anaweza kabisa kuwa na sura mbili ni hulka ya Wadanganyika inapofikia swala la Mshiko, wala haina Ubishi..Ni sawa kabisa na Ufisadi, rushwa na kadhalika...
Hapa hapa JF kabla ikiitwa Jambo forums kuna watu walikuwa humu humu tena wachangiaji wakubwa wakaanzisha usaliti na hata kumweka ndugu yetu Invisible ktk matatizo..wengine walisherehekea kufungwa kwa JF, leo vipi iwe ajabu kuona Salva yumo katika kundi la RA?... kumbukeni hawa wote walikuwa na JK toka achuke madarakani, tofauti zao zimejitokeza tu pale EL na mafisadi wengine walipochujwa...na kikubwa zaidi, asilimia 80 ya waasisi wa Mtandao wamepigwa chini... hiyo 20 iliyobakia lazima bado kuna Pumba..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom