Gotee na wengineo humu jamvini, Edward Lowasa anabaki ktk kumbukumbu za watanzania kwa mengi aliyoyafanya.
Ni waziri kijana, mkakamavu ndani ya ofisi ya waziri mkuu cigweyimisi 1990 kama chief whip, alijizolea umaarufu ktk kubadili maisha ya wabunge na zile shangingi TZC, majanga ya mafuriko na kuhimiza maendeleo, ktk zama za Mwinyi alihitimisha kwa kuzuia uvamizi wa viwanja vya Mnazimmoja na kuwaamuru wananchi wajitwalie mabati yale yaloizunguka Mnazi mmoja.
Baada ya hapo nyota ya Edward iling'ara sana hasa kwa sababu aliweza kujitambulisha kama mmoja wa viongozi chipukizi wanaoendana na mamlaka zao kiutendaji, UVCCM (Guninita) walim-rate kama no. 2 nyuma ya Salim Ahmed Salim. Tulio wengi tuliamini kabisa kama ni vijana basi Edward ni the best kwa nchi. Hilo halikuwa na ubishi kwetu.
Mchakato ulipoanza Guninita na wenzake walienda Addis na wakarudi wakiwa mikono mitupu, baada ya hapo tulishudia vijana wawili na mama wa makamo Anne Semamba Makinda wakipanda ndege ya kukodi, tukabaini baadae ni Eddo + Jakaya wamejitosa.
Jamii bado ilimuona ni Edward tu kwao, mara CC na NEC wakakaa na kumtosa Malecela alfajiri baada ya hapo Lowasa na akina Malima na Tumtemeke Sanga, Pius Msekwa, Mark Bomani... Nao wakatemwa. Kwa sababu watu walimpenda lowasa wakahoji nini kimemtokea kijana Eddo?
Mwalimu alipoulizwa juu ya kuachwa kwa Edward na wanahabari nyumbani kwa Msuya (waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais) alijibu hivi "Kama mnaona anafaa, au ana sura nzuri mchukueni mkanywe naye chai" baada ya hapo yakazuka mengi
1. Mwalimu amemkataa Lowasa kutokana na utajiri alionao ktk umri mdogo,
2. Mwalimu alihoji kama majumba aliyopangisha kwa balozi za Afrika ya Kusini kama zinalipiwa kodi?
Huo ndio ukawa mwisho wa Edward Ngoyai Lowassa, lakini niwakumbushe maneno ya front page ya Rai kabla ya CC na NEC (CCM) - "Kikombe hiki kiniepuke kwa mapenzi yake Mungu, Edward Lowassa" - ndivyo ilivyokuwa.
Eddo aliamua kumuunga mkono JMK kwa kila aliloweza bahati mbaya Mwalimu aliwashinda, JMK alikubali kwa shingo upande lakini Edward alionyesha dhahiri kupingana na kilichotokea, ni Edward Lowassa aliyelia hadharani na kusaga meno kwa hasira juu ya kile mwalimu alichoamua.
Ktk kundi hili wapo Guninita na wengi wengineo. Jinamizi hili ndilo lililomfanya Eddo kuwa nje ya baraza la kwanza la BWM, ilikuwa 1997 aliporejea akiwa waziri pale makamu wa rais mazingira, alifanya kazi yake vizuri sana mpaka alipopewa wizara ya maji ambako nako alifanya kweli. Ktk kipindi cha 1995-97 nje ya baraza la mawaziri alikuwa pro-government ktk michango yake mingi kama mbunge, misheni JMK kuwa rais hapa ndipo alipojiingiza matatizoni, wapinzani wake walipogundua tu kampango kao wakaanza kukumbushia tetesi za 1995 lakini walichelewa sana, Edward ni muhanga wa mafanikio ya Kikwete kupata nchi, hili si la siri na jungu, mvuto wa JMK kwa jamii ulivuka mipaka ya nchi lakini watu wengi walisita ktk utekelezaji maana hakuna rekodi za kutosha za kumfanya JMK kufaa kuvaa viatu vya Mkapa.
Wachache walishikiria issue ya Malima kama ndio uthabiti wa Kikwete lakini baadae watu wakasema nyuma ya ushindi wake kuna mtu wa kazi Lowassa hivyo hapa matokeo yatakuwa safi tu mwisho wa game, kasi ilianza na kila mtu alianza kuiona tofauti ya wawili hawa ktk ku- address issue za nchi na kuhimiza maendeleo, Lowassa alikuwa front na kila aina ya silaha aliyoona inamfaa mkuu akawa mtu diplomacy tuliamini mambo yako shwari, jungu likaanza jamaa anamfunika muungwana, kasi ilikuwa kubwa na tayari mentality za kidini zikaanza.
Nina mashaka yeye Eddo hakuligundua hili mapema lakini tayari waungwana wakawa kazini,zikaanza tetesi muungwana hapendezwi na spidi ya Eddo, zikaenda zikarudi mara Richmond kukurukakara hatimaye mzee Mwakyembe huyooo kumnyonga mpiganaji, mpiganaji akakubali yaishe...