Kampeni ya magazeti mapya ya Karamagi & Co. Dhidi ya JK

Kuna siku moja rafiki yangu mmoja alikwenda harusini akiwa amevalia vizuri sana tena alivyokuwa na pamba za uhakika kila mtu alisema kweli jamaa yule kapendeza sana. Halafu kumbe jamaa alikuwa na nafasi fulani kwenye ukoo wa maharusi, kwa hiyo alipata nafasi ya kutoa nasihi zake. Jamaa yule alitoa hotuba nzuri sana yenye maadili mazuri sana kwa maharusi na watu wtote waliokuwapo pale. Mojawapo ya maadili lilihusu maharusi kujiheshimu ili waweze kuheshimiwa na wengine.

Baada ya hotuba ile, jamaa akabugia pombe mpaka akajisadia kwenye nguo pale pale ukumbini na kulala chini akiwa hoi bin-taabani huku uharo wake ukiwa unasambaa hovyo hovyo hadi ikabidi sherehe ya harusi ifungwe.
Kesho yake gumzo lilikuwa jinsi jamaa huyo alivyojisadia kwenye nguo na kuzidiwa na pombe hadi akalala chini ukumbini huku akiwa na kinyesi kwenye nguo zake. Hakuna aliyekumbuka kuwa alikuwa jamaa alikuwa amevalia nguo nzuri na alikuwa ametoa maadili mazuri.

Inawezekana kweli Lowasa aliwahi kufanya mambo mazuri ikiwa ni pamoja na kukemea uuzwaji wa viwanja kiholela pale Dar, na kuhusu matumizi ya maji ya Ziwa Victoria. Hata hivyo, uharo wa rushwa aliolalia kwenye nguo ndio signature identity yake na wala hatutaisahau hata akijisafisha vipi. Kwa sasa hivi tunafahamu kuwa hata vile viwanja alivyokuwa akikemea uuzwaji pale Dar, baadaye vilikuwa uzwa na alipokea rushwa. Kila jambo afanyalo jamaa huyu huwa liko kalikulatedi kumpa ulaji fulani binasfi, siyo kwa maslahi ya taifa. Swala la maji ya Ziwa Victoria lilikuwa kalikulated kumfanya aonekane mchapa kazi ili aweze kuwania ama urais au nafasi kubwa zaidi serikalini.
 
Kichuguu,
Umeelezea vizuri sana. Nimejaribu kutafuta maneno ya kuelezea "uhodari" wa Lowassa katika utendaji kazi wake na ufisadi wake nikashindwa. Kwa hili nakushukuru kutupa wote hapa tuisheni. Hata wale wanaomshangilia Mkapa itabidi wafikirie jinsi alivyojitapikia na kujinyea kirushwa na hivyo ndivyo atakavyokumbukwa. You cannot serve 2 masters at the same time. Ama uamue kujihudumia au kuwahudumia Watanzania.
 
Netanyahu,

Mchango wa Lowassa kwenye jimbo lake la Monduli ni mkubwa sana kiasi kwamba kipindi kilichopita, hakupata mpinzani...alipita bila kupingwa! Vile vile katika uchaguzi ujao 2010, kutokana na maendeleo aliyopeleka, na mchango wake mzuri katika jimbo lake, atapita bila kupingwa! labda aamue mwenyewe kutosimama!
Ni kweli hakupata mpinzani kwa sababu ya kutumia jamaa wa special branch.
 
Katika siku za karibuni kumekuwa na magazeti luluki yaliyoanzishwa na JF ilikuwa ya kwanza kubaini mapema mikakati ya magazeti hayo

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-ya-karamagi-co-dhidi-ya-jakaya-kikwete.html

Lakini pamoja na hayo nikamkumbuka sana ndugu yangu, Ansbert Ngurumo katika makala yake hii ambayo naamini itawapa darasa waandishi na wahariri ambao bado wako usingizini. Mungu atawapa mwanga na kujua waendako.


Kosa kuu la Kikwete, Lowassa na Rostam

Ansbert Ngurumo


LIPO kosa moja kubwa sana la wanamtandao wa Rais Jakaya Kikwete. Kwa miaka mingi, wamejaribu kuung’oa muhimili wa nne wa dola - vyombo vya habari. Kwa kiasi fulani wamefanikiwa kuulegeza.

Mbinu kubwa waliyotumia ni kuwakumbatia (baadhi ya) wahariri. Wakawatumia, nao wakatumika; wengine wakafukuzwa hata kazi kwenye kampuni walizokuwamo, wakapewa kazi nyingine na wale wale waliowafukuzisha.

Wamewagawa wanahabari na kuwapa lebo za bei zao katika jamii, hata pale ambapo hawakuwalipa chochote. Taratibu, kwa makusudi au bila kujua, mtandao ulioongozwa na Kikwete, Edward Lowassa na Rostam Aziz umejikuta unaumba kizazi kipya cha mafisadi miongoni mwa wahariri.

Heri wangekuwa wameshirikiana na kizazi cha wazee, kinachostaafu kazi muda mfupi ujao. Ukubwa wa dhambi unatokana na ukweli kwamba wengi miongoni mwa kizazi hiki ni vijana, ambao kama Mungu amewajalia uzima, wataendelea kuongoza vyombo vya habari. Tutaweza kuwaongoa na ‘kuwabatiza?’ Au wao ndio watakaotuongoa sisi?

Je, wale waliowaharibu wahariri hawa, watafika mahali watambue kosa lao, wajute na kutubu na kuongoka pamoja ‘jeshi’ lao? Au ndiyo tukubali kwamba maangamizi ya taifa yamejikita katika kizazi hiki? Kwa nini kizazi chetu kijiruhusu kuwa cha laana kwa mingi ijayo?

Kuna usemi wa wahenga kwamba ukitaka kumuua mbwa, ua pua yake. Kina Rostam walijua kwamba ‘pua’ ya uandishi ni wahariri. Walidhamiria kuua pua za waandishi kwa nia mbili. Kwanza, wawasaidie kuingia madarakani bila kuwahoji, wailegeze jamii iwashabikie, iwaunge mkono. Hilo walifanikiwa.

Pili, walitaka waandishi wawasaidie kutawala. Wawasindikize katika kuandika na kuridhia mikataba mibovu. Wawe washirika katika kuchuma na kugawana ‘kasungura’ miongoni mwao, ikiwezekana wawarushie makombo (maana wahenga husema mbwa wa mfalme ni mfalme wa mbwa wengine).

Hili la pili lilifanikiwa kidogo, baadaye likashindikana kwa sababu jamii iliamka mapema kuliko wao walivyodhani. Ufisadi ukawa hoja kuu ya wananchi baada ya kuona mafisadi ndio wanaotawala!

Ingawa hawakuwa wameweza kuwakamata wahariri wote, kazi iliyofanywa na hao waliowekwa sawa, ilikuwa na kishindo kikubwa kilichoitikisa nchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, na kimeacha sumu kali katika fani ya uandishi wa habari. Matokeo yake, waandishi hawaaminiani, na hadi sasa ‘wanatafunana’ wao kwa wao kama samaki. Kikwete na kundi lake, hawawezi kukwepa dhambi hii.

Na ndiyo maana, hata serikali ilitaka kuwatumia hawa hawa kupitisha muswada (ambao yenyewe iliuita) wa uhuru wa habari mapema mwaka jana. Wadau wa habari waliuchunguza na kukuta umeficha hila nyingi za serikali na wapambe wao. Wakaukataa kwa kuwa muswada ulikuwa unalenga kuwakabidhi maadui wa uhuru mamlaka ya kuteka uhuru huo.

Ulikuwa utumwa mpya katika lugha tamu tamu. Wakubwa walikurupuka kutunga sheria mpya haraka haraka kulinda siri zao, kuwadhibiti waandishi ‘wakorofi.’

Mgawanyiko huu miongoni mwa wanahabari umeendelea kuwapo, hata baada ya wanahabari kushikamana na kuunda Jukwaa la Wahariri, Mei, 2007. Lakini mgawanyiko wa wahariri (wa jinsi hii) unalisaidiaje taifa?

Kwa kukumbushana tu, katika kuzindua Jukwaa la Wahariri, wanahabari hao walijipa malengo kadhaa, yakiwamo yafuatayo; Kwanza, walidhamiria kukilea ‘chombo’ hicho ili kikue na kutekeleza madhumuni ya kuanzishwa kwake.

Pili, walisisitiza kwamba jukwaa hilo si chombo cha kupambana na serikali na wala si cha kumkomoa mtu yeyote katika jamii, bali ni chombo chenye kazi ya kuwahabarisha, kuwaelimisha na kuwaburudisha wananchi, bila kusahau wajibu wa kuikosoa serikali na jamii pale zinapoteleza.

Tatu, waliazimia kukifanya chombo hicho kuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali kuleta maendeleo ya Watanzania. Hivyo, walijipa jukumu la kukutana na kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi kwa Watanzania, kuhoji utendaji wa viongozi na mchango wao katika maendeleo ya nchi na maslahi ya wananchi.

Nne, walisisitiza kwamba chombo hicho kingekuwa kiunganishi na sauti ya pamoja ya wahariri kwa niaba ya wananchi; ili jukwaa hilo liwe kwa manufaa ya wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, wajasiriamali na makundi mengine katika jamii.

Mara tu baada ya uzinduzi huo, wahariri hao walionywa mwanzoni kabisa juu ya utendaji wao. Aliyewaonya ni mwandishi mkongwe, Ndimara Tegambwage, ambaye huandika safu ya SITAKI katika gazeti hili.

Aliandika hivi: “Sitaki wahariri wakuu wa vyombo vya habari nchini waunde umoja utakaokufa haraka; kwa kishindo kikubwa na kwa aibu tupu. Kwani hadi sasa baadhi ya wahariri wamekuwa wakiishi kama ‘wapigania uhuru;’ wengine kama marafiki wakuu wa watawala; wengine kama watawala wenyewe na wengine kama ‘mbifemuki’ – vyovyote itakavyokuwa.”

Baada ya kuchambua kwa kina maana na lengo la jukwaa hilo, mwandishi huyo alihoji mambo kadhaa, akasema: “Je, umoja huu una ubavu wa kuvunja ‘kambi’ zilizotokana na ama utashi wa wahariri binafsi, shuruti za kimaisha, urafiki na watawala au ‘mlegezo wa maisha’ utokanao na rushwa na ufisadi kadha wa kadhaa?

Kwamba huu si umoja wa kurahisisha mahusiano kati ya baadhi ya viongozi wachache na wahariri ambao ni ‘baunsa’ wa langoni kwa shabaha ya kuendeleza usiri wa fikra na matendo ya serikali?

Kwani wahariri wakiamua habari ichapwe itachapwa, wakikataa itadoda na kutoweka. Uamuzi wao unadhihirisha uwezo mkubwa unaopaswa kukabidhiwa kwa watu makini.

Je, umoja umekuja bila kushawishiwa kuwa daraja au bomba la kupitishia ‘bahasha’ za kupoza nyoyo na kalamu? Na katika kambi zilizopo, kila moja ikijiita bora, suala la bahasha haliwezi kuvuruga umoja huu katika uchanga wake?

Yote haya yanasemwa kutokana na mazingira ya uandishi na waandishi, hasa wahariri, yaliyojitokeza tangu 2005 ambako waandishi na wahariri walishindana kuremba wagombea urais na viti vingine, ili baadaye wafikiriwe kuingia ‘utukufu wa kisiasa;’ si kwamba wagombee nafasi hizo na kuingia katika siasa au kuwa karibu na wanasiasa, bali wateuliwe kufanya kazi Ikulu, au wawe wakuu wa mikoa, wilaya au nafasi nyingine! Hivi sasa, kwa wengi, ni masimulizi ya matumaini yaliyopotea.”

Kama Ndimara angeamua kutaja majina ya wahariri, vyombo vyao na makundi yao katika hiki anachokieleza hapa, angefanya hivyo kirahisi. Anawajua wahariri wetu. Anaona kazi zao. Anajua uhusiano wao na waajiri wao na rafiki zao wa kisiasa. Anajua vishawishi vinavyowazonga, na anajua msukumo na msimamo wa baadhi yao.

Anawajua wanaoendekeza njaa, na ambao wameugeuza uandishi kuwa ukarani. Anawajua pia walio tayari kufa njaa, ili dhamira kuu ya kazi yao itimie. Anawajua waandishi wanaojiona kuwa sehemu ya serikali, na wengine walio upande wa wananchi.

Na katika vita hii ya sasa dhidi ya ufisadi, wahariri hawajashinda vita ya mafisadi kuwagawa katika makundi. Kundi moja linawatetea mafisadi, jingine linawamulika mafisadi.

Na kama wahariri wasingekuwa wamegawanyika hivi, Watanzania wangekuwa wameshashinda vita dhidi ya ufisadi tangu zamani. Lakini mafisadi walijua hilo hata kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Walijua nguvu ya wahariri, na walijua udhaifu wao. Na baadhi yao walijua hata bei zao!

Nguvu hizo, udhaifu huo na bei hizo, ndizo zimekuwa kinga madhubuti za mafisadi kwa miaka mitatu sasa. Hata wakibanwa vipi, wana mahali pa kutokea kuzungumzia, kupotosha mjadala au hata kujisafisha.

Na makundi haya yote yamo katika jukwaa la wahariri. Yanahujumiana na kudhalilishana. Na katika kufanya hivyo, yanawachanganya wananchi.

Kwa mfano mmoja wa hivi karibuni, yeyote aliyesoma habari za juzi katika magazeti kadhaa yanayoegemea kwa CCM na serikali, yakieleza jinsi wananchi wa Tarime walivyofanya fujo Alhamisi jioni na kuwatimua baadhi ya viongozi kwenye mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe; halafu akasoma gazeti hili likieleza habari tofauti, jinsi viongozi hao hao walivyopokewa kwa heshima zote na kusindikizwa hadi walipopaswa kwenda; na baadaye akasoma habari ikimnukuu msemaji wa familia ya Wangwe, kwamba familia inasikitishwa na kushangazwa na uandishi chonganishi zilizotungwa kwa lengo la kisiasa; atabaki anawashangaa wahariri.

Lakini baadaye imedhihirika kwamba kuna kundi lilipewa pesa lifanye fujo msibani kwa maslahi ya kisiasa, lakini bahati nzuri lilifahamika na kudhibitiwa, huku waandishi waliohusishwa walishaandika habari yenye tukio ambalo halikutokea!

Tutaidhalilisha taaluma kiasi gani kabla ya kushituka na kusema inatosha? Je, msomaji wa kawaida asiyejua makundi hayo ya wahariri, na mbinu zinazotumika kuwagawa, ataamini habari ipi na kupuuza ipi? Ni lini taifa litaondokana na kizazi hiki cha ufisadi uliojikita ndani ya mfumo unaotafuna hata taaluma za watu?

Ninavyoamini mimi, wanahabari hawana kosa kuwa na itikadi au kuwa wanachama kwa hiari. Kosa ni kujifanya hawana itikadi, huku wakifanya kazi za kueneza itikadi za vyama ambavyo wanadai hawaviungi mkono. Yawezekana kuna mawili; ama hawajui maana ya itikadi, au hawajui umuhimu wa kuwa na itikadi. Lakini kwa mujibu wa matendo yao, nao wana itikadi.

Bado nawatafuta wanahabari wasio na itikadi. Sijawaona. Labda wapo! Lakini wale ninaowajua, wanaochomoza sana katika maandishi yao, ni waandishi wenye itikadi - ama za kuambukizwa au zinazotokana na imani zao wenyewe.

Wale wenye itikadi za kuambukizwa, hawana msimamo. Ni vipepeo. Ni vinyonga. Hawaaminiki. Wanabadilikabadilika kulingana na urafiki au ugomvi walionao kwa wenye itikadi. Na katika siasa za Tanzania, hili ndilo kundi la wanamtandao, na ndilo limekuwa linashutumiwa kwa kuufanya uandishi wa habari kuwa ‘ukarani.’

Na imedhihirika kwamba hata ndani ya CCM, waandishi wenye kufuata itikadi thabiti ya CCM, hawana kiherehere, hawajipendekezi, hawatumiwi. Na hawasikiki sana hadi wakati wa uchaguzi. Wenye itikadi za kuambukizwa, ndio wanaosikika sana; ndio wanaotumiwa na wakubwa. Ndio wanaotuhumiwa kufanya ukarani!

Na baadhi yao ni wasomi ambao wangepaswa kutusaidia kuukomboa uandishi kutoka kwenye utumwa huu. Wenye itikadi zitokanazo na imani binafsi katika masuala kadhaa, wamejipambanua kama watu wenye msimamo. Hawatazami sura, cheo au uwezo wa kifedha wa mtu yeyote. Hawatafuti urafiki au maslahi binafsi bali wanaangalia picha pana zaidi; mustakabali wa jamii nzima.

Naamini kwamba kila mmoja wetu yumo katika mojawapo ya makundi haya. Ni lipi litaivusha Tanzania kuelekea huko tuendako, tunakotamani kuwarithisha watoto wetu? Katika mgawanyiko wetu, wananchi wanatuona. Upande mmoja kuna wanahabari wapambanaji dhidi ya ufisadi; upande mwingine kuna marafiki wa mafisadi, watetezi na mashabiki wao, wanaotumika kudhoofisha vita dhidi ya ufisadi.

Inasikitisha inaposemekana kuwa walio nyuma ya ‘ukarani’ huu ni wale wale waliokuwa wanahusishwa na ufisadi mkubwa katika miaka mitatu iliyopita; wale wale waliowatumia waandishi kuwachafua na kuwadhoofisha washindani wenzao kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2005; na wale ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakitapatapa kujisafisha na uchafu wa tuhuma za ufisadi.

Wanasiasa na wafanye watakavyo; maana ni wanasiasa. Lakini je, hawawezi kufanikisha njama zao bila kutumia waandishi? Iwe itakavyokuwa, huu umeshakuwa ugonjwa wetu; na waliotuambukiza ugonjwa huu tunawajua. Na hili ndilo kosa kubwa ambalo kizazi hiki hakitawasamehe iwapo hawatatubu na kuacha!

+447853850425
ansbertn@yahoo.com
Utakapojua Hujui Ndipo Utakapojua

Makala -Kosa kuu la Kikwete, Lowassa na Rostam
 
Inasikitisha inaposemekana kuwa walio nyuma ya ‘ukarani’ huu ni wale wale waliokuwa wanahusishwa na ufisadi mkubwa katika miaka mitatu iliyopita; wale wale waliowatumia waandishi kuwachafua na kuwadhoofisha washindani wenzao kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2005; na wale ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakitapatapa kujisafisha na uchafu wa tuhuma za ufisadi.

Wanasiasa na wafanye watakavyo; maana ni wanasiasa. Lakini je, hawawezi kufanikisha njama zao bila kutumia waandishi? Iwe itakavyokuwa, huu umeshakuwa ugonjwa wetu; na waliotuambukiza ugonjwa huu tunawajua. Na hili ndilo kosa kubwa ambalo kizazi hiki hakitawasamehe iwapo hawatatubu na kuacha!

- Ngurumo ninamkubali siku zote, huwa hachanganyi maneno Tanzania tunahitaji waandishi watatu tu kama yeye inatosha, nimeona makala moja ya Balile kuhusu Mboma kugombea ubunge, yaani nasikia hata kutapika.

Bravo Ngurumo, maana uandishi wako unakubalika hata na wakulu wengi wa taifa, ninakutobolea siri mkuu karibu wote huwa hawakosi nakala zako kwenye briefcase zao.
 
Hatujali chama. kama lengo lake ni kuwapinga mafisadi poa tu.

Article imesimama sana naikubali mkuu wangu.
 
Dah Huku mbagala ni saa karibu sita usiku. mzee ES siku njema mkuu na heri na fanaka za mwaka mpya!

Ufisadi utatukoma toka tuanze miaka hiyo 2005. Tupo pamoja. Halafu mbona wapiganaji wapya ndo wanatokomea?
 
Hivi wakuu si kuna wakati hapa JF tulisema Pastor Laizer aliyesimamia mapokezi ya Lowassa jimboni kwake baada ya kujiuzulu kwamba ni mwenda wazimu alipomsifia mkuu huyu? Halafu tukasema kwamba wananchi waliompokea huko jimboni kwake ni wenda wazimu! What happened to all that? Ooh my God, only in Tanzania.

Yaani kiongozi aliyetufikisha taifa kulipa dola laki moja na nusu kwa siku kwa ajili ya umeme ambao haukuwepo, na kuwaacha wananchi wakiishi kwenye giza, huku zile hela zikienda mifukoni mwake na washikaji zake, eti ni bora sana na ni mchapa kazi hodari?

Pleeeeeease somebody take me to another planet! Maana hapa on earth labda I am lost! Damn it!

Mkuu FMES inasikitisha. Ila wanasema penye udhia penyeza rupia. Niliambiwa kuwa wana-Apolo walisaidia sana katika mapokezi yale. Michangi mikubwa ya fedha hubadilisha akili za watu.
 
Hayo yaliyotajwa ndiyo yaliyomharibia Lowasa nadhani kuna mtu ana hamu tufyatue dark side of Lowasa humu ndani.

1.Mashangingi ya wabunge yaliyonunuliwa kuna tuhuma za kifisadi za hali ya juu ambazo pengine yeye mwenyewe ndiye aweza eleza alivyopata lile benzi la kutembelea baada ya manunuzi yale ya magari ya wabunge.

2.Fedha za maafa na mafuriko wakati ule zilifisadiwa.Labda atueleze aliwezaje kujenga jumba lile alilopangisha ubalozi wa Afrika ya kusini kwa hela ipi ambayo aliipata wapi kipindi kile?

3.Kufutwa kwa kibali cha ujenzi wa mnazi mmoja kulitokana na ugomvi wake na Kitwana Kondo aliyekuwa meya wa Jiji wakati huo wakati Lowasa akiwa waziri alihisi mwenzie kapata pengine bila kumshirikisha?!!! Kitwana au kumgawia?!!! Akaamua kufuta vile vya mwenzie Kitwana Kondo akabakiza vya kwake ambavyo navyo vilijaa harufu za kifisadi tu ambavyo viliuzwa kwa bei ya chini cha juu kikaenda kwa ....Utajaza.Vingine wakagawiana kiswahiba kifisadi.

Mabati yalibomolewa na wananchi si kwa amri ya Lowasa bali Christopher
Mtikila ndiye alihamasisha machinga kuvamia eneo hilo ambalo lina mnara wa uhuru na kubeba mabati na kutimuka.

Kusema nyota yake iling`ara kwa ajili ya hayo nina wasiwasi.

Kuhusu Richmond alihusika kabisa.Kwa nini kama suala lile aliliona linamzidi uwezo na lina utata kwa nini hakumpelekea faili makamu wa Raisi au Raisi mwenyewe alifanyie uamuzi.Kwa nini yeye alitoa "go ahead" Mradi fisadi wa Richmond uendelee wakati akijua kabisa ulikuwa una utata kama alivyojieleza bungeni? Kwani wakubwa zake Makamu wa Raisi na Raisi walikuwa wamekufa si walikuwepo kwa nini hakuwapelekea wao walifanyie maamuzi kama si ulaji rushwa?

Richmond siyo porojo wala kampeni za kumchafua.Tunasubiri tu. ngoja suala la EPA lishughulikiwe.Tutamshukia kama mwewe asidhani tumelisahau kawekwa kiporo.Tutamshukia tu labda akimbie nchi au akajifiche porini kwenye mashimo lakini hata akijificha kwenye mashimo tutamfuata huko huko kumfukua kama Saddam Hussein alivyofukuliwa.

Kikwete ana udhaifu wake mkubwa tu lakini kwa ufisadi kumlinganisha na Lowasa kwaweza kuwa ni kumwonea.Hajafikia kiwango hicho.Nyerere alimkataa Lowasa sababu ya ufisadi na Kilichomponza hata Kikwete akataliwe na Nyerere ilikuwa ni urafiki wake na Lowasa.Lowasa ndiye alimponza kipindi kile Kikwete.Nyerere alijua kuwa ukiwa rafiki na fisadi lazima na wewe una matatizo au utapata matatizo.

Kipindi cha utawala wa Kikwete Lowasa katoa mchango mkubwa wa kuharibu crediblity ya Raisi Kikwete kuliko waziri mwingine yeyote.Na ametoa mchango mkubwa sana kumfanya Kikwete anuke kifisadi mbele ya umma.


.

Nakubaliana sana na wewe Mkuu. Kwa kuongezea tu, UVCCM ndio waliopendekeza JMK na EL wachukue form za kugombea URais 1995. Na wao (UVCCM) ndio waliahidi kusaidia ushindi wao. Ikumbukwe pia kwamba, mwaka ule walijitokeza wagombea wengi kuliko wakati wowote wa chaguzi za ndani (CCM) siku za nyuma.

Wasiwasi wangu mkubwa kuhusiana na EL ni ubinafsi wake. Kuna issue moja ambayo hadi leo siielewi, inashangaza na inauma sana. Nayo ni ubomoaji wa jengo kubwa (apartments) karibu na nyumba yake aliyopangisha kwa ubalozi wa SA. Jengo lile lilibomolewa kwa kisingizio kuwa lilikosa hati zilizohitajika kulijenga (building permits). Na hata hati hizo zilipotolewa na wahusika, zilikataliwa na baadhi wa watendaji wa Municipal ya Kinondoni walichukuliwa hatua kutokana na kutoa hati hizo. Inasemekana Jengo lilibomolewa kwasababu kuwepo kwake kulizuia hewa nzuri kufikia nyumba yake (Ubalozi wa SA). Naamini kuwa kama jengo lile lingekuwa la mtu mwingine, lisingebomolewa. Na hata kama halikuwa na uhalali wa kuwepo, ingekuwa busara zaidi kutoza "fine" kubwa kwa wamiliki ili iwe fundisho, kuliko kuacha masalia yake yasiyopendeza kabisa.
 
Phillemon Mikael mkuu, kuna kitu kimoja umekisema katika mchango wako ambacho nadhani wanajanvi hawakichukulii seriously ingawa ni muhimu sana kwa utawala wa Jakaya; nacho ni role ya SANGOMA katika maamuzi. Ni kweli usiopingika kuwa waganga wa kienyeji wanainfluence sana na maamuzi ya muungwana kwahiyo kama alivyosema Mikael siyo ripoti ya Mwakyembe peke yake iliyomfanya Jakaya amtose Lowassa bali ni ushauri wa waganga wake wa kienyeji kuwa huyu bwana alikuwa anampiku mwaka 2010. Hata wakati wa mchakato pale DODOMA mwaka 2005 Jakaya alikuwaanatembea na SANGOMA wake kwenye Cruiser lake.; wengine anaimport toka West Africa!! sasa kwa imani potofu namna hiyo uongozi utaleta maendeleo au maaalbino wataachwa kuchinjwa kweli??
 
Phillemon Mikael mkuu, kuna kitu kimoja umekisema katika mchango wako ambacho nadhani wanajanvi hawakichukulii seriously ingawa ni muhimu sana kwa utawala wa Jakaya; nacho ni role ya SANGOMA katika maamuzi. Ni kweli usiopingika kuwa waganga wa kienyeji wanainfluence sana na maamuzi ya muungwana kwahiyo kama alivyosema Mikael siyo ripoti ya Mwakyembe peke yake iliyomfanya Jakaya amtose Lowassa bali ni ushauri wa waganga wake wa kienyeji kuwa huyu bwana alikuwa anampiku mwaka 2010. Hata wakati wa mchakato pale DODOMA mwaka 2005 Jakaya alikuwaanatembea na SANGOMA wake kwenye Cruiser lake.; wengine anaimport toka West Africa!! sasa kwa imani potofu namna hiyo uongozi utaleta maendeleo au maaalbino wataachwa kuchinjwa kweli??
...............duh!!!!!!!!!!!!....................JUJUMAN ndani ya IKULU?????
 
Phillemon Mikael mkuu, kuna kitu kimoja umekisema katika mchango wako ambacho nadhani wanajanvi hawakichukulii seriously ingawa ni muhimu sana kwa utawala wa Jakaya; nacho ni role ya SANGOMA katika maamuzi. Ni kweli usiopingika kuwa waganga wa kienyeji wanainfluence sana na maamuzi ya muungwana kwahiyo kama alivyosema Mikael siyo ripoti ya Mwakyembe peke yake iliyomfanya Jakaya amtose Lowassa bali ni ushauri wa waganga wake wa kienyeji kuwa huyu bwana alikuwa anampiku mwaka 2010. Hata wakati wa mchakato pale DODOMA mwaka 2005 Jakaya alikuwaanatembea na SANGOMA wake kwenye Cruiser lake.; wengine anaimport toka West Africa!! sasa kwa imani potofu namna hiyo uongozi utaleta maendeleo au maaalbino wataachwa kuchinjwa kweli??

Ndio maana muungwana huwa anapagawa wakati mwingine ggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrhhhh! Kweli Nyerere aliona mengi, aliweza kutueleza machache tu. Mengine tutasoma wenyewe kwa nyakati. Nilifikiri Muungwana kaacha masangomaism!
Mkuu Bulesi,
Hivi hayo Masangoma hayapokei 'rushwa' tuyape hoja zetu za mafisadi na mustakabali wa taifa?
 

Kampeni ya kummaliza kisiasa JK, Spika na wabunge kadhaa "wakorofi", imeanzishwa rasmi na Karamagi & Co. (Lowassa na Rostam) kupitia magazeti yao maalum ya AHSUBUHI NJEMA, TAZAMA, NYUNDO, TAIFA NA UMMA. Nia ni kuhakikisha JK anakuwa Rais kwa muhula moja tu na Spika Samuel Sitta na wabunge "wakorofi" hawarudi Bungeni mwaka 2010.

Magazeti hayo ambayo huchapishwa kila siku ya kazi kwa mpangilio, toka Jumatatu hadi Ijumaa, yanabeba ujumbe mahsusi wa ushawishi kwa umma kwamba: JK hana shukrani, kawatosa rafiki zake na kuwakumbatia "maadui"; Membe ni msaliti na anampotosha JK; Lowassa ni kiongozi safi na bora ambaye alionewa tu na Kamati ya Dk. Mwakyembe; bila Lowassa, Rostam, Karamagi, Makamba, Kingunge na wanamtandao wengine, JK hashindi uchaguzi wa 2010; Spika Sitta, Naibu Spika Anne Makinda na wabunge "wakorofi" wa CCM akina Anne Kilango, Mwakyembe, Selelii, Manyanya, Ole Sendeka, Kimaro, Zambi, Nkumba, Mpendazoe, Shellukindo (Bw. & Bi.), Mpesya, Ruth Msafiri na Nyalandu, ni wapinzani wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Magazeti haya yanahaririwa na waandishi walewale mamluki: Deodatus Balile, Manyerere Jackton, Charles Charles, Muhingo Rweyemamu, Prince Bagenda na Gama wa gazeti la HOJA. Baadhi ya makala huchangiwa na Salva Rweyemamu na Premy Kibanga wa Ikulu na Mbunge wa Kigoma Peter Serukamba ambaye alibubujikwa machozi na kuugua baada ya Lowassa kujiuzulu. Yalianzishwa kwa mtaji wa sh. milioni 300 alizotoa Karamagi kwa niaba ya Lowassa na Rostam, mara baada ya Lowassa kujiuzulu.

Taarifa ndani ya Chama Tawala zinasema magazeti haya yana baraka zote za Makamba. Ndiyo maana baadhi yake yanahaririwa kwenye ofisi za UVCCM na kwa kutumia kompyuta za jumuiya hiyo.

Kwa mujibu wa kikao cha KALOKIRO kilichokaa Morogoro hivi karibuni, magazeti hayo yatasaidiwa baadaye (karibu na uchaguzi mkuu) na magazeti ya RAI, MTANZANIA na THE AFRICAN. Mwakani, mtandao huo wa mafisadi unaanzisha kituo cha redio na televisheni. Lengo kuu ni kuwamaliza wote hao kisiasa na kumwinua Lowassa agombee Urais mwaka 2010.

Matoleo ya wiki mbili zilizopita za magazeti hayo yote yalikuwa na makala za kumsafisha Lowassa na kudai kuwa Sitta anamhujumu JK, Sitta ana lengo la kuhamia CHADEMA, Kimaro kapora shamba la chuo, Mwakyembe ni mkabila, Membe ni mfuasi wa Malecela, JK hana fadhila mfano wa dereva aliyesaidiwa kwa kusukumwa kutoka kwenye matope lakini akakataa kuwabeba waliomsaidia ili wasichafue gari lake n.k. NGOMA IMEANZA, MAKUBWA ZAIDI YAJA!

Nimesoma, hakuna hoja hapa!

Bye bye thread
 
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/22374-sauti-huru-anguko-la-mengi-kama-maxell-3.html

Mod na hii ya Sauti Huru ingewekwa humu kwani ina uhusiano mkubwa kwa kuwa nalo ni miongoni mwa magazeti yaliyoanzishwa mahsusi kuwatetea watu ambao jamii imeamini na serikali imeamini na kuwachukulia hatua. Hii ni hatari, lazima tukatae kulishwa sumu hii mbaya na tena bila hoja. Kuna gazeti moja limethubutu hata kusema kwamba VITA YA UFISADI NI VITA KATI YA WACHAGA NA WAHAYA na bado Mkuchika na jamaa zake wa Maelezo hawajachukua hatua kwa habari/makala inayolenga kuchochea mgawanyiko wa kikabila. HII NI HATARI KUBWA NA SIJUI hao UWT wanafanya kazi gani.

Lakini habari ya Sauti Huru sijui kama ni habari ama makala
 
Nimesoma kwa mshangao sifa anazotupiwa Lowasa,kabla ya kumpamba mtu kwa sifa ni bora uangalie uadilifu wake kwanza Mh: huyu hana tofauti na Mkapa kwa waliyowatendea wananchi wa Tanzania si watu wa kusifiwa hawa. Mkapa ni mung'unye ameharibikia ukubwani ameanza wizi ktk hatua za mwisho za kipindi cha pili cha uraisi wake. Lowasa nimebahatika kumjua kidogo ktk miaka ya mwanzoni mwa 80 nilipokuwa Arusha wakati huo nchi inanuka hamna bidhaa,chakula ,nguo nk naye alikuwa katibu wa CCM mkoa by then alishaharibika kwa ulafi. alipopewa uwaziri ndipo alipofungulia mbwa akasema mtanikoma, kiasi hayati mwl Nyerere akamwambia hafai kuwa raisi mtoto mdogo mwenye tamaa ya mali, bahati mbaya na huyo mtoto mkubwa alietupa ndio akawa MZINGA MBOVU unalipuka ovyo kwa tamaa na ufisadi. kwakifupi hawa jamaa ni magabacholi tu hawastahili sifayeyote. wamejivua heshima ya kusifiwa kitambo.
 
Nimesoma kwa mshangao sifa anazotupiwa Lowasa,kabla ya kumpamba mtu kwa sifa ni bora uangalie uadilifu wake kwanza Mh: huyu hana tofauti na Mkapa kwa waliyowatendea wananchi wa Tanzania si watu wa kusifiwa hawa. Mkapa ni mung'unye ameharibikia ukubwani ameanza wizi ktk hatua za mwisho za kipindi cha pili cha uraisi wake. Lowasa nimebahatika kumjua kidogo ktk miaka ya mwanzoni mwa 80 nilipokuwa Arusha wakati huo nchi inanuka hamna bidhaa,chakula ,nguo nk naye alikuwa katibu wa CCM mkoa by then alishaharibika kwa ulafi. alipopewa uwaziri ndipo alipofungulia mbwa akasema mtanikoma, kiasi hayati mwl Nyerere akamwambia hafai kuwa raisi mtoto mdogo mwenye tamaa ya mali, bahati mbaya na huyo mtoto mkubwa alietupa ndio akawa MZINGA MBOVU unalipuka ovyo kwa tamaa na ufisadi. kwakifupi hawa jamaa ni magabacholi tu hawastahili sifayeyote. wamejivua heshima ya kusifiwa kitambo.

- Mkuu Jujuman, saafi sana maneno mazito sana haya.
 
Ndio maana muungwana huwa anapagawa wakati mwingine ggggrrrrrrrrrrrrrrrrrrhhhh! Kweli Nyerere aliona mengi, aliweza kutueleza machache tu. Mengine tutasoma wenyewe kwa nyakati. Nilifikiri Muungwana kaacha masangomaism!
Mkuu Bulesi,
Hivi hayo Masangoma hayapokei 'rushwa' tuyape hoja zetu za mafisadi na mustakabali wa taifa?

Hakuna JARS zozote hizo ni imani potofu na zimepitwa na wakati harafu ni stori za vijiweni,kwanza humu duniani hakuna sangoma lolote sangoma ni wewe mwenyewe ama rafiki yako.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom