Kama Jeshi litafanya usafi tarehe 23-24, basi CHADEMA ifanye maandamano tarehe 25 wapite njia zikiwa safi

Kashishi yetu

JF-Expert Member
Mar 22, 2014
3,127
2,945
CHADEMA imetangaza kufanya MAANDAMANO TAREHE 23.

Katika hali ya kushangaza JWTZ nao tarehe hizo wamepanga kufanya usafI ingawa wangeweza kupanga tarehe nyingine ya kufanya huo usafi.

Hata hivyo suala la usafi ni suala muhimu Sana,, Hivyo CHADEMA nawashauri tarehe Hiyo wasofanye MAANDAMANO Yao Bali wapishe usafi ufanyike ili wakianza MAANDAMANO Yao WAPITE kwenye barabara ZIKIWA SAFI zilizosafishwa na Jeshi.

Kufanya MAANDAMANO kwenye mazingira machafu ni hatari Kwa Usalama wao.

Hivyo ni vizuri wakisubiria usafi ufanywe ili wake WAPITE kwenye mazingira safi na salama.

Naomba kuwasilisha.
 
kutoka hapa ngome kama msemaji wa jeshi,tunatazamia kuongeza siku za kufanya usafi,hata kurudia maeneo mengine yatakayoonekana kutotakata siku ya tarehe 23.
 
JESHI LITAENDELEZA USAFI KATIKA MUDA WOTE WA JANUARY!
NA USAFI UKIKAMILIKA HATUTATAKA UCHAFUZI WA MAZINGIRA!
 
kutoka hapa ngome kama msemaji wa jeshi,tunatazamia kuongeza siku za kufanya usafi,hata kurudia maeneo mengine yatakayoonekana kutotakata siku ya tarehe 23.

Jeshi limekosa kazi ..... watangaze kufanya usafi kila siku tujue moja!!
 
CHADEMA washiriki usafi kwa siku mbili 24/01/2024 na 25/01/2024.

Baada ya Usafi CHADEMA Waendelee na maandamano yao...
Hii ni akili kubwa mno!!

Pengine Chalamila atakuwa amesaidia maandamani kufanyika!!

CDM wajitahidi kuwahamasisha watu wao kujitokeza kwa wingi kufanya usafi!!

Naona kama Chalamila anachanganyikiwa hapo alipo
 
Active hivi nyie huwa mnatumia kigezo gani kuunganisha mada.

Maudhui ya mada yangu na ya hii mada yanafanana?

Mada ya huyu inataka CHADEMA wasubiri jeshi lifanye usafi ndipo waandamane wakati mada yangu inataka CHADEMA ishiriki usafi 24/01/2024 mpaka 25/01/2024 na baada ya hapo ndipo wafanye maandamano.

Hivi kusubiri jeshi lifanye usafi ndipo CHADEMA waandamane na kushiriki kufanya usafi pamoja na Jeshi kisha CHADEMA waandamane ni jambo moja??

Mnakera sana wakati mwingine.

CC: Paw
 
Hii ni akili kubwa mno!!

Pengine Chalamila atakuwa amesaidia maandamani kufanyika!!

CDM wajitahidi kuwahamasisha watu wao kujitokeza kwa wingi kufanya usafi!!

Naona kama Chalamila anachanganyikiwa hapo alipo
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Chadema akili KUBWA
 
Back
Top Bottom