Kagame hakuja msibani kumzika rais wetu, na alikaa miezi siku nyingi sana kabla hajatupa pole, Rais Samia unakwenda Rwanda kufanya nini?

Niambie msiba hata mmoja ambao Magufuli alihudhuria. Hata wewe mleta uzi usipokuwa na tabia ya kwenda kwa misiba ya majirani utasusiwa pale utakapopata msiba. Malipo ni hapa hapa.
 
Kwani bado hujaelewa tu?
1. SHH ndiye mtu pekee aliyekwenda kumuona LISU Nairobi, kutoka serikalini
2. SHH ndiye aliyesema tunaponya makovu kwanza, JIULIZE, HAYO MAKOVU YANAYOPONYWA, YALISABABISHWA NA NANI?
3. Ya kuingia nchi hiyo, nani wa mwisho kwenda kabla ya leo?
 
Kwa hiyo ulitaka Rais Samia arithi maugomvi ya watu? Meko mwenyewe alikuwa mtata kwa kila mtu.
 
Niambie msiba hata mmoja ambao Magufuli alihudhuria. Hata wewe mleta uzi usipokuwa na tabia ya kwenda kwa misiba ya majirani utasusiwa pale utakapopata msiba. Malipo ni hapa hapa.
Hili nalo neno..!!! Tena sisi wabongo, kuna watu walisusiwa marehemu wakazike wenyewe, wengine walisusiwa chakula ikabidi wakaitwe masela wa stend waje wafanye yao..!!
 
Banyamulenge bhana.
 
Kwamba hujui mwendazake aliwekeza Rwanda na hakutaka kulipa kodi na malori yake ya KESI INVESTMENTS.
Ugomvi wa Kagame na Magufuli ukisimuliwa utampongeza Kagame.
Wakati wenzake wanapambana na Corona yeye yuko Dodoma anapiga picha kwenye mawe anawabeza.
Sayansi ikajaribiwa na nyungu
Nyungu zinakakata moto
 
Shukran sana mkuu, umemjibu vyema sana,, yaani watu kama vile siyo binadamu wanashindwa kujua hata Kagame ni binadamu kama wengine, hawajua kuwa Kagame kama Rais wa nchi ni Taasisi! Yaani walitaka kwenye msiba hadi na yeye awepo....
 
Niambie msiba hata mmoja ambao Magufuli alihudhuria. Hata wewe mleta uzi usipokuwa na tabia ya kwenda kwa misiba ya majirani utasusiwa pale utakapopata msiba. Malipo ni hapa hapa.
Kwamba PK ni mmoja ya waliofariki jpm akagoma kwenda!!!

Jf imejaa watu wa ajabu sana aisee.
 
Mama ana watetezi wengi sana - kwanza wa ile dini yake , hawa hata afanye famba gani wako nae tuuuu piga ua galagaza, wengine wazenji, wengine kwa mbaali wanawake, na wengine ni akina sisi tunaomkubali tu. Hivyo nyie mnaoona mabaya tu tuvumilieni miaka 9 sio mingi Mungu akipenda
 
Mkuu unaongea jambo ambalo ama unapotosha au hauna facts, PK alituma salamu za rambirambi na bendera za rwanda kushushwa nusu mlingoti.Pia siku ya kuaga rasmi alimtuma Waziri Mkuu wake dodoma kumuwakilisha. Suala la Mama kwenda, ni muhimu kidiplomasia ikiwa kujitambulisha kwa majirani zake na pia kuendeleza maswala ya biashara na uchumi,kwani Rwanda ni mdau mkubwa sana katika matumizi ya bandari yetu.
 
Shukran sana mkuu, umemjibu vyema sana,, yaani watu kama vile siyo binadamu wanashindwa kujua hata Kagame ni binadamu kama wengine, hawajua kuwa Kagame kama Rais wa nchi ni Taasisi! Yaani walitaka kwenye msiba hadi na yeye awepo....
Some of our colleagues here are 'Foolish' by nature and they have actually been 'brainwashed' to hate Rwanda and His Excellence Paul Kagame in every 'angle' and 'aspect' of life.
 
Kwani ni lini ulisikia Magufuli kaenda kuzika nchi za watu?
Mambo ya nchi unalinganisha na mambo ya mitaani
 
Some of our colleagues here are 'Foolish' by nature and they have actually been 'brainwashed' to hate Rwanda and His Excellence Paul Kagame in every 'angle' and 'aspect' of life.
Ziara ya Mama imeniambia kwamba kagame anatakiwa aongoze Rwanda mpaka atakapoamua yeye
Sisi maneno meengi na siasa tu mara katiba mpya
Rwanda wanatengeneza VW,wanatengeneza simu sisi kila siku tunalia umeme hautoshi
 
Ningekuwa Mimi ndiyo Mama ( Mheshimiwa ) zile Ziara Mbili za kwenda katika Kiwanda cha Simu na Gari za Volkswagen alizopangiwa na Mwenyeji wake ningezichomoa Kimtindo.

Kilichofanywa na Rwanda ( hasa kwa hayo Maendeleo yake makubwa na ya haraka ) pamoja na kwamba imepitia 'Changamoto' nyingi za Machafuko ( Genocide ) kilitakiwa kiwe kimefanyika muda mrefu sana nchini Tanzania ( hasa kutokana na Utulivu wake wa Amani ) uliopo ila bahati mbaya imekuwa ni tofauti.

Kuna Mtu 'Katukanwa' kwa Akili Kubwa, ila Yeye 'hajashtukia' Mchezo na kaishia tu 'Kupozi' katika 'Ndinga' ya maana inayotengenezwa Kigali nchini Rwanda.

Na alichokifanya Rais Kagame ni kutuma that indirect Message' kuwa Waafrika 'We have to walk the talk and not talking the walk' kwani tunapoteza muda mwingi kwa Majungu, Wivu, Chuki na Uswahili Uswahili wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…