Lakini Kuna waislamu humu - Ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na naamini kuwa Taifa ni watu-sio mbuga za wanyama , migodi ya dhahabu au miti ya mikarafuu. Kama ni Taifa kwa nini lisijali maslahi ya watu wenye hilo Taifa?
Mkuu wangu heshima mbele, mimi ninaheshimu sana dini za wananchi wenzangu, na naomba uniamini kwamba marafiki wangu wengi wa karibu huwa ni Waisilamu, nikiwa NY nimesaidia sana ndugu wabongo wenzangu waliokwama pa kulala na chakula, na hata kuwatafutia kazi mpaka walipoweza kusimama wenyewe kwa miguu yao,
infact mmoja wao nilimkuta kwenye Subway akiwa hana pa kulala bali analala kwenye hilo treni for at least one month, to the time nilipomkuta, na 95% yao hawa ndugu zangu walipofanikiwa tu nikalipwa mateke, the matter of fact nikiwa na mmoja wao siku moja tulivunjiwa tukaibiwa lakini vilibiwa vitu vyangu tu lakini sio vyake na tukow awili tu kwenye apartment, My point sio kujigamba ila kukufahamisha how sensitive we are kama binadamu, na kwamba na sisi at the end of the day ni binadam pia,
Lakini hapa mbele yetu, kwenye hili la kujiunga na OIC huenda tunaongelea moja ya sababu muhimu ya kuwepo kwetu hapa JF, yaani uchungu wa Taifa letu it is about my nation baby which happens to be yours too, I respect that kwamba mimi na wewe ni wananchi wa taifa moja, na tunaweza kujadili kwa upeo na mapana, bila noma.
Siku ya kwanza tu niliposikia tu hizi habari, nilizungumza na viongozi wetu wengi sana, na kati ya viongozi karibu wote nilioongea nao hiyo siku, kuna mmoja ambaye yuko kwenye Jumuiya moja ya kimataifa ambaye aliwahi kuwa foreign na anaijua hii ishu kwa mapana na marefu, yeye ndiye aliyenifungua macho zaidi kwa kuniwekea karata zote za pande mbili mezani ili niamue mwenyewe kusuka au kunyoa,
Ninaomba nirudie tena kwamba sina ubaya na mwananchi yoyote wa upande wa pili wa this ishu, sina tatizo na mwananchi yoyote wa dini tofauti na yangu, lakini hapa kuna taifa letu, na hii ni ishu moja kati ya chache sana ninayokubaliana na Mwalimu, Baba wa Taifa kwamba sisi Tanzania kwa sababu sio taifa la Kiisilamu, hatuwezi kujiunga na shirika la dini ya Kiisilamu.
Na ninaomba nirudie kwamba kwenye hili I make no bones about it, ni kwamba ninafanya kazi around the clock kwa kutumia kila nguvu niliyonayo mwilini mwangu, ku-reach out kwa anybody ambaye ni politically influencial or connected ninayewaza kumfikia in our nation, kuwaomba kwamba waelewe msimamo wa baadhi ya sisi wananchi wa Tanzania. Hii safari ndefu sana imenifikisha mpaka kwa baadhi ya Wakuu wa wilaya na tarafa, madiwani, RCs na the rest, kwa sababu kwangu hakuna tena ishu nzito katika our time kama hiii.
Ninarudia tena siamini kabisa kwamba behind hii ishu kunaweza kua na any national debate kuanzia level za intellectualism, academism, ideologism, religionism au politically! It is just what it is kwamba ninaamini kuwa shirika la Kiisilamu linatakiwa kuwa na members ambao ni pure Islams, Tanzania we are not!
Ahsante Ndugu Zangu Wote na Hapa ninaweka Chini Kalamu, Back To Work.