Phillemon Mikael,
wanaofikiri tanzania inaweza kujiunga na OIC au MAHAKAMA YA KADHI wanaota ndoto za mchana...THAT WILL NEVER HAPPEN HERE ..........
Ndugu Mikael ukweli ni kwamba wale wanaofikiria kwamba Waislaam hawawezi kusimama kutetea haki zao basi mmepotea na nitasema hivi... NIA TUNAYO, SABABU TUNAYO na UWEZO TUNAO...
Haya ni maneno ya mwalimu wakati wa kumwondoa nduli Idd Amin sasa ikiwa kweli mnatangaza Udini bila shaka muwe tayari pia kupokea yanayokuja na udini...
Mkuu kwanza kabisa kila siku tunajinyonga wenyewe... Kama unakumbuka Zanzibar walitaka kujiunga na OIC, Zanzibar ambayo asilimia 99 ni waislaam tukaja na sababu zetu nje kabisa ya kwamba swala hili ni la kidini na serikali isiingilie. Tukasema hili ni swala la Kitaifa na kwa maslahi ya Taifa Zanzibar haiwezi kujiunga na OIC kama NCHI.
Ni katika mtazamo huo huo wa nchi tulikataa pia Zanzibar wasijiunge na taasisi mbali mbali za kitaifa kama NCHI - mfano FIFA, IOC (olimpiki) na kadhalika kwa sababu kikatiba nchi ilikuwa moja tu nayo ni Tanzania.
Cha ajabu hawa jamaa zetu walikubali kutojiunga na vyombo hivyo lakini bado bara hatukuishia hapo tu, timu zetu za mpira za taifa zilikuwa na wachezaji toka bara tu mara chache sana wamehusishwa na naweza kuhesabu Zanzibar walipohusishwa kikamilifu usijae mononi.. vile vile ktk timu za ziunazotuwakilisha ktk mashindano ya Olimpiki, Zanzibar tuliwaweka kando mara kibao...
Mkuu unajua unaweza kumsukuma mtu mara nyingi asifanye kitu lakini kuna wakati mtu huyo hufikia Ukutani, ikashindikana kumsukuma tena nyuma isipokuwa yeye kusukuma mbele ili apate nafasi ya kupumua.. Na hapoa ndipo tulipofika ktk maswala mengi ya Zanzibar..
Mkuu, tulikataa Zanzibar kujiunga na OIC kwa sababu Zanzibar haikuwa nchi, sawa sasa iweje leo nchi inapotaka kujiunga na chombo hicho hicho swala linageuka na kuwa hili ni swala la dini serikali haitakiwi kutoa maamuzi yanayolenga Upande mmoja!..Na wapo wanaosema serikali haitrakiwi kabisa kuingilia maswala ya dini wakati huo huo haohao wanaosema hivyo wanapinga Waislaam kuanzisha mahakama ya kadhi..iweje swala la mahakama ya kadhi ambalo ni swala la dini ya Waislaam lirudi ktk maamuzi ya serikali wakati mwanzo imekataliwa kuwa maswala ya dini yasiingiliwe na serikali!..
Nitarudia kusema tena ni kwa kutumia katiba hiyo hiyo Nyerere alivunja chombo cha kiislaam na kuunda BAKWATA, chombo cha serikali kwa Waislaam wakati KKK na vyombo vyote vya kikristu viliendelea na kazi zake bila kuingiliwa na serikali, yet Waislaam hawakuweka manunguniko yao hadharani.. chama cha Bakwata kikaendeshwa na serikali kwa miaka mingi hadi baadhi viongozi wa Kiislaam walipoamua enough is enough wanataka chombo cha Waislaam kwa waislaam, wakaunda BALUKTA..wakitumia hoja ambayo imependekezwa na watu wengi tu.. Kuwa maswala ya dini serikali haitakiwi kuweka mkono wake lakini ajabu ni kwamba BALUKTA ilipigwa vita na viongozi wa dini ya kikristu pamoja na viongozi wa serikali ikabidi Sheikh Kassim bin Jumaa mmoja wa waasisi wachukuliwe hatua kali.. Mateso aliyopewa kifungoni hakuweza hata kuchukua muda, baada ya kuachiwa week moja tu akafariki dunia...
Mkuu nikirudi nyuma kidogo, Zanzibar kukataliwa kwake kujiunga na OIC was pure roho mbaya, hatukuwa na sababu zaidi ya kuitumia katiba kwani kuna nchi kama Canada ina jimbo la Quebec ambao ni wanachama wa umoja wa nchi za Kifaransa pamoja na kwamba idadi kubwa ya wananchi wake hawana asili wala nasaba na Ufaransa.
Tazama nchi kama Switzeland, hii ina makabila matatu makuu, wapo Wafaransa upande wa Zurich, Wajarumani upande wa Basil na Benn, na Wataliani upande wa kusini Turin, na sehemu zote hizi wamejiunga na jumuiya za makabila yao huko Ulaya na wanazungumza lugha zao, lakini bado wameweza kudumisha amani kati yao kama nchi moja na hata wakienda nje wote ni hujulikana kama Waswiss...ama WaCanada.
Tazama Germany na Ausria hawa wote ni wajarumani na wanazungumza Kijarumani lakini wamekubali kuwepo mipaka kati yao kama nchi mbili tofauti..hakuna misukosuko kama yetu.
Hata hivyo kama nilivyokwisha sema mwanzoni hatuwezi kuiga nchi za Ulaya kujenga Taifa na umoja wetu, sisi kama Waafrika hatuwezi kabisa kusimama Kitaifa na tofauti kama hizo na kuna mifano mingi ya vita kutokea kwa sababu tu kabila fulani makazi yao ni nje ya mipaka ya nchi hiyo. Historia yetu ni chafu na tofaurti kabisa na nchi za Ulaya kiasi kwamba mfumo pekee unaoweza kujenga nchi yetu utatokana na sisi wenyewe katika mzingira yetu..
Sisi tutaijenga nchi yetu kwa kutazama WATU na MAZINGIRA tuliyopo badala ya kuiga nje na kwa neema yakle mwenyezi tanzania imekuwa nchi yenye makabila zaidi ya 120, na dini tofauti zaidi ya 10 sote tukiishi kama ndugu na familia moja pamoja na kwamba tuna tofauti zetu..tofauti ambazo zinaanza toka ktk familia moja moja hadi kitaifa..na hakuna familia hata moja inayotoa amri ama maamuzi ya ndani ya nyumba based on tribe or religion kama kuna mchanganyiko na hakatazwi mtu kufanya ya kabila ama dini yake kwa kuwekewa vikwazo vya marafiki..
Ni kitu gani haswa kinachowatisha wakristu wengi?.. Hakika ni matendo yao wenyewe, Wakristu wana vyombo vya kidini ambavyo kazi yake ni kuhubiri dini tu wakitumia misaada kama mwavuli wa kuingia ktk nyoyo za watu.. vyombo kama World Vision vinatoa misaada kidini..huwezi kufungua NGO Tanzania ambayo haifundishi Biblia ukapewa msaada na vyombo vyote vya kikristu hata kama watu wanakufa njaa kama Somalia na Ethiopia..lakini pamoja na ukweli huo vyombo hivi havikuonekana kuwa tishio kwa dini ya kiislaam kwa sababu dini ni Imani. Mtu yeyote anayeingia dini kwa sababu ya msaada basi huyo sii muumini wa kweli...
Hivyo tofauti na vyombo vya kikristu, OIC inaingia pale Uislaam umekwisha simama..Ni haramu kwa muislaam kumvuta mtu ktk imani ya dini kwa kutumia shida, udhaifu na umaskini wa mlengwa tofauti kabisa na mbinu za kikristu ambazo zinahamasisha zaidi kuingia kule ambako jina la Yesu hakijafika..Na hakika mbinu yao inamvuto zaidi kwa sababu asilimia kubwa ya population duniani ni maskini..na wameweka focus yao kubwa katika kuwavuta maskini..
wakristu wanahaha sana inapofikia swala la vatican hawapendi lihusishwe na swala la OIC wakati kisheria ni haki kabisa kutumia vigezo ktk kuwakilisha hoja yako..Lakini hakuna hata mkristu mmoja anayeweza kutuambia Muislaam anafaidika vipi na Vatican? ama kuna faida gani nchi yetu kuwa na Uhusiano na Vatican kama Taasisi. Nasema tena Vatican ni Taasisi hadi pale watakapo weza kutenganisha kati ya Pope na mtawala wa nchi hiyo. Nina hakika kama kutakuwa na rais mwingine mteuliwa mbali na Pope hatapewa heshima kama anayoipata Pope kwa sababu Vatican na Pope wanaheshimika zaidi ya kuwa nchi kwa sababu ya dini...
Kwa hiyo kama kweli Wakristu wanakataa kabisa nchi yetu kujiunga na OIC, basi kuna kila haja ya kutazama NGO zote za kikristu zinazofanya kazi Tanzania.. Kwa sababu hoja kubwa hapa ni kuwa nchi yetu haina dini kwa hiyo hairuhusiwi kabisa Taasisi yoyote kuingia nchini ikiwa na malengo ya kuboresha (kundi la watu) dini ama dhehebu moja..
Laa sivyo basi kuna hatari kubwa ya kuvunjika Muungano ambao mwalimu aliujenga kwa miaka 23.. na dalili zake zimefikkia kikomo..hakuna kurudi nyuma tena!