Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

mbona mnataka kuficha ukweli ? hivi tushasahau aliyoyasema Askofu Mkuu, Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dar es Salaam, Polycayo Kadinali Pengo kuhusus mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar na suala la kujiunga na OIC?
 
European union ni wanaulaya, mmarekani kashindwa kuingia kaishia kuchungulia.
Africa union ni ya wafrica, wengine wanaishia kutugawa tu, hawawezi kuingia kama si waafrika.
Islamic communities ni ya jumuiya za waislam, iweje nchi ndio iingnie? hapo mimi ndio hainiingii. Labda nchi nzima ingekuwa ya waislamu.
Najua inasemwa inaruhusiwa, je serikali yetu inayoendeshwa na sera zinazobadilika kwa muda mfupi kuendana na alieko madarakani, au nani anataka kufurahishwa tutaweza kwa miaka mingapi?

Kuna fees?
Masharti mengine nini?

Maslahi ya wananchi kwa maendeleo yao na taifa yanaletwa na wananchi wenyewe kwa jumuiya zao au mmoja mmoja. Na kwa mantiki hiyo hiyo Serikali inawajibu wa kuwahudumia wananchi wake kwa mujibu wa walivyojipanga.Iwapo huduma inatakiwa na mwananchi binafsi au kikundi Serikali inalazimka kutowa huduma hiyo na ndio maana utaona kuna jumuiya nyingi nchini mwetu na jumuiya hizo zote zina utaratibu wake wa kusajiliwa na mwisho wa siku muhusika mkuu itakuwa chombo cha Serikali.
Kwa mtiririko huo huo ndani ya Taifa hilo kuna kikundi cha watu wanaoitwa Waislamu na kwa bahati kikundi hichi ni zaidi ya nusu ya idadi ya wananchi wote wa Tanzania. Imetokea kuwa Hawa wananchi wanataka huduma fulani (OIC) na huduma hii haipatikani isipokuwa Serikali ijiunge, sasa tatizo liko wapi? Kwani Serikali ipo kwa kazi gani zaidi ya kuratibu harakati za wananchi katika harakati zao za maendeleo?
Hebu tuangalie mfano wa mikataba mbali mbali ya Kimataifa ya Kibiashara ambayo Tanzania inaingia kwa ajili ya kuwawezesha Wafanyabiashara mmoja mmoja kufanya biashara Kimataifa, kwanini serikali inapoteza muda na pesa za wananchi kwa kuwasafishia njia kundi fulani cha wananchi? Utasema biashara inanufaisha Taifa lakini wanaokuwa matajiri na kutanuwa kwa pesa za wananchi wote ni hao wafanyabiashara. Faida ya biashara hizo haipimiki kwa kipato binafsi cha mwananchi mmoja mmoja na faida ya Waislamu kujiunga OIC haitopimwa kwa kipato cha mtu binafsi pia bali huduma zitakazopatikana zitawasaidia wananchi wote au tuseme zaidi ya nusu ya Watanzania. Hata hivyo uzoefu tulionao Tanzania ni kuwa tuna utamaduni wa kutumia huduma kwa pamoja bila kujali dini inayotowa huduma hiyo.
 
ukisoma charter ya IOC moja ya objectives za jumuiya hii ni:
...to support the struggle of the Palestinian people, who are presently under foreign occupation, and to empower them to attain their inalienable rights, including the right to self-determination, and to establish their sovereign state with Al-Quds Al-Sharif as its capital, while safeguarding its historic and Islamic character, and the holy places therein... to empower them how??
naomba nieleweshwe kama sera ya nje ya nchi yetu inaenda sambamba na hili?
 
ukisoma charter ya IOC moja ya objectives za jumuiya hii ni:
...to support the struggle of the Palestinian people, who are presently under foreign occupation, and to empower them to attain their inalienable rights, including the right to self-determination, and to establish their sovereign state with Al-Quds Al-Sharif as its capital, while safeguarding its historic and Islamic character, and the holy places therein... to empower them how??
naomba nieleweshwe kama sera ya nje ya nchi yetu inaenda sambamba na hili?

there you go.........unakumbuka wakati ule Palestine ilipokuwa........choka mbaya kifedha........OIC iliwasaidia pia......kuna ubaya hapo.......hivi JKN (RIP) kuwasaidia Biafra ilikuwaje vile?
 
Ni kweli kabisa kuwa huwezi ukafananisha WCC,Vatican na OIC kwa namna yoyote ile.Ishu ya kujiunga OIC ni vritical na in anyway lazima tujiulize consequeces za kujiunga na kubaki tulivyo as a nation.Kama wapo wasioafiki lazima ziwepo sababu ambazo ziko shared na kila mtanzania na kama wapo wanaoafiki lazima ziwepo sababu ambazo zinakuwa shared na kila raia.
Tusipapatikie kujiunga OIC kwa sababu za kidini na wala tusipinge OIC kwa sababu za kidini.Tuwe na sababu za kitaifa.Tutafika tu
 
Ni kweli kabisa kuwa huwezi ukafananisha WCC,Vatican na OIC kwa namna yoyote ile.Ishu ya kujiunga OIC ni vritical na in anyway lazima tujiulize consequeces za kujiunga na kubaki tulivyo as a nation.Kama wapo wasioafiki lazima ziwepo sababu ambazo ziko shared na kila mtanzania na kama wapo wanaoafiki lazima ziwepo sababu ambazo zinakuwa shared na kila raia.
Tusipapatikie kujiunga OIC kwa sababu za kidini na wala tusipinge OIC kwa sababu za kidini.Tuwe na sababu za kitaifa.Tutafika tu

mAENO YAKO YANANIKUMBUSHA kauli ndani ya kitabu kilichotolewa na na Halmashauri Kuu ya Maaskofu ya Baraza la Kanisa la Pentekoste la Tanzania(PCT), mwaka 2000 kitabu kile kiliitaka serikali iitishe kura ya maoni kwanza, kabla ya kuamua kujiunga na (OIC), ili kupata ridhaa za Watanzania




Kitabu hicho, kilichopewa jina la "Amani katika Tanzania italindwa kwa:kutenganisha Dini na Mamlaka ya nchi", kinaeleza kuwa kitendo cha serikali ya Tanzania kutaka kujiunga na OIC si jambo dogo. Nijambo linalowahusu Watanzania wote, Waislamu na wasiokuwa Waislam, na hata wale wasiokuwa na dini yo yote. Zaidi ya hayo kile kitabu kilidai kuwasuala la OIC halifai kujadiliwa kijuujuu tu, kwa kupitia katika vyombo vya habari, na wala haifai kuachiliwa Bunge peke yake kuamua juu ya jambo zito kama hilo.


VILE VILE Halmashauri Kuu ya Maaskofu wa Kanisa la Pentekoste, kwa kupitia katika kitabu hicho, walisisitiza kuwa serikali iitishe kura ya maoni ili ipate kuelewa msimamo wa Watanzania wote, wa dini mbalimbali, juu ya jambo hilo...waliendelea kudai kuwa si kazi ya Bunge kutunga sheria za kidini, kwa kuwa OIC ni taasisi ya kidini, ni muhimu taasisi nyingine za kidini zilizopo hapa nchini nazo zishirikishwe kikamilifu katika uamuzi mzito kama huo.

In short Maaskofu wa Kanisa la Pentekoste, katika kitabu kile , walilitilia mashaka uhusiano huo kama utaanzishwa. Wawalidai edai kuwa lengo la misaada inayotolewa na taasisi hiyo ni kwa ajili ya kutaka kueneza imani ya dini hiyo katika nchi wanachama.....maneno ambayo hayana sana tofauti na wana JAMII FORUMS wanaoipinga OIC humu...wale maaskofu pia waliendelea kusema kuwa kama Tanzaniaitajiunga na taasisi hiyo basi itakuwa ni sawa na kuwasilimisha Watanzania bila ya nidhaa yao!

sounds familiar?

29.jpg


Huhitaji kuwa scientist wa BIG BANG ukaelewa kuwa kile kitabu kilitolewa na kanisa la Pentekoste, kama ni onyo kwa serikali isijiunge na OIC, baada ya kumsikia mgombea wa kiti cha urais wa Zanzibar mwaka 2000 Amani Karume katika madahalo ulioandaliwa na BBC, ambako alisema kuwa serikali imekwishafanya utafiti na imeona kuwa Tanzania ijiunge na taasisi hiyo, kwa kupitia serikali ya Muungano, na siyo kupitia serikali ya Zanzibar..yes that was back in 2000!!!

Binafsi sikuzote huwa nawapa heshima kubwa maaskofi kwa kuwa naamini kuwa wao walisoma theology kwenye shuleza seminary ambazo tunaambiwa kuwa wanaproduce wasomi waliobobea lakini kwa vyovyote vile, mtazamo huuu wa Maaskofu pamoja na wa wana JF wanaoipinga OIC kwa sababu tuu Maaskofu walisema na zaidi kwa sababu:

1)umekosa uadilifu

2)Ni mtazamo ulioelekezwa katika kuuangalia upande mmoja tu wa shilingi na kuupuuzia upande wa pili.

3)Ni mtazamo chongo! Ni sawa na mtu mwenye macho mawili lakini akaamua, kwa makusudi, kufumba jicho moja na kuangalia kwa jicho moja.

UHUSIANO WETU NA VATICAN​

Kama serikali ya Tanzania haifai kujiunga na OIC, bila ya kuitisha kura ya maoni kama baadhi ya watu humu mnavyodai, eti kwa sababu OIC ni taasisi ya kidini; basi lazima tukubali kuwa kwa hoja hiyohiyo, serikali hiyo ya Tanzania itakuwa imefanya kosa kuanzisha uhusiano, tena wa kibalozi, na Vatikano, ambayo ni taasisi ya kidini, na siyo nchi yenye raia!

Furthermore, uhusisano huo wa serikali ya Tanzania na Vatikan, ingawa ni uhusiano baina ya nchi hii na Kanisa Katoliki duniani, lakini jambo la kustaajabisha hakuna yeyote anayehoji juu ya uhusiano huo, si serikali wala makanisa ya Kikristo!!!! au ndio tunaendeleza double standards kama kawaida yetu?

Mheshimiwa Aboud Jumbe, ambaye kwa rate ya members wasio ambao JF inawaatract kila kukicha ambaye aliwahi kuwa Makamu Rais wa Jamhuri ya Miuungano wa Tanzania, na pia, Makamu Mwenyekiti wa CCM, katika kitabu chake alichokiita, "The Partner-ship" ambacho ninacho hapa amesema,
"Kwa mfano, kuwepo kwa ubalozi wa Vatican nchini Tanzania hakukupata kuhojiwa, pamoja na kuwa serikali hii inadai kuwa si ya kidini. Kanisa, CCM na serikali, vyote vimekaa kimya huku vikijua kutendeka kwa hilo lakini vitazibwa mdomo." (Uk.126).
mkapa019copy.jpg


Kama ningekuwa msemaji wa waislam wa Tanzania niaba yao, ningalikubaliana na matakwa hayo ya Maaskofu, kwamba iitishwe kura ya maoni, isipokuwa kwanza, kwa vile uhusiano wa Tanzania na Vatikan haujawahi kupigiwa kura hiyo ya maoni ili kuwauliza Watanzania kama wanautaka au la, tungelianza kuupigia kura hiyo uhusiano huo, ilitupate kuuhalalisha.

Vile vile kutokana na sensitivity ya kuala lenyewe kwa upande mwingine naafikiana kabisa na wazo la Maaskofu wa Kanisa la Pentekoste, kuwa jambo hilo lisijadiliwe katika vyombo vya habari, na pia lisiachiliwe Bunge kuamua peke yake. Nina sababu mbili kuu nazo ni:

1) kwa vile vyombo vingi vya habari Tanzaniai, aidha, vinamilikiwa na kusimamiwa na Wakristo basi kama vyombo hivyo vitalijadili jambo hilo, kuna kila aina ya uwezekano wa kuupendelea Ukristo kuliko Uislamu na kusababisha jambo hilo lionekane halifai. mfano ni IPP MEDIA ambao huhitaji kuwa na PHD ukajua kama siku zote wao wamekuwa biased against waislam

2) kama jambo hilo litapelekwa Bungeni, basi pia, kwa vile Wabunge wengi wa mabunge yote yaliyopita, katika nchi hii, wamekuwa ni Wakristo, bila ya shaka yo yote, watatumia jazba na ukereketwa wao kukwamisha mswada huo, kama walivyojaribu katika vika vya Bunge vilivyokwisha na mfano ni ile issue ya wao kupinga suala la wanafunzi wa kike katika mashule kuvaa sare zinazoendana na maadili ya dini zao!

Najua kuna watu watadai kuwa hii ni sumu lakini ukweli ni kuwa uwanja kama wa JF ndiko mahala pake kujadili hata yale tusiyopenda kuyajadili as long as tunajibizana kwa hoja. Na wakati watu wanakatazwa wasichanganye dini na siasa, kuna ushahidi kuthibitisha kuwa, Wakristo, kwa kupitia katika vitengo vyao vya kanisa, wamekuwa wakiandaa mikakati ya makusudi kuhamasishana wagombee nafasi za ubunge....again this is no brainer kwani kwa kuthibitisha hayo, Padre wa Kikatoliki, Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake alichokiita "KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA -1953 HADI 1985" ambacho ninacho hapa ameeleza kuwa ;
"Mwishowe, SSY ilitoa msisitizo juu ya jukumu la walei katika jamii. Haya yalitokea wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 1970.​
Dkt. Sivalon akaendelea kusema,
"Ingawa hakuna utafiti uliofanywa kuonyesha uhusiano kati ya SSY na wabunge waliochaguliwa, mmoja kati ya watu waliohojiwa alidaikuwa: SSY na Baraza vimeleta msisimko huu ambao umewaamsha Wakatoliki kupigania viti katika uchaguzi wa Wabunge na mimi nikiwa mmoja wao."​


Padre huyo anaendelea kusema,
"Baadaye huko Bungeni tulifanya utafiti usio rasmi na kugundua kwamba asilimia 75 ya waliochaguliwa walikuwa Wakristo, na kati ya hao asilimia 70 walikuwa Wakatoliki"​
( mwenye hiki kitabu atazame Uk.49).

Kwa hali hiyo, kama vyombo vya habari vya Tanzania pamoja na Bunge la nchi hii vitaachiwa vijadili juu ya suala hili, kwamba Tanzania ijiunge na OIC au isijiunge, basi tujue kuwa Wakristo waliomo katika vyombo hivyo, watatumia wingi wao kupinga serikali isiwe na uhusiano na taasisi hiyo! haikatazwi suala kujadiliwa lakini be prepared for one sided bias toka kwao...

Lakini kama suala hilo wataachiwa Watanzania walipigie kura ya maoni, ni wazi kuwa wengi wataliunga mkono kwa sababu katika nchi ambayo Waislamu ni wengi kuliko Wakristo,(according to STATE DEPARTMENT) ingawa baadhi ya waandishi wa Kikristo wamekuwa wakijaribu sana kuipindua sura hiyo ili kuonesha kuwa Wakristo ndio wengi kuliko Waislamu!

vILE VILE TUSISAHAU KUWA Ndugu Mohamed Said, mwandishi wa kitabu, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes", ambacho nacho ninacho hapa akieleza juu ya suala hilo amesema,
"D.B. Barret anatoa takwimu zinazoonesha Waislamu ni wachache Tanzania. Idadi ya Waislamu imefanywa ionekane kuwa ni asilimia 26, Wakristo asilimia 45, dini za kienyeji asilimi 28. Takwimu za Tanzania National Demographic Survey, kwa 1973,zimewaweka Waislamu katika Tanzania juu kidogo ya Wakristo, ni asilimia 40,Wakristo asilimia 38.9 na dini za kienyeji asilimia 21.1. Lakini kwa mujibu (wa Kitabu) "Africa South of the Sahara", Waislamu katika Tanzania wanaongoza kwa wingi, ni asilimia 60. Idadi hii imebaki hivyo hivyo katika matoleo yake yote tokea 1982."​

Kwa kuwa haikufanywa sensa ya makusudi ya kutaka kuelewa idadi ya Waislamu na Wakristo katika Tanzania, basi ni vyema tukafuata ushauri na Maaskofu wa Kanisa la Pentekoste, kuendesha kura ya maoni siyo kwa suala la kujiunga na OIC tu, bali pia na suala la uhusiano na Vatikano, kama hatukuja kushitukia OIC inakubalika na Vatikano inakataliwa, hapo ndipo tutakapoelewa wepi ni wengi Tanzania, ni Waislamu au Wakristo?

Na kwa nini tufikishane mpaka kwenye kuandaa kura ya maoni?

Kwa nini tuvutane?

Jambo liko wazi na kigezo tunacho! Ikiwa muasisi wa Taifa hilo, Hayati Mwalimu Nyerere,(ambaye ana watetezi wakubwa tuu humu JAMII FORUMS) ndiye aliyekuwa wa kwanza kuanzisha uhusiano wa kibalozi baina ya serikali yake na taasisi ya kidini ya kanisa Katoliki duniani, Vatikano, vipi sisi, tunaojifanya tunafuata nyayo za kiongozi huyo, na kudai kuwa tunayaenzi mema yake, tupinge serikali kujiunga na taasisi ya kidini ya OIC?

Au ni kwa sababu mtazamo chongo umetulevya mpaka tukaona uhusiano na taasisi ya Kikristo ni sawa lakini uhusiano na taasisi ya Kiilslamu ni dhambi?

Kwa nini hatufunui macho yote mawili tukaona sawasawa?

Ama swali la kutaka kuwasilimisha Watanzania bila ya ridhaa yao, hilo halipo na hata Kur'ani Tukufu inasema, Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia)katika dini, uongofu umekwisha pambanuka na upotofu (Al-Baqarah). Surely Maaskofu waliobobea kwenye theolofy wanalijua hilo kwa hivyo si sawa kutumia jazba katika kuangalia mambo ya dini.

Aidha, pamoja na watu kuleta info na links za OIC its quite clear kuwa misaada inayotolewa na OIC si ya kidini na wala haina lengo la kuwaingiza watu katika uislamu.

Kama taasisi ya kidini inapotoa misaada huwa lengo lake ni kuwavuta watu waingie katika dini hiyo basi na misaada inayotolewa na Vatikano, kwa kupitia kanisa Katoliki nayo itakuwa inalenga kuwaingiza Watanzania katika Ukristo...mbona waislam hawalalamiki kuhusu CARITAS ?

attachment.php


Kanisa Katoliki limejenga shule, zahanati na hospitali na zinatumiwa na Watanzania wote bila ya kujali tofauti zao za kidini, jee kanisa hilo nalo nia yake ni kuwabatiza wanaopata huduma hizo?


Jamani OIC inatoa misaada ya kijamii tu. Inajenga mashule, mahospitali, barabara, madaraja na mfano wa hayo, kwa ajili ya faida ya jamii nzima na siyokuwa Waislamu tu. Misaada hiyo haitolewi kwa vikudni binafsi, inatolewa kwa nchi nzima, ndiyo maana taasisi hiyo ikataka nchi inayotaka ifaidike na misaada hiyo ijiunge na taasisi hiyo.

Uganda na Mozambique si nchi za Kiislamu, na wala hazina Waislamu wengi; lakini serikali za nchi hizo zimejiunga na OIC na zinafaidika na misaada inayotolewa na taasisi hiyo, bila ya kulazimishwa nchi hizo kufuata imani ya Kiislamu. Chuki za kuuchukia Uislamu zisiwe ndiyo sababu ya kutowatendea uadilifu Waislamu.

na kama picha hiyo hapo chini utaona waislam hawana khiyana na serikali kama ikiacha kuwaingilia mambo yao
attachment.php


Just my 2 cents
 

Attachments

  • askofu.jpg
    askofu.jpg
    59.5 KB · Views: 99
  • Elders.jpg
    Elders.jpg
    60.1 KB · Views: 98
Last edited by a moderator:
GAME-THEORY,

..kuna kitu ambacho sikielewi kuhusu OIC, haswa ukizingatia jina lake. kwanini wanaruhusu nchi non-Islamic countries kuwa wanachama?

..je, ni Jumuiya ambayo imepoteza muelekeo? au ni Jumuiya ambayo out of progmatism wameona malengo yao ya awali hayawezekani ktk dunia ya leo?

..ninashangaa kwasababu jina lao linaelekeza kwenye UDINI, lakini operationally wanaonekana kuwa SECULAR zaidi.
 
GT hiyo post yako inapasha moto jamvi duh! Jamaa alikuwa anajitahidi kuchambua lakini hamna kitu. Eti watu wenye maoni tofauti na yeye anawaita ni wamekosa uadilifu, wanamawazo chongo duh! Eti vyombo vingi vya habari vinamilikiwa na Wakristo halafu katika kuorodhesha anataja IPP media peke yake. Kazi ipo!

Hoja nzito kama hii ya OIC haipaswi kujadiliwa kwa jaziba. Hapo ndo wenzetu mlipotushinda jaziba zenu nyepesi sana, sasa mnataka hoja ishinde kwa jaziba?

Naomba mjibu swali hili la Mwanakijiji "Je kunaubaya gani wa Tanzania kuwa na balozi OIC?"
 
GT hiyo post yako inapasha moto jamvi duh! Jamaa alikuwa anajitahidi kuchambua lakini hamna kitu. Eti watu wenye maoni tofauti na yeye anawaita ni wamekosa uadilifu, wanamawazo chongo duh! Eti vyombo vingi vya habari vinamilikiwa na Wakristo halafu katika kuorodhesha anataja IPP media peke yake. Kazi ipo!

Hoja nzito kama hii ya OIC haipaswi kujadiliwa kwa jaziba. Hapo ndo wenzetu mlipotushinda jaziba zenu nyepesi sana, sasa mnataka hoja ishinde kwa jaziba?

Naomba mjibu swali hili la Mwanakijiji "Je kunaubaya gani wa Tanzania kuwa na balozi OIC?"

Kinachotushtua na kututia wasiwasi ni hili shinikizo la Jumuiya ya Makanisa Tanzania (CCT) kumwonya Rais asimamishe mpango wa Tanzania kujiunga na OIC, kwa sababu nchi hii si ya Waislamu ni suala la kuvunja katiba, lakini kauli hii ya CCT inatuonyesha kuwa tatizo halikuwa ni uvunjaji wa katiba bali ni la udini!

Bwana Yesu hakukosea aliposema kuwa mtu kabla ya kuangalia kibanzi kilichomo katika jicho la mwenziwe kwanza alitoe boriti lililomo katika jicho lake mwenyewe!

Kwa taarifa yako in 1990's wakati Jumuiya ya Makanisa inaikataza serikali isijiunge na OIC kwa sababu hiyo ni taasisi ya Kiislamu, jee, uhalali wa Tanzania kuwa na uhusiano tena wa Kibalozi na Vatikano Makao Makuu ya Kanisa Katoliki?


Waunguja walisibu waliposema "Wafanye wao tu kijambo, tukifanya sisi liwe jambo!"
 
GT
kwanza nikupongeze kwa analysis yako nzuri.

Pili nakuomba utambue kujiunga na OIC bila kupiga kura tutakua tumekiuka kanuni ya OIC inayosema nchi inayotakiwa kujiunga iwe na majority waiislamu .

Hivyo sisi ktk nchi yetu bado hakujapigwa sensa ya kutambua ni DINI ipi ni majority ,hivyo kuendesha Sensa itakua kazi ngumu DAWA ni kupiga kura tutambue MAJORITY TZ ni WAISLAM ama WAKRISTU,ama wapagani.
Nawaunga mkono hao MAASKOFU.
 
Tutajuaje hizo kura za maoni kuwa ni sahihi......kama watu wanaiba kura wakati wa chaguzi......sasa hizo kura za maoni zitakapotoka........itabidi watu wakubali matokeo tu au ndio itakuwa mwanzo wa kilio kingine?
 
Halka,
nadhani Ngekewa kakujibu vizuri sana na imenipunguzia kazi kubwa... Ila kitu kimoja tu ningependa kuongezea hapa.
Hivi kwa nini msijiulize imekuwaje UN, Umoja wa MATAIFA duniani wameweza kuvitambua vyombo vya kidini hali umoja huo hauna dini kama tulivyo Tanzania?....
Hivi kweli kama mngekuwa ktk kamati ya UN kuhusiana na hizi Organisation... nini yangekuwa maamuzi yenu! mngeweza zitambua kweli na kushirikiana nazo au zingetambuliwa nyingine zote isipokuwa OIC..Je, ina maana sisi Watanzania (Wakristu wachache) tuna akili ya kutazama katiba ya OIC na kuitoa makosa kuliko hao waliowekwa huko UN...na ni sababu zipi hasa zilizowafanya wakasajili OIC ama vyombo vya kidini tofauti na jinsi mnavyofikiria swala hili kwa Tanzania!..

Wakuu,
Hili neno nchi haina dini mnalichukua vipi lakini?
NCHI haina dini then nambieni hiyo misikiti na makanisa yamejengwa juu hewani? how do they get hicho kibali cha kujenga sehemu hizi za dini bila serikali kufikiria dini inayohusika....maanake ikitazama maombi yanahusu dini moja inakuwaje watoe kibali hali maombi yanahusu dini ama dhehebu moja!...Acheni uhuni jamani acheni... basi tukijenga kanisa ni lazima liseme ni ka watu wote wa dini zote maanake nchi yetu haina dini.
Wakuu wangu hatushindani hapa ila tunajaribu kujenga hoja za msingi ili tupate kuelewa umuhimu wa OIC pamoja na kwamba serikali yetu imetupa info ndogo sana zinazohusiana na OIC..
Wengi humu wanajiuliza kwa nini OIC imelenga nchi ambazo zina Waislaam tu, ni kweli na sidhani kama Vatican, YMCA ama Redcross wanaweza kuingia nchi ambayo haina Wakristu na kama wataingia basi ujue watapeleka Masister na Mapadre kama viongozi wa kutoa huduma za misaada badala ya volunteer wasokuwa na imani ya dini hiyo..
Kwa chombo hiki cha Waislaam OIC pia hawawezi kwenda kutoa misaada sehemu ambayo dini ya kiislaam haipewi nafasi na ajabu ni kwamba sisi wote humu hujiuliza kwa nini nchi za Kiarabu zinapiga vita kanisa katoliki ama Ukristu wakati huo huo tumeshindwa kujiuliza kwa nini baadhi ya nchi nyingine zinapiga vita Uislaam!...Najua, shetani is always on the otherside....!

Kisha OIC imekubali sisi tujiunge ina maana tumepewa nafasi ambayo ni aghalab kutolewa na chombo hichoi kwa nchi ambazo hazina waislaam wengi kwa sababu OIC sio chombo cha kukopesha kwa interest (riba) kama ilivyo IMF halafu inatoa misaada bila kutoa masharti tofauti na vyombo vingine.
Tatizo la nchi zote wananchama wa OIC ni sawa kabisa na tatizo la nchi maskini zinazochukua mikopo au kupokea misaada..Mara nyingi kama sio zote misaada na mikopo hii huishia mifukoni mwa Watawala wetu...
Kwa nini Tanzania haiendelei pamoja na misaada yote tunayoipata ni kwa sababu tuna viongozi wabaya ndani ya nchi yetu, tusiwalaumu zaidi nchi za Magharibi pamoja na kwamba masharti yao ni magumu lakini ukweli ni kwamba ilitakiwa matunda ya mikopo na misaada hiyo ionekane achana na hilo deni tulojifunga lakini nchi zetu maskini, na hasa viongozi wetu anaiba hata mtaji...sasa kweli tutalaumu vyombo hivi hadi lini wakati sisi wenyewe ndio hamnazo..

Wakuu zangu sisi sote tuna ndugu zetu Bongo na tumejaribu kwa kiasi fulani kusaidia hata kwa kidogo kinachopatikana, lakini kama hicho kidogo unachotuma watu wanakinywa, maendeleo yao hayaonekani itakuwa je tulaumiwe sisi kwa kutoa misaada hiyo.. ati kwa sababu hali za ndugu zetu hazijabadilika!

Kuhusiana na swala la Palestina, nchi zote ikiwa ni pamoja na UN zinafahamu na kuamini kwamba Palestina iko under Occupation..sasa nyie mnapokataa na ku question malengo ya OIC mnakuwa na maana gani kama sio Udini na kufikiria vitu nje ya ukweli. tatizo kubwa ambalo Israel inashindwa kutoa Uhuru kwa Palestina ni sawa kabisa na Kaburu enzi zile za Botha, pia kila mara Israel imetumia sababu ya kwamba hadi siku wapalestina watakapo acha kuwashambulia na pia kukubali mipaka mipya ndipo wanaweza kupewa Uhuru wao...
Jamani, hivi kweli kuna watu kati yenu mnaamini kuwa WaPalestina hawapo under Occupation?..na mna hakika Tanzania haitambui kama Palestina wako under Occupation!...
Halooo!....I know U in there, come out come out! -
Wakuu mmejifungia katika kabati gani jamani mweeee!
 
Bado; hili swali hakuna anayetaka kujibu. Mkandara, GT na wengine naomba kujua 'Je kuna ubaya gani wa Tanzania kuwa na ubalozi OIC?
 
Bado; hili swali hakuna anayetaka kujibu. Mkandara, GT na wengine naomba kujua 'Je kuna ubaya gani wa Tanzania kuwa na ubalozi OIC?

Limeishaulizwa na hakuna anayetaka kujibu. Hauwezi kuwalazimisha. Hakuna anayeelezea kwa vipi kujiunga huku hakupingani na katiba ya nchi YETU. Pamoja na mjadala mrefu wa kuelezea u-inchi wa Vatican bado tunazidi kulinganisha vyombo hivi viwili. Mjadala badala ya kuangalia katiba inasemaje imebaki kuwa kwa sababu wakristu wamependelewa ( kuanzia Vatican, WCC hadi YMCA) basi sasa ni zamu ya waislamu kama vile dini au imani ni hizi mbili tu. Wote tumeshikilia misimamo yetu na hakuna aliye tayari kuangalia upande wa pili! Iliyobaki ni kila mtu ajisomee mtiririko mzima na kufikia uamuzi wake mwenyewe.
 
Nziku,

Nimekwisha lijibu isipokuwa sema hukuridhika na majibu yangu..
Nitarudia kwa ufasaha zaidi....
Mwanakijiji aliuliza kuna ubaya gani tukiwa na Balozi OIC, jambo ambalo nilisema halina mantiki hata kidogo kwa sababu ni lazima kwanza upendekeze hoja hii ya kuwa na balozi ukieleza mazuri ya kuwa na Balozi!... Hakutaja mazuri yake isipokuwa bi njia moja ya kuepuka kujiunga na OIC kuridhisha kundi moja la watu wasiopenda kujiunga (Wakristu) , yet hao hao wako radhi sisi kujinga na kundi la upande wao kwa sabau zao ambazo wanataka tuzikubali kulingana na mtazamo wao.
Pili, Mabalozi wote waliopo OIC ni wasikilizaji tu hawapati mikopo na misaada ipasavyo, misaada ambayo ingeweza sana kutusaidia mara nyingi hupitia UN badala ya sisi kwenda kuomba omba nchi za Magharibi kama anavyofanya Kikwete hata ktk maswala madogo sana kama elimu na Afya. Na Vatican ni ushihidi mmoja mzuri sana wa jinsi vyombo kama hivi vinavyoweza kutusaidia kwa sababu tumeweza kuona mazuri na mabaya yake lakini kwa ujumla mazuri ni mengi zaidi.

Kisha, kuna misaada mingi inakwenda leo Darfur kwa nembo ya UN ama imeandikwa kiarabu watu hamfahamu kwamba OIC huchangia kwa kiasi kikubwa sana, OIC inatoa michango mikubwa kama vyombo vingine vya kijumuiya isipokuwa kinachosikika zaidi ni UN. Lakini kama ukiwa mchunguzi sana utaona nembo yao ktk baadhi ya vitu wanavyopeleka nchi hizo..Na hakuna hata sehemu moja waliyolalamika kuwa misaada kama hiyo hupewa kwanza waislaam kabla ya Wakristu. Najua hofu yenu kubwa kwamba labda misaada ya OIC itakuwa kujenga shule na Hospital kwa waislaam tu.... jamani misaada inapitia serikalini tofauti na nyie ambao mnaweka masharti kwa wananchi moja kwa moja..bado tumebanwa na sidhani kama ni jambo zuri kutengana kidini inapofikia swala la kusaidiwa...Ikija Tanzania ina maana ni msaada kwetu sote Waislaam kwa Wakristu au nanyi mnaona itakuwa haramu kupokea msaada toka chombo cha Waislaam..

Tatu, nilimwambia Mwanakijiji kwamba ingekuwa vizuri kwanza utupe athari za kujiunga na OIC kwa kutumia mifano ambayo tayari OIC imekwisha ifanya katika nchi ambazo zina mchanganyiko wa waumini kama vile Uganda, Mozambique ama nchi zote nilizozitaja huko nyuma. Kisha kwa mapungufu hayo ndipo tunaweza kuona ubaya wa OIC kwa nchi yetu...na sio jinsi anavyojisikia yeye akiwa ktk kabati hilo la Udini..

Mwisho nitarudia kwa kusema kwamba ili Ubalozi OIC uwe na maana kwetu vizuri atupe faida ya kuwa na balozi OIC badala ya kujiunga kwetu na isiwe sababu ya kwamba kuna wakristu nchini ambao hawapendi... Ndio hapo nami nikauliza what if Waislaam nao wataanza kutazama vyombo vya kikristu kwa jicho hilo?..All along wamekuwa wakielewa haki ya Wakristu, waislaam na madhehebu mengine kuwa Uhuru waliopewa ni pamoja na kufanya Ibada zao bila kuingiliwa na serikali. Na ibada za dini hazina mipaka ya nchi, mtu toka Marekani anaweza kuja tanzania kufanya ibada yake, zaka au niseme misaada ya Vatican kwetu ni sehemu ya ibada ya Kikristu.. Na kama mnavyofahamu ktk nguzo tano za kiislaam ZAKA ni moja wapo na hawa OIC wamejikusanya hao masultan..wenye mshiko safi wakaamua kutoa zaka zao kupitia chombo hiki. Tanzania tumejaliwa kuwa ktk fungu la hao watakao pokea hizo ZAKA tena basi tofauti a Wakristu sisi zaka hizi zinapitia mkononi mwa serikali..Wakristu zinapitia Taasisi zao, serikali haioni hata nickle (ndululu)..

Sasa kama alivyopendekeza mwanzoni Rev . Kishoka kuhusiana na Waislaam kuwa na chombo chao kama Wakristu hilo lingekuwa na usawa zaidi lakini serikali ndio imeshatufunga kamba za shingo siku nyingi.. Kelele za Waislaam mnaziona kama kelele za mlalahoi - Kikwete husema kelele hizo hazimzuii kulala.
Waislaam hatuna chombo, hata huyo balozi ikiwepo lengo letu ni kupokea mikopo na misaada - Kwa nini tuwe wasilikizaji?...I mean ni sawa na mtu aniulize kwa nini tujiunge na UN badala yake tusiwe na balozi tu kule, mtu huyu hataki kusema ubaya wa kujiunga na UN isipokuwa kuorodhesha masharti asiyoyapenda yeye ya UN yanayohusu kuitambua nchi huru..
Kama hukubaliani na masharti ya UN then wewe ndiye mwenye problem, kuna tatizo ndani mwako! Kwa hiyo wakuu hapo mjue Utawala ama wananchi wako wanashindwa kuona upande wa pili kwa sababu wao hawaamini hivyo...Wanawake wanasema mwanamme anayekuchagulia marafiki sii mume hakupendi bali Possessive na Possessive isn't LOVE brothers...

Wakuu wangu msiwe ktk kundi la wale wanaopigania haki za wanyama na kupiga marufuku uvaaji wa FUR (majoho ya ngozi za wanyama) hali wao ni walaji wazuri wa nyama za wanyama (Pro steak)...
 
Mpaka sasa hakuna mtu aliyefanya jitihada ya kuchambua katiba ya nchi yetu na kutuhakikishia kuwa kujiunga na jumuiya hii hakupingani kwa namna yoyote na katiba yetu. Hebu tuache kuhusisha OIC na VATICAN ambavyo havihusiani kabisa na tujadiliane kuhusu kuhusu suala la msingi kabisa ambalo ni katiba yetu!
Mimi binafsi sina imani kabisa na viongozi wetu kama wamefanya homework yao vya kutosha kuhusu mambo haya sababu kama tumeweza kuingizwa mkenge kwa RICHMOND then anything can happen....
 
Back
Top Bottom