Rev. Kishoka,
mkuu soma tena maeleoz yangu niliyomwandikia Kichuguuu...Utaelewa zaidi..
Kichuguu,
Shukran mkuu kwa kuuliza swali ambalo nadhani sijaligusia vizuri pamoja na kwamba umeshalipatia jibu...
Unajua mkuu kujiunga na jumuiya ya nchi za kiislaam sio kama mnavyofikiria kuwa hizi ni NCHI za KIISLAAM - Quote n Quote - bali ni nchi zenye UMMAH wa kiislaam kwa kiswahili nadhani ina maana ya UMATI wa kiislaam...Misingi yake haihusiani na utawala wa nchi hiyo upo ktk mfumo gani, haina maana kabisa kwamba nchi hizi ni za kiislaam kiutawala kwani ukweli ni kwamba
1. NCHI za KIISLAAM kwa maana ya kiutawala nadhani hazifiki hata 10..
2.Kuna nchi zilizotambua Uislaam kama ndio dini yake yaani state religion na nyingine
3. Ni secular states, ambazo zote (1,2 na 3) kwa jumla yake sidhani kama zinafika 40 dunia nzima.
Hizi zote zimetokana na Utawala uliopo na pengine ndio culture yao tofauti na sisi Tanzania.
Kama Marekani leo hii unapozungumzia culture ya nchi hiyo Ukristu ni lazima usimamiwe na kiongozi yeyote na hupimwa jinsi gani ameshika values na integrity...
Lakini ukirudi ktk mada hii husika utaona kwamba OIC ina wanachama zaidi ya 50, 57 to be exact kiasi kwamba hapa hapa Africa kuna nchi zaidi ya 10 ambazo hazina sheria wala katiba inayohusiana na Uislaam. kuna nchi wanachama kama Mauritania, Benin, Cameroon, Ivory Coast, Gabon, Uganda, Mozambique, Sierra Leone, Togo ambazo hazipo kabisa kuendesha nchi zao kwa misingi ya kidini iwe kuitwa nchi ya kiislaam, ama islaam kuwa dini ya nchi zao wala hazipo ktk mfumo wa secular states lakini nchi hizi ni wanachama wa OIC. Wakuu hatupo peke yetu ndani ya OIC kama nchi zinazoheshimu haki ya wananchi wake kuchagua na kuabudu dini waitakayo.
Zaidi ya hapo nchi hizi hazikujiunga jana wala juzi kiasi kwamba tusiweze kuwa na mifano hai kuonyesha malengo mabaya ya OIC kuhusiana na tuhuma ama mbegu mbaya mnazojaribu kupandikiza..Sisi Tanzania tuna tofauti gani kubwa na nchi hizo tena basi yawezekana nchi hizo zina waislaam wengi kuliko hata sisi iweje OIC wasianze na huko?..
Maamuzi ya kubadilisha nchi iwe ya kiislaam sio swala dogo wala la kufanyika mzaha kwa sababu ni lazima kushirikishwa wananchi. Ukiondoa nchi za kiarabu utaona kwamba nchi nyingi sana zimefikia hata Uamuzi wa Islaam kuwa state religion umefikiwa baada ya kupigwa kura ama chama kilichoshinda kilitumia sera za kidini na zikakubalika na wananchi wake... Tanzania hatujafikia usingizi mzito kiasi hicho na kifupi haiwezekani!
Labda kwa kusherehesha zaidi kiarabu ktk matumizi ya neno hili Nchi za kiislaam ni pmaoja na usemi unaozingatia sio nchi as nchi mnavyoichukulia bali WATU yaani UMMAH yaani kwa kiswahili tunasema UMATI ambao unaheshimu utawala uliopo madarakani, pia tofauti zetu na watu wengine lakini bado tunakumbushwa kuwa na mshikamano. OIC ni chombo ambacho kinajaribu kuyatazama mahitaji ya watu wake kwa kupitia serikali kuu na binafsi nadhani hii ni muhimu zaidi kuliko kupitia vyombo kama Bakwata ambavyo kwa tamaa ya fedha wanaweza kabisa kukaribisha magaidi au kuingiza siasa ktk misaada hiyo iwe ya fedha ama mali.
Kiusalama (National security) nilishasema kuwa ni bora kabisa swala lolote linalohusiana na misaada ya kidini hasa Waislaam kupitia serikali kuu kutokana na kuepuka viongozi wa dini kuwa wapambe wa mission kama hizi kwani hawa pia ni rahisi kutazama kila kitu wakiwa ndani ya sanduku la udini.. Hivyo OIC pamoja na kwamba imeanzishwa na waarabu hao kina Sultan wa Saudia ambaye mwenyewe na familia yake hawana Uislaam hata kidogo zaidi ya jina kubwa, hawa ni viongozi wa kisiasa (Sultan) na bahati nzuri wana ushirikiano mzuri na nchi za magharibi pia OIC ni chombo pekee cha waislaam UN, hivyo sidhani kama wanaweza kuingia na agenda nje ya yale wanayotaka kuyafanya. Hawa ni Lobbiest tu wanaotumia jina la dini kuonyesha fadhila zao na kwa sababu sisi wahitaji sioni ubaya wake as long as we control the floor!
Kama OIC ingekuwa imehusika kwa kiwango fulani cha matatizo ya nchi wanachama, ama imehusishwa na UDINI basi bila shaka hoja hii ingepata uzito wa kuendeleza discussion hii lakini hoja zote zilizomo humu zinapikwa na kugeuzwa geuzwa ili mradi zionekane zina mvuto bila ushahidi wa matukio.
Mkuu kwa kumalizia tu ni kwamba kwa nini lakini mnakuwa hamna imani na Uislaam kama dini kuna kitu gani kimewahi kutokea kwenu kiasi kwamba mnachofikiria kwanza ni kuwa Tanzania inataka kubadilishwa kuwa Nchi ya kiislaam...
I mean kuna ishara zipi mnazoziona ambazo mimi sizioni..