sorry, I got to respond to this.
Nziku,
Mnapochambua katiba ya OIC unatafuta kitu gani?..
Binafsi ninaangalia ili kuona ni kwanini tunajiunga na jumuiya fulani. Tumeshaingizwa kwenye mikataba mingi ya ajabu ajabu kwa sababu hatukusoma "fine prints". Serikali inaposema "lazima tujiunga na IOC hakuna kugeuka" nasema sawa. Basi tuelewe hiyo jumuiya ina malengo gani, ina mfumo gani n.k Hivyo tunaangalia Katiba. Tusijiunge na kitu ambacho hatukijui. Kuna ubaya gani hapo?
Kukubali jumuiya fulani na kujiunga nayo ina maana unakubali Katiba yake. Leo nikiamua kujiunga CCM ina maana nakubali Katiba ya CCM, malengo yake, na itikadi zake. Kwa vile nchi inayotakiwa kujiunga ni ya Watanzania, kuna ubaya gani kwa Mtanzania kuangalia Katiba hiyo ambacho nchi yake inaingizwa? Unatushauri tusiiangalie?
Je, mlifanya hivyo kutazama katiba ya Vatican, ama taasisi ya kikristu inasema nini?..
Vitu viwili tofauti. Hadi hivi sasa Serikali ya Tanzania haijaamua kujiunga kama nchi kwenye CARITAS (shirika la misaada la Wakatoliki), na wala haijaamua kujiunga na Jesuit Refugee Services (JRS). Siku Kikwete akilazimisha Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Kikristu tutampinga vile vile na tutaangalia hizo Katiba za jumuiya hizo zinasemaje.
Unless una mfano wa Tanzania kutaka kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kikristu.
Kwenye suala la Vatican swali lako liko misplaced. Kwanini hujauliza mbona hatujaulizia Katiba ya Iran nchi ambayo inaoongozwa na kiongozi wa kidini, ambayo ni declared Islamic State? Kwanini umechagua Vatican tu isipokuwa kwa sababu ni nchi ya Kikatoliki na siyo Jumuiya ya Nchi za Wakatoliki? Hili la Vatican itabidi nilifafanua na kuonesha jinsi gani hoja zinazotolewa ni kinyume na mantiki, nyepesi na zenye lengo la kugusa hisia na siyo uhalisia.
Nitarudia kusema kinachotakiwa kutazama ni kwetu sisi tunahitaji nini wala sio katiba ya nchi ama jumuiya kwa sababu kama ingekuwa tunatazama hivyo basi Marekani na China wasingekuwa wanashirikiana kibiashara..
Wrong analogy. Kushirikiana kiuchumi ni tofauti na kujiunga na jumuiya ambayo mojawapo ya malengo yake ni kuwa na Economic Integration na baadaye Islamic Common Market. Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu ambaye atapinga kuhusiana kiuchumi na nchi za Kiislamu kwani tayari mahusiano hayo yapo. Tuna mahusiano ya kiuchumi na Saudia, Oman, Qatar, Iran, Libya, n.k n.k Sina tatizo hilo na wala siitahi kusoma Katiba za nchi hizo kujadili mahusiano yetu.
Tatizo ni kuwa suala la IOC siyo suala la mahusiano ya kiuchumi, ni suala la uanachama. Kwanini Tanzania isiwe na mahusiano ya kiuchumi na IOC au nchi wanachama wa IOC pasipo kulazimishwa kujiunga?
Kabati la Udini ni sawa kabisa na vita baridi iliyokuwepo kati ya nchi za magharibi na mashariki... na inamchukua mtu asiyefungamana na upande wowote kuweza kuona athari za pande zote..Tatizo lenu hasa mkuu wangu Mwanakijiji kama nilivyoandika hapo juu mnatazama athari za upande mmoja tu huo wa shetani lakini huu mwingine ni Saint...
Mzee kuweza kuelewa kabati la udini ni lazima uelewe consistence. Mtu aliye kwenye Kabati la Udini hachagui wapi Kabati hilo linafunguliwa. Ukifungua Kabati la udini, chini kuna udini, katikati kuna udini na juu kuna udini. Kuna Consistence.
Msimamo wangu ni kuwa Tanzania inaweza kuingia makubaliano baina ya nchi na nchi (bilateral agreement) na nchi zote za Kiislamu na kupata misaada ile ile pasipo kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu. Kwanini huo uwe udini? Ninaposema JK aweze kumteua Balozi wa Tanzania kwenye OIC (na Katiba yao inaruhusu hilo) na huyo mtu awakilishe maslahi ya Tanzania (siyo ya Waislamu wa Tanzania tu) kwenye IOC kuna ubaya gani? Mtu mwenye udini angesema hataki mahusiano na nchi za Kiislamu au jumuiya za Kiislamu.
Hivyo ukiangalia utaona kuwa wewe unaangalia suala hili kwa kuangalia dini zaidi kuliko hali halisi. Kwamba kwa vile mtu anatoa maoni tofauti na kujenga hoja iliyo dhahiri basi hatakii mema Uislamu. This is trivialization of reality.
Ndio hayo tunayaona na CCM wao kila siku wanasema Upinzani hauna hoja, watauza Uhuru na kuondoa amani iliyopo.. Kuna watu wanaamini kabisa Upinzani ni adui wa haki na utawala bora. hawapendi hata kusikia jina la Chadema na chochote kinachohusiana na Chadema ni evil..wakati huo huo sisi hapa tunachambua mabaya ya CCM na viongozi wabaya hatuhitaji kuuliza ni mazuri yapi yataletwa na Chadema ama kusoma katiba yao ili kukubali kuwepo kwa chama pinzani..
Mzee mtu atakayetaka kujiunga na CCM au upinzani bila kujua Katiba yao hatustahili. Haitoshi kushabikia tu bali kujua nini watu hao wanasimamia ili ukubaliane nao.
Sehemu mojawapo ya Katiba ya OIC inasema kuwa inataka kuhakikisha kuwa Wapalestina hatimaye wanakuwa na nchi yao na Yerusalemu kuwa makao yake makuu. Huu ni msimamo wa IOC, je huu ni msimamo wa Tanzania? Unataka kusema kuwa tunaweza kujiunga na Jumuiya ambayo hatuikubali malengo yake au Katiba yake na tukawa wanachama kamili?
these are scare tactics na Mwanakijiji kauvaa mkenge.
Scare tactis za vipi? Mimi sina hofu na mwislamu yeyote au jumuiya yoyote ya Waislamu. Nimekaa na kukulia kati ya Waislamu. Ninaujua Uislamu kuliko watu wengi sana. Mimi si miongoni mwa watu wanaolinganisha Uislamu na Ughaidi, au Uislamu na vitu vyovyote hasi. Nimejifunza toka Uislamu mambo mengi na mchango wa Waislamu na Waarabu katika maendeleo ya falsafa Ulimwenguni, sayansi na hisabati ni vitu ambavyo ni mjinga tu hatovijua.
Nilishasema hata huko nyuma sina tatizo kama Tanzania itaongozwa na viongozi wote waislamu! Kwa kadiri ya kwamba wanaoongoza kwa Katiba yetu. Wanaotishia ni wale ambao hawataki kucompromise na kutaka wapate kila wanachotaka kwa sababu ni waislamu na kuwa wasipopata basi "kunaweza kutokea machafuko". Wanaotisha ni wale ambao hawaachi kutumia lugha ya vitisho. Nafahamu wewe si mmoja wao. Lakini wapo ambao Tanzania isipojiunga IOC, wasipopewa Kadhi, wasipofanyiwa hiki au kile basi wanaona ni affront dhidi ya Waislamu.
Kweli mimi na wewe tunatofautiana lakini tofauti zetu zipo ktk Uislaam sio Ukristu!.. kwa sababu nakubali kwa kila wanalolifanya maadam walengwa ni wananchi wenzangu, sina njaa hiyo...
Hatuwezi kukubali kwa vile kinachotakiwa kufanywa ni kizuri basi tushangilie bila kuuliza kinafanywa na nani na kwa misingi gani. Jinsi ninavyokusoma ni kuwa unaona kama vile IOC itawasaidia Waislamu wa Tanzania na hawa wakristu wana "ka wivu" ka aina fulani dhidi ya mafanikio hayo. Unaonekana kama unataka kusema kuwa Wakristu wakubali IOC wasiwazuilie waislamu misaada. Kama hivyo ndivyo basi nadhani you are missing a point.
Sipingi IOC kutoa misaada kwa Waislamu. Ninachopinga ni kutuwekea precondition kuwa ili Waislamu wa Tanzania wapewe misaada basi LAZIMA tujiunge na IOC. This is daylight blackmail. Ina maana tusipojiunga na IOC hakuna misaada itakayotolewa? Kama ni hivyo unaona hilo ni sawa?
Leo hii kuna mashule na mahospitali ya Kikristu nchini, yanatoa misaada ya kila aina na jumuiya nyingine nyingi tu za nje zinatoa misaada. Hakuna mojawapo inayotaka tuwe wanachama kama nchi ili tupewe misaada. Kuna SIDA, IDA, USAID, JICA n.k hakuna inayosema ili tuwasaidie Watanzania basi nchi yenu iwe mwanachama. Kwanini IOC itake hivyo? Misaada hii inayofungamana na uanachama ni misaada ya kupokelewa kweli?
Kisha mkuu wangu hakuna kitu ambacho sisi tunategemea zaidi ya kile ambacho siku zote mmekuwa mkitusisitiza kufanya..Tumekuwa tukilalamika kuhusu mashule ya dini, hospital za dini, huduma za kusaidia maskini za kidini.. Na majibu yenu wala sii muda mrefu mlikuwa mkisema na nyie Waislaam jengeni zenu!...hatuna chombo isipokuwa hiki sasa mnaanza kuwa na sababu hadi mnaingia ktk makabati ya katiba kufukua fitna..
Mkandara, hivi IOC imewahi kutoa msaada gani kwa Waislamu wa Tanzania hadi hivi sasa? Je Waislamu wa Tanzania wamewahi kuomba msaada gani toka IOC? Waislamu wana haki na wajibu wa kupata misaada kutoka sehemu mbalimbali na tayari wanafanya hivyo. Kuna misaada inayoingia kupitia taasisi nyingi tu za Kiislamu na hakuna mtu anayepiga kelele, linapokuja hili la OIC kwanini hadi tuwe wanachama ndio tusaidiwe?
Sasa kama hilo ni muhimu kuna ubaya gani kuangalia Katiba ya hiyo jumuiya ili tujue tunajiunga na kitu gani? Unataka tujiunga kichwa kichwa halafu huko mbeleni tuanze kugongana ilikuwaje tujiunge?
Binafsi niliona mna point nzuri sana mlipotoa hoja ile, kama kweli wakristu wameweza kujipanga wakasaidia ommunity zao inakuwaje nyie waislaam mshindwe hali nyie ni matajiri zaidi ya Wakristu ambao wanategemea zaka na sadaka za watu..
Mzee sijui ni nani amewahi kusema kuwa Waislamu wa Tanzania ni matajiri zaidi kuliko wakristu au vice versa kwani hilo linahitaji takwimu na vigezo vya takwimu hizo. Na sijui kama huo utajiri unatokana na dini ya mtu. Na je ni kweli wakristu wanategemea zaidi zaka na sadaka? Kuna haja ya kuangalia hicho ulichonacho ili niweze kukubali au kupinga so far sina sababu ya kujibu mere speculation.
Nilijiuliza swali hili nikiwa nje ya kabati na ndio maana nilisema mapungufu ya waislaam waziwazi jambo ambalo nina hakika hakuna mkristu wala wewe unaweza kusema mapungufu ya Ukristu. Kwa sababu hu question lolote ndani ya dini yako...
Watu wanaweza kuzungumzia mambo yao au ya wengine. Tukitaka kuangalia mapungufu ya dini za watu n.k tunaweza kufanya hivyo. Hilo hata hivyo halihusiani na OIC. OIC ni taasisi ya kidini, yenye malengo ya kidini, inayoongozwa na Katiba inayotambua dini fulani rasmi. Tanzania kama nchi haiwezi kujiunga huko. Hilo halisemi lolote juu ya mapungufu ya Uislamu au nguvu zake.
Hata hivyo organisation zote hizi pamoja na kwamba zinawasaidia watu wote katiba zao zinatatanisha.. maamuzi ya uongozi na ajira zao yanatatanisha lakini kama utakuwa nje ya sanduku la udini utaweza kuona kwa urahisi kwa katiba zao zimeandaliwa hivyo...
Katiba hazitatanishi; zinajieleza wazi ili kusiwe na utata. Katiba ya OIC iko wazi na ndio maana nchi zaidi ya 50 zimekubali kujiunga nao. Tanzania ikijiunga ina maana inakubaliana na Katiba hiyo, siyo utata uliomo kwenye Katiba hiyo.
Mwanakijiji Mbondei kuoa mke Mbondei sio Ukabila hata kidogo mkuu wangu...
Hili ni kweli, lakini Mbondei akisimama na kusema kuwa wenye kustahili kuolewa na Wabondei ni Wabondei, na ndoa zozote kati ya Mbondei na mtu mwingine hazitambuliki, na ya kuwa hata zile za Wabondei zifungwe kwa Kibondei huo ni ukabila.
Ninachopinga mimi a kuendelea kusisitiza ni ule mtazamo wa coca cola ndani ya chupa ya cola (OIC) na vyombo vingine vya kidini aidha Vatican au YMCA ambavyo ni sawa na cocacola ndani ya glass..
Once again, Vatican siyo chombo fulani cha Kidini, Kanisa Katoliki ni chombo cha kidini. Hili sijui tutalielewesha vipi. Huwezi kulinganisha Vatican na IOC au YMCA. Ukifanya hivyo itabidi useme Iran na Syria ambazo zina balozi nchini ni vyombo vya kidini. Hivi Mkandara hadi hivi sasa hukubali kuwa VATICAN ni nchi kamili na hakimiya?
sasa tunabishana tofauti kati ya vitu hivi hali kinywaji kilichomo ndani ya chupa au glass ni kile kile...kisha tunajaribu ku define tofauti ya glass na chupa hali kinachotakiwa kuutazamwa hapa ni kinywaji chenyewe yaani Cocacola.. yenyewe!
Tatizo ni kuwa wengine hatunywi Coca Cola, lakini wanataka kutulazimisha!
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu usinielewe vibaya sikusema wewe mdini isipokuwa nimesema umo katika kabati la udini...
Katika hili Kabati nadhani wewe nawe una droo yako hapo hapo mkuu. Lakini sidhani kama mimi au wewe tunaangalia suala hili kwa udini kwa sababu kama nikweli basi kile unachodai mimi nimo sidhani kama wewe uko mbali nacho.