Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Nianze kwa kuwashukuru wana JF kwa kuwa pamoja katika jukwaa hili lisilokuwa na upendeleo kwa jamii.
Baada ya kusoma Biblia nilikutana na Sura moja katika Biblia inayosimulia kisa cha wana Israeli kudai mtawala juu yao. naomba tukisome kisa hiki kwa kuwa kuna mambo yana fanana sana na maamuzi ya Watanzania kumpitisha kikwete kwa kura nyingi huku wakidharau ushauri wa Baba wa Taifa. Kifupi ni kwamba baba wa taifa alifahamu uwezo wa ndugu kikwete ndo maana alimuangusha mwaka 1995. Lakini watanzania hilo hatukulijua, tukachukulia suala la umri kama kigezo, ila hicho hakikuwa kigezo halisi.
Habari hii imeanzia awamu ya nne ambayo sikuihusisha hapa kwa maana imelaumiwa kwa rushwa na kupindisha sheria. Kwa manufaa yako unaweza kusoma aya ya 1 - 3 ili kupata ujumbe sahihi.

Tusome:
Samwel 8:4-22

4.Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samwel huko Rama; 5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote. 6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, Waliposema tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba BWANA. 7 BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. 8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumiakia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe. 9 Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.

10 Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya BWANA. 11 Akasema, mfalme atakayewamiliki ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, kwa magari yake, na kuwapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake. 12 Naye atawaweka kwake kuwa maakidajuu ya elfu, na maakida juu ya hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake. 13 Na binti zenu atawatwaa kuwa wafanyaji wa marhamu, na wapishi, na waokaji. 14 Atatwaa makonde yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake. 15 Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape maakida wake, na watumishi wake. 16 Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng’ombe zenu walio wazuri sana, na punda zenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe. 17 Atawatoza fungu la kumi la makundi yenu; nanyi mtakuwa watumwa wake. 18 Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; BWANA asiwajibu siku ile. 19 Walakani hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu; 20 ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atoke mbele yetu na kutupigia vita vyetu. 21 Samweli akayasikia maneno yote ya watu akayanena masikioni mwa BWANA, 22 BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawafanyie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Enendeni kila mtu mjini kwake.

Nawakilisha!!!
 
Utangulizi:

KWANZA, natoa shukrani za wazi kwa Sheikh Ido Mohammed Iddi wa Msikiti wa Mnyamani kwa kuwa mstari wa mbele kuzungumzia haki ya Waislamu kuwa na Mahakama yao ya Kadhi kama ilivyo Zanzibar, Kenya na sehemu nyingine Afrika. Yeye na viongozi wengine wa Kiislamu tunaomba wasikate tamaa maana ushindi ni wa Allah -Subuhana wa taalaa na sio viumbe hapa duniani.

FAIDA ZA MAHAKAMA YA KADHI
Baada ya kusema hayo, leo napenda kuanza kwa kuzungumzia faida za kuwa na Mahakama ya Kadhi na hasara zitakazotokana na kutokuwepo kwa Mahakama ya Kadhi-kama ilivyo kuwa huko nyuma, ilivyo sasa na baya zaidi hali itakavyokuwa huko mbele.

Faida za mahakama ya Kadhi pamoja na mengineyo zaweza kugawanya katika makundi matatu makubwa: Faida katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo wa kudumu na usiobeba dhambi mbele ya Mungu hususan, kuhusu kifamilia na maisha ya kila siku ya Muislamu; faida zitakazotkana na kutatua matatizo ya maingiliano ya kiuchumi na kijamii kwa Waislamu; na faida zitakazopatikana kutokana na kutatua matatizo ya Uongozi, Usimamizi na Uadilifu miongoni mwa viongozi wa misikiti na taasisi mbalimbali za Kiislamu.


Matatizo ndani ya familia na jamii za Kiislamu:

Kundi hili la kwanza la hoja ni kuhusiana na maisha ya kila siku. Hapa tunaonesha madhambi Waislamu wanayolazimishwa kuyabeba kwa sababu ya kukosekana mahakama ya Kadhi:
  1. . Hukumu za ndoa kufanyika kwa mujibu wa sheria za Kiislamu na Kitabu cha Mwenyezi Mungu-Al-Furqhan.
  2. . Talaka hazitatolewa tena nje ya kile kilichoamrishwa na Mwenyezi Mungu na mahakimu ambao wakati mwingine si Waislamu.
  3. . Ujanja unaofanywa na watu kurithi pale wasipostahili kurithi utafichuliwa na watakaomrithi mtu kwa kiasi kikubwa watakuwa ni wale tu wanaostahili haki hiyo.
  4. . Familia zinazotekelezwa zitatunzwa na mifuko maalum itakayopatikana kutokana na zaka na sadaka za Waislamu ambayo baadhi yake itapewa ofisi hiyo ya Kadhi.
  5. . Mayatima watalindwa hasa pale wanapokuwa wadogo lakini wazazi wao wameacha mali mbalimbali ambazo zitakuja wafaa ukubwani.
  6. . Wazee wengi wa Kiislamu, hasa katika mikoa ya Pwani na kwingineko, ambao kwa sasa wanaishi kwa dhiki na ukata mkubwa wataangaliwa kwa namna moja au nyingine na mahakama hiyo na hivyo kuondoa uwezekano wa watu wa dini nyingine kuwaritadisha watu hao uzeeni kutokana na ufukara wao na kukosa taasisi ya kitaifa inayowajali na kuwatunza wazee
Matatizo ya mahusiano ya kiuchumi na kijamii
  1. . Masuala ya elimu na taasisi za elimu za Kiislamu yatapata ofisi moja au mbili za kuyasimamia na hivyo kupunguza udhaifu na uendeshaji mbaya uliopo hivi sasa.
  2. . Aidha taasisi za tiba za Kiislamu zitakuwa chini ya macho makali ya idara za ofisi ya Kadhi ili kuona haki inatendeka kwa kutolewa huduma muhimu kwa gharama zinazokubalika ndani ya wakati tuliomo.
  3. . Masuala ya kibenki na taasisi za fedha yataangaliwa ili yaendane na kutowaingiza Waislamu katika dhambi wasiyoiona au kuijua.
  4. . Kadhalika shughuli za huduma mbalimbali na biashara zitasimamiwa ili zikidhi haja ya wateja Waislamu na wasio Waislamu na vilevile kuhakikisha kuwa biashara zote zinakuwa za halali kwa upande wa Waislamu na zinazofanyika kwa njia ya halali bila kuwapunja, kudhulumu au kuwanyonya wateja.
  5. . Masuala ya uwekezaji na mitaji ambayo sasa yanafuata utaratibu unaoendana zaidi na dini nyingine yatapata usimamizi wa kuhakikisha kuwa sasa yanaendana na maagizo ya Mwenyezi Mungu.
  6. . Juu ya yote maingiliano na wasio waislamu yataratibiwa ipasavyo na kuhakikisha Waislamu wanawatendea haki watu wengine na wao pia wanatendewa haki na watu wengine ikiwemo watawala na viongozi wa dini nyingine.
  7. . Mahakama ya Kadhi itatoa mchango mkubwa katika kutenganisha masuala ya dini na kisiasa na hasa misikitini jambo ambalo sasa limekosa mtu wa kudhibiti.
  8. . Mahakama ya Kadhi itachambua Taassisi za Kiislamu zilizopo ili kuzifuma upya ziondokane na viongozi wabovu na waovu ili Waislamu warejeshe imani kwa viongozi wao pamoja na umoja na mshikamano ndani ya taasisi hizo zinazoyumba kwa sasa kutokana na kuvamiwa na siasa na wanasiasa.
  9. . Kuchochea imani, uzuzi na ubunifu miongoni mwa Waislamu ili waweze kuwaamini viongozi wao kwani kila kitu sasa kitakuwa wazi chini ya Ofisi ya Kadhi na hivyo kuwezesha Waislamu kutunisha mifuko yao mbalimbali na kuacha kabisa kwa taasisi za Kiislamu kutegemea serikali au wanasiasa na ruzuku katika kuendesha mambo yao.

Matatizo ya taasisi, uongozi, na viongozi wa Kiislamu
  1. . Ofisi yaKadhi pia itakuwa mstari wa mbele katika kulinda mali za Waislamu. Tofauti na ilivyo sasa ambapo baadhi ya Waislamu na wasio waislamu wanaweza wakauza au kununua mali za Wakfu za Waislamu na kulindwa na sheria isiyo ya Kiislamu kutokana na udhaifu wa kutokuwa na Mahakama ya Kadhi ambayo ingelikuwa ina hakiki mali zote za Waislamu na kuwekea mikataba lakiri isiyoweza kubadilishwa ila kwa amri ya Mahakama hiyo tu.
  2. . Baadhi ya taasisi, wilaya, mikoa hadi ngazi ya Taifa zina viongozi wabovu ambao wanalindwa na wanasiasa na mahakama zilizopo. Endapo mahakama ya Kadhi itakuwapo basi itawashughulikia viongozi wabovu na waovu kwa namna inayochunga mambo ya Waislamu yasikwame.
  3. . Inasemekana kwamba mali bila daftari hupotea bila habari. Misikiti na taasisi nyingi za Kiislamu karibu katika ngazi zote zina matumizi mabaya sana ya fedha na hakuna wa kuwawajibisha kutokana na kutokuwepo na Mahakama ya Kdhi ambayo ingelikomisheni wataalamu wa mambo ya fedha wa Kiislamu kubuni na kuanzisha mfumo wa uhasibu kwa ajili ya misikiti na taasisi hizo utakaopaswa kufuatwa na wote na vilevile kuwa na wakakguzi wa shughuli za dini na za kibiashara kwa Waislamu ili kuona hakuna wajanja wanofanya vitu vyao ndani ya taasisi hizo wakati wote. Kiujumla Ofisi ya Kadhi itawezesha Waislamu kuweka taratibu za uhasibuna utunzaji madaftari na utunzaji kumbukumbu za fedha au mali, mapato na matumizi miongoni mwa misikiti na taasisi nyingine za Kiislamu.
  4. . Ofisi hiyo ya Kadhi itakuwa pia na majukumu ya kuwasimamia wakaguzi maalum wa Kiislamu kukagua mali za waislamu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu na kuwachukulia hatua wanaokiuka taratibu na miiko iliyowekwa tofauti na ilivyo hivi sasa.
  5. . Ofisi ya Kadhi itakuwa na mchango mkubwa pia katika kusaidia kusimamia makadirio na utozaji wa zaka tofauti na ilivyo sasa ambapo kutokana na kutokuwa na Ofisi ya Kadhi Waislamu ndio walio wengi katika lindi la umasikini kwa sababu umekosekana mfumo unaokubalika wa kukusanya zaka na kuwaondoa Waislamu waliomo katika umasikini kutoka kwenye lindi la ufukara unaowatia katika ukafiri kirahisi mno,
Hasara za Waislamu kunyimwa haki yao ya msingi ya kuwa na Kadhi:
  1. . Kesi za ndoa kuhukumiwa ndivyo isivyo (yaani nje ya Kitabu cha Allah).
  2. . Masuala ya talaka kuamuliwa kinyume cha sheria za Kiislamu.
  3. . Wenye kustahili mirathi kunyimwa au kupunja na wasiostahili mirathi kupewa urithi usio halali.
  4. . Familia, yaani, mke na watoto wanaotekelezwa kucheleweshewa haki yao kutokana na mlolongo wa mashtaka kama haya mahakama za kawaida. Ugumu mkubwa katika kutambua kama waliotekelezwa kweli ni nasaba kwa mme au ni watu wa kupachikiwa.
  5. . Mayatima wa Kiislamu kulelewa na wasio Waislamu na hivyo kuwa katika hatari ya kupoteza au kupotoshewa imani yao.
  6. . Wazee wengi wa Kiislamu kuendelea kuteseka uzeeni kutokana na kukosekana kwa huduma nzuri na ya uhakika kwa watu kama wao katika jamii.

Aidha, haya pia yataendelea kuwasibu Waislamu tofauti na wenzao wa dini nyingine ambao dini zao zina mifumo ndani kwa ndani inayoshughulikia masuala kama haya lakini wao Waislamu hawana:

  1. . Elimu na taasisi nyingine za Kiislamu kuendelewa kuendeshwa ovyo ovyo kwa sababu hakuna mlezi wa taasisi hizo ambaye hawezi kuwa mwingine ila Muislamu muadilifu na mcha-Mungu ambaye ni kadhi na bingwa wa sheria na hukumu za Kiislamu kuhusu masuala husika.
  2. . Huduma za tiba kwa Waislamu zimekuwa zikibadilika lakini nazo zinakabiliwa na matatizo ya menejimenti, kiutawala, kiuendeshaji, kifedha na kimaendeleo kwa kukosa msimamizi mkuu kama Kadhi na Ofisi yake.
  3. . Katika miaka hii ambapo Waislamu wamefunguka macho kuhusu dhambi ya RIBA ni muhimu Waislamu kuwa na Kadhi ambaye kwa mashirikiano na Maulama wa ndani na nje wanaweza kupitishwa fatwa mbalimbali kuhusu masuala ya kibenki na kifedha. Kukosekana kwa mahakama ya Kadhi kunachangia kwa kiasi kikubwa Waislamu wengi kula kuchwao kuingia kwenye dhambi ya KULA AU KULISHA wengine RIBA.
  4. . Kutokana na kutoijua DINI yao vyema maelfu ya Waislamu sasa hivi wamejiingiza katika uwekezaji na mitaji haramu. Haya yote yamesababishwa na kukosekana kwa Mahakama ya Kadhi ambayo ingelibainisha kinaugaubaga ni uwekezaji na mitaji ipi ni halali na ipi ni haramu kwa Waislamu.
  5. . Kwa ujumla Mahakama ya Kadhi ambayo inapingwa na Wakatoliki ni chombo cha kuhakikisha kuwa mahusiano kati ya waumini wa dini hizi mbili yanafanywa bora zaidi na hapaachiwi mianya ya vikundi vidogo vidogo ndani ya dini zetu inayoweza kutumika kuvunja umoja na amani wa nchi hii.

Tofauti na baadhi ya watu wanavyoamini Mahakama ya Kadhi haitaingilia :
  • . kesi zinazowahusu wasio Waislamu.
  • . haitahukumu nje ya Sheria za Kiislamu ambazo zinakubalika katika jamii ya kisekula ya leo.
  • . Haitokata watu mikono wala kupiga watu mawe.
  • . Haitashughulika na masuala ya watu wa dini zingine haya yataachiwa mahakama za kisekula.
  • . Badala ya kuorojesha amani na mshikamano kati ya Watanzania itasaidia sana kuhakikisha kuwepo kwa umoja na amani ya kudumu inayojengwa juu ya misingi ya haki na usawa.
  • . Haitotumia fedha za seikali isipokuwa kwa kiwango kile kile ya mizigo ya kesi itakayopunguziwa mahakama za kisekula.

Hitimisho:
Ni hitimishe kwa kusema kwamba, Kuwepo kwa mahakama ya Kadhi hautokuwa ushindi wa upande mmoja, kwamba hawa wameshindwa na wale wameshinda. La, hasha! Ushindi huu ni ushindi kwa wote, Kwa Waislamu, kwa Watu wa dini nyingine, kwa wasiojua wanachokipinga na kwa Watanzania wote kwa ujumla. Kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi ni kuwepo kwa figa la tatu kwa Jamhuri ya Muungano ambayo hadi wa leo imekuwa ikisimamia juu ya mafiga mawili- figa na Kanisa Katoliki na ubalozi wa Vatican nchini na lile la Serikali ya Kisekula peke yake na kulisahau figa la tatu-Mahakama ya Kiislamu.

Yeyote atakayeikataa Mahakama ya Kadhi haitakii mema Tanzania na hawatakii mema Watanzania. Mungu Mkubwa na hana mpinzani! Mungu Ibariki Tanzania, na pia Wabariki watu wote wanaokuabudu wewe tu!
 
Last edited by a moderator:
please peleka kwenye Dini au habari mchanganyiko........silencer nimekuona fanya kazi yako Mkuu
 
please peleka kwenye Dini au habari mchanganyiko........silencer nimekuona fanya kazi yako Mkuu

Huyu sheikh aliposema kwamba ni figa la tatu kwa sababu ya mimi mswahili napenda pilau nikajua kwamba labda anazungumzia upishi wa pilau,hii hapa siyo mahala pake,na pia hili swala lisitumike kutuondoa kwenye mjadala wa hotuba ya muunguzaji na mzugaji wetu!
 
We dont need this now, isitoshe hii ishajadiliwa sana tu. fanya upekuzi kabla hujapost shekhe
 
wandugu leo Ijumaa tuvumilie haya natumaini ma MoD watakapoona inafaa waihamisha au kuiunganisha na ile main thread ya Mahakama ya Kadhi. Lakini kwa leo na kwa vile ni TGIF.. basi tumvumilie tu ndio mwanzo wenyewe huu.
 
Utangulizi:

Yeyote atakayeikataa Mahakama ya Kadhi haitakii mema Tanzania na hawatakii mema Watanzania. Mungu Mkubwa na hana mpinzani! Mungu Ibariki Tanzania, na pia Wabariki watu wote wanaokuabudu wewe tu!

Hapo hamjapewa hiyo mahakama yenuya Kadhi mnaanza kututisha, mkipewa itakuwaje. kwani nyinyi hiyo mahakama yenu lazima muanzishiwe na serikali?
 
Hivi kwa nini watu wengine ni wagumu kuelewa.Nchi inaongozwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Na Jamhuri yA Muungano wa TANZANIA haina dini.

Hakuna aliyesema mahakama ya kadhi ni mbaya bali ni kinyume na katiba yetu na tume ya kurekebisha sheria wamepewa jukumu la kutafuta maoni iwepo au isiwepo.

Na hiki ni chombo tu cha kiislamu na nchi hii ni mchanganyiko wa dini mbalimbali za wakristo,wapagani,wahindu,n.k.hawa nao wakitaka misingi yao ya imani iwekwe kwenye katiba patakalika?
 
please peleka kwenye Dini au habari mchanganyiko........silencer nimekuona fanya kazi yako Mkuu
Pole mkuu Ogah,

Wavumilieni wanaopindisha hoja kwa maslahi yao lakini no worries, nipo sana hapa! Nitajitahidi kuweka kila kitu sawa within a week.

wandugu leo Ijumaa tuvumilie haya natumaini ma MoD watakapoona inafaa waihamisha au kuiunganisha na ile main thread ya Mahakama ya Kadhi. Lakini kwa leo na kwa vile ni TGIF.. basi tumvumilie tu ndio mwanzo wenyewe huu.
Mwanakijiji,

Shukrani kwa input yako! Hii hoja sioni sababu ya kuihamisha kwakuwa ni political issue. Nimeshaiweka sawa, nimeiweka tangia tulikotokea, tuliko na natarajia itatumiwa vema tunakoelekea.

Hapo hamjapewa hiyo mahakama yenuya Kadhi mnaanza kututisha, mkipewa itakuwaje. kwani nyinyi hiyo mahakama yenu lazima muanzishiwe na serikali?
Mkuu kigarama,

Ndilo tatizo la mijadala, hatuwezi kufanana mawazo. Mtu mmoja hawezi kuwakilisha waislam au wakristo wote.

Hivi kwa nini watu wengine ni wagumu kuelewa.Nchi inaongozwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Na Jamhuri yA Muungano wa TANZANIA haina dini.

Hakuna aliyesema mahakama ya kadhi ni mbaya bali ni kinyume na katiba yetu na tume ya kurekebisha sheria wamepewa jukumu la kutafuta maoni iwepo au isiwepo.

Na hiki ni chombo tu cha kiislamu na nchi hii ni mchanganyiko wa dini mbalimbali za wakristo,wapagani,wahindu,n.k.hawa nao wakitaka misingi yao ya imani iwekwe kwenye katiba patakalika?
Labda nisisitize kitu hapa:

Suala la mahakama ya Kadhi ni suala ambalo ningependa hapa tulijadili kwa mapana bila kuingiza tofauti zetu za imani, tuliangalie kwa maslahi ya taifa na pindi mtu unapochangia katika hoja hii utambue kuwa mawazo yako yana umuhimu mkubwa na kuna watu wanaoyafuatilia kwa ukaribu ambao wanalifuatilia suala hili na wanajaribu kuangalia maoni yetu kama wananchi.

OLE wao watakaoonekana kuupindisha mjadala huu, hoja zao zitafutwa tu! Nimeombwa sana hoja zote za Kadhi niziunganishe ili wafuatiliaji waweze kuzifuatilia kwa ukaribu na kuyafanyia kazi maoni ya watanzania.

Ahsanteni kwa mliowahi kuchangia katika hoja hii na naomba kwa wale wageni katika hoja hii wajaribu kuisoma tangia tulikotokea ili wapate kuja na maoni mbadala na yenye manufaa kwa taifa letu!

Invisible
 
Hakuna madhara kujiunga na OIC - Serikali

2008-08-23 10:14:10
Na Beatrice Bandawe, Dodoma

Serikali imesema hakuna madhara yoyote kwa Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (IOC).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, aliyasema hayo jana bungeni wakati akifunga mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake jana.

Akiwasilisha hotuba hiyo juzi, wizara hiyo iliomba iidhinishiwe Sh. 69,405,738,700 ambapo kati ya hizo Sh. 52,355,164,900 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, Sh. 10,500,000,000 kwa ajili ya maendeleo na zilizobaki kwa ajili ya mishahara pamoja na maduhuli ya serikali.

Waziri Membe, alisema serikali mwaka huu, imefanya kikao na Baraza la Wawakilishi kuhusu suala hilo na kugundua kuwa nchi 21 zimejiunga na Umoja huo.

Alisema kati ya nchi hizo, zimo pia nchi za Wakristo ambazo zimejiunga na hazijapata madhara yoyote.

``Tumeshakusanya takwimu za nje na kuona hakuna madhara yoyote ya kujiunga na IOC, bora tu kufuata taratibu,`` alisisitiza.

Alisema suala hilo lilileta utata awali kwa sababu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, Bw. Ahmed Hassan Diria, alipeleka ombi la Zanzibar kujiunga kwenye Umoja huo bila kuishirikisha Serikali ya Tanzania.

Hata hivyo, alisema suala hilo limefanyiwa kazi na serikali na kuona kuwa hakuna madhara kujiunga na IOC.

Akichangia mjadala wa wizara hiyo juzi jioni, Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Bw. Manju Msambya, alisema Tanzania kujiunga na IOC kuna faida nyingi kuliko watu wanavyodhani.

``Kujiunga na IOC kutatupunguzia adha ya kupata bei kubwa ya mafuta,`` alisisiza na kutoa mfano wa nchi za Kiafrika za Guinea, Gabon, Cote de Viore na Msumbiji kuwa zimejiunga na Umoja huo na kupata manufaa makubwa ya kiuchumi.

Bw. Membe, pia aliwatoa hofu Wabunge juu ya uraia wa nchi mbili kwa Watanzania wanaoishi ng\'ambo kuwa hauna madhara yoyote.

Alisema ni budi Wabunge wakubali hoja hiyo kwa kuwa hakuna suala la kuhatarisha maisha na kwamba itawasadia Watanzania hao kushiriki kuendeleza nchi yao, wawapo nje.

``Wabunge tubadilike, hakuna suala la kuhatarisha maisha na naomba litakapoletwa hapa bungeni suala hilo, tulipitishe,`` alisema.

Kuhusu malalamiko yanayotolewa na Watanzania wanapokwenda kuomba Viza katika balozi za nje nchini, Bw. Membe, alisema serikali imepokea malalamiko mengi na serikali imeshaziandikia barua nchi hizo.

Alizitaja nchi zinazolalamikiwa kwa kuwa wasumbufu wakati wa kutoa Viza kuwa ni Canada, Uingereza na Marekani.

Hata hivyo, alisema kwa taarifa zisizo rasmi, Marekani ipo kwenye mchakato wa kuwapatia Watanzania wanaoomba Viza za kwenda nchi hizo za muda wa miaka sita.

Alisema taarifa hizo alidokezwa na Balozi wa Marekani nchini.

Akichangia mjadala huo, Mbunge wa Chalinze (CCM), Bw. Ramadhani Maneno, alisema wananchi wanapata usumbufu wanapokwenda kuomba viza kwenye balozi za nje.

Bw. Maneno, alitaka kujua pia nani anastahili kukaa kwenye chumba maalum (VIP) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Hoja hiyo pia iliungwa mkono na Mbunge wa Kasulu Mashariki (CCM), Bw. Daniel Nsanzugwanko, aliyesema kuwa VIP ni vurugu tupu Dar es Salaam na baadhi ya watu wamegeuza sehemu ya kuvutia sigara.

Bw. Membe akijibu suala la viza, alisema baadhi ya Watanzania wanatumia vibaya njia ya kupata viza kwa kutoa takwimu na taarifa zisizo sahihi.

Akizungumzia malalamiko ya baadhi ya Wabunge juu ya matumizi mabaya ya vyumba vya VIP, Bw. Membe, alisema matatizo mengine yanatokana na viongozi wenyewe kwa kutaka kutumia vyumba hivyo kwa ukoo wake mzima.

Hata hivyo, alisema vyumba hivyo vitumike kwa watu maalumu na kuwataka viongozi kutumia vizuri fursa hiyo.

Kuhusu Chuo cha Diplomasia cha Dar es Salaam, ambacho kina ubia na nchi ya Msumbiji, Bw. Membe, alisema serikali iko kwenye mchakato wa kutafuta hati ya chuo hicho ili iweze kukimiliki yenyewe, baada ya Msumbiji kuanzisha chuo chake kama hicho.

Akizungumzia safari za Rais Jakaya Kikwete, nje ya nchi, Bw. Membe alisema ``Rais wetu anaalikwa sana duniani kwa sababu ya vipaji vyake na uwezo wake wa kutatua migogoro.``

Aidha, alisema Uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) aliupata bila kupingwa na kuongeza kuwa mzigo alionao hivi sasa unatokana na kujiamini kwake na mafanikio yake.

Alisema mbele ya safari mafanikio ya safari hizo yataonekana.
 
Fundi Mchundo,

Mkuu hata siku moja siwezi kuku under estimate kwani kufanya hivyo nisingeendelea na mjadala bali ningekuwa nakuzungumzia wewe kwa mapungufu yako...

Unachozidi kukosea ni pale unapotunga sababu kwa kufikiria tu kwamba labda hivi ndivyo ilivyokuwa...Lakini mimi bila kutazama rangi za watu nazungumzia reality na ndivyo ilivyokuwa..

Kwanza umesema ati East African Muslim Welfare Society (EAMWS) kilikuwa hakipendwi na waislaam kwa sababu kilikuwa chama cha wahindi badala ya Waswahili... mkuu hili umetoa wapi?... lini maswala ya dini yakaingiliana na rangi za watu.. hivi kweli unataka kunambia kuna kanisa hata moja ama shirika la dini ambalo limewahi kukataliwa kwa sababu ni la wazungu?.. hao hao wazungu, Waarabu na wahindi ndio waliotuletea dini ama ustaarabu wa imani hizi leo iweje mswahili asiyekuwa na dini wala elimu ya dini hiyo akatae mwongozo unaotaka kuieneza dini hiyo...

Mkuu soma vizuri malengo ya EAMWS kisha utazame upande wa pili ambao wapo wazungu na hizo Community-based institutions - NGOs au makanisa ambayo walipinga hata Uhuru wetu wamekuwa bado wakifanya kazi zao hawakupigwa marufuku.. na zinazidi kuingia nchini pamoja na kwamba malengo yao sio sawa kabisa na yale ya wakati wa mkoloni.. naweza kusema makanisa ya wakristu wa enzi zile walisaidia kwa moyo mmoja nchi zetu ktk elimu kuliko vyombo vya siku hizi hizi NGOs za kufungashiwa ambazo vimejiingiza zaidi ktk uchumaji, yet havikupigwa marufuku....Kisha basi mbona huyo AghaKhan yupo Kenya toka enzi hizo na sehemu yenye waislaam wachache sana na hakuna upinzani kama tuliouona Tanzania.

Mkuu sidhani kama huko ndiko unakotaka kwenda na kama nilivyosema haya maswala ya kupoint vidole watu wengine hayawezi kutusaidia kujenga isipokuwa kubomoa. haiwezekani kitu kimoja kiwe kibaya kwa muislaam lakini kizuri kwa mristu ama pagani..

Pili, umezungumzia ati East African Muslim Welfare Society kilikuwa banned kwa sababu ya Mwenyekiti wake - Abdallah Fundikira. Mkuu hapa sijui ni kipi maanake kuwa mwenyekiti haina maana wewe ndiye unayetoa maamuzi ya ndani... na ajabu umemtumia kwanza AghaKhan mara imekuwa Findikira ndio sababu hadi umehoji uwezo wake wa kukirudisha baada ya Mwinyi kama vile Fundikira ndiye mwenye kuhodhi chombo hicho ama Mwinyi ndiye mwenye sheria na katiba ya kupigwa marufuku.. au kwa sabuabu Fundikira na mwinyi wote ni waislaam!..ktk siasa zetu Devil siku zote huwa ni upande wa pili haiwezekani kuwa within!.. kina Bush hao na hizo axis of Evil..Basi kwa taarifa yako Aghakhan kisha rudi akitumia development network yake AKDN..ambayo ndiyo ilikuwa ikitoa misaada na ajabu ni kwamba hakuwahi kuondoka Kenya na wala EAMWS haikufungiwa wakati wao nadhani ndio walitakiwa kupinga kuliko hata sisi ukitaka kutazma rangi za dini.

Tatu, Upinzani wa kutaifishwa mali haukutokana na chama cha kiislaam hata kidogo unless unataka kusema hata kina Kambona pia walikuwa waislaam halafu basi tazam report inavyojigonganisha yenyewe.. Ikiwa waislaam ndio walikuwa na upinzani mkubwa wa utaifishaji badala ya wahindi na waarabu iweje tena hao hao waislaam wafurahie kutaifishwa kwa shule za wakristu?.. Mkuu mara nyingi habari kama hizi soma between the lines...

Si kweli hata kidogo kuwa AghaKhan ndiye mwanzilishi wa EAMWS isipokuwa yeye ndiye alikuwa sponsor mkubwa wa chombo hicho.. Kama vile leo NGO ya Ukimwi nchini inavyosaidiwa na Busha haina maana Bush ndiye mwanzilishi na yule mwenyekiti wake mathlan mkewe Kikwete atakuwa ni mmiliki hivyo kama Chadema wakiweza kushinda ni lazima wakipige marufuku...

Mkuu jaribu kulitazama swala hili kwa fikra huru badala ya kujengewa hoja na hawa watu ambao kila siku wanasema waislaam (sio waarabu) ni wajinga kuamini kuwa wanapo kwenda kupigana vita wakifikiria kuwa Ukifa utakwenda mbinguni! yet hao hao wazungu na wakristu ama dini nyinginezo walipokuwa wakipigania Uhuru wao iwe Marekani, France, Uingereza wote hawa walitumia maneno hayo hayo..Kwanza walikamata makanisa wakachukua imani za watu na kuwatumia kupigana vita yao.. hakuna Mfalme hata mmoja hakuwa na uhusiano wa juu na kanisa ktk kila maamuzi na neno la Mungu lilikuwa ndio hamasisho la ushindi wote wa vita wa chi zote za Ulaya...Leo mwarabu ati kwa sababu tu anasema Kiarabu kwa maandishi ya kiarabu kuwa Mungu ni mkubwa - Allah Akbar basi bila shaka wanatumia Uislaam kueneza chuki..sijui mwarabu mkristu atasemaje tofauti na mwarabu muislaam anapofikia mahala pa kusema Mungu ni mkubwa..

Hizi ndizo propaganda nazozipiga vita. propaganda ambazo zinatugawa sisi kwa rangi zetu badala ya kutazama kitu kilichopo mbele yetu. na kama umeisoma vizuri hiyo makala uliyoiweka hapo nyuma utaona yapo madhara makubwa ya korti ya kadhi kama nilivyoisema huko nyuma kuwa cha muhimu ni kuzingatia WATU na MAZINGIRA waliyopo..period

Kuna kipande hiki hapa nimekipenda sana na ndivyo nilivyosema toka awali kwa sababu mkuu mimi huwa sisahau yaliyopita. Nina kumbukumbu nzuri ya historia ya nchi yetu hasa ktk maswala ya kijamiii.. Hii ndio sehemu ya sisi kuitazama zaidi kwa sabau hata wakristu wanaitazama hivyo hivyo inasema hivi:-

Before 1971 Moslems, as well as Christians and Hindus, followed their own marriage and divorce laws. Traditional judiciary systems of the different ethnic groups practising customary law were also in force. In addition, one could marry monogamously in a civil marriage. To counteract religious and ethnic exclusivism in favour of increased national consciousness, the government presented its aim in its 1969 White Book to create more uniformity in the sphere of family laws. The other important aim was to improve the position of the woman. One of the tangible proposals was that the minimum marital age for boys was to be eighteen and for girls fifteen. The fifteen-year limit for girls was presented with reference to UN recommendations. According to sharia puberty decides when a girl is marriageable.

The proposal that caused the most serious debate was the idea that a man who wanted to marry a second wife had to get permission from his first wife. The proposal that would forbid men to punish their wives corporally was also met with some resistance as well as the installation of an obligatory reconciliation agency for couples on the verge of divorce. If the agency failed to reconcile the parties concerned the husband in a Moslem marriage would legally be able to pronounce the divorce formula talaka...

In questions concerning for example polygyny, Moslem critics like.......have gained some support from the Christian quarter. Christian criticism is, to some degree however, part of a wider propaganda campaign against Islam. It may be noted that many Christian men, especially outside the circles of leadership, actually have defended polygyny, albeit with reference to traditional African culture rather than to Christian belief. This was especially obvious during the parliamentary debates preceding the law changes in 1971.

Kwa hiyo hapa bado kuna mapungufu ktk haki za wanawake hasa ktk maswala ya ndoa!.. iwe kwa wakristu ama waislaam sote tunaikwepa sheria za kidini na hakuna kati yetu anayetaka isipokuwa ni lazima solution iwepo kuwapa haki wanawake na watoto wanao olewa ktk mfumo kama huu..
 
Mkandara,Fundi-Mchundo,mkamap,....

..ninavyoelewa kukitokea matatizo ya mirathi/ndoa na shauri likaenda mahakamani wahusika huulizwa kama wanataka shauri lao liamuliwe kwa taratibu za Kimila,Kiserikali,Kiislamu,au Kikristo.

..Mahakama pia ina uwezo wa kutafuta ushauri wa wasomi wa Kiislamu/Kikristo kusaidia kutatua shauri lililoko mbele yao.

..Binafsi napenda kuelimishwa hii Mahakama ya Kadhi italeta tofauti gani katika kuamua masuala ya ndoa,talaka,na mirathi, kwa ndugu zetu Waislamu tofauti na ilivyo sasa hivi.

..Pamoja na kutokuwepo Mahakama ya Kadhi, serikali inatambua ndoa za Kiislamu. Serikali vilevile ktk kuamua mirathi na talaka zinazowahusu Waislamu huzingatia sheria za dini hiyo ikiwa wenye shauri watapendekeza.

..vilevile ningependa kuelimishwa kuhusu mipaka ya mamlaka na madaraka ya Kadhi Mkuu, na zaidi utaratibu utakaotumika kupatikana/kumteua Kadhi Mkuu.

..Zanzibar walipitisha sheria ya Kadhi Mkuu kuteuliwa na Raisi kwa mapendekezo ya Waziri wao wa sheria na katiba. Baadaye kukazuka mgogoro kwamba Waziri wa Katiba alikuwa ni Mkristo, Brig.Gen.Adam Mwakanjuki.

..wasiwasi wangu ni kwamba suala hili likitumbukizwa kwenye KATIBA basi tunatoa nafasi kwa Non-Muslims[wasiohusika nalo] kuweza kuliingilia.

..wako wabunge ambao sio Waislamu, pia Raisi wetu,Mwanasheria Mkuu,Waziri wa Mambo ya ndani, wanaweza kuwa sio Waislamu kwa nyakati tofauti. Kadhi Mkuu akiwa ndani ya katiba basi kuna uwezekano akawa anadhibitiwa kwa namna moja au nyingine na hao[possible Non-Muslims] niliowataja hapo juu. Hali hiyo nadhani inaweza kutuletea migogoro ya kujitakia.
 
Jokakuu,

Tatizo sio mahakama ya kadhi hilo kwanza..
Sisi hapa JF tusitazame kwa ufinyu hiki chombo ila tutazame issue inayopiganiwa kwa kuwatazama Watu na Mazingira waliopo, kisha tujenge mapendekezo yetu kwa kuanisha sababu za kukubali ama kutokubali mahakama ya kadhi..Mahakama ya kadhi haiwezi kutoa suluhu hata kidogo isipokuwa ni kuonyesha nia ya kushughulikia tatizo lililopo..

Kwanza umesema mahakama zetu huwa zinauliza mahusika wanataka sheria gani! Hili ni kosa la kwanza kabisa kwani serikali haiwezi ama haitakiwi kuamua kesi kwa kuuliza mshitaka au mshitakiwa kwa sababu ni ktk mazingira haya hawa watu wawili huwa hawakubaliani na ndio maana wamekwenda ktk sheria. Mahakama haitakiwa kabisa kutokuwa na sheria moja kwa wananchi wake wote..

Pili, kama nilivyosem hapo awali waislaam dini yao inaruhusu wake zaidi ya mmoja ambayo kwa msahafu wa Wakristu ni polygyny.. Hata hivyo kutokana na mazingira tunayoishi Waislaam hawafuati sheria za ndoa hizi kidini zaidi wanatumia mila na desturi za kiafrika wakichanganya na dini kidogo..Wakristu pia pamoja na kwamba wake wengi ni haramu lakini mazingira yetu yanatuonyesha kwamba wao pia wanaoa nje ya sheria ya ndoa za dini.. Hivyo hivyo madhehebu mengine yote utakuta wananchi wa Tanzania wanafuata zaidi mila na desturi hivyo unapopitisha sheria ni muhimu sana ufuate sheria moja ambayo inaweza kutumika kote... kisha basi ndoa za siku hizi ni mchanganyiko waislaam kwa Wakristu na Mapagani, ibada zote za dini hizi imekuwa HIARI ya muumini kufuata ama kutofuata lakini ktk dola ni lazima kuwepo na utaratibu wa kuhakikisha sisi sote hatuendi overboard kwa kutumia mila hizi mbaya zinazodhalilisha wanawake na watoto.

Hivi sasa wanawake wengi wanaolewa ovyo kwa kuahidiwa uongo mtupu, Watoto wengi wanazaliwa nje ya ndoa za kidini na hawana haki ktk sheria za dini zote iwe waislaam ama wakristu.. Hivyo kwa sababu hili ni tatizo sugu inabidi lazima serikali itafute sheria moja kwa ajili ya tatizo hilo.

Navyoelewa mimi waislaam kwa kutaka Mahakama ya Kadhi ni kutokana na kutokuwepo sheria inayowalinda wanawake..kesi nyingi sana zimekuwa zikiamriwa kiholela tena against wanawake na watoto... Kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo ndio maana waislaam wame raise hii issue kama vile tulivyoomba uzinduzi wa chombo na sheria inayowahukumu MAFISADI, muswada wa utunzi wa sheria hiyo lazima umeanzishwa na watu ambao wamekereka na mfumo uliopo sasa hivi na hakuna sheria moja dhidi ya Ufisadi...sasa ni ufinyu wa kifikra kama tukianza kuwatazama wale walioleta hoja ya Ufisadi kama wanatoka chama gani... kama ni Dr. Slaa basi issue nzima haina maana kwa sababu ni issue ya Dr.Slaa na Chadema ni matakwa ya Chadema kwa Chadema..tukitoa visingizio kuwa hapa Tanzania sio kila mtu ni Mwana Chadema na fisadi hivyo sheria hiyo haituhusu.

Nachosema mimi ni kwamba hata kwa hawa ndugu zetu wakristu, hutuwezi kuendelea na sheria ya dini inayokataza kuoa mke wa pili hali wafuasi wake wengi wanaoa wake zaidi ya mmoja na watoto wamezaliwa ambao hawatambuliki kulingana na sheria za dini.. Hawa watu hatuwezi kuwaaacha ati kwa sababu wamekiuka maadili ya dini laa hasha ni kitu kinachotokea na kwa kasi ya ajabu sana. naweza kusema Tanzania ya leo hakuna mtu asiyekuwa na mistress, mke zaidi ya mmoja na watoto wengi wamezaliwa nje ya ndoa ama ktk ndoa ya kiislaam ama kiasili.. hawa watu wanatakiwa haki pindi inapofikia ktk maswala ya kuvunjika kwa ndoa ama mirathi.. wanawake wengi na watoto hawa wamekuwa hawana haki mbele ya sheria ya dini ama katiba, hakuna sheria moja inayoweza kuamua kwa maslahi ya hawa waathirika... na inaonyesha kwamba we don't care!

Kwa hiyo ni lazima tutafute njia bora ya ku deal na swala hili.....kuomba mahakama ya kadhi iwe kama ni hamasisho la kuitazama upya sheria zetu na kwa nini waislaam wamejenga hoja hii..hapo itakuwa rahisi kwetu kufahamu tatizo liko wapi na litafutiwe solution.
 
Mkandara,

..hatuwezi kuwa na sheria moja katika masuala ya ndoa ambayo kwa kiasi kikubwa yanahusisha imani za dini.

..nilichojaribu kuelekeza ni kwamba kama wenye shauri watajitambulisha kama Waislamu, au Wakristo, basi serikali huwapa "option" ya kuamua kama wanaona haki itatendeka ikiwa shauri lao litaamuliwa kwa kuzingatia misingi ya dini za Kiislamu, au Kikristo.

..pia kuna utaratibu unao-accomodate wale ambao wanapendelea kesi zao ziamuliwe kwa kuzingatia mila na desturi za makabila yao. mwisho kuna ambao wanapendelea masuala yao yaamuliwe kwa taratibu na sheria secular za serikali.

..mimi siyo Mwanasheria lakini huo ndiyo uelewa wangu kuhusu masuala haya.

..ume-raise suala muhimu sana la haki za watoto wanaozaliwa nje ya "ndoa." kwa taratibu za kimila watoto hao wana haki za mirathi. sijui haki za watoto hao ktk ndoa za Kikristo na Kiislamu.


..kwasababu wewe mwenzetu unaelekea kuwa na uelewa kuhusu suala la Kadhi, hebu tuelimishe sheria hiyo itawasaidia vipi watoto waliozaliwa nje ya "ndoa."
 
Jokakuu,
hatuwezi kuwa na sheria moja katika masuala ya ndoa ambayo kwa kiasi kikubwa yanahusisha imani za dini.
Mkuu unajua kwamba sheria zote za nchi zetu zinatokana na dini? jaribu kutofautisha kati ya Uhuru wa dini ku practice maswala ya dini zao na pale sheria inapoingia kwa sababu hakuna sehemu ambayo dini haiku cover..

Maswala ya ndoa kama nilivyosema sio ya dini ni kanyaboya tu kuuhadaa ulimwengu. Kaa kweli maswala ya ndoa ni ya kidini inakuwaje kuna wakristu wameoa wake zaidi ya mmoja..... na wanakwenda funga kanisani, nyingine msikitini, nyingine ofisi ya halmashauri...hapa kuna dini gani..watu wanaoana kwa madhehebu tofauti, dini tofauti iweje hili swala liitwe la kidini hali hakuna sheria ya dini hata moja inayofuata... Hii ibada gani?

waislaam wanaoa bila idhini ya mke wa kwanza tena bila sababu kubwa za msingi ambazo zilikubalika kidini..watu wanaangusha bash Diamond kama vile hakuna jana wakati Akhdi imefungwa msikitini.. na wanakolea vile vile...tena basi hawakuanza jana mapenzi wala ulabu.

Mkuu nitarudia kwamba nchi yetu haina dini kwa maana kwamba haifuati wala kupendekeza mtazamo fulani wa dini sii kwa sababu ya ndoa tu ndio uhuru huo unapatikana. Kila nchi duniani siku hizi inaweka madai ya kutokuwa na dini na moja ya kusimamia uhuru huo ni kwa serikali kutochukua hatua zinaoegemea upande fulani wakati huo huo waumini wa dini zote wana uhuru kamili wa kufanya ibada zao ambazo haziingiliani na maswala ya jamii nyingine. akapo changanya uhru huo basi bila shaka mnauondoa uhuru mliopewa... kama vile Kikwete akivyozungumzia kuhusiana na uhuru wa habari.

Tatizo la ndoa nchini ni kwamba hii sio ibada tena isipokuwa imekuwa ni ktk kudefine ndoa kama ni kitendo cha mwanamke na mwanamme kuoana..Hakuna definition inayosema muislaam asioe nje ya Uislaam na akifanya hivyo sheria ya dini itumike...wakristu pia wanaoa nje na pengine kuzaa kabla hata ya ndoa na hakuna sheria inayopingana na utiifu wa ibada hiyo... Mkuu bado nipo pale pale WATU na MAZINGIRA ndio kinachotakiwa kutazamwa kwani sisi dini ni hiari na imani ambayo unaweza kubadilika kesho...
 


There is no harm in Tanzania joining the Organisation of Islamic Countries (OIC), the government said yesterday.

Foreign Affairs and International Cooperation minister Bernard Membe made the announcement here when winding up debate on his ministry`s 2007/09 budget estimates.

According to the minister, a meeting between the government and members of the House of Representatives held this year to discuss the issue had resolved that there was nothing wrong for Tanzania to join the OIC.

He said they had come to learn that 21 countries in the world, including Christian countries, had joined the organisation.

``We have already collected enough information about the mater. We are convinced that there is nothing wrong with Tanzania joining the OIC,`` Membe said.

He said the issue was wrongly handled by former minister for foreign affairs Hassan Diria, who applied for Zanzibar membership in the organisation without involving the Union government.

In the early 1990s, Zanzibar attempted to join the OIC, but was refused permission by the Union government on grounds that, being part of the union, it had no mandate to join international organisations.

However, yesterday Membe said the government had thoroughly worked on the issue and come to the conclusion that there was nothing wrong for Tanzania to join the organisation.

Earlier on, debating on the budget estimates of the ministry of Foreign Affairs and International Cooperation yesterday evening, the MP for Kigoma South, Manju Msambya said Tanzania would benefit a lot by joining the OIC.

``Joining the OIC would help the country get rid of high prices of oil,`` he said, adding that Guinea, Gabon, Ivory Coast and Mozambique had joined the organisation.

The House endorsed the ministry`s budget yesterday. Membe had asked the House to endorse 69,405,738,700/- for recurrent and development expenditure.

SOURCE: Guardian

Comment on this article


 
Last edited by a moderator:
Kama ni kujiunga kama convention sio problem ila kama kuna policy ya kushika uislam hapo si poa!!! Italeta matatizo mobu
 
Ok hakuna ubaya waliouona,na inawezekana kweli hakuna ubaya na tutapata faida hizo zinazosemekana.Lakini Je imawezekanaje ukawa member wa jumuiya ya kiislam na wewe usiwe muislam?kwa maana nyingine Tanzania itakuwa inchi ya kiislam itakapo ingia ktk uanachama wa inchi za kiislam naitatakiwa kufanya zile sifa ambayo mwanachama anatakiwa kuwa nazo.
Lakini pia sijui uanachama huu unataka nini?Hatuna budi wanainchi kuwekewa huo mkataba ili tuchue itakuwaje.

Naomba ufafanuzi akinifu.
 
Bob,

najitahidi kukusoma....ya kwamba

1. kuna tatizo.........na suluhisho lake halina budi kujumuishwa kwenye sheria mama

Kama hiyo hapo juu ni sahihi.........nafikiri approach ya kutumia mahakama ya Kadhi is not appropriate.......kwa sababu naona inawakwaza sana wengine walio na imani tofauti

Suggestion
kama tatizo lajulikana basi....mtu/mbunge/mwakilishi aje na hoja akianisha mapungufu ya sheria mama i.e. its not covering some aspects ambazo zina-affect jamii.......NOTE "zina-affect jamii nzima"..............na kwasababu hiyo amendment zifanyike to suit.

......nafikiri mahakama ya Kadhi within Islams ikitakiwa kuanzishwa sioni wa kuizuia..........

.......in addition, najaribu pia kutafuta kumbukumbu ni wapi na wakti gani hizi mahakama za kadhi bara zilisimamishwa ku-exist
 
Vitu vingine nafikiri vinahitaji ....elimu zaidi kwa umma na hatimaye......referrundum
 
Back
Top Bottom