Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

We must have principles. Uganda and Mozambique may have joined the OIC but two wrongs do not make a right. Moreover, it is manifestly false logic to say that we should join the OIC because “there is nothing wrong for us to do so”.

There is something fishy in being a member of an Organization of Islamic Countries when you are not an Islamic Country. The fishiness of it does no become diminished “because Uganda and Mozambique have joined”. What are the explicit and implicit objectives of the OIC?

The Chinese say that a journey of a thousand miles starts with one step. What is the end objective of those who are pushing us to join the OIC? It is my thesis that if we give in and agree to join the OIC, then this weakness will be exploited by demanding that we have Islamic Courts in our constitution. The same false argument that “there is nothing wrong in having those courts, even some neighboring countries have them” will be used.

We are neither an Islamic Country nor a Christian Country. We are a secular nation. Tanzanians have religion, but the state of Tanzania has no religion. If Tanzania becomes a member of an Organization of Islamic Countries then this principle will have been violated. We must resist this.

I have no doubt that Membe has been ordered by JK to insert us into the OIC. I doubt that our elected leaders (MPs) have the will or ability to resist this bad move. It is a very bad move indeed. It is an abandonment of the principle of separation between state and religion.

Augustine Moshi
 
MagobeT,
Mkuu soma vizuri maelezo wa watu kabla hujahukumu...
Kama hukuelewa nilichoandika itakuwa vigumu sana mimi kukufahamisha na naweza kutumia hoja za kipuuzi kama zako...
Mathlan ni wapi kumeandikwa Papa ni rais wa Vatican?...Lini papa kasimama UN kama rais wa Vatican?, mbona sijasikia demokrasia ikipiganiwa Vatican huyo rais hukaa miaka mingapi na kuna vyama vingapi vya Upinzani..
Kama Zanzibar sio NCHI kwa tafsiri mnayoitoa nionyeshe ishara hizo huko Vatican..

Mkuu naweza kuzua maswali mengi kuhusiana na Vatican na tukaendelea kubishana hadi kesho kwa jambo la kijinga kabisa, hali sisi wote tunafahamu kwamba Vatican sio NCHI tu bali pia ni TAASISI ya kidini. Kama taasisi, Vatican pia ina lengo la kuendeleza Ukatoliki kwa maslahi ya Wakatoliki wakati nchi yetu haina dini...ndilo swali la kina Mwiba hawakusisitiza tuvunje husiano kama mnavyotaka kuepusha hoja za msingi... badala ya nyie kufikiria ktk kipimo hicho mnazua sababu za kuibeba vatican hali hamkubali sababu zozote zinazohusiana na OIC..

How do U expect Muslim watakubali sababu zenu ambazo kwa fikra zao hakuna tofauti na OIC kama taasisi..

Ndugu Mkandara, kweli kwa hayo niliyochangia ndiyo yanayosababisha hata useme hoja zangu ni za kipuuzi? Kutoelewa kunasababishwa na kimojawapo au zaidi ya havi:
1. Inawezekana sikukuelewa wakati wewe unaeleweka.
2. Inawezekana sikukuelewa kwa sababu hueleweki.
3. Inawezekana nimekuelewa na huoni kama nimekuelewa.
4. Inawezekana hukueleweka na sikukuelewa pia.

Katika kujadili kitu mtu anaweza asielewe (wakati yeye anaona ameelewa na hii ni 'experience' ya kawaida kabisa na siyo 'strange') na ukigundua hivyo inabidi wewe unayeelewesha umweleweshe bila kutumia maneno kama hayo uliyotumia.

Watu wote wangekuwa na mawazo kama wewe basi hakuna ambaye angemfundisha mwenzake na hata kuelimishana au kueleweshana kwenye hii 'platform' kusingewezekana.

Kwani ni amri kuwa Mkandara akisema kitu lazima kieleweke na kisipoeleweka basi asiyekielewa ni mpuuzi? Nadhani wewe ni miongoni mwa wale ambao hamtaki kuulizwa swali ila mnataka kuuliza maswali na kujifanya ni hoja zenu tu ni za maana.
 
naomba kuuliza tena vikao huko oic ataenda nani kwa Tanzania?
mfano summit meeting,
mawaziri wa afya
mawaziri wa kilimo,
je wanapokea wawakilishi wakristu?
 
Hivi tunaingizaje suala la uhusiano wa Tanzania na Vatican kama kisingizio cha Tanzania kujiunga na OIC????
kwani OIC wanafungua ubalozi hapa kama vatican au?
 
Mkandara,Magobe T,Rev.Kishoka,...

..mimi nafikiri tujiunge tu na OIC. tumebishana kuhusu suala hili for more than 15 years na bado tuko palepale tulipoanzia.

..tujiunge tu ili wananchi tupate wasaa wa kutafakari na kujadili masuala mengine ambayo pia yana umuhimu kwa taifa letu.

..watu wanadai OIC, lakini wanasahau kwamba financiers wakubwa ni nchi zinazojitambulisha kama Islamic Republics ambazo tayari tuna mahusiano nazo mazuri tu na ya muda mrefu.

..tayari tuna uhusiano na Saudi Arabia, Iran, Kuwait, Egypt, Malaysia, Indonesia, Pakistan, na nchi nyingine zinazojitambulisha kama Islamic Republic.

..kama ni misaada basi hizo Islamic Republic zingeshatusaidia na kumaliza matatizo ya Waislamu na Watanzania kwa ujumla.

..tumeshasaidiwa sana tu na kwa muda mrefu. kuna kipindi tulikuwa tunaongoza Afrika nzima kwa kupewa misaada na mikopo toka kila kona ya dunia.

..tumepata misaada toka kila mahali, scandinavia,eu,uk,usa,china,india,korea, iran,kuwait fund, saudi fund,you mention. ukweli ni kwamba bado tumekwama.

..OIC itakuja, hapana shaka watasaidia hapa na pale kama hao waliowatangulia, lakini nina hakika hawawezi kutukomboa toka kuwa nchi masikini kwenda kujitegemea.

..binafsi sijaona nchi iliyoendelea kwa kusaidiwa. inafika wakati tunapaswa kukusanya nguvu zetu wenyewe ili tuinuke kimaisha na kiuchumi.

..mjadala huu na hatua ya kujiunga na OIC ni moja ya hatua za sisi kujitambua kama Taifa.



Mimi
kwa mtazamo wangu,wewe ndio umechora mstari kwenye hili swala.
Pongezi zangu mkuu.
 
Haya maamuzi we all look like headless chicken!Tz si haina dini according to katiba?
mungu ibariki Tz
 
We must have principles. Uganda and Mozambique may have joined the OIC but two wrongs do not make a right. Moreover, it is manifestly false logic to say that we should join the OIC because "there is nothing wrong for us to do so".

There is something fishy in being a member of an Organization of Islamic Countries when you are not an Islamic Country. The fishiness of it does no become diminished "because Uganda and Mozambique have joined". What are the explicit and implicit objectives of the OIC?

The Chinese say that a journey of a thousand miles starts with one step. What is the end objective of those who are pushing us to join the OIC? It is my thesis that if we give in and agree to join the OIC, then this weakness will be exploited by demanding that we have Islamic Courts in our constitution. The same false argument that "there is nothing wrong in having those courts, even some neighboring countries have them" will be used.

We are neither an Islamic Country nor a Christian Country. We are a secular nation. Tanzanians have religion, but the state of Tanzania has no religion. If Tanzania becomes a member of an Organization of Islamic Countries then this principle will have been violated. We must resist this.

I have no doubt that Membe has been ordered by JK to insert us into the OIC. I doubt that our elected leaders (MPs) have the will or ability to resist this bad move. It is a very bad move indeed. It is an abandonment of the principle of separation between state and religion.

Augustine Moshi

....Mwl Moshi,
"Hivi hujui kwamba tutafaidika kwa misaada, mikopo isiyo na riba na kwamba bei za mafuta zitakuwa stable hapa nchini?" if you know what i mean!!

........Mwl asante kwa mchango wako..........ila usipotee sana Mwalimu....tunahitaji hekima zako hapa JF non-stop!
 
Hapa nchi sasa inataka kubinafsishwa, tulimuona Diria kama mbaya sasa tunaendelea hukohuko. Jamani muungwana anataka kutupeleka wapi???, Kila kilichokataliwa enzi za Mkapa sasa tunaambiwa hakina madhara.

Kazi ipo
 
Kila kilichokataliwa enzi za Mkapa sasa tunaambiwa hakina madhara.

Mkereketwa,usishangae sana,JK hana tofauti na Bush wa sasa,aliingia madarakani kutimiza aloshindwa baba ake.Jk hapa anakamilisha yaliyomshinda Mzee wa Ruksa.Usijeshangaa Tz ikabatizwa "The United Islamic Republic of Tanzania".U just wait...watasema.."no harm"..just a name.
 
Ushauri wa bure...
Wakristu wajitenge waanzishe nchi yao...Tanzania imeshakuwa nchi ya kiislaam pamoja na kwamba kuna Taasisi kama YMCA, Taasisi za umoja wa wanawake wa kikristu duniani, Vatican na kadhalika ambazo zote zinafahamika na kupewa baraka na UN...
Ikiwa serikali imesisitiza kujiunga na OIC kitu ambacho hakikubaliwi na wakristu wengi ni bora tujitenge uwe mwanzo wa nchi kutambuliwa kutokana na imani ya dini kabla nchi nzima haijabatizwa kuwa Nchi ya kiislaam..

Nasubiri makombora!... kwi kwi kwi! -ama kweli sisi Wadanganyika! -
Elimu pekee haiwezi kumkomboa mwananchi!
 
Ushauri wa bure...
Wakristu wajitenge waanzishe nchi yao...Tanzania imeshakuwa nchi ya kiislaam pamoja na kwamba kuna Taasisi kama YMCA, Taasisi za umoja wa wanawake wa kikristu duniani, Vatican na kadhalika ambazo zote zinafahamika na kupewa baraka na UN...
Ikiwa serikali imesisitiza kujiunga na OIC kitu ambacho hakikubaliwi na wakristu wengi ni bora tujitenge uwe mwanzo wa nchi kutambuliwa kutokana na imani ya dini kabla nchi nzima haijabatizwa kuwa Nchi ya kiislaam..

Nasubiri makombora!... kwi kwi kwi! -ama kweli sisi Wadanganyika! -
Elimu pekee haiwezi kumkomboa mwananchi!

Sikuelewi una maana gani? kujitenga duu

Na hata tukijitenga waislamu nchi yao na wakristu nchi yao wewe unadhani ni upande upi ambao utakua rahisi kulia makombora?? teh teh teh teh kiding.
 
Na hata tukijitenga waislamu nchi yao na wakristu nchi yao wewe unadhani ni upande upi ambao utakua rahisi kulia makombora?? teh teh teh teh kiding.
...
Without kidding.... Ukweli ni kwamba Upande wa waislaam utalia makombora kwanza maanake hamkawii kuvamia nchi...teh! teh! teh!...

Mkamap,
Tuache utani mkuu wangu nakuomba wewe na wengine wote mnaopinga OIC mnipe jibu la hoja yangu ifuatayo... hakuna kuzunguka mbuyu nambieni mnavyojisia bila kuvaa ngozi ya kondoo..

Nakuombeni mnambie vitu VITATU vinavyowafanya muupende UISLAAM kama dini..na kama vitatu ni vingi nambieni japo KIMOJA....

Najua hamtaweza kujibu isipokuwa kuanzisha hoja nyingine, nina hakika kiasi hicho!
 
...
Without kidding.... Ukweli ni kwamba Upande wa waislaam utalia makombora kwanza maanake hamkawii kuvamia nchi...teh! teh! teh!...

Mkamap,
Tuache utani mkuu wangu nakuomba wewe na wengine wote mnaopinga OIC mnipe jibu la hoja yangu ifuatayo... hakuna kuzunguka mbuyu nambieni mnavyojisia bila kuvaa ngozi ya kondoo..

Nakuombeni mnambie vitu VITATU vinavyowafanya muupende UISLAAM kama dini..na kama vitatu ni vingi nambieni japo KIMOJA....

Najua hamtaweza kujibu isipokuwa kuanzisha hoja nyingine, nina hakika kiasi hicho!


Mimi naupenda uislamu pia ukristu kwa kua na kitu kimoja common nacho ni
Ni uijio wa kikoloni ktk ardhi yetu pia uijio wa ukoloni ktk fikra zetu.
 
Mimi
kwa mtazamo wangu,wewe ndio umechora mchari kwenye hili swala.
Pongezi zangu mkuu.

...mdini wewe tunakujua huna lolote,kwanini usiende kujiunga na sheikh ponda mtengeneze jamhuri yenu ya kiislam mwembechai? good news watu kama wewe na divisive politics zenu za udini hamna support zaidi ya malunatics wenzenu wanaoteka misikiti kariakoo.
 
...
Without kidding.... Ukweli ni kwamba Upande wa waislaam utalia makombora kwanza maanake hamkawii kuvamia nchi...teh! teh! teh!...

Mkamap,
Tuache utani mkuu wangu nakuomba wewe na wengine wote mnaopinga OIC mnipe jibu la hoja yangu ifuatayo... hakuna kuzunguka mbuyu nambieni mnavyojisia bila kuvaa ngozi ya kondoo..

Nakuombeni mnambie vitu VITATU vinavyowafanya muupende UISLAAM kama dini..na kama vitatu ni vingi nambieni japo KIMOJA....

Najua hamtaweza kujibu isipokuwa kuanzisha hoja nyingine, nina hakika kiasi hicho!

Mimi mmisheni hivi kweli unanitarajia nipende uislamu? Nawapenda waislamu kama vile ninavyowapenda wahindu, wabuddha,wayahudi na wasio na dini. Lakini mapenzi yangu ni kwa dini yangu, ukristu. Nitaupendaje wakati simtambui Mtume Mohamed S.A.W kama mwokozi wangu? Nitakapoupenda uislamu, nitaslimu. Lakini hii haina maana kuwa nauchukia uislamu. Ninauheshimu lakini sina mapenzi nao. Kama vile nisivyotarajia muislamu kuwa na mapenzi na ukristu maana hawezi kuupenda ukristu bila kumtambua Kristo kama Mwana wa Mungu. Hii nayo haina maana kuwa anachukia ukristu au wakristu!
 
WANAOSHAWISHI NCHI YETU IJIUNGE NA OIC WAJIBU KIKAMILIFU HOJA ZILIZOWEKWA BAYANA KATIKA MAKALA HII HAPA CHINI. HOJA HUJIBIWA KWA HOJA, HEKO MKUU MWANAKIJIJI

KATI ya mambo ambayo sikutaka kuyagusa kwa kina ni suala la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC). Inaonekana serikali ya Rais Jakaya Kikwete imedhamiria kuwa liwalo na liwe Tanzania itakuwa mwanachama wa jumuiya hiyo.

Wamechukua uamuzi huu wa woga baada ya kushindwa kuchukua msimamo wa kijasiri kuwa Tanzania kama nchi huru isiyo na dini haiwezi na haipaswi kujiunga na jumuiya hiyo, kwa kuwa jumuiya hiyo ina malengo na misimamo inayokinzana na maslahi ya taifa letu.

Sababu kubwa ambayo watawala wameitoa inayoonekana ndiyo pekee inayowafanya kuiingiza nchi yetu kwenye OIC ni kutaka kusaidiwa. Yaani tumekuwa wategemezi kiasi kwamba kutokana na kupenda kusaidiwa tuko tayari kuuza hadhi yetu kama nchi na uhuru wetu ili tupate misaada.

Inaonekana serikali yetu mbele ya wanaotoa misaada inanywea na kufyata mkia na kukubali kuburuzwa alimradi tupewa misaada. Huu ni msimamo wa watu waoga.

Baadhi ya watu wanapinga Tanzania kujiunga na taasisi hiyo kwa sababu wanafanya hivyo wakiangalia Tanzania na kusema Katiba yetu hairuhusu hivyo.

Hiyo hoja kwa kweli inaweza isiwe na nguvu sana. Binafsi napinga Tanzania kujiunga na taasisi hiyo kama nchi, kwa sababu taasisi hiyo ni nini, ikoje na ni ya nani.

Hoja yangu ni kuwa Tanzania haipaswi kujiunga na OIC kwa sababu malengo na dira ya jumuiya hiyo ni kinyume kabisa cha kila kitu kinachoifanya Tanzania kuwa Tanzania.

Hata hivyo, hilo haliondoi uwezekano wa jumuiya yoyote ya Kiislamu nchini kuwa mwanachama au mshiriki wa aina fulani ndani ya OIC au kuizuia serikali kufanya kama walivyofanya Marekani yaani kuwa na mwakilishi mtazamaji (observer).

Uamuzi wa kujiunga na OIC ambao umechukuliwa na Rais Kikwete ni uamuzi ambao lazima upingwe na kila Mtanzania mwenye kutaka umoja, usawa na haki kwa kila raia.

Je, kutojiunga na OIC ina maana Tanzania isipewe misaada na nchi wanachama wa OIC? Jibu la swali hili linaonesha ni jinsi gani Tanzania imepoteza ujiko wake wa kidiplomasia.

Ina maana ya kwamba Wizara yetu ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa chini ya Bernard Membe, imeshindwa kuingia majadiliano na hatimaye makubaliano ya nchi na nchi (bilateral agreements) kati ya Tanzania na nchi moja moja wanachama wa OIC.

Mtindo huu upo duniani na unatumiwa na nchi nyingi, Kama Canada imekuwa ikifanya majadiliano ya kulinda wawekezaji wake kwa kuzungumza na nchi moja moja badala ya kundi zima. Na zaidi si lazima kwa nchi hizo kujiunga katika ushirika fulani ili zipatiwe misaada na Canada.

Inashangaza kuona kuwa OIC - aidha kwa kututega au kwa kutumia nguvu zake za kiuchumi - zimetubania na kutuwekea ngumu kuwa pasipo Tanzania kuwa mwanachama wa OIC basi hakuna misaada kutoka jumuiya hiyo.

Kama hili ni kweli, basi yawezekena walioiteka nyara Tanzania si mafisadi tu bali pia kikundi cha nchi fulani ambacho hakipo tayari kuisaidia Tanzania na watu wake wote isipokuwa kwanza tupige magoti na kujiunga nacho! Hili linatisha.

Lakini kabla ya kuwalaumu OIC hebu tuangalie wao wenyewe wanasema nini kuhusu jumuiya hiyo.

OIC imekataa kutambua Azimio la Umoja wa Mataifa Juu ya Haki za Binadamu. Nchi wanachama wa OIC kutokana na kuunganishwa kwao na imani ya dini ya Kiislamu ililikataa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu (ambalo Tanzania imekubali) na kupitisha Azimio lao la Cairo, Misri, kuhusu haki za binadamu.

Kukataa kwao lile la Umoja wa Mataifa kumetokana na kutambua kuwa baadhi ya mambo yaliyomo kwenye Azimio la Umoja wa Mataifa yanapingana na mafundisho ya dini ya Kiislamu.

Ibara ya 24 ya Azimio la Cairo inatangaza wazi kuwa "Haki zote na uhuru unaotangazwa kwenye Azimio hili vyote viko chini ya Sharia za Kiislamu" na ibara ya 25 inasema "Chanzo pekee cha kuelezea na kufafanua vipengele vya Azimio hili itakuwa ni Sharia ya Kiislamu".

Hii ni haki ya jumuiya ya OIC kuchukua msimamo unaoendana na lengo na makusudio yake. Je, Tanzania ikiwa mwanachama kamili wa jumuiya hii inalitambua Azimio la Cairo kuhusu haki za binadamu?

Lakini zaidi tuangalie makusudio na malengo ya OIC ili tuone kama yanaendana na makusudio ya nchi yetu na kama yanalinda maslahi ya Watanzania wote (si kikundi kimoja cha Watanzania).

Ibara ya kwanza ya Katiba ya OIC ina vipengele vinavyoelezea majukumu yake na malengo yake. Inataja malengo yapatayo 20, ambayo ni ya kutufanya tufikiri ni kadhaa.

La kwanza ni lengo namba nane linalosema mojawapo ya malengo ya OIC ni "kuwaunga mkono na kuwawezesha wananchi wa Palestina kuweza kutumia haki yao ya kujiamulia mambo yao wenyewe na hatimaye kuunda taifa lao hakimiya (sovereign), likiwa na Al-Quds Al Sharif (Yerusalemu) kama makao yake makuu na kulinda alama za Kihistoria na Kiislamu pamoja na maeneo matakatifu yaliyomo".

Tunapojiunga na OIC ina maana ya kuwa Tanzania sasa imechukua msimamo wa kupigia kampeni kuwa Palestina iwe na makao makuu Yerusalemu na kulinda mambo ya "kihistoria" na alama za Kiislamu lakini kutotambua na kulinda alama za Wayahudi. Tukijiunga na OIC kama nchi tutakuwa tumeamua kuwa wenye haki ya Yerusalemu ni Wapalestina na Wayahudi hatuwatambui.

Lengo la tisa linasema kuwa ni "kutilia mkazo mahusiano ya Kiislamu katika biashara na uchumi baina ya wanachama; lengo likiwa kufikia muungano wa kiuchumi (economic integration) na hatimaye kufikia soko la pamoja la nchi za Kiislamu".

Je, Tanzania tuna malengo hayo? Je, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ina malengo ya kuifanya Tanzania siku moja tuwe kwenye soko la pamoja la nchi za Kiislamu? Inaonekana CCM wameamua hilo tayari na sasa ni kulitekeleza tu.

Lengo la 11 la OIC linasema kuwa "ni kutangaza, kueneza na kuyatunza mafundisho ya Kiislamu na tunu ambazo msingi wake ni kiasi, kuvumiliana, kueneza utamaduni wa Kiislamu na kutunza urithi wa Waislamu".

Lengo hili ni zuri na linaendana kabisa na jumuiya yenyewe. Tunapotaka kujiunga nao ina maana tumelikubali na tutafanya hivyo. Je, hilo ndilo serikali ya CCM iliwaahidi Watanzania kwenye kampeni zake za 2005 chini ya rais Kikwete?

Jibu inaonekana "ndiyo". Kuwa serikali ya Tanzania kwa kukubali kuingia kama mwanachama kamili wa OIC inataka kutimiza lengo hilo.

Ibara ya pili ya Katiba hiyo inaelezea kiujumla kuwa malengo yote 20 (hata yale yasiyotaja moja moja Uislamu) yataongozwa na mafundisho ya Kiislamu.

Hivyo, hata malengo yanayohusu kusaidiana kiuchumi, sayansi, na teknolojia yote yanazunguka kwanza katika msingi wa mafundisho ya Kiislamu. Je, tuko tayari kuyashika hayo kama taifa?

CCM na serikali zake mbili inaonekana imeamua kutoa jibu la ndiyo. Hivyo ni kama uzugaji kwa Balozi Seif Iddi kudai kwamba OIC haihusiani na sharia za Kiislamu, naomba aangalia hiyo Katiba ya OIC vipengele nilivyovitaja.

Swali ambalo nilikuwa najiuliza ni Tanzania itajiunga kwa misingi gani kwenye OIC wakati yenyewe siyo nchi ya Kiislamu?

Jibu linapatikana ibara tatu kipengele cha pili cha Katiba ya OIC. Kipengele hicho kinasema kuwa "Nchi yoyote ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa, yenye Waislamu wengi kuliko dini nyingine (Muslim Majority) na inakubali katiba hii, ambayo itatuma maombi ya kujiunga itaweza kukubaliwa unachama pale tu itakapopitishwa na Baraza la Mawaziri wa Nchi za Nje kutokana na vigezo vilivyowekwa na baraza hilo".

Kwa vile serikali yetu chini ya rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje, Membe, wameamua kuliingiza taifa letu kwenye OIC ina maana ya kuwa wametambua na kukubali kuwa Waislamu ni wengi zaidi kuliko watu wa dini nyingine nchini na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Waislamu wengi (muslim majority).

Kama hili ni kweli, swali langu kwa Membe ni lini walifanya sensa ya kutambua dini za watu?

Baada ya kuisoma katiba hiyo na kuielewa vizuri na nyaraka nyingine naweza kusema kwa uhakika wa wazi kabisa kuwa Tanzania kama nchi haipaswi, haistahili na isilazimishwe kamwe kujiunga na OIC.

Hili kwangu halina mjadala isipokuwa kwa wale wanaotumia hoja za nguvu (dola); kwamba kwa vile wao wana vimulimuli na wanapigiwa saluti nchini basi wanaweza kuiingiza Tanzania kokote kule kama alivyosema Balozi Seif hivi karibuni.

Je, niseme kuwa Tanzania isishirikiane na OIC katika mambo ya maendeleo na kupokea misaada kutoka OIC? La hasha. Ninaamini kuna njia kubwa mbili za Tanzania kuweza kushirikiana na OIC kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya hiyo ambazo nina uhakika Watanzania hawatakuwa na matatizo nayo.

Njia ya kwanza inapatikana katika ibara ya nne (1). Katika ibara hiyo katiba ya OIC inasema kuwa wapo wanachama watazamaji ambao wanaweza kukubaliwa nafasi hiyo. Inasema hivi "Uamuzi wa kuipatia nchi yoyote mwanachama wa Umoja wa Mataifa hadhi ya Uangalizi (Observer status) utatolewa kwa makubaliano ya Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje tu kwa vigezo ambavyo Baraza hilo limeweka".

Kipengele hiki ndicho kilichoziwezesha nchi kama Bosnia na Herzegovina, Urusi, Marekani, Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwa watazamaji wa OIC. Naamini Tanzania inaweza kuhusiana na OIC kwa Rais Kikwete kumteua balozi maalumu wa Tanzania kwenye Jumuiya ya OIC bila nchi yetu kuwa mwanachama.

Naamini hili litakuwa ni ‘compromise' kati ya wale wanaotaka tuwe na uhusiano rasmi na OIC na wale ambao hawataki kabisa kuwa na uhusiano huo. Endapo tutakuwa na uhusiano wa utazamaji na wakati huo huo kuingia mikataba ya ushirikiano na nchi wanachama kati ya nchi na nchi (kama ambavyo tumekuwa tukifanya) basi hatutakuwa na matatizo mengine mengi ya kikatiba.

Hapa naomba nijibu baadhi ya mapingamizi ambayo yamekuwa yakitolewa na wale wanaotaka Tanzania iwe mwanachama rasmi wa IOC.

Pingamizi la kwanza; Lazima tujiunge OIC kwa sababu mbona hatulalamiki kwa Vatican kuwa na ubalozi wake nchini? Hoja hii ina lengo la kugusa hisia na vionjo vya watu kuliko kushawishi akili.

Mtu anayetoa hoja hii anafanya hivyo bila kugusia upande mwingine kuwa Iran, Palestina, Libya, Syria zina balozi zao nchini. Nchi hizi zote nne na hasa Iran ni nchi za Kiislamu.

Iran hasa kiongozi wake wa juu kabisa ni kiongozi wa kidini kama alivyo Papa. Kwa nini basi wanapouliza swali hili hawaulizi uwepo wa ubalozi wa Irani nchini?

Jibu ni jepesi. Wanafahamu kuwa Vatican kama vile Iran ni nchi kamili licha ya kuwa ina viongozi wa dini kama wakuu wake. Lakini kosa jingine ni kuwa wanapolinganisha OIC na Vatican ni kulinganisha machenza na ndizi.

Moja ni jumuiya ya nchi mbalimbali na nyingine ni nchi kamili. Endapo Tanzania ingekuwa mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kikristu duniani basi hoja ya kujiunga na OIC isingekuwa na utata wowote ule.

Mojawapo ya jumuiya za kimataifa za Kikristo ambazo zinafanya kazi nchini na kutoa misaada ya kila aina kwa Wakristu, Waislamu, na Wasioamini ni Caritas. Tanzania si mwanachama wa Caritas na misaada yao haiitaji tuwe wanachama kwanza. Kwa nini misaada ya OIC itutake tuwe wanachama kwanza?

Pingamizi la pili; Tukijiunga na OIC tutapata misaada mingi kwa Waislamu pia kwa ujumla tunaweza kupata bei nafuu ya mafuta na misaada mingine ya kiuchumi. Hoja hii nayo ina lengo la kuchezea hisia za watu.

Kama kuna jumuiya ambayo tungetakiwa kweli kujiunga nayo ili kupata unafuu wa mafuta ingekuwa kama OPEC na si OIC. Hadi hivi sasa sijasikia ni nchi gani mwanachama wa OIC ambayo imepata unafuu wa mafuta kwa sababu ni mwanachama wa OIC na si vinginevyo. Ingekuwa bei ya mafuta inaweza kufanywa rahisi kwa kujiuinga na OIC basi nyingi duniani zingeshajiunga.

Lakini kubwa zaidi na nimelisema hapo juu ni kwamba tayari tumekuwa na ushirikiano na nchi nyingi zilizomo kwenye OIC. Tumekuwa na ushirikiano na Qatar, Saudi Arabia, Oman, Iran, na nyinginezo nyingi, kati ya hizo zimekuwa zikitoa misaada ya aina mbalimbali.

Kwa maneno mengine ni kuwa nchi nyingi za OIC zinatoa misaada tayari kwa Tanzania bila kutulazimisha kuingia OIC. Ni kitu gani zaidi tutakipata kwenye OIC ambacho hatuwezi kukipata kwa kujadiliana na nchi kwa nchi?

Ninaamini kuwa uamuzi wa kuiingiza OIC ni uamuzi wa kibabe ambao lengo lake halihusiani na mafanikio yoyote ya kiuchumi isipokuwa kuwaridhisha watu wachache ambao wanaona pasipo kupewa hicho basi "Waislamu wanapigwa vita".

Kama lengo la kujiunga OIC ni kuwasaidia Waislamu (kama Katiba ya OIC inavyosema) basi jumuiya ya Bakwata au nyingine ya kimataifa ya Waislamu nchini inaweza kujiunga OIC kwa mujibu wa ibara ya nne (2) ya Katiba ya OIC.

Sidhani kuna Mtanzania yeyote ambaye atapinga Bakwata au jumuiya nyingine ya Watanzania kujiunga na OIC kwa kutimizia malengo ya jumuiya hiyo.

Vinginevyo, tuseme ukweli kuwa uamuzi huu ni wa papara, woga na wenye msingi wa kuendeleza mgongano usio wa lazima kati ya Wakristo na Waislamu. Ni uamuzi unaokwepa kushughulikia matatizo ya kweli ya Waislamu na badala yake kuwageresha kama kwa pili kwa kuiingiza nchi kwenye OIC.

Waislamu wanaofikiri kuwa kujiunga na OIC kutatatua matatizo yao na jamii yetu wanajidanganya. Tayari Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine mengi ya kimataifa yanafanya kazi nchini.

Kama tungekuwa na uongozi wenye kujali maendeleo ya wananchi tungekuwa tumeendelea zamani. Tulichozoa ni kuzugwa na hatuwezi kukaa bila kuzugwa.

Sasa wamefikia mahali pa kuwazuga Waislamu kwa kuwapatia OIC kama pipi tofi ili wanyamaze kulalamika. Binafsi ningewasihi ndugu zetu waislamu kudai Tanzania iingie makubaliano na nchi kadhaa ambazo zina lengo la kutoa misaada kitu ambacho ni bora na rahisi zaidi kuliko kujiunga na jumuiya kubwa yenye malengo mengi.

Vinginevyo wakati umefika wa jamii nzima kupinga uamuzi wa serikali kuliingiza taifa letu kwenye OIC kinyume cha katiba yetu, tukipingana na Katiba yenyewe ya OIC na kwa hakika ikichochea mgongano usio wa lazima.

Tutawakatalie watawala wetu hawa ili wajue kuwa hatukubali. Ikibidi maandamano ya mshikamano kufanyika basi yafanyike, vinginevyo huko mbeleni msishangae bendera ya nchi nyingine ikipeperushwa Ikulu. Ndipo tutakuwa tumechelewa na kugundua kuwa Taifa letu tayari limeuzwa.

Unaweza kusoma Katiba ya OIC kupitia
http://www.oic-oci.org
Niandikie: mwanakijiji@klhnews.com

Source: Tanzania Daima Sept. 3 - 2008
 
Fundi Mchundo,

Exactly!.. maneno yako yanatafsiri kubwa sana kuhusiana na OIC.. Tena umesherehesha vizueri sana uliposema unawapenda Waislaam kama vile unavyowapenda Mabudha na kadhalika....

Mkuu sasa tazama kwa undani maelezo yako mwenyewe, utagundua kuwa huwapendi waislaam kama Waislaam isipokuwa kama binadamu..Ni dini ya kiiislaam inayowafanya watu hao wawe Waislaam hivyo basi huwapendi hawa waislaam ikiwa huupendi Uislaam..unawachekea kichina tu mkuu.
Tatizo lako kubwa ktk usemi wako ni pale unaposema huwezi kuupenda Uislaam kwa sababu ktk fikra zako unafikiria kupenda kitu ni lazima kiwe na maslahi na wewe!... Yaani kinakuhusu wewe kwa namna fulani ndipo mapenzi yako unaweza kuyapima...Ni sawa na wale wasioweza kumpenda mwanamke unless amemkubali ama mwanamke huyo anaweza kuwa na mahusiano naye..Ni ktk mtazamo huo unajaribu kuitazama OIC hali haikuongezei mzigo wala kupunguza riziki zako.

Ndivyo haswa inavyoonekana kwa wakristu wengi na hakika wapo Waislaam wenye kuitazama dini ya Kikristu kama wewe. Utanisamehe tu kwa kuwa nitatumia neno moja ambalo hutalipenda isipokuwa nadhani linaweza kukuamsha kidogo ukaweza kutazama nje ya hilo box... Hawa watu ambao hawawezi kusifia ama kupenda dini ama kitu nje ya matarajio yao huwa wamefutikwa ktk lindi la Utumwa. Ni kutokana na maneno uliyofundishwa, elimu uliyopewa kuwa haiwezekani kukawa na mazuri Upande wa pili.. Ni tactic ambayo Bush na Alqaeda wanaitumia kuvuta maskini hawa wasiofahamu...Ni kina Bush na Alqaeda wanaosambaza udini na fikra za kwamba hakuna mazuri upande wa pili isipokuwa shetani kasimama - EVIL...

Sasa tofauti kubwa kati yangu na wewe ni kwamba mimi naelewa kuwa EVIL ni kati ya sisi wote binadamu kwa rangi zetu, dini zetu, jinsia zetu na kadhalika....Muislaam anaweza kuwa evil kuliko hata kafir yule asiyeamini wala kuabudu kabisa Mungu. Ukristu haufundishi somo la mashetani isipokuwa neno la Mungu..
Mkuu kwangu mimi kama nilivyokwisha sema dini ni imani ambayo inafundisha elimu ya Uungu.. Yesu, Muhammad, Moses, David wote hawa mimi nawaona kama waandishi wa somo hilo kwa nyakati tofauti. Yesu kuwa mtoto wa Mungu haiwezi kunifanya mimi niamini zaidi Biblia laaa hasha! - wala sisomi Kuran kwa sababu ya nafasi ya Muhammad kwa Mungu, kinachonifanya niamini Biblia au Kuran ni mafundisho yake, hata kama Yesu/Muhammad angekuwa mtoto wa Firaun na kaweza kunipa neno la Mungu kwa kina kile ningeamini na kuabudu Mungu huyu huyu tunayemuabudu leo...
Ni kama vile somo la hesabu (Maths) huwezi kabisa kusema fulani ali INVENT mathematics isipokuwa Mungu mwenyewe... Kina Newton na calculus au Euclid na Geometry na wengine wengi tu walivumbua how mathematics worked..Na katu huwezi kusema nani bingwa zaidi kati yao laa sivyo sii elimu tena..pia historia ya maisha yao haiwezi kunifanya mimi nisiamini calculus kwa sababu tu Newton alikuwa mlevi na mtoto wa haramu.

Kwa hiyo mkuu wangu bado unanikumbusha sana maandishi yangu kuhusiana na vitu hivi viwili....1. NJAA na 2. IMANI yaani hivi ndio vinaturudisha nyuma zaidi......kwa sababu unapoamini kitu chochote hali una njaa basi hata elimu yako inasinyaa kichwani...
OIC is just an organisation ambao tunaweza kuwaweka Segelea any minute tutakapo hisi wanajaribu kupotosha nchi.. viongozi wake ama waanzilishi wake wote hawana Deplomatic Immune..hawana jeshi wala hawatembezi msahafu kila nyumba.

Kwa kumalizia, umemsikia Mkuu wangu mwalimu Augustine akisema ati kujiunga kwa Mozambique ni makosa na two wrong can't make it right!... jamani hivi lini umeona wrong ikiwa na positive results!.. kitu chochote wrong ni kile ambacho kimetoa jibu ama matokeo mabaya... Hofu iliyopo hapa kijiweni ni matokeo ya sisi kujiunga na OIC sasa kama Mozambique au Uganda kumetokea mfarakano baina ya Waislaam na Wakristu then tunaweza kusema kwamba hii kitu haitufai na wrong kwetu kujiunga..ila utakuta wanataka sisi tuwaambie faida zake..at the same time haitufai na wrong!

Sasa subiri utaona kundi jingine likijitokeza ikija issue ya Duo citizenship!... huwezi kuona mtu mwenye uraia nje akipinga isipokuwa wale wasiokuwa na Uraia nje...sababu za kupinga utawasikia wakisema tuwaeleze faida zake!.. as if sisi tumebeba faida mgongoni mwetu wapate kuziona tukifungua sanduku. Why wanapinga?... yale yale NJAA na IMANI waliyojengwa na CCM ya Utaifa kuwa yeyote mpinzani wa CCM sio Mtanzania na kibaya zaidi ni kwamba wanaamini kabisa sisi wote tuishio nje tunapingana na CCM, ndio maana tunaishi nchi za nje!.. IMANI!...

Nziku,
Maswali ya mwanakijiji hayana sura kabisa kwa sababu yupo ndani ya kabati la Udini.. sasa nambie tunapofikia swala la Duo citizeship utatumia vifungu gani vya katiba kuhalalisha duo citizenship?..
Ni nyie mnaosema kila siku kwamba swala na NDOA na MIRATHI ni swala la dini na madhehebu yake sasa ilikuwaje lipo ktk katiba?...kwa nini tuna sheria za ndoa na mirathi hali hili ni swala la dini!....
 
Kisingizio cha Serikali cha kwamba OIC itasaidia nchi kwa kutoa mafuta kwa bei rahisi si ya kweli kwani bei ya mafuta yanaendana na market na kuna nchi moja tu inayopata mafuta bure inaitwa North Korea. Mafuta ya Tanzania yanatawaliwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya BP ambayo inategemea visima na inatoa bei kutokana ma market. OIC ni udini na faida yake ni hiyo tu! ukweli ni kwamba tunarahisi mwislam na marafiki zake wanajaribu kumfurahisha kwa hilo bila kujali Katiba ya nchi. Mwinyi alivyokuwa rahisi ilikuwa hivyo hivyo na mabanda ya nguruwe kuvamiwa. Tufate katiba
 
Kisingizio cha Serikali cha kwamba OIC itasaidia nchi kwa kutoa mafuta kwa bei rahisi si ya kweli kwani bei ya mafuta yanaendana na market na kuna nchi moja tu inayopata mafuta bure inaitwa North Korea. Mafuta ya Tanzania yanatawaliwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya BP ambayo inategemea visima na inatoa bei kutokana ma market. OIC ni udini na faida yake ni hiyo tu! ukweli ni kwamba tunarahisi mwislam na marafiki zake wanajaribu kumfurahisha kwa hilo bila kujali Katiba ya nchi. Mwinyi alivyokuwa rahisi ilikuwa hivyo hivyo na mabanda ya nguruwe kuvamiwa. Tufate katiba

....wanatuona hatuelewi na bila aibu eti tutapata mafuta ya bei rahisi,huyu moron membe seems hana idea zaidi ya kuwa robot tuu na hajui katiba wala international oil business inavyo operate,sijawahi kuona mtu hazimo kama membe na huyu ana ambition ya kuja kuwa raisi...mungu atusaidie tuu na hawa kina Membe!
 
Mkuu Mkandara, najua kabisa katika hoja hii ya OIC hakuna anayeweza kukushawishi kwani umeshakubali kutokukubaliana na mawazo pinzani. lakini Mkuu ni kutafuta misaada kutoka nchi za OIC ndo tu kunafanya tushawishike? au ninyi wenzetu mlioshawishika ndo mnajua maslahi yaliyojificha!

Haitoshi kujibu tu kwamba huwezi kutojibu eti kwasababu maswali ya mwanakijiji hayana sura kabisa kwa sababu yupo ndani ya kabati la Udini..udini upi wakati amechambua na kunukuu katiba ya OIC? Mkuu wangu mkandara bora kuwa mkweli.
 
Back
Top Bottom